Jf, Twitter na Facebook zama za barua na S. L. P

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,645
155,016
Haya maisha tunayoishi leo nadhani yangekuwa matamu zaidi enzi za barua za kuandika kwa mkono na kisha kuzituma kwa posta.

Facebook sijui ingekuwaje?
Jf ingedhibitiwa na skrining ya shirika la posta.
Barua zote zenye kueleza uozo wa serikali bila shaka zingegongwa muhuri RTS return to sender
 
S.L.P 000
Dar,

Kwako Bujibuji

salaam sana ama baada ya salaam mimi ni mzima.

Dhumuni la waraka huu ni kukumbushia enzi za barua baada ya kuchakachuliwa na mitandao ya kijamii.

Je unajisikiaje kupata barua hii?

Wasalaam,
dadako

afu juu ya bahasha naandika (before you open guess who?'
 
Last edited by a moderator:
Hofu na mashaka ni kwenu.
Vipi wenzetu mvua huko ?
Sisi huku mahindi ndiyo yameaanza kutoa mbelewele.
Mara upatapo barua hii tutumieni dagaa.
Pia hiyo Telegram money oder T.M.O haijafika.
N.b usisahau dagaa.
Wasalaam.
 
GO AND TROT STEP BY STEP THEN STOP TO BUJIBUJI
S.L.P. ....
MAHALI. TANZANIA
hiyo ni bahasha kwa mtumiwaji. siku hiz hatai jf yenyewe hapa natumia simu sasa hivi. shikamoo wazungu.
 
Ukimaliza ukurasa, unaandika PTO

Umenikumbusha mbali sana, nimechekajeee....! Hafu mwanzo nilikuwa hata sijui manake, nikawa najiandikia tu, hata Kama hakuendelei, jamaniiii...hahahaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom