JF ni zaidi ya udaku wa siasa

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,416
2,264
wapendwa, jaribuni kutembelea sehemu mbalimbali za JF, kwani kuna mengi ya kujua na kujifunza...
 
ushauri mzuri maana watu 'tunabanana' sana kwenye siasa kana kwamba maisha ni siasa tu. utakuta hata post nyingine zinazostahili kuwa katika uchumi/biashara au masuala ya jamii n.k yanaingizwa kwenye siasa na watu wanaendelea kuchangia tu
 
Leo nimeikumbuka hii nikacheeka!

Halafu siku hizi bila breaking nyuzziii za kutokea kisutu au ccm na chadema kubwagana kwenye chaguzi.... basi karibia kila kitu kimeshakuwa documented!!! ndo' maana wengine tunaangaza macho kwenye majamvi mengine na kuwaachia akina Mkjj, Kitila, Halisi, Kasheshe na makundi yao ukumbi wao mpenzi wajitanue... :)
 
Inaonyesha watu wengi humu tunapenda sana maswala ya kisiasa.
Tumesahau maswala ya kijamii na kiuchumi zaidi.
Hivi mahakimu wa Kisutu bado hawajarudi toka likizo?Breaking news ziendelee pamoja na tetesi.
 
Halafu siku hizi bila breaking nyuzziii za kutokea kisutu au ccm na chadema kubwagana kwenye chaguzi.... basi karibia kila kitu kimeshakuwa documented!!! ndo' maana wengine tunaangaza macho kwenye majamvi mengine na kuwaachia akina Mkjj, Kitila, Halisi, Kasheshe na makundi yao ukumbi wao mpenzi wajitanue... :)
Je una maoni gani kuhusu hawa watu wa Wind East Africa na mradi wao wa umeme wa upepo wa megawati 50 ambao utaanza kuzalishwa mwakani?
 
Wazungu wanasema "You are what you eat!"

Inaonekana chakula chetu kikuu watanzania ni udaku - uwe wa kisiasa, kizinzi, au kimajungu.

Hivi mmeona traffic ya kwenye thread ya "Jabir Kigoda wa BOT" ilivyo kubwa? Yaani kuna visitors kibao wamepiga kambi humo kabisa...wakisubiri maudaku yaendelee kumwagwa.

Oh well, it is what it is.....unfortunately!!
 
Shabash another richmond?
:D
Hapana, huu ni mradi ambao utapunguza sana kutegemea umeme wa nguvu za maji na dizeli. Ni mojawapo ya miradi inayokwenda sambamba na matumizi mbadala ya uzalishaji umeme.
 
Hivi mmeona traffic ya kwenye thread ya "Jabir Kigoda wa BOT" ilivyo kubwa? Yaani kuna visitors kibao wamepiga kambi humo kabisa...wakisubiri maudaku yaendelee kumwagwa.

Oh well, it is what it is.....unfortunately!!
Wabongo bwana tukikaa kwenye siasa mnaongea tukija na kuliweka kwenye forums nyinegine mnaongea.......
 
Napenda kujua tu. Nimecheki na majikwaa mengine nikaona kuna deficit ya uchangiaji wa mada mbalimbali. Huku JF kuna mzizi gani? Mbona kuna msongamano sana na watu kila siku wanajisajili?
 
Some ppl talk openly still banned. Others ripped off their threads & posts. Kuna sababu zaidi
 
kibunango,
Unajuwa muruwa wa kila nyanja ya kijamii umeharibiwa na wana siasa kuanzia uchumi, siasa yenyewe, hata jamii, sekta nyingi zimekwama maendeleo yake kutokana na ufisadi wa wanasiasa na siasa zao, ndo maana mazungumzo yoyote hayawi sawa kama hutakuta wanasiasa ni tatizo.Sema afya, barabara, maji safi,usalama,n.k utajikuta unarudi kule kule katika siasa kwa kuwa tu muruwa wa mambo hayo na mengine unaharibiwa na wanasiasa.
 
Ni kweli kila kitu kinaongozwa na siasa. Ila kupitia jamvi hili nimegundua kuwa watanzania walio wengi (japo si wote) hawana tena technicalcompetence ya kuchambua mambo yaliyo nje ya siasa. Ukianzisha thread ya kiufundi katika nyanja ya uhandisi, udaktari nk utaona ghafla inavamiwa na mawazo ya kisiasa. Ina maana wahandisi, madaktari, etc waliomo humu hawajabobea kwenye fani zao??? Kimsingi. Nenda utembelee majamvi mengine kama yahoo answers, linkedin, etc utauliza swali na kupata majibu maridhawa mpaka unafurahi. Sasa humu JF, tunahitaji nini jamani ili tujikwamue? Jamani, siasa ipo na itaendelea kuwepo na kututawala, lakini si kila mtu ajizamishe asilimia 100 karika siasa japo tusiinyamazie pia.
 
Kibunango au unahamasisha watu tutembelee na kule mambo ya kikubwa nini? maana naona kama wateja wamepungua sana siku hizi huko:D
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom