JF Focus: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Kwa vile mkuu Zomba ameomba nafasi ya kwenda masjid tunaenda mapumzikoni, tutarejea wote saa moja na nusu East African time (19:30 EAT).
Tutakapo rudi tutaendelea na swali la saba. Asanteni wote.

Tumepigiwa sim na Matola, anaomba mjadala uendelee kesho. Alijitolea kwa kuchangia katika mjadala huu kupitia internet cafe kwa muda wa masaa sita, ila sasa anaona it's getting too late. Kesho asubuhi nitarudi kuwajulisheni muda kamili wa kuendelea mjadala. In the mean time tuendelee kukusanya comment na masuali ya members wote katika thread ya "side comments"
 
Update muhimu:
Jamani wana JF kuna mambo ni personal zaidi, lakini hili lililonipata naona ni janga, mama yangu mzazi amefail step na alikuwa amefanyiwa oparesheni ya neuron surgeon sasa ametonenesha ile sehemu aliyofanyiwa oparesheni, nimeshinda MOI leo na sikuweza kufanya chochote, Nampenda Mama yangu siwezi kumteleza.

Natumia fursa hii kuwaomba radhi wana JF kwamba wanisamehe kwa kutokupatikana leo, nadhani kwa waelewa wanajuwa vyema uchungu wa Mama. Roulette mimi ndio nimerudi nyumbani sasa hivi wakati waliofunga wanajiandaa kupata daku. tusameheehane ndugu zangu, nina majonzi.
 
Kwa mara nyingine tena tunakutana kujadili tathmini ya mika saba ya utawala wa Rais Kikwete, mgeni rasmi ni zomba. Matola kaomba samahani kwanai ana matatizo ya kifamilia ambayo hayajamruhusu kuonekana ila atahojiwa pia pale atakapo pata nafasi. Tunamuombea mama Matola apone haraka.
Mkuu Zomba, kama upo tayari naomba utwambie ili tuendelee na swali la sita litakalo husika na tuhuma zinazotolewa dhidi ya Rais Kikwete na Ikulu kwa ujumla. Karibu mkuu zomba
 
Last edited by a moderator:
Swali la sita:

Kurugenzi ya Ikulu imekuwa ikijibu haraka sana tuhuma zinazotolewa dhidi ya Rais Kikwete na Ikulu kwa ujumla. Mifano ni zile taarifa za Wikileaks kuwa Rais alinunuliwa suti na pia tuhuma zilizotolewa na Godbless Lema kuwa Rais Kikwete alihusika kwa Lema kushindwa kesi yake na hatimaye kupoteza ubunge wake. Hata hivyo, kuna tuhuma nyigine tena nzito zaidi ambazo Rais Kikwete hajawahi kuzijibu. Mojawapo ni ile ya kuodhoreshwa na Dr Slaa katika orodha ya watuhumiwa 11 wa ufisadi pale Mwembeyanga. Mpaka sana Rais hujajibu tuhuma hizi nzito wala kuchukua hatua. Huoni ni vema Rais akatoa maelezo kwa kirefu kwa sababu tuhuma zilizotolewa ni nzito? Itakuwa kosa mtu akimuita Rais fisadi kwa kushindwa kujibu tuhuma za ufisadi zinazo na zilizokwishaelekezwa kwake? Naamini swali hili halitaleta hisia zozote mbaya kwa sababu fisadi ni neno ambalo hivi sasa linatumika vizuri hapa nyumbani.

Mkuu, una dakika kumi na tano kujibu swali hili, baada ya hapo tunaweza kuuliza swali la ufafanuzi au kuendelea moja kwa moja na swali la saba. Karibu Mkuu, na asante sana kwa uvumilivu na uelewa wako.
 
Nadhani dhanna nzima ya neno "fisadi" inakosa mshiko. Ikumbukwe kuwa ufisadi unaweza kuwa wa aina nyingi sana, ufisadi wa wizi, ufisadi wa ngono, ufisadi wa mali, ufisadi wa kuharibu tu, ufisadi wa kuchukuwa wake za watu.

Ukitazama kwa mantiki hiyo pana utaona mtu anarusha shutuma kuwa fulani ni "fisadi" lakini haainishi ufisadi wake ni nini. Huyo ni kama debe tupu haliishi kutika ni wa kumpuuza tu na hafai kujibiwa.

Ukitazama shutuma nyingine zilizojibiwa, kama ulivyozieleza hapo juu, utanielewa naongea nini, hizo zipo "specific". Lakini "general term" ya ufisadi ujibu ni nini? ufisadi upi?

Nadhani umenielewa.
 
Ningependa kuwakumbusha members wote kua wanaweza kuuliza maswali yao katika thread hii: (Link to the thread). Baada ya swali lakumi, tutachagua maswali tano kutoka thread hiyo na kumuuliza Mkuu Zomba. Karibuni.
 
Nadhani dhanna nzima ya neno "fisadi" inakosa mshiko. Ikumbukwe kuwa ufisadi unaweza kuwa wa aina nyingi sana, ufisadi wa wizi, ufisadi wa ngono, ufisadi wa mali, ufisadi wa kuharibu tu, ufisadi wa kuchukuwa wake za watu.

Ukitazama kwa mantiki hiyo pana utaona mtu anarusha shutuma kuwa fulani ni "fisadi" lakini haainishi ufisadi wake ni nini. Huyo ni kama debe tupu haliishi kutika ni wa kumpuuza tu na hafai kujibiwa.

Ukitazama shutuma nyingine zilizojibiwa, kama ulivyozieleza hapo juu, utanielewa naongea nini, hizo zipo "specific". Lakini "general term" ya ufisadi ujibu ni nini? ufisadi upi?

Nadhani umenielewa.
Nimekupata, ila naomba members watakao kua na swali kuhusiana na jibu lako waliwasilishe katika thread ya side comment. Tunaendelea na swali la saba.
 
Swali la saba, mkuu Zomba, una dakika kumi na tano tena, kwa kujibu swali hili:

Kumekuwa na maongezi ndani na nje ya nchi kuwa Rais Kikwete anasafiri sana nje ya nchi. Baadhi wanadai kuwa safari za Rais Kikwete hazina manufaa zaidi ya kuongeza matumizi kwa taifa. Nini maoni yako juu ta safari za Rais nje ya nchi? Unafikiri zina manufaa yoyote kwa taifa? Kama una "tangible data" tunaomba utoe pia.

Karibu mkuu.
 
Kweli kabisa, kwa mara ya kwanza katika tanzania tumeona Rais anaesafiri sana, si nje tu ya Tanzania bali hata ndani ya Tanzania.

Wengi wanasahau kuwa Dunia ya sasa ni kama kijiji, usafiri wa uhakika unaifanya dunia iwe ndogo.

Isitoshe, Tanzania kwa miaka kadhaa ya nyuma ilikuwa inafata mfumo wa kidiplomasia za siasa "political diplomacy". Kuanzia wakati wa Rais Mkapa mfumo huo ukaanza kubadilishwa taratibu kuelekea kwenye "Business Diplomacy" tukaona wawekezaji wa nje wanaanza kuingia nchini kwa kiasi kikubwa.

Muendelezo wa kasi zaidi, ari zaidi, nguvu zaidi wa falsafa ya "Business Diplomacy" ndio unamfanya Kikwete asafiri sana. Matokeo mema ni mazuri na mengi sana.

Tumeona Gas ikipatikana kutokana na mialiko na safari za Kikwete kwenda kuwahakikishia wawekezaji usalama wa Tanzania hiyo ni faida kubwa sana ya hizi safari.

Tumeona utalii ukikuwa:

Utalii ni Sekta inayokua kwa kasi na mchango wake kwenye pato la Taifa umekuwa ukiongezeka kila mwaka na kwa sasa ni zaidi ya asilimia 17.5. Aidha, sekta huchangia asilimia 25 ya mapato ya fedha za kigeni.
Source: Mali Asili na Utalii | Kikwete 2010

Na mengine mengi sana ambayo dakika kumi na tano haziruhusu kuyainisha yote lakini ikibidi ntayaainisha kwenye nyuzi ya side comments.

Kwa kifupi, safari za Kikwete zina tija na mafanikio makubwa sana ya ajabu. Unajuwa kuwa Tanzania tuna Hoteli Bora duniani ya mwaka jana? ipo Serengeti.

int.jpg
_44431919_bush_pres416ap.jpg
 
Asante kwa jibu hilo. Tutasubiri data zaidi kwenye nyuzi ya side comment. Nilipata pia habari ya hotel bora duniani inayo toa safari experience ya kipekee kabisa. Nina swali la ufafanuzi:
Ukichunguza msafara wa Raisi Kikwete utakuta mara nyingi unawatu wengi, je hao watu wote wana umuhimu? Pia kufatana na jibu lako political diplomacy inaonesha matunda mazuri ila kuna umuhimu wa kujiuliza kama safari hizo anahitaji kufanya Raisi Kikwete mwenyewe au leadership nzuri ingependeza angewawezesha mawaziri wake na wahusika wengine, yeye akaishia kutoa vision na muongozo. Sijui unasemaje kuhusu hili wazo ambalo tumeliona likirudi sana katika critics za safari hizi.
 
Msafara wa Kikwete una watu wengi sana, ukiondoa wale muhimu wa Serikalini wanaokuwezo kwenye msafara na kama nilivyoeleza huko juu, Rais anasisitiza katika "Business Diplomacy" na utakuta wengi wa wanaosafiri katika misafara ya Rais ni wafanya biashara wanaoalikwa amma "direct" kutoka Ikulu, au kupitia "chamber of commerce" au kupitia wizara ya viwanda na biashara au wizara ya utalii na mali asili. Mimi binafsi nimeshaalikwa sana na nilikuwepo kwenye msafara wa Rais ulioenda Brazil .

Kumbuka wafanya biashara wote tunaoalikwa tunaenda kwa gharama zetu, na ukifatana na msafara wa Rais faida za kukutana na wafanya biashara makini ni kubwa sana na opportunities ni nyingi na nzuri sana.

Kwa hili Kikwete anastahili kila sifa.
 
Swali la nane:

Hivi karibuni mbunge wa Ubungo Mh. John Mnyika alitamka bungeni kuwa tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete. Unadhani Rais Kikwete ni dhaifu na kwa nini?

Najua swali hili limejibiwa katika side comments, ila ingependeza ujibu tena na utoe ufafanuzi wako binafsi: je ikiwa kweli yeye ndie Rais bora wa Tanzania hadi sasa, unadhani ni kwanini watu wanamlalamikia sana Raisi Kikwete kuliko rais wengine wote kuhusu udhaifu wake na wa serikali zake?

Tuchukue dakika kumi na tano kujibu hili swali, halafu tuendelee na swali la tisa.
 
Kwanza kabisa demokrasia wakati wa Kikwete imekuwa pana zaidi kiasi watu wanaweza kuhoji kila kitu bila kubughudhiwa wala kukerwa.

Hili la udhaifu ulioongelewa na Mnyika mimi nalichukulia kama ukosefu wa adabu wa Mnyika na utoto wa kisiasa. Ningemshauri ajifunze kwa wazee wa upinzani kama kina Cheyo, Mrema, Mbatia, ambao yuko nao bungeni na huwaoni kuleta maneno ya kuudhi kujitafutia umaarufu.

Utawaona hao magwiji wa upinzani hata wanapotoa vijembe basi huwa vina mantiki na hata Rais anapenda kuwasikiliza kufanyia kazi ushauri na maoni yao.

Upinzani kazi yake ni moja. Kupinga lakini si kutukana, hapo Mnyika kakosea sana tena sana na kajishushia hadhi yake sana, kwa kauli kama hizo sidhani kama atapata kuwakonga nyoyo wale wasio upinzani. Ikiwa upinzani ni huo Tanzania basi wajuwe wana kazi kubwa sana.
 
Asante kwa jibu lako. Nikikusoma vizuri (karibu kunikosoa) naona unacho kipinga ni neno "dhaifu". Nikitumia hoja za Mh Mnyika nabadili swali na kuuliza: Je unadhani "mapungufu" ya Raisi Kikwete pamoja na serikali yake yanaweza kua ni sababu ya Tanzania kufika hapa tulipo (Assumption yake ilikua hapa tulipo tuna hali isio kua nzuri sana)? Kama sio Raisi Kikwete na serikali zake (kuanzia 2005), nani alaumiwe?
 
Unajuwa ukisema mapungufu hapo mimi nakuwa sikubali kwanini isiwe jitihada za Serikali yake. Sidhani kama upinzani duniani utakosa kukosoa hata mafanikio, hiyo ndio kazi ya upinzani tena ni "Rasmi".

Lakini ukitazama data na ukweli utaona kuwa kuanzia mwaka 2005 kila takwimu (pitia baadhi nimeziainisha juu huko) na ukweli unaonesha ni mafanikio makubwa yakuvunja rikodi za awamu zote za kabla yake katika kila nyanja, kwanini hilo hatulisemi na kulisifu? kwa kuwa ni upinzani tu?

Natamani aje mmoja hapa anioneshe mbona hapa Kikwete hakufanya jema zaidi kama Rais fulani wa kabla yake. Mpaka leo sijapata wa hilo.
 
Back
Top Bottom