Jf vote of no confidence to pm. Hapa tunahitaji vote ngapi?

KOMBAJR

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
5,827
1,271
Katika Kuhitimisha Hotuba yake Mh.Zitto amesema kuanzia kesho watakuwa na karatasi mlangoni kuandika jina na kusaini ikiwa kama kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu!Na idadi ambayo inahitaji ni 70 tu!


Mytake: JF kama jukwaa huru kama mazungumzo ya siku mbili i mean jana na leo kuhusu mwenendo wa serikali na watu tuliyowapa dhamana ya kuongoza wamedhihirisha kushindwa kwa vitendo.

Toa Maoni na sababu zisizo pungua Tatu na zizizo zidi sita ambazo zinafanya hii hoja kumwajibisha waziri mkuu kuwa na mashiko!

Naomba kuwasilisha mod naomba ufanye kazi ya urefa hapa mwisho wasiku tutawasilisha kwa wahusika kwamaana JF pia inawakilisha wengi!
 
Sababau
1.ubadhirifu
2.kutokuwawajibisha wabadhirifu
3.kulindana
4.kuhujumu nchi
5.kutokuchukua hatua za kuinua uchumi na mfumuko wa bei
 
Kanyaga Twende hata Mubaraka alidondokea pua kwa style ya mtandao.....inawezekana!ni uthubutu tu
 
Hujaeleweka sana unataka nini lakini hoja ya Zitto ina mashiko sana. Moja uzembe uliokithiri wa mawaziri wetu ambao wapo chini ya waziri mkuu Pinda.

Kama Pinda anashindwa kuwawajibisha basi awajibishwe yeye.
 
Kitu bila chenga mkuu mbona umejibu vyema hapa nilichokuwa na maanisha wakati Zitto wanaendelea na move yakukusanya majina 70 bungeni na sisi hapa tunakusanya idadi ya wanaounga mkono hoja ya kwanini PM asipigwe chini ila lazima tutoe sababu za msingi.
 
Sababu ziko wazi mkuu. haina haja ya kuzitaja. Neno 'naunga mkono hoja linatosha.

Mimi naunga mkono hoja ya kamanda zito kwa asilimia zote.
 
kilichozungumzwa ni kuwa wabunge hawawezi kuwawajibisha mawaziri kwa sababu ni wateule wa baba riz ila kwa upande wa serikali linaweza kum-wajibisha Waziri mkuu ambaye licha ya kuwa ni mteule wa JK pia bunge lilimpigia kura ili kumthibitisha.
hivyo serikali aidha iwawajibishe mawaziri husika au PM awajibishwe na wabunge.
 
Leo Zitto na wenyeviti wengine wa Bunge nimewakubali. Zitto kaongea zaidi straight and firm, wengine Cheyo na Mrema japo wameibana lkn ni kama kuna saa walikuwa wanapulizia hivi. Big up Zitto na kamati nzima
 
Either way...wewe kama wewe Kuku asiyetaga na ambaye anataga na kula mayai bora yupi?
 
sasa kama waziri asubuhi anawaambia wabunge kuwa hawalipii deni la ndege mbovu ya kukodi,
kumbe washalipa na wanampango wa kuwapa wadeni bandari ya mtwara kufidia deni unataka nini kifanyike?
 
Kwa mujibu wa katiba ya JMT Ibara ya 52, kazi na mamlaka ya PM ni kama ifuatavyo,

(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

(2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.

(3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

Kwa hiyo ikithibitika kuwa PM kwa namna moja au nyingine ameshindwa kutimiza wajibu wake ndio ibara ya 53A itafanya kazi.
Binafsi namuona pinda kama sio strong kabisa na ni muhimu akapatikana waziri kichaa kurekebisha mambo, ila pia nafikili Kwa mtazamo wangu mimi, tuna matatizo makubwa katika sheria zetu na ndio maana baadhi ya viongozi wa kiserikali wanashindwa kutimiza wajibu wao.
 
sababu ni nyingi mno,cha mhimu kama mawaziri hawataki kuwajibika basi pinda chaliiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Tupia hapa sababu zizizozidi 5 kwanini apigwe chini chalii angu!
 
Automaticaly mawaziri wakipaga chini na yeye atakuwa anangoja nini?uwajibikaji muzeya!
 
Heshima kwako Kiongozi wa kuelimisha umma..........hayo yote hapo juu ameyanya below poverty line au "E" kwenye geji ya wese!
 
Piga nyama chini...... Ila duh idadi ya mawaziri wakuu wastaafu inaongezeka kodi zetu hili nalo inabidi tuliangalie kwa jicho la tatu
 
sababu ambazo ninaona zinampasa waziri mkuu kuwaibika
1- kushindwa kuwawajibisha mawaziri wake ipasavyo
2- kushindwa kusimamia vizuri kwa umakini shughuli za kisaerikali kiasi kwamba hawezi kuyatetea makosa yanayoikabili serkali
3- kuwaachia watu wachache wakaitafuna nchi wakat idadi kubwa ikighubikwa na umaskini uliokithiri
4-kuhatarisha amani ya nchi kwa kiasi kikubwa, kwani watu hawapendi wala kuwa na imani na viongozi wao.
5-kupanda dhana potofu ndani ya vijana wadoogo kuwa bila kuiibia serikali huwez kutoka kimaisha hivyo kuipa rushwa na wizi mianya mikubwa zaidi
6- kwa uwajibikaji mbovu wake inafsi na watendaji wake ameisababishia serikali hasara kubwa sana na kuitia katika mzigo mkubwa wa madeni.
 
Piga nyama chini...... Ila duh idadi ya mawaziri wakuu wastaafu inaongezeka kodi zetu hili nalo inabidi tuliangalie kwa jicho la tatu

huyu hatakuwa mstaafu, kwani kaondolewa madarakani na atakuwa kama raia wengine tu. Namshauri GL aendelee kusugua goti ili kieleweke.
 
katika hili mtu hahitaji kuumiza kichwa sana! waziri huyu hayupo serious kutosha, hiyo tuu ni sababu kutosha. ukitaka kuongeza ni dhahili ameshindwa kumshauri raisi katika mambo ya msingi, ameshindwa kujibu hoja za msingi na "kuapeal to mercy" ameshindwa kuwawajibisha mawaziri! nk. hafai!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom