JF Kritsmas & Mwaka Mpya: Self Check, Tupo Wapi?

Apr 27, 2006
26,588
10,374
Ndugu zangu wana-JF, na wengineo wote tunaoshirikiana hapa kwa njia mbali mbali katika kuelimishana na kuhabarishana, in a timely manner.

- Ninaomba kuwapa heshima zangu za dhati, na hasa ndugu yangu Maxence Melo, kwa busara nzito sana alizoanzo huyu kijana mdogo sana kiumri hasa katika kuiendesha hii Taasisi, ambayo sasa sio siri kwamba ni chombo kikubwa na muhimu sana kitaifa, katika kupata habari muhimu sana za kisiasa, na hasa uchambuzi wa kina wa ishus nyingi za uongozi, zinazohusu taifa letu.

- Halafu tena ninaomba kutoa heshima kubwa sana kwa wachangiaji wote JF, kwamba michango yenu ni lulu nzito sana kwa taifa ingawa huenda mingine haieleweki sasa lakini huko mbele ya safari itaeleweka na tuendelee hivyo hivyo.

- Sasa hoja yangu ya msingi ni kwamba, tunafikia mwisho wa mwaka na we have been in this game kwa muda mrefu sana sasa, siku zote watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri, yaani Great Thinkers as we are, huwa wanafika mahali wanakaa chini na kujiuliza, huku wakijiangalia kwa jicho kali sana bila kujidanganya kwamba wapi wamefanya vizuri, na wapi wamekosea na jinsi ya kurekebisha walipokosea.

- Ninaomba wakuu tutumie nafasi hii kujaribu kuangalia yale yote ambayo tungeyafanya tofauti ili Mwakani tuweze kuwa wakali zaidi kuliko Mwaka jana. Hakuna sababu ya kurudia mazuri yetu maana yanafahamika na taifa zima, lakini JF ni lazima tuweke mfano kwa taifa kwa kuwa na tabia ya kujiangalia wenyewe, kabla ya kusubiri kuambiwa na wengine, halafu kuanza kuita wengine wana wivu na chuki na sisi wanapojaribu kutusaidia kimawazo!

Ahsanteni Ndugu Zangu na Kheri Kritsmas, na Mwaka Mpya Kwa Wana-JF Wote Popote Mlipo.


William.
 
1.Tuiwezeshe JF.........hili ni jambo tunaloomba kila mwanachama hapa JF alifahamu.....until such time.......ambpo JF itakuwa na vitega uchumi vyake.........inaniuma sana kuona tangazo........eti........... "JF tumezidiwa/kufungwa"

2.Wana JF tujikumbushe rules za Jamvi letu.....ili kuwapunguzia mzigo usio kuwa wa lazima hawa Mods wetu
 
1.Tuiwezeshe JF.........hili ni jambo tunaloomba kila mwanachama hapa JF alifahamu.....until such time.......ambpo JF itakuwa na vitega uchumi vyake.........inaniuma sana kuona tangazo........eti........... "JF tumezidiwa/kufungwa"

2.Wana JF tujikumbushe rules za Jamvi letu.....ili kuwapunguzia mzigo usio kuwa wa lazima hawa Mods wetu

- Nafiri hili limeeleweka, michango yetu ni muhimu sana katika kuisaidia jamvi kuendelea kuwepo, ambapo sio siri wote tunanufaika nalo sana.

William.
 
Krismas njema Mkuu na asante kwa Heri ya Krismas na Mwaka Mpya.

Mungu atuzidishie hekmah yake, ili mwaka 2010 tuweze kuwa bora zaidi katika fikra pevu, endelevu na akili tulivu katika kujenga Taifa letu kwa kutumia JF.


Thanks
 
Back
Top Bottom