JF: Rankings, Reputations na Maswali Mengineyo..

Jamani naomba tusibaguwane kwa pesa humu ndani, ranking ziende kama zilivyo na isiwepo hata hiyo premium. kwani SI KILA atowaye ataka ajulikane kama katowa. Mtu kama katowa, katowa tuu, si kwa kujulikana, na ambae hana asidhalilishwe kwa kupewa karangi au kacheo cha kumfanya ajione inferior. Ranking ziwe za uchangiaji wa posts tuu.
Nakuunga mkono kamanda.Kuna member alisema kuwa atakuja RA nae atapewa maandishi ya kijani.Sidhani kama kuna umuhimu wa member kuchangia JF na kuonekana au kujulikana.

Itafikia kipindi wale watakaotoa kiwango fulani hapa watakuwa na room yao ya kukata ishu.

Ni maoni yangu tu
 
Itafikia kipindi wale watakaotoa kiwango fulani hapa watakuwa na room yao ya kukata ishu.

Haya ni maneno mazito na ya msingi! Tafakari...

Inanikumbusha Ujima (wakati binadamu tulikuwa sawasawa na upande mmoja), na sasa tunahama, tunafuata mfumo wa Ukabaila...Sounds more like it! Bado kidogo mtaanza kutu-own huku ndani.
 
Admin naona umeamua ku ignore opinions zetu. Watu wa pesa wameshapakwa rangi! OK. Mimi hata nikichangia please leave me na "weusi wangu tii" hata font iache hivyo hivyo. Sitahitaji ulimwengu mzima ujue nimetoa pesa. Sasa na ambao hawatatoa kabisa itakuwaje?
 
Hatuwezi kukubaliana wote...........
Kwwa hiyo wachache "nyie" mkishakubaliana ndio inakuwa mtakavyo?
Soma thread uuelewe upepo. Au na wewe unashindwa kusoma alama?
Au ndio unaleta kiburi cha "umeshalipia"???. Ni kwanini huu uamuzi usipigiwe kura ??
 
SteveD
Mawazo mazuri natumai Invisible and co-moderators watayashughulikia. Labda pia wakati mchakato huu unaendelea ni vyema moderators wakatoa utaratibu wa kuchangia fedha forum hii pamoja na accounting ya michango ya wadau itakuwa inakuwa handled vipi.

Naona rangi ya Premium members imebadilika toka kijani kuja nyeusi. na labeling imebadilika pia.
Hapo awali niliomba utaratibu wa kuchangia naona sijapata feedback yoyote.
 
Mama lao,

Kilichofanyika sio kulipia tu, mimi binafsi nimetoa ahadi, ninangoja nipewe bank account nikatumbukize elf tano ya kibongo. Wala sio kuwa nacho ndio chote. Bali ni ushauri wa mara ka mara na kujitolea chochote.

Ruhksa kabisa kujitolea. Ukiangalia hizo rangi kila mtu anasema kivyake hakuna waliokubaliana kabisa.

Ndio maana nikasema hatuwezi wote tukakubaliana, na ikitokea hivyo ujue kuna unafiki ndani yake, kama walivyokuwa wanamfanyia JKN (RIP)

Hope umeelewa!
 
Naomba kupatiwa maelezo japo kidogo, hivi vyeo humu ndani vinapatikana namna gani, maana nimeona kuna title kadhaa kama vile:
Member
Junior Member
Senior Member
JF-Senior Expert Member
Senior & JF Premium Member

Je upatikanaji wake huu ni wa kupigiwa kura za siri, kuchaguliwa au just upendeleo. Maana nilishtuka kuona eti hata X-Paster naye ni JF-Senior Expert...! Mhh nikahisi sasa huku si kuvishana viremba vya kuchorwa? I mean ukoka, maana baada ya muda ukipigwa na jua tu vimenyauka... Wajameni wale wanao itwa monamodireta!!au sijui majinireta, hapana nimekumbuka ni Forum Moderators, wanifahamishe yanakuwaje mambo haya...?!
Naomba kujiwakilisha
 
kuna thread inajibu hilo swali lako. lakini vyeo vinategemea na count ya posts, mfano ukifikisha 250 kama sijakosea basi unakua JF Senior and Expert Member. U-Premium ni kama una/umechangia ki fezwa..........nadhani inatosha kwa ufupi!!.
 
Naomba tafwadhali unipatie address ya hiyo thread please
 
......Dotori kesha wahi kuuliza swali kama lako, Bubuataka kusema nae aliuliza juu ya premium membership inavyopatikana.

google neno JF Ranks, I believe utapata hits juu ya thread ya Dotori and hopeful Bubuatakakusema.
goodluck!!
 
Naomba kupatiwa maelezo japo kidogo, hivi vyeo humu ndani vinapatikana namna gani, maana nimeona kuna title kadhaa kama vile:
Member
Junior Member
Senior Member
JF-Senior Expert Member
Senior & JF Premium Member

Je upatikanaji wake huu ni wa kupigiwa kura za siri, kuchaguliwa au just upendeleo. Maana nilishtuka kuona eti hata X-Paster naye ni JF-Senior Expert...! Mhh nikahisi sasa huku si kuvishana viremba vya kuchorwa? I mean ukoka, maana baada ya muda ukipigwa na jua tu vimenyauka... Wajameni wale wanao itwa monamodireta!!au sijui majinireta, hapana nimekumbuka ni Forum Moderators, wanifahamishe yanakuwaje mambo haya...?!
Naomba kujiwakilisha

Ha ha hah ha....!!!! Ngoja nicheke peke yangu tu, potelea mbali majirani wakiita ambulance ya wagonjwa wa akili!!
 
Mawazo mazuri Steve D lakini hivi ni kwa nini tunaidharau rangi nyeusi kiasi hiki? kwanini rangi nyeusi, rangi ya ngozi zetu ndio iwe chini? Arent we proud of our colour?

Wallahi nilikuwa sijui kuwa rangi ya ngozi zetu ni nyeusi, hivi inafanana na makaa eeeh!? Au kama haya maandishi yaliokozwa weusi? Wewe usiku unaonekana kweli au mpaka ukicheka? (Joking), weusi ni kiza na kiza maana yake kitu kisicho na nuru na kisicho na nuru hakina baraka, na kisicho na baraka hakifai... Je hao unao wahisi kuwa weusi hawana nuru, Je huku si kusapoti mawazo ya kibaguzi na kitumwa...? Hao walio anzisha dhana hii walikuwa na niya ya kuwadharirisha wakaazi wa Afrika, walifikiri kuwa watu hawa hawapatikani kwengine isipokuwa Afrika tu, lakini Afrika ni bara lenye mkusanyiko wa race zote...?! Kama kule Australia wapo watu wenye kufanana na wakaazi wa Afrika. Mi nahisi weusi hauna maana ya u-Afrika. Nakumbuka hata walipotaka kuja huku walikuwa wanasema wanakuja kwenye bara la giza (Dark Africa). Wengine waridiriki hata nkuja na tochi wakifikiria kuwa huku hakuangazwi na jua, lol...!

Naunga mkono utumiaji wa Iron or Steel (lol, kama ikiwezekana), Broze, Silver, Gold au hata Almasi (Diamond) au Tanzanite, au tutumie vyeo vya kiafrika kama vipo... Haswa vya ki-Tanzania! Inawezekana visionekane na radha lakini ndo kuthamini utamaduni wetu kwani hata hao tunao waita weupe (!?) wanathamini utamadununi wao, hata kama hauwapi radha maridhawa, lakini muda unavyokwenda wanajikuta kuzoea kile walicho kianzisha.

Naomba kuwakilisha Hoja.
 
Ndugu wadau na mods katika siku za hivi karibuni na kipindi kilichopita wadau mbalimbali humu,wamekuwa wakiuliza sana juu ya vigezo vinavyotumika kurank jf members,majibu yamekuwa yakitolewa,wapo wanaoridhika labda wapo pia wasioridhika.Sio mbaya sisi sote ni wa moja,mie mwenzenu katika kufikiria sana,nimeonelea nipendekeza hivi: Pamoja na mfumo tulionao sasa wa rank za member.junior member,senior member na senior jf expert member nk.tureform mfumo huu au kuuongezea nyama kidogo,kwa vigezo vilivyopo sasa.Ndio kuna wale ambao labda kwa namna moja au nyingine wanaiwezesha jf kifedha na hivyo kuendelea kuwa hewani,hilo halibishiki kwa kuwa kila mtu anafahamu kuhost tovuti hii lazima tulipia tena vijipesa vingi tu.Hawa wenzetu tuwape status maalumu ya heshima labda "kama senior honorary member" au meritocrat member nk,ili mradi tu tuoneshe tunavyoappreciate michango yao na kwamba mtu yeyote akitaka kuingia katika kundi hilo la heshima,basi afuate vigezo hivyo nasi tutampa tuzo hiyo ya kuitwa hivyo.

Pili,kuna wadau wenzetu humu ni wachangiaji wazuri sana,hoja zao huwa zinaconvince sana na kwa kweli huleta maendeleo chanya.Watu hawa pia uanzishwe mfumo wa kuwatambua na kuwapongeza au kuwatunza,na hii ni kwa admins kutafuta utaratibu ambao sisi wanachama kila baada ya kipindi fulani tutapiga kura au kupendekeza mwanachama wau wanachama tunaofikiri wapewe hiyo eshima kwa mchango wao wa kifikra humu ndani,hii yaweza kuwa wakapatikana kwa thread (yaani kutokana na kuchangia sana katika thread fulani au general) kwa wale watakaotokeza mara nyingi basi tunawachangua walau watu 25 wanapewa hadhi fulani, labda "prior member au senior associate member au hata huo usinia expert member" watu kweli waoneshe expertism fulani katika mada husika au mada fulani fulani.

Na kwa wanaobakia mfano junior member,member,senior member hapa uendelee kutumika utaratibu wa kawaida aidha ni wa credit au number of posts mtu alizoziweka ama kuchangia.wadau mtanisaidia zaidi kuboresha hili wazo.

Angalisho.Hata hivyo wale wanaopewa honorarium kwa kwa kuthamini michango yao kifedha hiyo hadhi yao iwe "ceremonial tu" yaani sijui wataalamu wa kiswahili ceremonial kwa kiswahili ni nini?yaani wasiwe na nguvu ya maamuzi kuwazidi wengine,maamuzi mengo yashiriishe wadau na hawa bwana wasidominate mawazo ya wengine.Labda kwa namna moja ama nyingine watu wengi tunaweza kuwaridhisha kwa mtindo huu.Nadhani kuna mtu aliuliza ina maana mimi nikilipa hela let say 10,000 nitatoka kwenye ujunior member hadi senior au expert member? ili kuondoa mkanganyiko kama huu tuweke merit.

Mnaonaje wakuu,hebu tuchangiane mawazo,hili nimelifikiria haraka haraka tu ili kuboresha mfumo,nikalipost hapa kabla halijanitoka.Mnakaribishwa kukosoa,kuboresha au kutoa mwelekeo chanya mwingine.
 
Augustoons,
Wazo zuri sana, ila mimi naona tayari liko incorporated kwenye vikorombwezo vingine vilivyomo, sema labda watu hatuvitumii tu. Check thread hii:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=7889

Nafikiri inamaelezo yanayohusiana na hilo, au basi yanayokaribiana na yako.

Kingine hapa cha kukumbukana ni kuwa, karibia kila kitu kinawezekana, kile ambacho tunaweza kukifikiria kuhusiana na software. Tatizo lililopo ni kuwa, software tunayotumia vBulletin, imejengwa na watu, na vitu vingine ni vigumu kuviongezea na kuacha kila kitu intact bila ku cause security risks au stability ya software. Pia uwezo wakufanya hivyo bila ku breach terms of use ya software na copyrights. Otherwise, kuna additional utilities ambazo zinaweza kununuliwa za kuongezea madoido hapa, ila ndiyo hivyo tena... mifuko ni mifupi... lol!!

SteveD.
 
SteveD kumbe na wewe ni Mod au adimin wa jf? sikuwa najua!
 
Naona kuna mabadiliko katika upangaji wa vichwa vya mada toka align left kwenda align center. Kimtazamo haipendezi, bora kurudisha upangaji wa awali.
 
SteveD kumbe na wewe ni Mod au adimin wa jf? sikuwa najua!

MF, ufisadi ulioufanya kwenye tamko lako hapo juu 'ninauchukia' ndugu. Umeuliza swali na kujijibu mwenyewe tena kwa msisitizo wa uhakika badala ya kusubiria ujibiwe.

Mindhali ulishauliza, ngoja tu nikujibu kinamna nijuavyo mimi:

--vipi kama napendelea tu kutoa ushauri na mapendekezo kwa ajili ya maendeleo ya jf?
--vipi kama nami natumia software kama hii ya jf pahala pengine hivyo kuijua undani wake kwa kiwango fulani?
--kifupi, kuna forum mbalimbali najishughulisha nazo, ku-share knowledge na ideas ni jambo muhimu na nipendalo. Sihitaji kuwa mod au admin kufanya hivyo. Msimamo wangu uko dhahiri tangu nijiunge na jamvi hili mid last year. Natumaini nimeeleweka. Akhsante.
 
Back
Top Bottom