JF na moyo wa kushukuru

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,416
12,604
Leo nilikuwa napitia status za baadhi ya members humu ndani na kushtukia kuwa kuna idadi kubwa ya members hawana moyo wa shukrani au wana viburi na majivuno ya kutotambua michango ya wenzao.

Utakuta mtu kagongewa thanks zaidi ya 40 mpaka 60 lakini yeye hajawahi kugonga hata moja au amegonga thanks chini ya 5, sasa hapa unajiuliza kwamba yeye huyu haoni ubora wa michango ya wengine na kuamini kwamba yeye tu ndio mwenye michango bora pekee? Au anaogopa akigonga thanks kwa wengine atashusha status yake?

Mi naona mods waje na kitu na kama comparison au limit ya thanks unazoweza kupokea kwa kuhusianisha na unazotoa na kuwe na meseji kwa wachoyo zikiwakumbusha kuthamini michango ya wengine like, "Mr Kanigini you have reached your limit of thanks you can receive as compared to what you have given out, so you are strongly advised to give out a number of thanks so that you get the room to receive".

Nawasilisha.
 
Tenda wema uende zako, usingoje shukrani. Aidha, kumbuka shukrani haiombwi kama ulivyoonyesha kuna watu ni wagumu kutoa shukrani hata kama utakuwa umeokoa maisha yake.
 
kumbe usiposema thanks nalo ni kosa. asante kwa taarifa!

Sio kosa perse ila impliedly unaonekana huthamini kitu mwenzio alichofanya, kumbuka tu hata katika maisha ya kawaida mwenzio akufanyie kitu kizuri afu we kimya kimya upokee bila kusema asante, hapo huna kosa la kukupeleka mahakamani ila yule mtu aliyekufanyia kitu kile hatajisikia vizuri.

Mi nakumbuka wakati ni mdogo bibi akikupa kitu ukapokea bila kusema asante anakuita anakwambia ebu naomba mara moja nikubadilishie, ukimpa ndio basi tena hupati kitu.

Maofisini kila siku utasikia "tatizo bosi wetu ha-appreciate kazi zetu, anatuvunja moyo kujituma ..."
 
Back
Top Bottom