Wanachama wa JamiiForums waliotangulia mbele ya haki (Fariki) R.I.P

Sisi wengine tukifa itakuwa vigumu sana kwa watu kujua humu.

Kiongozi ! Mz Nyani ! Hii habari inagusa moyo! Hivi leo mimi au wewe, yule, afe and then pasiwepo wa kujua ! Terible ! Wewe kama mmoja wa Super senior member also celebrity hapa Jf unalisemeaje hili ?
 
Nilimjua kuwa Marehemu ni member wa JF alikuwa analalamika kuwa amepigwa BAN na nilipomuuliza kuwa anatumia ID gani akaniambia hawezi kuniambia, ingawa nilitamani kuijua ID yake kwani nilimwambia ID yangu ya hapa JF lakini akakataa kuniambia ID yake. Kwa hiyo sikuweza kumlazimisha, nilijaribu kutaka kuijua lakini sikuweza kufanikiwa mda mwingi alikuwa ana browse kwenye simu yake. Kwa hiyo nilishindwa kuijua.
Tunamwombea apumzike kwa amani..
 
Mi nikikaribia kuondoka ntawajulisha.

RIP kwa waliotangulia.

Lizzy ! Kwenye issue kama hii ya habari za UMAUTI WA KIFO ! unaleta mzaha ? Wewe utajuaje kwamba uko njia 1 ? Kwamba umekaribia kufa ? Utautoa wapi uwezo huo ? Mi hii maneno imeni'pain vya kutosha. Ni mtandao upi utakaotutambulisha vifo vyetu hapa ? Japo na sie tuje zawadiwa RIP ?
 
Mimi huwa namkumbuka sana yule mwenzetu aliyejiita Mpenzi wa Islam. Huyu alinigusa sana kwa jinsi alivyokuwa mpole na kutumia lugha ya kistaarabu katika majadiliano katika jukwaa la dini. Pamoja na baadhi ya wachangiaji walikuwa wakitumia matusi na kashfa nzito nzito dhidi ya dini ya Kiislam, Mpenzi wa Islam hata siku moja hakukashifu, kumtukana mtu/dini au kutumia lugha ambazo si za kistaarabu bali alijibu kwa kujaribu kuwaelewesha wachangiaji hao. Nilipenda sana kusoma michango yake na hadi nikamuomba urafiki hapa jamvini. Nilipenda sana kukutana naye na tayari nilishapanga kumtafuta pindi nafasi ingeruhusu lakini kabla ya kufanikiwa kufanya hivyo akafariki. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu na wengine wote waliowahi kuwa wanachama wa jamvi hili mahali pema peponi~AMEN.


Well said bak... It's like he left with all the wisdom in that forum
 
Last edited by a moderator:
Kila nafsi itaonja umauti, mwenyezi mungu awapumzishe kwaa amani wote waliotangulia mbele ya haki.

Kweli kunaumuhimu wa kufahamiana na baadhi ya member, ambaye yuko tayari itakuwa poa, nipo Mbeya.
 
...kifo ni fardhi, hakiepukiki!

Hata mimi nipo radhi id yangu kuwa revealed siku ya ahadi (roho ikiacha mwili.)
Kuna ninaofahamiana nao alhamdulillah, na kwa wale tusofahamiana inshaallah
panapo majaaliwa...


Niliumia sana siku ya msiba wa mwenzangu Felix Chambi aka Makene niliyepotezana nae miaka mingi kisha kuja kusoma; https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/9206-felix-makene-afariki-dunia.html na haswa kwakujua kumbe naye alikuwa member mwenzetu tukijibishana hoja & viroja humu.
 
ni kuandika tu katika last will
unaweka id na password na unasema wajulishe wanajf umerest in peace.

Ila kwa jinsi ambavyo nimejenga bond na baadhi ya members itakuwa ngumu sana kumeza.

R.I.P waliotangulia.
 
...kifo ni fardhi, hakiepukiki!

Hata mimi nipo radhi id yangu kuwa revealed siku ya ahadi (roho ikiacha mwili.)
Kuna ninaofahamiana nao alhamdulillah, na kwa wale tusofahamiana inshaallah
panapo majaaliwa...


Niliumia sana siku ya msiba wa mwenzangu Felix Chambi aka Makene niliyepotezana nae miaka mingi kisha kuja kusoma; https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/9206-felix-makene-afariki-dunia.html na haswa kwakujua kumbe naye alikuwa member mwenzetu tukijibishana hoja & viroja humu.

Mosquito ! Maneno yako mswaki wa mti hayahitaji dawa ! Ni kama vile wewe hapa waitwa MBU kuna wengine WALIMWEUSI, MCHICHAPORI, BADILITABIA, NYANINGABU, BUJIBUJI, KIPIPI, SMILE, HEART, BWABWA, mie mwenyewe JUDGEMENT n.k n.k unayaonaje haya majina ? Ofcoz ni majina bandia ! Unadhani ni wangapi humu wanachart na ku'share comment na hawajuani acha sura tu hata miji waishio hawatambuani ! Kuna wakati hua najiuliza nini mantik ya ku'hide habari za utambulisho wetu sahihi sipati jibu ! Je ? Kama mimi na wewe pengine tulisoma au tuliwahifanya kazi pamoja tutajuanaje ? Kama imeshindikana tupo hai, tukifa itakuaje ?
 
kuna member nilikua nawapenda sana siku lkn siku hizi siwaoni,na walionesha sana kuipenda sana JF ndo nikapata mawazo kuwa huwenda wako kama mm na labda wamefariki hivyo hakuna wakutujulisha.Kwa kweli kuna member humu nawapenda sana kwa michao na picha niliyojijengea juu yao hivyo japo sijui hata wanafananaje nawezaa kulia nikisia wametutoka.So ni mawazo kama haya ndo yamekua chanzo cha hii thread..

Hapo blue amina.

ooh, najua mimi ni mmoja wao........................ nuikutoe hofu tu kuwa mi mzima kabisa japo kuna wakatyi nilipata kahofu kidogo juu yako baada ya kutokukuona kwa muda mrefu..................... nimefurahi kukuona tena kwenye avatar yako bomba kama kawaida...................

mi najuana na wanaJF wawili ama watatu hivi..................... so nikitangulia mtajulishwa tu, usijali mammy................... possibly and vice versa...................
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Kweli aisee, hivi kuna Member wa JF huku KAZIMZUMBWI?
Kama yupo basi tukutane pale kwa Mzee Mambaligwa karibu na ule muembe uliokuwa ukitumika kwa shughuli za Mkole na Ngoweko.
Pale kuna kijiwe kizuri sana cha Kahawa. Nitakuwa nimevaa Kanzu ya nyeupe na Makubazi na Mawani yenye fremu za plastic.

MTAMBUZI samahani kama nitakua nimekusoma wron' uelekezi wako hapa unaonesha kabisa una kila elements ya mzaha.
Sasa kama niko sahihi kwa mpango huo Jf membars mtajuana kweli ?
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom