JF Focus: Side Comments: Exclusive Interview with JamiiForums founder - Maxence Melo

Status
Not open for further replies.
Just ask. Kwa leo atajibu yale yalio pokelewa mwanzo ila baadae akipata muda anaweza kuendelea kujibu pole pole.

alright, nauliza hivi; kuna adhabu ya ban ambayo hutumiwa kama namna ya kumrekebisha tabia mtu pale anapovunja sheria jukwaani. Adhabu hii pia ni source mojawapo kubwa ya multiple IDs hivyo kwa namna moja au nyingine jf mnaweza kuwa na takwimu ambazo si sahihi kwa idadi ya users. Unaongeleaje hapo? Napendekeza mfikirie namna nyingine ya adhabu na sio ban.
 
King'asti ......Mwanangu labda sijaelewa, Je na sisi wadau tunaruhusiwa kuuliza maswali au tunatakiwa kutulia na kunywa kahawa huku tukishuhudia ukiendelea na interview yako.........?
 
Last edited by a moderator:
King'asti ......Mwanangu labda sijaelewa, Je na sisi wadau tunaruhusiwa kuuliza maswali au tunatakiwa kutulia na kunywa kahawa huku tukishuhudia ukiendelea na interview yako.........?

Ndio mkuu Mtambuzi na nyie mnaruhusiwa kuuliza maswali kwenye hii thread ya side comments na sio kule kwenye interview.
 
Last edited by a moderator:
Ahsante sana Mods wote na King'asti kwa uendeshaji wa zoezi hili....

Ningependa kuwa msomaji tu zaidi, ila itanipendeza kujua kuhusu suala la "
Mapato ya JF"

Max, mna mipango gani zaidi ya kuboresha mapato?

Nina uhakika hii ni changamoto kubwa, na pia ni kweli michango yetu subscriptions haijitoshelezi sana ukilinganisha na kazi mnayopiga na mahitaji ya JF kwa ujumla....!

Mungu awatangulie sana mzidi kuwa wajasiri katika yote!
 
Suali zuri sana jG. Litajumuishwa.
 
SWALI1: Ninapoangalia JF kila siku inafikia hadi visitors elfu 14 plus kwa kila siku.Je, kama Founder wa JF ulitarajia kitu kama hiki? Na kama hapana, unajisikiaje ukiona JF inavyopanda chati kiasi hicho.
SWALI2: Hivi karibuni imeonekana kwamba JF ni chanzo kikubwa cha habari kwa media hapa Tanzania, na baadhi ya media(esp.print media) zimediriki ku-copy na kubadilisha lugha kidogo katika kile kilichoandikwa JF,kama Founder unajisikiaje kuona JF inakuwa 'mhimili' wa habari Tanzania.
Asante sana.
 
Swali kwa Max: JF ni jukwaa huru na slogan yetu ni 'WHERE WE DARE TALK OPENLY' lakini wadau wengine wanapofunguka wanakula BAN, je huoni kama ni kukandamiza uhuru wa maoni?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom