JF ninaomba sala zenu leo ni kura za maoni!

Ingawa sijuhi utendaji wako,ila kwa kua umeonyesha nia ya kujiamini na kutaka kusimamia mawazo yako kwa manufaa ya taifa letu nakutakia kila la kheri mkuu,kua wewe mtoto wa aliyekua kiongozi fulani wa nchi hakukunyimi haki yako ya kupigania vitu fulani kwa interest ya taifa letu,as longer as unajipigania mwenyewe una baraka zangu kaka ingawa mimi sina imani na sio muhumini kabisa wa chama chenu (C.C.M) ,unaweza ukajenga hoja nzuri na ukawa ni mtendaji mzuri lakini kumbe kamati kuu ilishapitisha majina yake!otherwise wishing u all the best!
 
- Well, ninakusikliza sana mkuu una amini kwamba matatizo ya maisha yako yameletwa na watoto na ndugu wa Viongozi kushiriki kwenye uongozi, tatizo lako huwataki hutaki Mbowe mkwe wa Mtei awe Mwenyekiti wa Chadema na hutaki mimi niwe mbunge, umesikikia sana mkuu, na UWE NA SIKU NJEMA SANA!

William.


Mkuu maisha yangu ni murua kabisa wala silalamikii ugumu wa maisha kwani naamini nina maisha yenye nafuu kuliko mamilioni ya Watanzania. Nachoamini serikali ikishajaa wanandugu haiwezi kuwa na ufanisi kabisa. Hiki nicho ambacho serikali hii na zilizopita za CCM zimekuwa zikifanya. Hata hao CHADEMA kama wataendelea na sera ya kupeana vyeo kindugu mwisho wao uko karibu kama wa CCM. Tatizo la nchi hii ni hakuna ufanisi wala uwajibikaji na yote ni kwa sababu watu wanapeana vyeo/madaraka kwa kujuana na kwa sababu ni mtoto wa fulani. Naamini utashindwa.
 
Jitahidi kuongea kiswahili fasaha maana ukiongea american English utakosa kura za Lusinde, Ngonyani, Lameck Airo, nk. Hawa wote elimu zao darasa la saba.

Tell me brother: Hivi EAC ina idadi ya watu wangapi? Na pato lake kwa mwaka ni kiasi gani?
 
- Well, nimekuisikia sana mkuu, Kenya wana viwanda vingi sisi hatuna, lakini sisi tuna Ardhi Kenya hawana sasa ni muhimu nikiwa mbunge huko kupigania taifa letu kuitumia Ardhi yetu katika-balance hiyo gap ili tuwe na uwiano kiuchumi kabla ya kuingia kwenye sarafu moja. Na ninaamini ni muhimu sana Tanzania tukajikita kwenye ajira za vijana, ambao coming 2015 watakuwa ndio 65% ya wapiga kura, kwa hilo CCM tunahitaji kuwa makini nalo sana!

- Otheriwise, mkuu nimekusikia sana kuhusu comparative.

William.

Orait mkuu tuseme kuwa hizo ajira za vijana zinapiganiwa kwa sababu wao ndo wataconstitute 65% ya wapiga kura si ndio...

Maana yake ni kwamba ajira za vijana zinatafutwa lengo likiwa kupata kura zao mwaka 2015.

Ila kwa nia njema tu, kama hilo ni tatizo, ungeulizwa swali kwamba ni kwa vipi utaongeza ajira za vijana il hali serikali imesitisha ajira, na kucut off matumizi yake kwa 50% (hivyo kufanya suala la ajira kuwa gumu zaidi), lakini pia kuna vijana wanamaliza vyuo mbali mbali kila mwaka, hawajui waaajiriwe wapi (hoja ya kujiajiri hapa haina mashiko, hakuna mazingira hayo hapa kwetu)

jengine nimepata wasi wasi kama unapoenda EAC unaliona suala la Ardhi na single currency tu...mbona hayo ni 'ya kawaida' sana...una kitu gani 'unique' ambacho genuinly kitawashawishi wana CCM wakuchague?

Kila la heri!
 
Jana nilipita pale feri soko la samaki.
Nilikuwa nimevalia vizuri na kujipulizia unyunyu,lakini kutokana na shombo ya samaki,nilitoka pale nanuka shombo!
Mkuu,CCM imeoza na inanuka shombo!
Hivyo regardless the best you are,nawe utanuka tu!
Sala yangu hupati!
 
CCM ndio kikwazo cha maendeleo ya Taifa letu...nadhani kabla ya kukufanyia maombi upit kura za maoni,inabidi kwanza chama chenu kiwe safi,la sivyo maombi yetu yatakua ni makelele mbele za Mungu.
CCM na wote mnaotafuta dhamana huko EAC hamna jipya na wala usijitete kwa kutolea mifano ya Airline na Railway...mbona hata baada ya anguko la EAC, Tanzania ilifaidika kwa kubaki na viwanda muhimu na bado CCM imeviua? mbona tulikua na shirika imara la RTC lakini CCM imeliua? Posta na Simu(TTCL na TP) iko wapi leo?
Tafadhali sana usitafute huruma kwa mgongo wa maombi,hata tukiomba na kupayayuka sana Mungu hadhihakiwi.
 
Jitahidi kuongea kiswahili fasaha maana ukiongea american English utakosa kura za Lusinde, Ngonyani, Lameck Airo, nk. Hawa wote elimu zao darasa la saba.

Tell me brother: Hivi EAC ina idadi ya watu wangapi? Na pato lake kwa mwaka ni kiasi gani?
maswali kama haya william sio ya kupuuzia inabidi ujue vitu kama hivi, when eac collapsed na kwa nini etc
 
wasiwasi wangu ni ufahamu wako juu ya international relations, pia unaonakana kujua vitu vichache sana juu ya EA community iliyokufa na sababu ya kufa...inshort nakufananisha na mwenzako sioi sumari ambae hakua bongo wala hakuwah kuwa na upepo wa kisiasa ghafla tu kwasabu yy ni mtoto wa kigogo(marehem) then akaibuka kutaka jimbo nadhani unajua kilichomtokea.
 
- Haya wakuu nimewasikia sasa ngoja niende kwenye Viwanja vya Bunge, Karimjee kusubiri muda ufike tuingie ulingoni, MBARIKIWE WANANCHI WOTE NA MUNGU WA MBINGUNI!

LONG LIVE TANZANIA, NA LONG LIVE JF!

William.
 
Kila la heri kaka! Ila bado nina wasiwasi mkubwa sana hata kama utapata huo ubunge,unaweza kubebwa na upepo mkali unovuma ndani ya Chama chako.
 
Wana JF, leo ninakwenda kusimama mbele ya Wabunge wote wa CCM kuomba kupitishwa kwenye kura zao za maoni ya kugombea Ubunge wa EAC, ninaamini niaenda pale nikiiwakilisha JF sasa ni muhimu sana leo tukaweka tofauti ya itikiadi zetu pembeni na kwua kitu kimoja katika kuombeana na kutakiana heri, kupita kwangu ni kupita kwa JF.

- Nimesema huko nyuma na ninasema tena mimi Mwanachama wa CCM, tena hai na wa muda mrefu sana toka mwaka 1982 nikiwa JKT Oljoro kwa mujibu wa sheria ya mwaka mmoja baada ya kusomeshwa bure na Serikali ya Awamu ya kwanza. Nia na madhumuni yangu siku zote ni mabadiliko ya mwenendo wa kisiasa kwa taifa letu, ili tuweze kusonga mbele kulingana na wakati, ninaamini kwamba wengine wakija na ideas kutoka upinzani na wengine tukija na the same ideas kutokea ndani ya CCM, siku moja tutalisaidia taifa letu kufikia pahali linapotakiwa kwa nyakati hizi za kisayansi.

- Kwa kifupi ninataka kwenda EAC, ili kulisimamia taifa langu kwenye masuala ya interest za kiuchumi na hasa Ardhi yetu nikiwa ninajua kwamba nchi zingine Nne za Jumuiya hazina sheria za serikali za kusimamia Ardhi zao kwa sababu hata hiyo Ardhi hawana tena yote ilishanunuliwa na wananchi wao, sisi tu ndio bado tuna Ardhi inayosimamiwa kisheria na serikali yetu. Pia ninataka kuhakikisha Tanzania haturudii tena makosa ya nyuma ya kushirki kwenye Jumuiya iliyokufa mwaka 1977, ambapo ilipokufa sisi tuliumia sana kwa sababu tulikuwa tumejikita sana huko, infact mpaka leo kuna areas kama za Airline na Railways, bado tumeshindwa ku-recover, sitaki Tanzania tukimbizwe na Kenya walivunja Jumuiya ya kwanza kwenye One Currency na Political Federation, ninasema kwamba tujifunze kuwa EU sasa hivi iko matatizoni ni kwa sababu ya mbio mbio za kuanzisha jumuiya hiyo bila utafiti wa kutosha.

Kwa hayo machache ninaomba kuwaomba JF wote leo tujaribu kuombeana heri ili tupite kwa sababu kupita kwangu ni kupita kwa JF pia!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA NA PIA AIBARIKI JF KUMKOMA NYANI1

William.

Duh Kweli Bongo Tambarare!! Watu waliokaa Ughaibuni Ambapo hawaijui Hata Mipaka ya Tanzania inapofika kipindi Cha Kutafuta Ulaji Hupiga Magoti Kuomba Kula?? Refer Makala Mvomero!!
 
- Haya wakuu nimewasikia sasa ngoja niende kwenye Viwanja vya Bunge, Karimjee kusubiri muda ufike tuingie ulingoni, MBARIKIWE WANANCHI WOTE NA MUNGU WA MBINGUNI!

LONG LIVE TANZANIA, NA LONG LIVE JF!

William.

Kila la kheri kwenye uteuzi. Umeorodhesha mambo ambayo unadhani utayasimamia; Ardhi na single currency ni mojawapo! Ila la kuangalia ni kuwa utaenda kuendeleza na kutetea sera na maoni ya chama chako (CCM) kuhusu vitu hivyo. Sina uhakika sana kama CCM ina sera zinazoeleweka kuhusu hii EAC. Ila naamini ukishinda utakachokisimamia ni sera za CCM ndani ya EAC, labda utuhakikishie kuwa hayo uliyoyasema ni sehemu ya sera za CCM ndani ya EAC.
 
Jana nilipita pale feri soko la samaki.
Nilikuwa nimevalia vizuri na kujipulizia unyunyu,lakini kutokana na shombo ya samaki,nilitoka pale nanuka shombo!
Mkuu,CCM imeoza na inanuka shombo!
Hivyo regardless the best you are,nawe utanuka tu!
Sala yangu hupati!

Mpeni Live Huyu Ndugu!! Magamba watampenda Vipi Kama waliamua Kumreplace Baba Yake na Kichaa!! No Matter how Much Kichaa atawacost?? Kweli Magamba Hawana Adabu!!
 
- Well, nimekuisikia sana mkuu, Kenya wana viwanda vingi sisi hatuna, lakini sisi tuna Ardhi Kenya hawana sasa ni muhimu nikiwa mbunge huko kupigania taifa letu kuitumia Ardhi yetu katika-balance hiyo gap ili tuwe na uwiano kiuchumi kabla ya kuingia kwenye sarafu moja. Na ninaamini ni muhimu sana Tanzania tukajikita kwenye ajira za vijana, ambao coming 2015 watakuwa ndio 65% ya wapiga kura, kwa hilo CCM tunahitaji kuwa makini nalo sana!

- Otheriwise, mkuu nimekusikia sana kuhusu comparative.

William.


Ale Mswanu du. Nakutakia kila la heri
 
Huku JF hatupigi kura,nenda huko NEC kaombe kura,kwanza mm sijui umefanya nini na utafanya nini?? Tofauti yako na Lusinde nini?? Mimi wagogo wameniudhi sana,hamtaki kuwasadia wagogo wenzenu,Dodoma hujafanya chochote, je huko EAC ndo utafanya kazi?? Labda wakuchague tuu kwa jina la baba yako!
 
Nawatakia kila la Kheri Willium Malecela ,Mrisho Gambo na Shy-Rose Bhanji.Wabunge wote wa CCM na wapiga kura wa leo naomba muwape kura vijana hawa.Najua mko online mnaifuatilia thread hii.Chagueni watu wenye uwezo na uzalendo wa dhati kwa Tanzania

Ni wakati wa kupigania maslahi yetu EAC kwa vitendo zaidi.Inahitaji weledi wa hali ya juu kwenye uchumi na masuala ya siasa za kimataifa.Taifa letu limekosa fursa hii adimu kwa muda mrefu.Kuna mambo ambayo mimi naona yatauletea balaa la kiuchumi na kisiasa kama tutaendekeza haya yaliyofikiwa na watangulizi wenu huko EALA.Kuna maamuzi yanayostahili kuangalaiwa kwa upana and critically especially on Monetary unification

A monetary union with neither macro-economic nor sectoral policies convergence is a risky venture that may jeopardize the common market and the eventual political federation

Politically managed transition of the East Africa Commission to an East African Economic Union Authority should review the idea.Furthermore,the East Africa Monetary Authority should lead to an E A Central Bank. We need a unified federal treasury.

Tuangalie maslahi ya taifa critically,maslahi ya EAC kwa kuzingatia dhana ya kiuchumi ya Pareto optimality(kufaidika bila kujeruhi maslahi ya wengine). Kuna wanaobeza Regional bloc,hao sikubaliani nao.Tuboreshe polocy na mkataba wetu wa EAC.Kupinga regional bloc siyo sahihi,labda tuangalie maboressho ya mkataba kwa kutumia mifano hai ya muundo wa blocs nyingine kwa tahdhari kubwa na kuepuka matatizo kama ya Ugiriki huko EUROZONE.Kupinga per se siyo sahihi kwa dunia ya leo tunapoongelea New Economic International Order(NEIO)

That is outright fallacy - if you are trying to insinuate that economic regional blocs are not 'fashionable' today . If anything the EU , as a successful model of an economic regional bloc , has grown in strenght and influence enought to validate the thinking that small nations must unite to trade effectively and beneficially with the 'superpowers' , secure the welfare of citizens more robustly, grow miltarily , exchange technology and specialist knowledge, utilise diverse information sharing, etc . Even as no one will admit to it , I think most of us know that the EU was inaugurated to challenge the growing economic might of the USA back then. Today the union has more or less achieved its objectives with how the EU is actually now an influential economic zone.

EAC is still impotent because African member nations are not committed to its success . This is why we must all consistently speask against actions that undermine EAC. The bloc may not work well now but nothing stops me and you agitating for perseverance with EAC in recognition of how it is a highly neccessary union for all our magnified success. We all tend to think of success as isolated to ourselves only and this is why we are consumed with competing against each other always.Tanzania this,Kenya blah blah etc.. The divide-and-conquer tactics of our colonial Master worked too well. It's a pity we are still unable to re-program our thinking to date!

EAC has not failed because an economic trade bloc is a bad idea. It is not working because of the hypocrisy of a people who want to copy the models of success elsewhere while those same people lack the unity, mutual respect and dedication to end result that make the economic blocs we admire (like the EU) work as well as they do.

Shy-rose,Willium Malecela na Mrisho Gambo kila la kheri.Maslahi ya Tanzania na EAC kwanza
 
- Mkuu nimekusikia, isipokuwa naomba ukaangalie tena kumbu kumbu zako kuhusu majina ya wagombea waliopo sasa maana huenda hauko current, Millya is my friend and I respect as a humanbeing na mkuu uwe na siku njema sana!

- Otherwise sidhani kama wewe unaandika hapa kutokana na siasa za baba na mama yako unless kuna something I am missing hapo kwenye hoja zako!

William.

Mkuu, mimi nakuombea kheri ingawa najua una wakati mgumu sana. Kwa kuwa umeshatuthibitshia kuwa TAIFA Kwanza na huko EALA hakuna milengo ya Vyama vya Siasa Mungu akupe neema yake.

Hata hivyo nakukumbusha kuwa 2015 ikifika, nenda kagombee Jimboni Mtera, tena kwa tiketi ya upinzani.
 
Back
Top Bottom