JF vs FACEBOOK

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,832
Jamani labda mi ndio mshamba kabisa. Nilijiunga na facebook tangu mwaka juzi, huko naona kumejaa ujingaujinga na usharabaro, kila mtu anakutaka. Hapa Jf sina muda mrefu lakini nina furaha na amani, napata changamoto mbalimbali, najifunza mambo mengi na yenye manufaa.

Wadada wenzangu wao wako busy na facebook, ukiwauliza wanaenjoy nini wanasema kuchat, ukiwaambia habari za JF wanasema we Ambilikile kweli (mshamba).

Sasa mshamba sijui ni mimi au wao ambao hawabenefit kitu. Jf is a place to be, thats why niko online kanzia asubuhi hadi usiku mzito.

I am the luckiest one kuwa miongoni mwa wana wa hii familia kubwa ya JAMII FORUMS
 
facebook ni nzuri, sawa, but not as good as jamii forums,, hilo halina ubishi dada yangu,, hakuna sehemu utapata newz mbali mbali, tena very current kama JF.

Pia, kwa upande wangu mimi, nimetolea kujua mambo mengi sana mapya na ya zamani, this is just because of how the jf family wanavyochambua mada, yani wanaelezea vizuri kiasi kwamba u wont miss even a single point, japokua mimi sii msomi sana, lakini kwa sasa naweza nikaa na mtu ambaye ana masterz ya political science n we can talk the same language in politix...

God bless jamii forum..
 
Jf ina majukwaa mbalimbali, ni wewe na mood yako tu. Ukichoka siasa unatwist kwenye Mambo ya Kikubwa unakutana na dada Maria Roza, anakupa nakshi za ukweli na siku zako zote zitakuwa tamu milele daima.
 
Facebook ni nzuri ila matumizi ya wabongo nikatika ufirauni nawabongo wanatumia theruthi ndogo sana ktk facebook kama chat,uploading basi ila facebook inamambo mengi yakujifunza endapo utaingia kwenye link zake!!

But JF unapata fleva ya kitanzania! Ukiwa nje yatanzania unajisikia kama umenyenyuliwa ulipo nakushushwa Tanzania!!

Hivyo hiyo ndiyo tofauti ya facebook na JF, JF for everything
 
Nilijiunga FB lakini baada yakuona ujinga mwingi nilijitoa...sikubahatika kuona faida yoyote ukilinganisha na JF...
 
Jf ina majukwaa mbalimbali, ni wewe na mood yako tu. Ukichoka siasa unatwist kwenye Mambo ya Kikubwa unakutana na dada Maria Roza, anakupa nakshi za ukweli na siku zako zote zitakuwa tamu milele daima.

hebu fikiria jukwaa kama JF Doctor, yaani sina hata la kuelezea kwa jinsi lilivyo sheheni makala mbali mbali za afya.
 
Jamani labda mi ndio mshamba kabisa. Nilijiunga na facebook tangu mwaka juzi, huko naona kumejaa ujingaujinga na usharabaro, kila mtu anakutaka. Hapa Jf sina muda mrefu lakini nina furaha na amani, napata changamoto mbalimbali, najifunza mambo mengi na yenye manufaa.
Wadada wenzangu wao wako busy na facebook, ukiwauliza wanaenjoy nini wanasema kuchat, ukiwaambia habari za JF wanasema we Ambilikile kweli (mshamba). Sasa mshamba sijui ni mimi au wao ambao hawabenefit kitu. Jf is a place to be, thats why niko online kanzia asubuhi hadi usiku mzito. I am the luckiest one kuwa miongoni mwa wana wa hii familia kubwa ya JAMII FORUMS


Kule FB ulikuwa unatumia ID gani?

Hapa nimefurahi kuijua jinsia yako....siku zote nlikuwa natamani niijue jinsia yako.

Tukirudi kwenye mada....ni makosa na hatari kubwa sana kuzilinganisha FB na JF.......Vitu viwili tofauti kabisa! Ni sawa na kulinganisha JWTZ na Mgambo wa City.
 
hebu fikiria jukwaa kama JF Doctor, yaani sina hata la kuelezea kwa jinsi lilivyo sheheni makala mbali mbali za afya.

Ayah, hizo 'free download' link zilizojaa kwenye JF Store? Facebook watu huingia kwa ushawishi, jees kwa kuwa wengi wapo huko, JF unajuiunga for real interest...
 
Nadhani JF na FB ni vitu viwili tofauti kabisa, ingawa zote ni social media.

