Jf ilinikutanisha na tapeli wa mapenzi

Mmhh
hii itaendelea kutokea kwa wote wanaotafuta mapenzi.
Mapenzi hayatafutwi iwe mitandaoni au huku mitaani tunapoishi,
mapenzi yanatokea kama zao la mahusiano mazuri.

Nakuunga mkono sema tu moile haina thanks ningekugongea
 
wengi wanaotapeliwa
ni matapeli pia..........

sijui ni kwa nini mtu aamini watu wa mtandao na asiwaamini wa mitaani wakati watu ni hao hao
 
sioni faida ya kudanganyana
wewe kama unatafuta wa starehe si useme tu natafuta wa starehe sitaki ndoa wa commitments
mbona wapo weengi humu wako tayari kustarehe na waume na wake za watu bila kuanzishiana threads????/
 
  • Thanks
Reactions: BPM
lakini kumbuka mazingira mnayokutana na mwenza pia hutengeneza maisha na aina ya kuishi au mahusiano
 
Wakuu, heshima mbele,

Najuta sana kumtafuta partner humu JF yani pamejaa usanii hapa usipokuwa mjanja kama mimi unalizwa hivi hivi unajiona.


Kipindi kile nilikuja na swala la kutafuta mchumba hapa, kweli huyo aliyejidai mchumba alipatikana bada ya kuchuja chuja na kufanya trial and error. kumbe mchumba hakuwa mchumba bali tapeli wa mapenzi tu. mkasa ulikuwa hivi....... jamaa alisema yuko single na mara ya mwisho kuwa na msichana ni mwaka mmoja uliopita.baada ya kuchat sana kupitia mtandao huu wa JF na email ilibidi tupeane mawasiliano ya simu, na majina ya facebook account. Ukweli mawasiliano yalikuwa hot sana. Simu zilikuwa hazikauki, meseji ndo dahhh siwezi sema, kutwa kuchwa ni kuchat na kupena meseji za mahaba. Ila kwenye facebook friend list yake ilikuwa imefungwa huwezi ona nani ni rafiki yake na huwezi post kwenye wall yake pia.

Basi, sisi tukiwa kwenye mapenzi motomoto na kuliwazana (ila sikuwa mwepesi kutoa tundi ndio ninachoshukuru na kujivunia) kumbe jamaa ana girlfriend wake wa long mie sikujua, basi siku moja niliona friend request ya mdada mmoja hata simjui ameni-add mie bila hiyana kabla ya kumu-accept nikawa natumiana nae inbox kujua ni nani na ni wawapi.....bi dada akaniambia nimuadd kwa faida yangu, ila akawa anadadisi sana kuhusu mahusiano yangu ya kimapenzi, sikuwa muwazi sana hadi aliponitajia jina la facebook la huyu kiumbe tulokutana JF. Huyu binti alisema yeye na huyu fisadi wa mapenzi ni wachumba wa long time ila yeye anafanya kazi mkoani huwa anakuja dsm mara chache sana. Nilimuuliza kuhusu uthibitisho ili niamini maneno yake then alinitumia hadi ushahidi wa pics ambazo sio za kawaida yani za mitego mitego ya kimapenzi zinazoonesha wako na mahusiano live (picha zilionesha hata dates za muda wa karibuni), kuforwad emails za huyu kiumbe wanazotumiana kila leo za kimapenzi n.k.

Ukweli baada ya hayo yote hasira zilinipanda ila nikazituliza nikapata ujasiri wa kumuomba kijana anipishe tugawane ustaarabu. kijana alisita huku akisistiza nimwambie why, mie nikamwambia nimeona siwezi match nae, yeye akawa anasisitiza bado ni mapema mie ku conclude hivyo. Nilipoona anasisitiza nikamwambia live kwamba ana msichana mwingine hivyo ni bora nimpe nafasi ili apumue vizuri! Kijana alibisha hadi leo hii.., pamoja na kumforwadia emails zake lakini wapi bado anakataa.

Hili tukio nimeona nililete ili kuwaasa wasichana wenzangu na hata kaka zangu ambao nao wako kwenye process ya kuisaka ndoa wawe makini sana. mimi kwa hili naweza sema ni Mungu ameniokoa kwani nilikuwa ninaelekea mbali na kuzamia kabisa! huwa nimefikiria ilikuwaje huyu dada akanijua kupitia facebook? au alipewa password na hyu kaka? hapana Mungu aliamua kunionesha na kuniokoa.

Wanawake wenzangu na kaka zangu tumuombe sana Mungu ili atupatie wanaume na wanawake wa ukweli na sio matapeli.

Mbarkiwe sana.

ubarikiwe weweww uliemkosa kosa mume wa mtu na huruma zako
siku nyingine usirudie tena
 
Chunga sana, kuna kisa kililetwa juzijuzi na mwana JF wa zamani kuhusu haya mapenzi ya kwenye mtandao kumbe mtu alikuwa unausambaza UKIMWI makusudi kabisa. Pole.

Hapa duniani kuna watu wamewekea moyo wa shetani kabisa.
Haya mambo ya kubanjuana bila kujuana afya hayafai hata kidogo.
:A S 39:
:confused2::nono:
 
Back
Top Bottom