JF Garden (Bustani ya Jei Efu)........

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,513
11,276
Hizi Ndumu Bana!

Eti nilikuwa ninaimajini kwamba Jei Efu imegeuka Kabustani halafu wana Jamii wamegeuka viumbe tofauti tofauti.

Kuna watu nimewaimajini eti wamekuwa Viwavi Jeshi, Vinyonga, Sungura, Mchwa, Kunguru n.k

Kuna huyu Mbaba nilimuimajini kama Kobe aisee, simtaji..

Kuna huyu dada aliyetulamba vibuti akaenda kwa yule mshamba mshamba jirani yake, yeye nime muimajini kama Kipepeo, maana ndiyo za vipepeo kuruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Nanihii, na misifa yake yote eti nimemuimajini kwamba ni Komba, i donti noo wai kwa kweli.

Halafu kale kabrazameni kalikotunyang'anya yule Dada nimekaimajini kama fuko, yaani kanafukua fukua mpaka kanaharibia wenzake pozi.

Mzee nanihii Bana naye nilimfikiria kama wale wadudu wanaotoa miiba, labda sababu ya unoko wake kwa vibinti vyake humu.

Halafu kale ka'mke ka yule Brazameni Mapua nimeka'imajini kama Mbu, sijui ni kadogo kama mbu nako ni kadogo na kasumbufu kama mbu?

Huyu nanihii sasa ndiyo ameniacha mdomo wazi, si nimemfikiria kama Kinyonga Bana, labda kwa sababu anawezaga kujibadilisha any time. Kuna wakati anajiita mara mzungu, mara mchina, mara Msela, mara Manzi..

Dada yetu Mod nikamfikiria kama Twiga, manake naye sam taimz anakuwaga na mapozi kweli. Eti ooh, natoa zawadi ya laiki wa atakayenifurahisha.

Mshikaji wangu nanihii si nikamu'imajini kama Sisimizi, labda kwa sababu daily wenye nguvu wanampokonya Manzi.
Sista duu Mibanghe nikamuimajini kama Nguchiro, sijui kwa nini Yarabi.

Mamdogo Mashambani nikamuimajini kama Farasi, manake mishe mishe zake ni balaa. Eti siku hizi anauza dawa za kienyeji!
Kuna vijamaa nilivifikiria kama vindege vidogo vidogo, labda kwa sababu kila siku viko bize kutongoza huku mara kule.

Balaa ilikuwa Mshkaji wangu Baba Paroko, yeye nimemuimajini kama Tembo, halafu kumbe ulikuwa kifungoni arifu.. Pole!

Kuna visungura kadhaa niliviona pia kwenye Imajinesheni zangu, eti hadi hundred na kale kamkoa kapya ka kusini nimewafikiria kama Sungura, dizaini ni vijanja janja sana hivi vijamaa.

Kuna baadhi pia niliwafikiria kama Upepo, manake wakiamuaga huwa wanaweza kubadilisha kweli hali ya hewa humu Jamvini.

Kuna Sista Nanihii (za kupotea Bibie?) Yeye nilimuimajini kama Chui, manake ukimzingua huwa hakawii kukurukia shingoni.

Mimi mwenyewe nimejiimajini kama...

Hebu ngojeni, narudi.

Mapendo.
TANMO
 
Halafu kale kabrazameni kalikotunyang'anya yule Dada nimekaimajini kama fuko, yaani kanafukua fukua mpaka kanaharibia wenzake pozi.

TANMO
Hahahaaaaaaa TANMO huu utani wa ngumi aisee....na ntaendelea kufukua sio kwa Preta tu hata Bishanga muulize anajua maumivu yake!
Hebu lala sasa uone utaota nini tofauti na ganja
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimajinije mkuu? napenda mamiss na vitoto vya shule. mia

Mkuu yaani wewe nilikui'majini hivi:
Yaani wewe na mwenzako Mkoa Mpya Jirani na Rukwa..

Kuna visungura kadhaa niliviona pia kwenye Imajinesheni zangu, eti hadi hundred na kale kamkoa kapya ka kusini nimewafikiria kama Sungura, dizaini ni vijanja janja sana hivi vijamaa.
 
Back
Top Bottom