JF Focus: Tathmini ya Utawala wa Rais Kikwete (2005-2012)

Mwali kwa sabab swali la kwnza linahusu na michezo pia, hapa nitakuwa muongo na mnafki kama sitompongeza Rais Kikwete kwa kuamsha upya morari ya Watanzania katika kuipenda timu yetu ya Taifa na kumleta kocha Maximo, kwenye sekta ya michezo hili nampa Rais JK kudos.

Sekta ya barabara sintoiongelea kwa sababu kinachofanyika sasa ni kuzinduwa miradi ambayo iliasisiwa na Mkapa akiwa na Jembe lake Magufuri, Rais Kikwete hana lolote la kujivunia kuhusu sekt ya barabara za nchii zaidi ya kubebeshwa lawama pale alipomuondow Magufuri wizara ya ujenzi na kasi ya ujenzi wa barabara ukapunguwa.
 
Asante Mkuu Matola kwa majibu yako, muda wako umeisha. Sasa namkaribisha Mkuu Zomba kumuuliza Matola swali la ufafanuzi wa majibu alio toa kwenye swali hili la kwanza. Mkuu, una dakika tano kuuliza swali lako. Baada ya hapo, tutaendelea na swali la pili.

Karibu Mkuu Zomba.
 
Asanteni wote, Kana mna mengine kuhusiana na swali hili la kwanza mtandelea kujibu baada ya mjadala huu, sasa tunaendelea na swali la pili
 
Swali langu la pili, ataanza kujibu mkuu Matola:

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, Rais Kikwete alitoa ahadi nyingi tuu ambazo alisema atazitekeleza kama angechaguliwa kuwa Rais. Baadhi ya hizo ahadi zimeonyereshwa Jukwaa la Siasa. Je, unafikiri anaweza kutekeleza ahadi zote alizotoa kabla ya uchaguzi mkuu ujao?

Mkuu, una dakika kumi na tano kujibu swali hili, baada ya hapo nitamkaribisha Zomba. Karibu Matola.
 
Swali langu la pili, ataanza kujibu mkuu Matola:

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, Rais Kikwete alitoa ahadi nyingi tuu ambazo alisema atazitekeleza kama angechaguliwa kuwa Rais. Baadhi ya hizo ahadi zimeonyereshwa Jukwaa la Siasa. Je, unafikiri anawea kutekeleza ahadi zote alizotoa kabla ya uchaguzi mkuu ujao?

Mkuu, una dakika kumi na tano kujibu swali hili, baada ya hapo nitamkaribisha Zomba. Karibu Matola.

Ndugu wana JF hapa huitajiki kuwa Political analyst kujuwa kwamba hapa JK aliwatapeli Watanzania kwasababu alijuwa wazi yeye akishapata Urais hatorudi tena kuomba Uongozi. Huu ni Uhuni na uwongo mtupu.

HIZI NDIZO AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI:-


  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Asante kwa jibu lako, sasa namkaribisha mkuu Zomba kujibu swali la pili. Mkuu, una dakika kumi na tano kujibu swali hili (unaweza kutumia post zaidi ya moja ila tafadhali usizidishe muda). Karibu.
 
Swali langu la pili, ataanza kujibu mkuu Matola:

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, Rais Kikwete alitoa ahadi nyingi tuu ambazo alisema atazitekeleza kama angechaguliwa kuwa Rais. Baadhi ya hizo ahadi zimeonyereshwa Jukwaa la Siasa. Je, unafikiri anaweza kutekeleza ahadi zote alizotoa kabla ya uchaguzi mkuu ujao?

Mkuu, una dakika kumi na tano kujibu swali hili, baada ya hapo nitamkaribisha Zomba. Karibu Matola.

Ahadi zote za Rais zimetekelezwa sioni hata moja ambayo haijatekelezwa kwa hatua fulani au nyingine.

Kama kuna mtu ana ahadi ambayo haijatekelezwa aainisha hapa. naona Matola kaweka list ya vitu 69, ambayo ni kidogo sana kutokana na ahadi za Rais. Kikwete anatekeleza mengi sana zaidi ya ha yo 69.

Wengi hawaelewi kuwa ahadi ya Rais ni agizo kwa watendaji, sasa hesabu wilaya zote na kila wilaya imeahidiwa na zote zinatekelezwa.

Sioni hata moja amabyo haitekelezwi mpaka sasa, jee kuna anaeijuwa?

Kuna zingine zimekuwa ni World Record, mfano alipoahidi chuo Kikuu Dodoma, kilichukuwa exactly miaka miwili kuanza kuchukuwa wanafunzi toka kuahidiwa.
 
Asante sana kwa jibu lako mkuu Zomba.

Matola, kama unavyoona hapo juu, Mkuu zomba anasema kua hizo ahadi 69 ulizo taja kwenye post zako zimesha tekelezwa. Je kuna ahadi yoyote haija tekelezwa utufafanulie? Una swali lolote la kumuuliza Zomba kufatana na jibu lake? una dakika tano kupost swali lako. Karibu.
 
Mkuu Matola, tunakuongezea dakika tatu za kumuuliza Zombaa swali la ufafanuzi wa majibu yake. Kama huna tafadhani jitokeze, tuendelee na upande wa Zomba, kama atakua na swali kwako, lenye kuhusiana na ahadi a Rais Kikwete. Karibu mkuu Matola.
 
Ni matumaini yetu kua Matola (ambae aliomba radhi kwa matatizo alio pata na computer yake) atauliza swali la ufafanuzi mwisho wa mjadala huu, tunajaribu kuokua muda. Sasa tunamkaribisha mkuu Zomba kumuuliza Matola swali la ufafanuzi wa jibu lake la pili. Tunampa dakika tano kuulia swali hilo. Karibu Mkuu.
 
Ndugu wana JF hapa huitajiki kuwa Political analyst kujuwa kwamba hapa JK aliwatapeli Watanzania kwasababu alijuwa wazi yeye akishapata Urais hatorudi tena kuomba Uongozi. Huu ni Uhuni na uwongo mtupu.

AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...


  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora

Mwali naomba ruksa nimjibu kila alchobandika Matola hapo kimoja kimoja kila tunavyoendelea, na kwa ushahidi kabisa kuwa ahadi zinatekelezwa, naanza na hiyo ya kwanza na ushahidi huu hapa kuwa inatekelezwa, "feasibility study tayari":

http://www.dailynews.co.tz/index.php/parliament-news/7700-railway-line-rehabilitation-to-cost-41bn

The proposed new railway line to connect Rwanda and Burundi to Tanzania's port of Dar es Salaam has reached implementation stages.
 
Ni matumaini yetu kua Matola (ambae aliomba radhi kwa matatizo alio pata na computer yake) atauliza swali la ufafanuzi mwisho wa mjadala huu, tunajaribu kuokua muda. Sasa tunamkaribisha mkuu Zomba kumuuliza Matola swali la ufafanuzi wa jibu lake la pili. Tunampa dakika tano kuulia swali hilo. Karibu Mkuu.

Mimi sina swali kwa Matola ila namkumbusha tu kuwa hiyo listi yake mbona ni ndogo sana, Mheshimiwa Rais ana ahadi nyingi sana kuliko hizo anazozitekeleza. Moja ambayo ameisahau ni ile kubwa kuliko zote "Hafi mtu kwa Njaa" Tanzania.

Naona kaisahau hiyo. Nataman ningekuwa na muda nimkubushe zote, ni nyingi sana zaidi ya hizo 69 alizoweka yeye na zote zipo katika awamu fulani ya kutekelezwa.
 
Mwali naomba ruksa nimjibu kila alchobandika Matola hapo kimoja kimoja kila tunavyoendelea, na kwa ushahidi kabisa kuwa ahadi zinatekelezwa, naanza na hiyo ya kwanza na ushahidi huu hapa kuwa inatekelezwa, "feasibility study tayari":

http://www.dailynews.co.tz/index.php/parliament-news/7700-railway-line-rehabilitation-to-cost-41bn
Kwa sababu ahadi ni nyingi na kwa vile Matola hakuuliza swali la ufafanuzi, naomba tuendelee na maswali mengine, unaweza kupost huo ushahidi baada ya mjadala kumalizika. Kwa sasa tunaendelea na swali langu la tatu ambalo utaanza kujibu wewe.
 
Swali langu la tatu ni kwa Mkuu Zomba, ambae ana dakika 15 kulijibu:

Akihojiwa na gazeti la Washington Post hivi karibuni, Rais Kikwete alisema kuwa tatizo kubwa linalomkabili ni upungufu wa resources. Rais alisema kama akipata dola bilioni moja kwa mwezi kama mapato ya serikali, anataifanya Tanzania kuwa mbingu. Unakubaliana na Rais kuwa tatizo linalomkabili kama Rais ni lack of resources? Unadhani akipewa hizo bilioni moja kila mwezi anaweza kuifanya Tanzania kama mbingu?

Karibu Mkuu Zomba
 
Ndugu wana JF hapa huitajiki kuwa Political analyst kujuwa kwamba hapa JK aliwatapeli Watanzania kwasababu alijuwa wazi yeye akishapata Urais hatorudi tena kuomba Uongozi. Huu ni Uhuni na uwongo mtupu.

AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini


From NESTORY NGWEGA in TANGA, 3rd December 2011 @ 12:17, Total Comments: 0, Hits: 480

Tanga regional administration has allocated special areas for investment in order to attract investors in the industrial sector to industrialize and revive the region's economy in the coming few years.

Areas which have been allocated are Mwambani with 25 hectares, Neema special economic zone 400 hectares, Gofu industrial area 15 hectares and industrial park in Pongwe 20 hectares.

Inaugurating celebrations to mark fifty years of independence in Tanga Region on Saturday, Tanga Regional Commissioner, Chiku Gallawa, said that the government is making extra efforts to revive the industrial status of the region to become famous as it was shortly after independence.

"Deliberate efforts are being taken to revive industries in the region, we want to restore the old industries and at the same time to attract investors for new industries. This is possible and we need to work together and create a friendly environment for investors," he said.

Soma zaidi:Daily News | Tanga set to revive industries
 
Back
Top Bottom