JF Karibuni Tanzania Professionals Network

Sanctus,

Nitakutumia Jina la mtu anayeweza kuwatengenezea site nzuri, ngoja nim-contact kwanza ili anipe link za site alizotengeneza uziangalia kwanza!


GM, nitashukuru sana Mzalendo. Kwa kweli hata mimi binafsi suala la Website bado sijaridhika nalo . . . . You know first impression inaweza kumpa mtu yeyote picha ya vile ulivyo. Kwa TPN website it should not be that way.

Thank you my bother (I hope so . . . ) for your support on this matter.
 
Nimefurahi kwa hili.

Na ndio maana katika post zangu kama culiangalia nilikuambia ya kwamba nimedownload almost kila kitu katika site ya TPN maana nataka kusoma na kuelewa na yale mapungufu ambayo nadhani ntawa nimeyaona nina hakika kabisa utanisaidia na kunifanya nikaelewa na kufanya mimi na wewe twende sawa.

Mpaka sasa nasoma na nahitaji kupata msukumo kutokana na yale ambayo nayatazama na kuyafikiria kwa fikra zangu mimi, kisha Mh Rais wa TPN utanisaidia kuboresha Fikra zangu butu juu ya Malengo ya TPN!

Nina uhakika TPN haiwezi kuwa saa iliyosimama...tofauti na Asasi nyengine zisizo za Kiserikali natumaini ya kwamba kuna Mwanga at the end of the Tunnel maana mpaka sasa ninaendelea kuwa katika kiza husiana na TPN. Nikikamilisha which i hope itawa mapema sana ntawasiliana na wewe official ili unifafanulie zaidi. Na natumaini ya kwamba one to one, eye to eye itawa informative zaidi.

One last thing ni kwamba, Katiba zinatoa muongozo katika asasi zote, za serikali na zisizo za kiserikali lakini wanao-determine direction ya hizo asasi na namna ambavo zinafanikisha malengo zake na kwa njia zipi ni Viongozi.

Nawakilisha.

Mzalendo mwenzangu Mzozo wa Mizozo, kwa dhati ya moyoni bado nakushukuru kwa kuzidi kutafuta muda wa kutoa mawazo ya kuboresha. Binafsi kutokana na michango yenu nimegundua mapungufu ambayo kwa hakika yanataka marekebisho. Hili ni la kujivunia kwa kuwa mawazo yenu hapa JF yamezeza kuboresha.

Napenda nikuhakikishie kitu kimoja, TPN inaweza isiwe clear katika maandishi yake au website, lakini kwa wale members walio ndani ya TPN na ambao wamepata nafasi ya kuhudhuria event za TPN, bila ya shaka wanayo picha kamili ya nini TPN inafanya na wapi inaelekea. Naahaidi mapungufu mnayoyapata na kutujulisha tutayarekebisha. Nakukaribisha sana kuniandikia binafsi na hata kuonana kama utapenda.

Mwisho napenda tena kutambua michango yako yote. Natambua pia mimi kama moja wa viongozi wa TPN ninayo dhamana ya kuonyesha dira. Nitajitahidi kadiri niwezavyo na kwa commitment ya hali ya juu katika kipindi changu hiki cha uongozi kuonyesha njia. Napenda kutoa mwito pia kwa wale wenye nia ya kweli ya uongozi na vipaji, kijitokeza ili kwa pamoja tuweze kushirikiana.
 
Sanctus, karibu sana. Nakumbuka tumewahi kuwa mawasiliano huko nyuma. Miye nawaunga mkono kabisa. Tatizo langu ambalo kidogo umeligusia hapo juu linatokana na mchanganyiko wa jina na mission yenu.

Jina linasema ni "Tanzania Professionals Network"; katika kulielewa hili mnasema katika membership kuwa ni "

Membership is open to Tanzanian Graduates from a higher Institution of learning. There also is membership for corporate organisations and honorary membership"

sasa hili lina matatizo kadhaa:

- Je wahitimu ambao siyo Watanzania na wanafanya kazi katika Tanzania wakiwa na leseni au vyeti vya kitaaluma vya Tanzania hawaruhusiwi kuwa full membership au wanapewa huo wa heshima? Kw. Madaktari, wahandisi, washauri n.k?

- Je wale waliohitimu katika vyuo ambavyo si Higher Learning (kwa maana havitoi shahada labda vyeti tu) kama waliosomea fani za Ukatibu Muhtasi, Ukarani wa Mahakama n.k hawastahili kujiunga na mtandao huu kwa sababu hawakujiunga na Higher Learning Institutions?

- Jina linasema ni "Professionals" lakini kama ambavyo niliwahi kulisema hili awali ni kuwa professionals siyo sawa na intellectuals au wanataaluma. Kama lengo ni kuwa mtandao wa wasomi basi siyo kila mtu aliyehitimu higher learning anaweza kuwa kweli kwenye kundi la wasomi. Msomi, ni mtu aliyebobea katika elimu ya fani yake, unless kuna haja ya kudefine mtaaluma ni mtu mwenye sifa gani. Siamini kuwa kila anayetoka na shahada ya kwanza anaweza kujiita msomi. Usomi wa mtu siamini kama unaweza kupimwa kwa kuangalia alivyograduate isipokuwa kwa kuonesha mtiririko wa kazi, uzoefu na mchango wake wa kitaaluma katika fani yake.

- Lakini inaposemwa kuwa ni "professionals" kwa mtu mwingine inaonekana ni pana zaidi kuliko definition ya "graduate". Je fundi seremala ambaye amejifunza useramala alipokuwa sekondari na baada ya kazi na uzoefu wa muda mrefu amekuwa ni gwiji katika fani yake anaweza kuwa memba? Jibu langu kwa haraka ni hapana, kwa sababu hajagraduate. Lakini tukiuliza is he a professional? the answer is in the affirmative. Sasa kama ni professional na mtandao ni kwa ma professional kwanini yeye haingii?

- Kwa kutilia mkazo elimu ya kizungu (western education) na jinsi ambavyo tunatambua mtu kasoma (kwa kuonesha cheti) mtandao unatenga jamii kubwa ya professionals wa tanzania ambao hawakuhitimu katika vyuo vyenye mfumo wa kizungu lakini wamejifunza kupitia kile kinachoiwa "the school of hard knocks". Ipo haja ya kuangalia jinsi gani hawa nao wanaweza kushirikishwa.

- Kwa vile mnasema mission ya TNP ni "To stimulate and promote effective use of the POWER OF THE BRAIN among Tanzanians in addressing and solving their various Social, Cultural, Economical; Developmental and Psychological Problems" inaonekana kuwa Brains ambazo kwenu zina uwezo wa kuaddress and solve hayo mliyoyataja ni zile zilizograduate tu. Je hakuna watu wengine wenye bongo ambazo ziko sharp na mchango wao unaweza kuhitajika katika mjadala huu lakini hawakupitia katika vyuo vya mfumo wa kimagharibi ili kuthibitishwa kuwa wamesoma?

Ninachoona kwa upande wangu ni kuwa, kama hii ni taasisi ya wasomi wa vyuo vikuu, basi itajwe hivyo na kuwa "Tanzania Intellectual Society" or a "Network of Tanzanian Intellectuals" or "The Association of Tanzanian Academicians" or similar titles. Mkifanya hivyo basi wengine tujua tunaingia katika taasisi gani au kama tutaona hatustahili kuingia kwa taasisi hiyo. Lakini kama lengo ni professionals wa Tanzania, ipo haja ya kuredefine na kupanua wigo wa maana yenu na wito wenu.
 
Naungana mkono na Mtsimbe katika kuomba juhudi za pamoja kuleta maendeleo ya Tanzania. Pia sipingi wazo la kukutanisha wanataaluma wa kada tofauti katika mtandao mmoja, kwani hii husaidia kurahisisha mambo..... Wazo ambalo naona ni gumu kidogo ni lile la kuingia katika mtandao huo wale wafukuaji mambo hodari wa JF.... hawa wanahitaji kubaki hukohuko waliko, vinginevyo future ya JF itakuwa at stake. Nadhani si kila mtu, especially mafisadi na watu wanaofanana na neno hili hufurahia JF, hivyo kwao sehemu ya kwanza kwenda kujua who is who in those hot issues za JF itakuwa katika mitandao kama hiyo. Angalizo lingine ni kwa wana TNP kuboresha site yenu, kwani wenyewe mmesema kuna wanataaluma mbalimbali, pia muwe na objectives ambazo ziko specific. ni hayo tu!


Mzalendo Paullih, asante kwa maoni yako. Bila shaka kama umepitia maelezo yangu mengi utagundua kuwa nimeafiki wazo la kutotumia majina kwa wale wanaotaka. Nadhani sababu zilizotolewa na wewe ni za msingi kabisa.

Hili la kuboresha tovuti na kuwa na focused objectives tumeliona na tumekubali lifanyiwe kazi. Hivi tunavyoongea natumaini kuna watu wanatafuta ufumbuzi wa hilo. Tafadhali karibu sana na jisikie huru kutuma maoni yako
 
Originally Posted by gm
Sanctus,

Nitakutumia Jina la mtu anayeweza kuwatengenezea site nzuri, ngoja nim-contact kwanza ili anipe link za site alizotengeneza uziangalia kwanza!


GM, nitashukuru sana Mzalendo. Kwa kweli hata mimi binafsi suala la Website bado sijaridhika nalo . . . . You know first impression inaweza kumpa mtu yeyote picha ya vile ulivyo. Kwa TPN website it should not be that way.

Thank you my bother (I hope so . . . ) for your support on this matter.

Sanctus,

Kuna bwana mmoja namfahamu mbongo katengeneza hizi sites hii hapa na ingine hii hapa niandikie email au PM nitakupa contacts zake email yangu taskmgt@gmail.com.
 
Lakini viongozi wengi wa NGO's na serikali huwa wanatamba kwamba huwa hawana uhusiano na vyama vya siasa lakini ikifika wakati wa uchaguzi ni hao hao huwa tunawaona wanakimbia kuchukua fomu za kugombea katika vyama. je hizo kadi za uanachama huwa wamezipata lini?
Utangundua wengi ni wanafiki tu. Ukitaka kujua unafiki wao utasikia wanasema wameombwa na wazee huko majimboni. Ebo hivi wazee wa majimbo ndiyo wanawakilisha mawazo ya jimbo zima?

HAKI HAIZIKWI NA IKIZIKWA UFUFUKA TU.:lol: . . . .


Mzalendo Mchukia Ufisadi hakika haki ya mtu haipotei . . . TPN tunatafuta pia haki ya kumiliki mali kutokana na rasilimali zet, kuwa na pesa kihalali nk.

Nashukuru kwa angalizo lako na binafsi nitalizingatia. Kimsingi TPN si mwanachama wa chama, dini, kabila wala jinsia yoyote ingawa wanachama wako huru kufuata wanaachoamini katika itakadi na imani yao.

Ukweli wangu mimi binafsi si mwanachama wa chama chochote na wala sijawahi kuwa na wazo la kujiunga na chama chochote. Pengine hili linatokana na ukweli kuwa napenda sana kuangalia OUTPUT kuliko siasa zenyewe. Pia naamini sana katika uwezo wa mtu. Nina imani kuwa vyama vya kisiasa vikiimarishwa na kuwa na Demokrasia ya haki na ya kweli na wananchi waelewe vema haki yao ya uraia huenda OUTPUT ikawa nzuri zaidi kuliko ilivyo sasa. Pia kufuata Maadili ya uongozi ni kitu muhimi sana.
 
Kufuatana na Katiba ya TPN mtu yeyote anaweza kujiunga na TPN ili mradi tu awe na mawazo ya kimaendeleo (Positive Attitude).

Kuhusu membership, kwa uhakika membership iko open kwa Wanataaluma wote waliopo ndani na nje ya nchi. Na hata sasa tunao wanachama ambao wako nje ya nchi. Nadhani itabidi tuliangalie hili kimaandishi tuliboreshe vipi bila kuleta mkanganyiko.

Naomba tena ufafanuzi.

Nisichotaka kuruka kukisema kabla sijapata ufananuzi mzuri ni kwamba wewe Raisi wa chama cha watu wenye digrii na mashirika ya biashara unashindwa kueleza hata qualification za uanachama. Utawezaje kufanya makubwa zaidi?

Kwamba unataka kuonekana kwamba ni cha wote wakati sivyo.

Sitaki kuruka kusema kwamba wewe sio mkweli kabla hujafafanua.

Unasema chama chenu cha wenye digrii na mashirika ya biashara ni cha wote kwa sababu kuna lile kundi la tatu, la honorary membership. Hiyo honorary membership unapewa kwa heshima au yeyote anapata? Kama yeyote anapata basi clause ya qualification za uanachama kwa nini ina neno "uhitimu"? Ni katiba yenu au wewe Raisi ndio hau make sense?

Raisi naomba utumie nafasi nyingine tena kufafanua ni nani anakubaliwa kundini mwenu.

Au, ahidi kwamba maneno matamu yako mlisahau kuyaweka kwenye katiba na mtayaweka. Isipokuwa kama neno la Rais ndio Katiba.

Assuming wewe ni Rais.

Maana umesema tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz

Kwa mtaji wa hiyo email address, unaweza ukawa Katibu au karani mpokea barua wa Rais.

Naomba jitambulishe wewe nani kwenye chama cha waliohitimu na Mashirika ya Biashara.

Tena.
 
Maelezo bado yananipa maswali mengi kuliko majibu.... tupo pamoja bado Sanctus.

Bado napiga hatua na I sincerely hope that there will be light at the end of the tunnel.
 
Lakini viongozi wengi wa NGO's na serikali huwa wanatamba kwamba huwa hawana uhusiano na vyama vya siasa lakini ikifika wakati wa uchaguzi ni hao hao huwa tunawaona wanakimbia kuchukua fomu za kugombea katika vyama. je hizo kadi za uanachama huwa wamezipata lini?

Utangundua wengi ni wanafiki tu. Ukitaka kujua unafiki wao utasikia wanasema wameombwa na wazee huko majimboni. Ebo hivi wazee wa majimbo ndiyo wanawakilisha mawazo ya jimbo zima?

Mzalendo Mchukia Ufisadi nashukuru sana kwa angalizo lako. Ni kweli baadhi ya watu wanafanya NGO kama ngazi ya kupatia madaraka ya kisiasa.

Napenda kukuhakikishia kuwa TPN haina dini, kabila, chama wala jinsia ingawa wanachama wake wako huru kufuata wanachoona ni bora.

Mimi binafsi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa na wala sijawa na mwelekeo huo. Penginepo ni kwa kuwa napenda sana kuangalia OUTPUT kuliko siasa za vyama. Ningependa sana kuona kuna demokrasia ya kweli inayozingatia ukweli na uwazi baada ya wananchi kupewa elimu ya kutosha na kisha kuachwa wachague wanaachotaka kwa uhuru wao.

TPN ingawa haina chama lakini ina malengo ya kuwaondolea wanachama wake umasikini kwa kutumia fursa zilizopo. Hebu na tuungane wote ili kuweza kufaanya sehemu yetu. Mafanikio ni dhahiri kama tukiungana na kuwa na nia ya kweli.

Ningep
 
Naomba tena ufafanuzi.

Nisichotaka kuruka kukisema kabla sijapata ufananuzi mzuri ni kwamba wewe Raisi wa chama cha watu wenye digrii na mashirika ya biashara unashindwa kueleza hata qualification za uanachama. Utawezaje kufanya makubwa zaidi?

Kwamba unataka kuonekana kwamba ni cha wote wakati sivyo.

Sitaki kuruka kusema kwamba wewe sio mkweli kabla hujafafanua.

Unasema chama chenu cha wenye digrii na mashirika ya biashara ni cha wote kwa sababu kuna lile kundi la tatu, la honorary membership. Hiyo honorary membership unapewa kwa heshima au yeyote anapata? Kama yeyote anapata basi clause ya qualification za uanachama kwa nini ina neno "uhitimu"? Ni katiba yenu au wewe Raisi ndio hau make sense?

Raisi naomba utumie nafasi nyingine tena kufafanua ni nani anakubaliwa kundini mwenu.

Au, ahidi kwamba maneno matamu yako mlisahau kuyaweka kwenye katiba na mtayaweka. Isipokuwa kama neno la Rais ndio Katiba.

Assuming wewe ni Rais.

Maana umesema tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz

Kwa mtaji wa hiyo email address, unaweza ukawa Katibu au karani mpokea barua wa Rais.

Naomba jitambulishe wewe nani kwenye chama cha waliohitimu na Mashirika ya Biashara.

Tena.

Kuhani,

Nafikiri kwa maelezo niliyotoa katika page ya TPN kwenye site inaonesha kuwa Sanctus ndiye president. Mengine atakujibu.....



The current leaders of the TPN Executive Committee were elected on 29th July 2007 at the AGM. The Executive Committee then appointed the Matron and Trustees

1. Executive Committee Members

Sanctus Mtsimbe – President (B.Sc; M.Sc.); Business Development Manager; SimbaNET


Method Bakuza – Secretary General (B.Com); Director; Mayo 1999 Co. Ltd


Ms. Consolata Maimu – Treasurer ((Adv. Dip; Post Grad. Dip; MBA); System Auditor; TASAF


Jackson Mayunga – Member of the Executive Committee (B.Sc; Post Graduate Diploma); Head of ICT; Stanbic Bank


Ms. Janet Mbene – Member of Executive Committee (Adv. Dip; BA; MA); Director & Lead Consultant; SME in Action; DSM


Hamza Kondo – Member of the Executive Committee (2 Diplomas; Post Graduate Diploma); President; Tanzania Journalists Association, MD Sena News Agent


Ms. Rachel Mwalukasa – Member of the Executive Committee (B.Com); Senior Retail Manager; Barclays Bank; DSM


Ms. Aiwerasia Ngowi – Member of the Executive Committee (B.Sc; M.Sc; PhD); Senior Principal Research Scientist; Tropical Pesticides Research Institute; Arusha


Dr. Donald Olomi - Member of the Executive Committee (Bachelor of Commerce (Honours), an MBA and a PhD in business administration from Tanzania, Canada and Sweden respectively.); Senior Lecturer and Director of the University of Dar es Salaam Entrepreneurship Centre (UDEC).


Hon. Dr. Batlida Burhani - Member of the Executive Committee (B.A (Public Admin. & International Relations, M.A (Development Studies), PhD (Planning Studies). She is a Member of Parliament and Minister of State, Prime Ministers Office
 
Ndugu Mtsimbe,

Mimi nina swali ambalo ni very serious. TPN inawezaje kuwasaidia wabunifu -- inventors na innovators -- ktk ku-implement ubunifu wao? Kwa mfano, kuna mtu ninayemfahamu ambaye ana inventive idea khs nishati m'badala, lkn hana pesa za kuiendeleza wala kuilipia hataza (patent) wazo lake hilo. Hili likiwa km wazo linaloweza kuleta mabadiliko bora nchini; je, TPN inawezaje kuwasaidia watu km hawa?

Mzalendo Raibow, tumewahi kuliongelea hilo katika TPN. Ukweli ni kuwa watu wabunifu kama hao na wao pia ni Wanataaluma. TPN inaweza kuwatambua kwa kuwapa Awards na kisha kuwapromote.

Changamoto iliyopo ni ya kifedha kwa sasa. Lakini kama nilivyoeleza kuna mikakati ya kuanzisha TPN Fund kwa ajili ya mambo mbalimbali. Pia TPN kwa sasa ina contacts nyingi za sources za fund na za kibiashara. Kwa wale walio na jitihada ya kweli, tunacho kitengo maalumu ndani ya TPN ambacho kinashughulikia mambo kama hayo.

Tafadahli mwombe mbunifu wetu awasiliane na TPN ili tuangalie nini kinaweza kufanyika.
 
Mzalendo Mchukia Ufisadi nashukuru sana kwa angalizo lako. Ni kweli baadhi ya watu wanafanya NGO kama ngazi ya kupatia madaraka ya kisiasa.

Napenda kukuhakikishia kuwa TPN haina dini, kabila, chama wala jinsia ingawa wanachama wake wako huru kufuata wanachoona ni bora.

Mimi binafsi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa na wala sijawa na mwelekeo huo. Penginepo ni kwa kuwa napenda sana kuangalia OUTPUT kuliko siasa za vyama. Ningependa sana kuona kuna demokrasia ya kweli inayozingatia ukweli na uwazi baada ya wananchi kupewa elimu ya kutosha na kisha kuachwa wachague wanaachotaka kwa uhuru wao.

TPN ingawa haina chama lakini ina malengo ya kuwaondolea wanachama wake umasikini kwa kutumia fursa zilizopo. Hebu na tuungane wote ili kuweza kufaanya sehemu yetu. Mafanikio ni dhahiri kama tukiungana na kuwa na nia ya kweli.

Ningep

Hongereni sana kwa hili. Lifanikiwe.

Je na mafisadi ambao wameshathibitika kwa asilimia 80 wanaruhusiwa kujiunga TPN? je kuna sheria zozote za kuhakikisha mnawafilter out members wanaojihusisha na ufisadi? Inaonyesha kuwa wengi wa mafisadi ni graduate an corporate elites.
 
Hata mimi nina rafiki yangu anakipaji kikubwa cha designing mnaweza kumsaidia?he is a great painter and drawer.he designs very good clothes na shoes infact one of his designs Kelly Rowland aliinunua.

Mzalendo mwenzangu Kevo, tafadhali mwombe mbunifu wetu awasiliane na TPN. Mara nyingi kinachofanyika anapata nafasi ya kuelezea ubunifu wake au biashara yake katika events zetu za Networking. Pia anatakiwa aelezee yeye binafsi anataka TPN au members wamfanyie nini. Katika hali hii members hutoa mawazo yao ya kuboresha.

Na kama shida yake pia ni Mtaji, Ujasiliamali au Masoko nk basi anaweza akapata support ya kimtaji kupitia sources mbalimbali zilizopo TPN kwa sasa.
 
Nafikiri kwa maelezo niliyotoa katika page ya TPN kwenye site inaonesha kuwa Sanctus ndiye president. Mengine atakujibu.....

Ahsante.

Naona alisahau kidogo tu kutuambia yeye ni nani kwenye chama cha Wahitimu na Mashirika ya Biashara.
 
Asante kwa maelezo Mazuri..

Mzalendo Gembe . . . I like your quote "As long as I am leader, Our position is not going to change from that of our forefathers. I do not want the responsibility for selling the rights of our children yet unborn"

Natamani sana nielewe zaidi kilichomo mawazoni mwako kuhusu usemi huo. Mimi pia ni mmoja kati ya viongozi wa TPN. Tafadhali nielimishe zaidi nielewe.

Otherwise nashukuru sana kama umeridhika na maelezo niliyoyatoa.
 
Ahsante. At least now kidogo umeandika kwa hata mtu akisoma kidogo anajua TPN inasimama for what. But mbona mko 'Vague' mno. Malengo ni mengi mno yaani ni kwamba its unclear, kwangu mimi inakuwa ni shida sana kupata Muelekeo kamili wa Mtandao huu.

The way things are going is like TNP is trying to do everything the just like the American way of Shooting, "Firing Enough Bullets and Hoping to Hit the Target" LOL....

Mkulu Mzozo wa Mizozo nashukuru sana na nimekupata. Naahidi tutayarekebisha na naomba unitumie maoni yako. Wakulu naomba mkiweza tuwasiliane. Napenda niwape changamoto tuje tusaidiane. Mapungufu mengine yanayoonekana huenda yakawa na maana ya kukosa watu wengine ambao wanaweza kutenda mambo kwa vitendo.
 
Hongereni sana kwa hili. Lifanikiwe.

Je na mafisadi ambao wameshathibitika kwa asilimia 80 wanaruhusiwa kujiunga TPN? je kuna sheria zozote za kuhakikisha mnawafilter out members wanaojihusisha na ufisadi? Inaonyesha kuwa wengi wa mafisadi ni graduate an corporate elites.

Mama umefika... umenipa burudani kwa hiyo input yako. Ni ukweli mtupu.

Jambo jengine kwa Mzalendo mwenzangu Mtsimbe, hapa tumekuwa tukienda hoja kwa hoja na wewe kuanzia asubuhi na mapema, na so far umeiwakilisha vema TPN. Unahitaji pongezi.

Lakini je huwezi kuwa na member mwengine wa TPN ambae ni mwanaharakati wa JF ili nae/nao waweze kuchangia katika hili ili sisi tuweze pata mwanga zaidi? jaribu kuwaalika katika mjadala huu, ama kama utaniruhusu naweza watumia mail members wote kupitia ile mailing list yenu kisha waje hapa katika mjadala tupate mambo kwa wingi na undani zaidi.
 
Mie binafsi nimeridhika kwa maswali na duku duku zangu na pia kama anavyosema Mzozo wa Mizozo unahitaji pongezi kwa kutumia siku yako ya leo na mda mwingi kujibu maswali na duku duku mbali mbali. Keep it up Bro! kama wenzako wa TPN wanaweza basi wakupe tafu kidogo, hapa watu tunalala na kukesha hapa!! LOL usiogope lakini!
 
Bandugu samahani kama nitakuwa nimechelewa ku-comment kwenye mada hii.

Karibu sana Ndg Mtsimbe na tunashukuru kwa ukaribisho wako, however nasikitika kuwa TPN walini-disappoint the first day i tried to contact them/you rather. One might say you or your collegues were busy......but there was no sense of acknowledgement whatsoever............nakumbuka ilikuwa mkijitayarisha na mkutano na professionals (or something like that) pale Dar.......you had posted your agendas and i had my comments sent to you all........well sitaki kusema kwamba ilikuwa ni dharau...........kwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza.
........The point is please try to respond to people's comments.........otherwise binafsi baada ya hapo sikuwa hata nataka kusikia chochote kuhusu TPN...............anyhow karibu JF.............na tuelimishane


Mzalendo Ogah, kwanza kabisa naomba nichukue fursa hii kukomba radhi ya dhati kwa hayo yaliyotokea. Ukweli ni kuwa kwa uzoefu wangu wa muda mfupi wa kudeal na wanataaluma tuna tatizo la kunena kuliko kutenda.

Katika kipindi kile cha matayarisho kilikuwa kigumu sana hasa kwangu binafsi kwa kuwa nilichaguliwa na wenzangu kuwa mratibu mkuu wa mkutano na bahati mbaya team ya uratibu haikuwa active kwa vitendo. Hii ilisababibisha binafsi kuwa na workload kubwa ambayo kwa kweli ilikuwa ni vigumu kuimanage. Hatukuwa na resources zozote kipindi hicho zaidiya zile resources binafsi na za kujitolea.

Kwa mfano, kuna waliopiga simu, waliotuma SMS, waliotuma email na waliofika kuniona physically. Wakati huo huo nilikuwa na majukumu ya kikazi na kibiashara.

Nakumbuka wakati mwingine ilinilazimu nilale saa 8 za usiku. Nilijitahidi kurespond kwa wengi ambao zaidi ya 500 waliconfirm kuhudhuria. Inawezekana sikukujibu au inawezekana message haikukufikia.

Kwa lolote ambalo litakuwa ni kweli naomba tena nikuombe radhi ya dhati na kukukaribisha rasmi sasa tuje tuungane sote. Karibu sana.
 
Nakushukuru sana Sir Mtsimbe, kama kuna waliokuunga mkono huko JF nadhani ni watu wazima na wanajua walifanyalo. La msingi ni kuwa malengo ya hizi community mbili ama community hii na TPN Org yanaweza kufanana lakini njia za kufikia malengo ziko tofauti sana, sasa member wa JF akienda TPN unamtaka abadili namna ya kujishughulisha kama hatapenda kujulikana maana ukiwa TPN huwezi kupiga kelele, vinginevyo utashtukiwa...? Ukiwa TPF huwezi kutoa siri unazozijua, utashtukiwa...? Huwezi kusema lipi linawezekana maana utaulizwa ushahidi ambao utafanya watu wagundue wewe unajua mengi...? na kama ulishayasema mahala pengine..., ndio umenaswa hivyo...! Those JF concretes shall remain Rigid in order for JF to remain strong and loud.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom