Nadhani namkumbuka huyu Dr. Ruhumbika. Niliwahi kumsikia miaka mingi iliyopita, in the seventies, kwamba alikuwa ni mmoja wa Watanzania wa kwanza kuandika vitabu, long, long before Mwakikagile came on the scene.
In fact, I believe he's far more known in Tanzania than Mwakikagile is, especially in academic circles. Lakini hata hivyo, Watanzania wangapi wamewahi kumsikia?
Kuna mwingine, Dr. Peter Palangyo, ambaye namkumbuka nilipokuwa Tambaza High School. Alikuja darasani kwetu mwaka wa 1969 nilipokuwa Form V na yeye alipokuwa PhD student in USA studying literature. Nakumbuka pia kwamba Mwakikagile ni mmoja wa wanafunzi katika darasa letu aliyemuuliza maswali kwa sababu alikuwa na hamu sana ya kuwa mwandishi. Aliletwa darasani na headmaster wetu Bori Lilla ambaye sasa ni marehemu. Dr. Palangyo pia ni marehemu.
Wangapi nchini Tanzania wamemsikia Dr. Palangyo? I think he wrote a novel way back then.
Kuna waandishi wengi ambao ni Watanzania. Na ni kweli wengi wao wako nchi za nje. Kwahiyo, ingawa mjadala huu ulianza kuhusu Godfrey Mwakikagile, tukumbuke kwamba kuna wananchi wenzetu wengi ambao wameandika vitabu vingi na kabla ya Mwakikagile kuanza kuandika.
Ni muhimu tuwakumbuike pia. Pia ni muhimu tujue wako wapi na wanafanya nini. Lakini pia inatubidi tuelewe kwa nini hawaishi na hawafanyi kazi nchini Tanzania.
Mwalimu Nyerere alisema Tanzania itajengwa na wenye moyo. Lakini haimanishi wenye moyo ni wale tu wanaoishi nchini Tanzania. Pia haimanishi kwamba wanaoishi nchi za nje hawawezi kulitumikia taifa lao kwa njia mbali mbali hata wakiendelea kuishi ng'ambo.
I hope others will post more details about other Tanzanians abroad on what they have done and on what they continue to do in their fields, as Julius has done here about Dr. Ruhumbika.
Last edited: