JF Unilateral Ceasefire...?

JF Unilateral Ceasefire...? No such a thing.

Kuna kila dalili kuwa tunawafikia na wanapata imapct.

Wao wachape kazi tuliyowapa.

Walipoingia kazini waliapa. Wafuatie viapo vyao vya uogozi..

Wanazijua sheria za nchi wazifuate.

Wanajua maadili ya Taifa na maadili ya uongozi...hatuna tatizo nao...Watekeleze.

Wao ni viongozi..its ok. Sisi ni wananchi ..sawakabisa. Wanaelewa kuwa wote sisi ni watu.

They need food , na sisi pia. wanahitaji shelters na sisi pia . wana mahitaji.. na sisi pia... Tusichopenda na amabacho kitaleta tatizo ni kuwa ..Hatutaki Kuwe natofauti kati ya sisi na wao kwenye mambo ya muhimu kama haya. UTU NI UTU hakuna tofauti. Na hilindio chimbuko la hii nchi.

Utu ni utu tu! Unilateral...cfire kwa nini? Au haelewi nini?

Wafanyekazi yao Tu ..all will be very ok! Amani na utulivu mbele !
 
Kuna mambo yametokea hapa JF katika wiki hizi chache ambayo yamewafanya watawala washtuke kidogo. Ndio wamekuwa wakishtushwa na yanayoendelea lakini haya makubwa matatu yamefanya kutoa ushauri wa kuitaka JF ipunguze mwendo kidogo na kuwapa nafasi ya kupumua.

- Kuibuliwa kwa kashfa Shirika la Posta ambapo baadaye wafanyakazi watano walijikuta wakiwekwa pembeni kwa hatua za kinidhamu. Mambo hayo yalitakiwa yamalizike ndani "kwa ndani" na kutolewa hadharani jinsi ile hakikuwafurahisha watu wengi. Wanasema wenye manung'uniko wangefuata taratibu.

- Ukodishaji wa Airbus (dege letu kubwa kabisa) na jinsi ambavyo mambo yaliendeshwa. Uvujaji wa habari za ATC licha ya kutofanyiwa kazi na wakubwa kufuatia agizo la "mkulu" mmoja mwenye maslahi ya kibinafsi kuliwaudhi wahusika wengi kwani lolote walilokuwa wanapanga kufanya liliibuliwa hadharani. Watu wengine wasiopungua watano wakapoteza kazi zao kwa kudhaniwa kwa namna moja au nyingine wanahusika na uvujaji huo.

- Kuibuliwa kwa barua ya Jim Sinclair ambayo ilichambuliwa na kufanya ionekane kuwa jamaa ana ubia na kumlazimisha kuandika barua ya kujieleza kwa wadau imemsumbua mmoja wa wakulu kwani imemfanya aonekane kama poodle wa Jim. Hakufurahishwa na jinsi watu walimshambulia mwekezaji na kukawa na hofu kuwa tunaweza kusababisha wawekezaji waanze kukimbia.

- Kuibuliwa kwa deni la Mkullo masaa machache kabla ya yeye kusoma bajeti kulionekana ni mbinu ya aina fulani kumchafulia. Siku chache baada ya statement ile kuanza kusambazwa mtandaoni Bw. Mkullo ameanza haraka ya kulipa deni lake na hivyo kushughulikia jambo hilo ambalo anaamini lingemletea picha mbaya hasa kwenye mjadala ujao wa wizara yake.

- Kilele cha kukerwa huko nako kumetokea masaa machache yaliyopita ambapo Bajeti ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania ilipatikana hapa kwanza kabla ya kupatiwa Wabunge! Hiki inadaiwa kimemuudhi hata JK kwani amshangazwa inakuwaje bajeti yetu jinsi ilivyo inasomwa karibu masaa ishirini na nne kabla ya ile ya Wakenya, Waganda, Rwanda na Burundi! Hili la kuvuja kwa bajeti limeanza kuwasumbua watu fulani fulani kwa kuonesha uzembe au kutowajibika.

- Lakini kilichowaudhi baadhi ya watu ni jinsi habari za "sanaa ya jadi/kisasa" kuonekana kutumika Bungeni na habari hizo kufika JF kabla ya vyombo vya usalama na hivyo kuharibu jitihada za uchunguzi. Inadaiwa kitendo cha kuweka habari za "mbunge" huyo hapa na kile kilichojiri inadaiwa iliwapa nafasi wahusika kuanza kujaribu kupoteza ushahidi hasa baada ya habari kuonesha kuwa tukio lilikuwa ni Jumanne kumbe ni la Jumatatu na haikuwa kwenye mkutano wa wabunge wa CCM bali baada ya briefing ya wabunge wote. Hili la habari hizi ambazo wabunge walitaka zimalizike kimya kimya kwani zinaweza kumuabisha mtu zimewafanya wawe waangalifu sana na vyombo vinavyochunguza vimesikitika kuwa wao wamepata habari toka kwa waandishi waliopitia kwenye mtandao na baadaye kuthibitishiwa na uongozi wa Bunge.

Mambo hayo na mengine madogo madogo ambayo yanajulikana JF kama "datas" yamesababisha ujumbe utumwe japo si kwa maneno kamili kuwa JF katika jitihada za kumwaga data yawezekana wakawa wanaharibu mambo mengi ya uchunguzi, upelelezi n.k Ujumbe huo unaashiria kuwa kama kuna mtu anaona kitu chochote serikalini hakiendi sawa afuate taratibu za malalamiko na kama ni suala la uhalifu afuate vyombo vya kisheria badala ya kuweka taarifa kwenye mtandao ambako hajulikani ni nani na ni vigumu kufuatilia. Zaidi ya yote, inashauriwa tuwe tunasubiri taarifa rasmi ili kuwe na uhakika wa kinachosemwa badala ya kueneza tetesi, uvumi, propaganda na "vijimaneno" ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama, amani, mshikimano na utulivu wa nchi yetu.

Swali kwenu: Je JF na wale watoa data watangaze unilateral ceasefire? Tuendelee kuwa mahali pa kujadiliana mambo mengine lakini mambo ya kuleta habari nyeti tuyaweke pembeni hadi tupate taarifa, ushahidi na vielelezo kamili?

Mwanakijiji,

Unataka ceasefire na mwizi wa mali yako? Mtu amekuibia ng'ombe wako, ceasefire hapo ni kwa yeye kurudisha kwanza alichoiba.

Unataka ceasefire gani na serikalii hii ambayo imejaa mizengwe, ufisadi, ushirikana, na kukomoana?

JF haitaji kufanya ceasefire na mtu, usemi wetu ni ule kumkoma Nyani Giladi, tukianza kumwangalia huyu nyani wote tutaona huruma, tutaamua kumuacha japo kala mahindi yetu yote.

Bahati mbaya Nyani mwenyewe, hiyo sura ya huruma ni janja yake tu ya kupitisha muda ili aendelee kutuibia vizuri. Kama serikali inataka ceasefire basi iwashughulikie mafisadi kwanza, wote akina Chenge, Ballali, Mramba, Mgonja, Lowassa, Mkono na wengine. Pia iwafute kazi akina Hosea, Mwanyika na wazembe wengine.

Bila ya hivyo hakuna cha ceasefire na badala yake inabidi mapambano yaongezwe, unapoona adui anazidiwa sio muda wa kupumzika au kuonyesha huruma, ni muda wa kuongeza kipigo.

Idumu JF.
 
JF Unilateral Ceasefire...? No such a thing.

Kuna kila dalili kuwa tunawafikia na wanapata imapct.

Wao wachape kazi tuliyowapa.

Walipoingia kazini waliapa. Wafuatie viapo vyao vya uogozi..

Wanazijua sheria za nchi wazifuate.

Wanajua maadili ya Taifa na maadili ya uongozi...hatuna tatizo nao...Watekeleze.

Wao ni viongozi..its ok. Sisi ni wananchi ..sawakabisa. Wanaelewa kuwa wote sisi ni watu.

They need food , na sisi pia. wanahitaji shelters na sisi pia . wana mahitaji.. na sisi pia... Tusichopenda na amabacho kitaleta tatizo ni kuwa ..Hatutaki Kuwe natofauti kati ya sisi na wao kwenye mambo ya muhimu kama haya. UTU NI UTU hakuna tofauti. Na hilindio chimbuko la hii nchi.

Utu ni utu tu! Unilateral...cfire kwa nini? Au haelewi nini?

Wafanyekazi yao Tu ..all will be very ok! Amani na utulivu mbele !

Umesema yote .Sina la kuongeza hapa .Wao wafuate hayo hapo juu na sisi tutaona kama ni kweli then tutajua vita ipiganwe.Wana Usalama , Polisi , Jeshi nk wanatumia maguvu sasa sisi tutamia akili na kalamu .
 
Wajue tu kuwa mapambano yanaendelea......Naomba JF kama kuna uwezekano kuwa na radio station.....maanake dataz zinazopatikana hapa ni kwa wachache tu wenye access ya internet....hebu jiulize hizi dataz zingewafikia wakulima wale wa jembe sijui ingekuwaje.

Wananchi wengi haswa wale wa vijijini hawajui kinachoendelea ndio maana nawalumu vyama vya upinzani.....hawa wananchi inabidi waeleweshwe kuwa nchio inaliwa.

Mkubwa naungana nawe,

Lazima tuwe na mpango mahsusi kufikisha taarifa kwa Wadanganyika mpaka vijijini. Vita hii HAITOKOMA na wala wana JF hatutoishinda kama hatuibuki na mkakati wa kuongeza idadi ya Wadanganyika WANAOSONONEKA nasi kwa dhati. Naamini sana NGUVU ya UMMA. Hapa ndipo mahakama ya kweli ya MAFISADI ilipo. Rejea Mashtaka ya Dr. Slaa kwa Wadanganyika, jikumbushe kadhia walizopata wabunge pamoja na serikali baada ya hapo utagundua umuhimu wa kuwa na njia ya mawasiliano inayofikisha ujumbe mahsusi kwa wengi.

Hii siyo hoja tena, kwa cyberspace JF imeikamata dunia kwa watumiaji wa Kiswahili. Inabidi sasa tuangalie jinsi ya kuwafikia wasiofikwa na mawasiliano ya tech hii ya mtandao.

Fursa iliyopo, natumaini wengi mmesikia kuanzishwa kwa Universal Communication Access Fund (UCAF). Si muda mrefu mfuko huu utaanza kutoa pesa kusaidia Wajasiriamali wanaotaka kufikisha mawasiliano ya Radio, Simu, internet etc vijijini. Uzuri wa nchi kama Tanzania serikali mara kadhaa hujifanya BANK ISIYOKOPESHA KWA KUTAFUTA FAIDA. Ila kwa bahati mbaya fursa hii wamekuwa wanaifaidi sana wageni. Namaanisha TUNATAKIWA KUJIPANGA ILI TUTUMIE FURSA HII NA ZINGINE KUJENGWA NA MITAJI YA SERIKALI TUNAYOTAKA KUIIMARISHA ILI IWATUMIKIE WATANZANIA.

Mwenye hoja kinzani na hii kuwa Serikali yetu haigawi mitaji bure ajiridhishe na yafuatayo:

1. Je, Rostam Aziz amewahi kurejesha pesa aliyokopwa na NBC enzi zile chini ya serikali?
2.Je, viwanda vya ngozi vilivyouzwa kwa mkopo kwa Rostam na kisha amevibadili kuwa godown baada ya kuuza machine (most being stainless steel) amewahi kuilipa hata senti serikali?
3.Je, Manji alinunua jingo la NSSF kwa TShs. ngapi na kasha kuliuza kwa shirika hilo hilo ndani ya muda mfupi kwa TShs?
4.Waweza pia kujiridhisha na mitaji iliyoanzisha akina Kagoda, Gree Finance, Meremeta, etc

NI HAYO TU............!
 
Cha kuwasaidia ni kuwashauri wawapeleka mafunzo maafisa wao wa usalama wa taifa na vyombo vingine ili wakajifunze kutumikia taifa badala ya viongozi na chama tawala. So long as vyombo vyetu vitaendelea kufanya kazi kwa minajili ya kujipendekeza kwa viongozi wa kisiasa na chama tawala wataendelea kupwaya na itafika mahala wananchi watawadharau na hawataheshimu chochote wanachowaambia.

Kuna haja pia wale wanaojifanya spin doctors wa serikali wakachukue mafunzo. Ni wazi kwamba mtu kama Salva ile kazi haiwezi. Walikosea sana walipodhani kwamba kwa kuwa alikuwa anaandika makala basi angeiweza kazi ya spin doctor. Amefeli vibaya mno.
 
- Kuibuliwa kwa barua ya Jim Sinclair ambayo ilichambuliwa na kufanya ionekane kuwa jamaa ana ubia na kumlazimisha kuandika barua ya kujieleza kwa wadau imemsumbua mmoja wa wakulu kwani imemfanya aonekane kama poodle wa Jim. Hakufurahishwa na jinsi watu walimshambulia mwekezaji na kukawa na hofu kuwa tunaweza kusababisha wawekezaji waanze kukimbia.

Kama ni wawekezaji wa kweli, hawawezi kuacha kuheshimu nchi yetu!! Huyo wa kukimbia atakua feki na ni bora aende...
- Kuibuliwa kwa deni la Mkullo masaa machache kabla ya yeye kusoma bajeti kulionekana ni mbinu ya aina fulani kumchafulia. Siku chache baada ya statement ile kuanza kusambazwa mtandaoni Bw. Mkullo ameanza haraka ya kulipa deni lake na hivyo kushughulikia jambo hilo ambalo anaamini lingemletea picha mbaya hasa kwenye mjadala ujao wa wizara yake.

They should thank JF

- Kilele cha kukerwa huko nako kumetokea masaa machache yaliyopita ambapo Bajeti ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania ilipatikana hapa kwanza kabla ya kupatiwa Wabunge! Hiki inadaiwa kimemuudhi hata JK kwani amshangazwa inakuwaje bajeti yetu jinsi ilivyo inasomwa karibu masaa ishirini na nne kabla ya ile ya Wakenya, Waganda, Rwanda na Burundi! Hili la kuvuja kwa bajeti limeanza kuwasumbua watu fulani fulani kwa kuonesha uzembe au kutowajibika.

Hii yaweza kuwa sawa...

Mambo hayo na mengine madogo madogo ambayo yanajulikana JF kama "datas" yamesababisha ujumbe utumwe japo si kwa maneno kamili kuwa JF katika jitihada za kumwaga data yawezekana wakawa wanaharibu mambo mengi ya uchunguzi, upelelezi n.k Ujumbe huo unaashiria kuwa kama kuna mtu anaona kitu chochote serikalini hakiendi sawa afuate taratibu za malalamiko na kama ni suala la uhalifu afuate vyombo vya kisheria badala ya kuweka taarifa kwenye mtandao ambako hajulikani ni nani na ni vigumu kufuatilia. Zaidi ya yote, inashauriwa tuwe tunasubiri taarifa rasmi ili kuwe na uhakika wa kinachosemwa badala ya kueneza tetesi, uvumi, propaganda na "vijimaneno" ambavyo vinaweza kuhatarisha usalama, amani, mshikimano na utulivu wa nchi yetu.

Swali kwenu: Je JF na wale watoa data watangaze unilateral ceasefire? Tuendelee kuwa mahali pa kujadiliana mambo mengine lakini mambo ya kuleta habari nyeti tuyaweke pembeni hadi tupate taarifa, ushahidi na vielelezo kamili?

Hakuna jipya, JF zipo kila nchi na usalama na amani haviharibiki kwa kusema ukweli!!! Cha maana ni kutokuwa wazushi basi.
 
Hakuna jipya, JF zipo kila nchi na usalama na amani haviharibiki kwa kusema ukweli!!! Cha maana ni kutokuwa wazushi basi.

MTM wanasahau kwamba JF ni pamoja na wale wote ambao wanamzunguka Rais maana ndiyo wanatupa nyaraka na nyeti kwa kuto kufurahi Rais na kundi anavyo fanya kazi .JF wamesambaa sasa hata kuwauzia sasa ni issue kubwa mno .

JF ni kilma mpenda maendeleo , haki ya Mtanzania na Tanzania .
 
Bwana eee! wasitueleze habari zao za ajabu ajabu! aah, mtandao wao wa kero umeugua utapiamlo, ukituma hoja au kero kila siku utaambiwa swala lako bado lashughulikiwa lakini kibaya zaidi ni hoja ngapi huandikwa kwenye magazeti au mikutano ya hadhara na Gov ikatake action? hadithi za nyamaza mwanangu takuletea ndizi tushaziacha Kindergaten, mwendo mdundo tu!
 
Swali kwenu: Je JF na wale watoa data watangaze unilateral ceasefire? Tuendelee kuwa mahali pa kujadiliana mambo mengine lakini mambo ya kuleta habari nyeti tuyaweke pembeni hadi tupate taarifa, ushahidi na vielelezo kamili?

Hapana lazima tuendeleze mapambano
 
Jamani haya maonyo muyachukulie serious. Kuifuatilia serikali namna hii sio vizuri. Haya mambo ya kuendekeza issue ya Chenge kuwa ni ushirikina wakati ukweli ni kuwa Chenge alikuwa anatafuta kiti cha kukaa bungeni ni mfano mojawapo.

Shauri yenu, msije sema mie sikuwaambia.
 
UMUHIMU, UMAARUFU, UHALALI na ULAZIMA wa kuwepo JF unatokana na TABIA na MATENDO mabovu ya VIONGOZI( kama tunao!) na WATAWALA wetu. Wakibadilika tu wakatenda HAKI muda wote; JF itaendelea kuwepo lakini kwa staili ingine kabisa.
Vinginevyo, JF kwa sasa ni zaidi ya chombo cha habari na muda si mrefu inaweza ikawa zaidi ya BUNGE.
 
JF lazima iseme madhali serikali inakataa kusema.
hivi umesikia wapi kuwa polisi haifanyi uchunguzi mpaka iaibishwe hapa JF! vyombo vya usalama tanzania vimelala fofofo na ndio maana wananchi wamevumbua njia mpya ya kuchukuwa hatua.
 
Either JF is doing the right thing, the right way and wrong time (to them) or JF is doing the wrong thing completely.

The question I have is why is Serikali and Usalama (Polisi, PCCB, TISS, AG) always 10 steps behind JF in uncovering, investigating and providing prognosis (analytical assesment) on everything that involves Corruption, Economic Sabotage and white colar crime?

If they can answer that, then we could make pact with them and dance to the same tune. Otherwise, their lack of responsiveness is prompting everyone kumwaga Dataz!

POST OF THE YEAR...
mkuu umesema kweli na ukweli huuma always
 
Jamani haya maonyo muyachukulie serious. Kuifuatilia serikali namna hii sio vizuri. Haya mambo ya kuendekeza issue ya Chenge kuwa ni ushirikina wakati ukweli ni kuwa Chenge alikuwa anatafuta kiti cha kukaa bungeni ni mfano mojawapo.

Shauri yenu, msije sema mie sikuwaambia.

...kwa hiyo alikuwa anatafuta kiti cha kukaa baada ya session ya bunge?? au usiku ule kulikuwa na bunge la kalumanziras????? waungwaaanaaaa!!!!!
 
Mkubwa naungana nawe,

Lazima tuwe na mpango mahsusi kufikisha taarifa kwa Wadanganyika mpaka vijijini. Vita hii HAITOKOMA na wala wana JF hatutoishinda kama hatuibuki na mkakati wa kuongeza idadi ya Wadanganyika WANAOSONONEKA nasi kwa dhati. Naamini sana NGUVU ya UMMA. Hapa ndipo mahakama ya kweli ya MAFISADI ilipo. Rejea Mashtaka ya Dr. Slaa kwa Wadanganyika, jikumbushe kadhia walizopata wabunge pamoja na serikali baada ya hapo utagundua umuhimu wa kuwa na njia ya mawasiliano inayofikisha ujumbe mahsusi kwa wengi.

Hii siyo hoja tena, kwa cyberspace JF imeikamata dunia kwa watumiaji wa Kiswahili. Inabidi sasa tuangalie jinsi ya kuwafikia wasiofikwa na mawasiliano ya tech hii ya mtandao.

Fursa iliyopo, natumaini wengi mmesikia kuanzishwa kwa Universal Communication Access Fund (UCAF). Si muda mrefu mfuko huu utaanza kutoa pesa kusaidia Wajasiriamali wanaotaka kufikisha mawasiliano ya Radio, Simu, internet etc vijijini. Uzuri wa nchi kama Tanzania serikali mara kadhaa hujifanya BANK ISIYOKOPESHA KWA KUTAFUTA FAIDA. Ila kwa bahati mbaya fursa hii wamekuwa wanaifaidi sana wageni. Namaanisha TUNATAKIWA KUJIPANGA ILI TUTUMIE FURSA HII NA ZINGINE KUJENGWA NA MITAJI YA SERIKALI TUNAYOTAKA KUIIMARISHA ILI IWATUMIKIE WATANZANIA.

Mwenye hoja kinzani na hii kuwa Serikali yetu haigawi mitaji bure ajiridhishe na yafuatayo:

1. Je, Rostam Aziz amewahi kurejesha pesa aliyokopwa na NBC enzi zile chini ya serikali?
2.Je, viwanda vya ngozi vilivyouzwa kwa mkopo kwa Rostam na kisha amevibadili kuwa godown baada ya kuuza machine (most being stainless steel) amewahi kuilipa hata senti serikali?
3.Je, Manji alinunua jingo la NSSF kwa TShs. ngapi na kasha kuliuza kwa shirika hilo hilo ndani ya muda mfupi kwa TShs?
4.Waweza pia kujiridhisha na mitaji iliyoanzisha akina Kagoda, Gree Finance, Meremeta, etc

NI HAYO TU............!

Na Umkamate-Vilivyo!

Omutwale, inaonekana kwenye nyekundu unayafahamu na ya Kijani ni hivi...Umewapa ulaji mafisadi!

Kwa rangi nyekundu...
1. Ni ngapi?

2.Hivi Viwanda vinaitwaje?

3.Hilo 'Jingo' la Manji na 'kasha' lake? Ni kiasi gani? Ni ngapi?

4.Ningependa kupata waraka unaoeleweka, kuhusu hii ya nne.

SYK
 
Mkuu mwanakijiji,

kama kawaida yako umeleta another jambo ambalo naona ni controversial.

Unilaterla ceasefire maana yake ni kusalimu amri bila kuongojea na adui nae asalimu amri.

Kwa mfano Iran leo wanaweza kuamua kufanya Unilateral Ceacefire kwa kuacha kuendelea kutengeneza nyuklia bila ya nchi zingine kama Marekani, Israel, Uingereza India na zingine kufanya hivyo.

Pia Iran haiwezi kufanya Ceasefire eti kwa sababu inashinikizwa na nchi ambazo pia zina silaha hizohizo na zinaonekana ni tishio kwa Iran.

Lakini pia Uinilateral Ceasefire inaweza kufanyika baada ya kufanya mashambulizi makali kwa adui na kumwambia yuleyule adui kwamba sasa tukae chini na tuzungumze, lakini baada ya kumtia majeraha.

Sasa kwa suala la JF kuchukua uamuzi wa unilateral Ceasefire nafikiri halipo.

Yeyote anaeona mashambulizi ambayo ni ya kuchagiza watu wasiwe mafisadi na kufilisi nchi ni makali,akae pembeni.
 
Mimi nashauri tuwabane mbavu na kujiweka sawa kuwa na massive campaign against wao na Chama chao mwaka 2010 .We can do it kama Sinclair kalazimika kuandika barua kuomba msaha sabau ya JF na yeye ndiye ana ubia na Rais na Urais kwa nini tusiwashinde ? Tujiandae tumechoshwa na longo longo.

mhhh hii mbona sijaielewa?
 
Lakini kuwe na ushahidi ! sio mtu analeta data flani alafu hana ushahidi wa maana.:glasses-nerdy:
 
Mmj,nilisoma ripoti ya meremeta pia japo si jf,sijaelewa,unataka na JF iwasaliti watanzania kama Mengi na ipp?
 
Back
Top Bottom