Lengo la facebook ni kumrahisishia member kutangaza vitu vyake binafsi na kujua nini kinaendelea ktk maisha ya members wengine. kuna forum pia unaweza jiunga na ku-discuss. member anaweza kua mtu ao organisation fulani.

JF ina-focus zaidi kwa habari na ina -encourage member kuchangia katika habari mbali mbali. Sio lazima members wengine wajue wewe ni nani na unafanya nini, muhimu zaidi wajue unafikiria nini kuhusiana na topic.

Mimi ni member wa Jf kwa jina la russianroulette na inanipa liberty ya kuchangia kwa topic yoyote. Kwa FB nipo kwa jina langu mwenyewe na nahakikisha kila kitu ninasema namaanisha na naweza kujitetea in case of anything.
 
fb ni kuweka picha zenye fake smiles kuimprest the opposite sex,..ndicho nilichogundua huko,masharobaro kibao,.ukiweka mada ngumu za ukombozi watu hawako interested,..jf is nothing but a struggle,emancipation of the exploited tanzanian population,.long live jf
 
Ukiondoa mafirauni wachache waliomo humu JF ambao wamejaa fikra mbinuko, naomba nisiwataje, JF imesheheni vichwa vya maana kutoka kwenye professional tofauti. Pia JF ina member wa rika tofauti kuanzia vijana wa secondary mpaka wazee hivyo usishangae kuona mtu akikupa details za kina Kingunge wakati anasoma nao shule ya msingi.

Mimi pia nimejua vitu vingi sana kupitia jf ingawa mara nyingi nimekuwa sichangii zaidi ya kufurahia michango ya member wengine.
 
Jf makes my day,nimewashawish ndugu zangu na staffmate wangu wajiunge,napata hbr fast,nilipata hbr za kifo cha prof kamuzora early than mwanae,mimi ndo nilimjuza,
zaid ya yote nikiwa alon inaniliwaza sana
 
Kiukweli ni kutaka kufananisha panzi na mwewe!!!

Tunapaswa kama wadau wa JF kuinyanyua na kuiweka mbali zaidi ya hapa ilipo... kwa maana kuinyanyua JF ni kuinyanyua Tanzania pia.

Inapaswa watanzania wajielewe, japokuwa ni wachache wanaotumia mtandao kwa sasa, ila nawahakikishieni wadau ndani ya miaka mitatu ijayo hata kina Ambilikile watakuwa wanatambua namna ya kuutumia. Tumefanya jitihada za ziada na tunaendelea kuzifanya ili watanzania waweze kutandaa na ni jukumu la kila mmoja wetu kufanya hivyo. Tatizo ambalo tunalo kwa sasa wengi wa watanzania hawajui kutumia mtandao kwa faida zaidi ya kutazama picha za ngono na upuuzi mwingine!

FB ina mambo chungu tele kutokana na muelekeo halisi wa mhusika. Sishangai dadaangu unapojikuta unaletewa maneno ya mahaba na kutakwa kwenye FB, hizo ndizo "akili za kitanzania" ndio maana nilipata kuandika "WAKATI WENZETU WANA-JENGA NA KUWEKA MASHULE NA VYUO MBALIMBALI SISI TUNAJENGA MABAA GROSARI NA NYUMBA ZA KULALA WAGENI KILA MAHALA!!!
 
Watanzania hatuishiwi maneno..2na maneno mengi sana with no actions! JF na FB zote ni social media na zina contents tofauti..utumiaji vibaya wa hizi sites ndio unaoleta shida..! mbona kuna ambao pia wanajitoa JF kwa madai kuna mambo ya kijinga..! kinachotakiwa 2fahamu ni impacts zake ktk jamii
kwa upande wangu naweza kusema jf imekaa kimaendeleo zaidi (kwa maana ya kuhusisha nyanja zote kijamii) na fb imekaa kirafiki zaidi japo zote unaweza kupost links na ukapata more informations!
Nakumbuka kuna kipindi BBC walikua wakijadili jinsi gani fb ilivyokua iki2mika ktk siasa na ukuaji wa demokrasia(political campaign) kwa hiyo kikubwa hapa ni matumizi tu..!
Bt tukiitumia vizuri jf tutafika mbali sana in-terms of exposure
 
JF mwisho wa mambo..kule FB wamejaa wajingawajinga wanatongozana tuuuu,mpaka majuzi kuna rafiki yangu mke wake kalala na jamaa alilipata humohumo FB...tena yule dada kakamatwa na mumewe analia kama punda jike!!!
 
Back
Top Bottom