JF kungeruhusiwa matusi ningemtukana Ngeleja

Status
Not open for further replies.

Mizizi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,275
391
Jamani mnisamehe, kwani inaniuma sana, leo asubuhi nimeenda ferry nikanunua samaki wangu wa laki nikitegemea watanifikisha mwisho wa mwezi.

Yani nimerudi mida hii samaki wote wameoza, ndani mnanuka, nauliza kulikoni naambiwa umeme ulikatika. Lakini kwa nini tunanyanyasika hivi?

Kama ni mgao si wewe Ngeleja ulisema umeisha? Kama umejirudia mbona hujatoa tangazo la mgao?

Nina hasira sana. Kwa kuwa hapa tz hakuna fidia juu ya hasara za namna hii basi ningeomba jf waruhusu hata kwa issue kama hizi tufidie kwa kuwatukana watu kama hawa.

Yani humu kungeruhusiwa matusi ningemtukana sana Ngeleja
 
Mod naomba usinipige Ban, kwani mm ni mtu wa kipato cha chini sana, laki kuipoteza ni kama nimepoteza gari. Sina uwezo tena wakupata hiyo pesa kwa wakati huu
 
Mkuu!!
Pole sana nimecheka kwa masikitiko.
Hiyo ilishawahi kitokea hata kwangu,
Nyama, samaki na viungo vya mboga vyote vilioza...

Dah pole sana tena sana. Ndio hivyo waziri wa Nishati Boya tu hana analofanya zaidi ya kufuata na kutekeleza maagizo R.A
 
Mod naomba usinipige Ban, kwani mm ni mtu wa kipato cha chini sana, laki kuipoteza ni kama nimepoteza gari. Sina uwezo tena wakupata hiyo pesa kwa wakati huu

Please mods, msimpe BAN huyu jamaa na hii thread iacheni bila ku edit naamini mpaka kesho asbh wadau wadau watakua wametoa michango yao
 
Wacha kumtusi anaendeshwa kwa remote huyo jamaa ukimtizama anatia huruma sana maana nafsi inamsuta jinsi Dhambi alizobeba zinakaribiana na za shetani...

Vumilia tu mwanangukesha kupiga kofi shavu la kushoto mgeuzie shavu la kulia nalo alipige kofi... atakuelewa tu...
 
Mod naomba usinipige Ban, kwani mm ni mtu wa kipato cha chini sana, laki kuipoteza ni kama nimepoteza gari. Sina uwezo tena wakupata hiyo pesa kwa wakati huu

Please mods, msimpe BAN huyu jamaa na hii thread iacheni bila ku edit naamini mpaka kesho asbh wadau wadau watakua wametoa michango yao
JF haiwezi kuvumilia yodi moja ya matusi. Tutumie lugha ya kistaarab tunapokuwa tunaelezea machungu yetu wakuu.

Post ya kwanza na heading vipo edited
 
Huyu ngeleja sio mzalendo wa nchi hii, anasikiliza warabu na wahindi ndio anaendesha nchi yetu king'ombe ng'ombe! Ametutajia wamiliki feki wa dowansi, ametutajia mipango hewa ya umeme!

Ngeleja jiulize ww mwenyewe nafsini mwako, unafanya kazi ya nani?
 
Hayo masamaki hata kama yangekuwa hayajaoza, vitamini na ladha nahisi vingeisha. Pole sana mizizi.
 
JF haiwezi kuvumilia yodi moja ya matusi.
Tutumie lugha ya kistaarab tunapokuwa tunaelezea machungu yetu wakuu.

Post ya kwanza na heading vipo edited

Ni sawa mkuu unachosema, na tunaheshimu sana utaratibu wa humu, ila anachotufanyia huyu Ngeleja ni zaidi ya matusi! Ametufanya wa tz ni wajinga sana.

Hapa wanakata umeme makusudi ili wakamilishe hilo dili lao la mitambo yao waliyoibadilisha jina. Ila mkae mkijua, hata muiite symbioni sijui nini, sisi tutaendelea kuijua kama richmond mpaka 2015.
 
Yaani hiyo nchi ni vichekesho.... hivi na wale wa*uni walochukua ile kitu ya do-ones si waliwasha mashine kimya kimya.. sasa umeme wao unaenda wapi kama si kuchota mpunga wa nchi kimya kimya!!!:confused2:
 
Hayo masamaki hata kama yangekuwa hayajaoza, vitamini na ladha nahisi vingeisha. Pole sana mizizi.

Mpendwa ingekuwa hivo mbona nchi zilizoendelea wangekuwa na kwashakoo wote, kila kitu kina wekwa kwenye friji tena zaidi ya huo mwezi alokuwa aweke mizizi
 
Pole sana MIZIZI kwa yaliyo kupata! Nami yamenikuta! nimeunguliwa home theater system mpya ya sh.850,000 baada ya kutoka kuinunua nikiwa natest mara umeme ukakatika na kurudishwa, hata nyumbani haijakaa dakika 5!, nikapeleka kwa mafundi wa mitaani wakashindwa, na wakachomoa baadhi ya vitu, kupeleka kwa ajenti wa Natioanal panasonic mpaka leo sijafanikiwa, MPAKA LEO HII NASIKIA VIMIZIKI VISIVYO CHUJWA

Nina uchungu mkubwa na TANESCO. Tangu mwaka 2002 wanaongelea umeme wa dharura!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Tanzamia TUMELOGWA! tumebanwa na tunashindwa jinsi ya kujinasua! Serikalini kuna ubabaishaji mkubwa.

NA NATANGAZA RASMI KUWA NCHI ZENYE MACHAFUKO ZILIANZA HIVI, MPAKA IKAFIKIA POINT WATU WAKAJIMWAGA BARABARANI KUDAI HAKI KWA NGUVU. SIKU ZAJA.
 
Yaani hiyo nchi ni vichekesho.... hivi na wale wa*uni walochukua ile kitu ya do-ones si waliwasha mashine kimya kimya.. sasa umeme wao unaenda wapi kama si kuchota mpunga wa nchi kimya kimya!!!:confused2:

we Ngeleja, si umo humu jamvini? Hebu jibu hoja haraka ili usiendelee kutukanwa kimoyomoyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom