JF Focus: Interview with Maxence Melo

Good question. Suala la usalama wa JF Owner, bila shaka limerekodiwa, na likichaguliwa litajibiwa hapa hapa.

hili ni swali muhimu kwa sababu kumekuwepo na accusations nyingi kutoka kwa viongozi dhidi ya jf.wanashindwa kutambua umuhimu wa maoni ya wanajf ambayo hayawezi kuelezwa maofisini au mikutano ya kitaifa.
 
Noted mkuu.
 
Pongezi wameshatoa wengi, swali langu ni kuwa how is JF funded? If its through conteibutions or otherwise, would you be kind to indicate all of its funding sources and or provide audited financial reports at least annually?

Note: I am askingnthis because JF has been associated with several prominent political figures and or parties particularly, when a several topics are deleted or edited without consent of the primary author or a member with ' mlengwa wa kushoto' ideas is banned!
 
Roulette,
Kwanza nawapa pongezi za dhati Maxence Melo, Mike McKee, Invisible, na Mods wote wa JF pamoja na members wote wa JF kwa kuifikisha hapa JF na inaendelea kukuwa kasi.

Roulette, kuna umuhimu sasa kuwaalika wanasiasa ambao ni members humu JF (Verified User) kutoka vyama vyetu vya siasa kufanya Interview humu JF kwa mpangilio wa masuali kutoka kwa members wa JF.

JF Daima
 
Last edited by a moderator:
Binafsi natoa pongezi za dhati kabisa kwa Maxcence Mello na uongozi wote kwa ujumla.Kiukweli baadhi yetu tunaiamini JF kama source ya ukweli kwa habari yoyote,binafsi kipindi JF ilipofungwa kwa matengenezo nilikuwa kama mgonjwa vile. Hakika JF iko ndani ya damu!

Sasa Swali: Imetokea baadhi ya watu wanajiunga na JF kwa nia mbaya ili kuuchafua mtandao huu uonekane hauna maana. Njia wanazotumia kuuchafua mtandao huu ni kuleta tuhuma za uongo dhidi ya watu wengine hasa wale wanaopendwa na jamii ili wachafuke. Tuhuma hizo zinakuwa hazina source yoyote ya habari sasa je Uongozi utatumia njia zipi kukomesha hali hii?

Na swali la Nyongeza Uongozi utatumia njia gani kudhibiti watu wanaosajili ID nyingi tofauti ambazo zinakuwa ni maalum kujadili na kuchafua baadhi ya watu?
 
Ahsate sana Roulette kwa thread hii muhimu sana,

Kwanza kabisa, nakupongeza wewe na wakuu wote katika timu ya uendeshaji wa JF (chini ya kamanda Max) kwa kazi ngumu ila muhimu sana mnayofanya ya kuiendesha, tena kwa mafanikio makubwa. Huwa mara nyingi nasema kwamba, hata kama mambo mengi yanatushinda na tunaonekana vilaza/viazi (wajinga wa kutupa), JF imeonesha pasipo shaka kwamba Watanzania tunaweza kubuni na kutekeleza mambo yetu kwa kiwango cha juu kabisa cha mafanikio!!

Pili, naomba nikiri kuwa mimi binafsi nimekuwa nikiguswa sana na JF kama network na manufaa ambayo sisi members na wadau wengine wanayapata. Hata hivyo, ningependa kujua mpango mkakati wa kibiashara wa JF (JF business strategic plan) kwa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu (short term, medium and long term business strategies) ambazo zitaonesha jinsi management ilivyojipanga kuhakikisha hili jukwaa halifi kama policies zetu including ujamaa zilivyokufa kifo cha ajabu ajabu.

Pia, naomba Max atueleze ni kwa jinsi gani management ya JF imejipanga kuwashirikisha members katika kuipa uhai JF (financing and running) ili kuwapunguzia mzigo wadau wachache ambao wamekuwa wanatumia muda wao na resource zao nyingi kuhakikisha JF inaendelea kuwepo hewani!

Naomba niishie hapa ili wadau wengine waongezee!
 
Last edited by a moderator:
Roulette,
Kwanza nawapa pongezi za dhati Maxence Melo, Mike McKee, Invisible, na Mods wote wa JF pamoja na members wote wa JF kwa kuifikisha hapa JF na inaendelea kukuwa kasi.

Roulette, kuna umuhimu sasa kuwaalika wanasiasa ambao ni members humu JF (Verified User) kutoka vyama vyetu vya siasa kufanya Interview humu JF kwa mpangilio wa masuali kutoka kwa members wa JF.

JF Daima
Asante sana kwa pongezi Mkuu wangu. Nadhani limewafikia wahusika, na mimi kama Mod na kama member nalipokea kwa mikono miwili.

Wazo lako ni nzuri sana, na kwa sasa tupo katika mazoezi ya kuendesha live interviews na live debates. Tulianza na tathmini ya utawala wa kikwete, tukawashirikisha wakuu zomba na Matola. Mjadala uliendelea vizuri hadi pale tulipopata matatizo ya kifamilia. Hata Hivo Mwali na Zomba walijitahidi na wakamaliza maswali yote bila shida, na members wote waliridhika (to some extent).

Leo tunaingiza utaratibu wa interview, na kesho tunaweza kuleta article na kuwaalika members wawili, watatu au wanne waje kuchambua hiyo article kwa mtindo wa debate vile vile. Yote haya ni katika kujaribu kuifanya JamiiForums kua interactive zaidi. Mwanzo wote ni mgumu ila practice makes perfect. Asante sana kwa mchango.
 
Last edited by a moderator:
kuna habari nyeti zinaletwa hapa janvini lakini ndani ya muda mfupi zinafutwa bila maelezo ya kutosha..hali hii inatia shaka sana.. Kwa mfano habari za kiuchunguzi kuhusu kutekwa kwa Dr.ulimboka hapa ni marufuku kabisa..uhuru wa kutoa maoni huko wapi maxence melo?
Pia kuna juhudi nyingi za kutaka kuifuta jamiiforum,tumesikia mara mbili bungeni likisemwa hili.. Umejipangaje mkuu..?
 
Binafsi natoa pongezi za dhati kabisa kwa Maxcence Mello na uongozi wote kwa ujumla.Kiukweli baadhi yetu tunaiamini JF kama source ya ukweli kwa habari yoyote,binafsi kipindi JF ilipofungwa kwa matengenezo nilikuwa kama mgonjwa vile.Hakika JF iko ndani ya damu!
Sasa Swali: Imetokea baadhi ya watu wanajiunga na JF kwa nia mbaya ili kuuchafua mtandao huu uonekane hauna maana.Njia wanazotumia kuuchafua mtandao huu ni kuleta tuhuma za uongo dhidi ya watu wengine hasa wale wanaopendwa na jamii ili wachafuke.Tuhuma hizo zinakuwa hazina source yoyote ya habari sasa je Uongozi utatumia njia zipi kukomesha hali hii? Na swali la Nyongeza Uongozi utatumia njia gani kudhibiti watu wanaosajili ID nyingi tofauti ambazo zinakuwa ni maalum kujadili na kuchafua baadhi ya watu?
Bila shaka pongezi lako kwa uongozi wa JF limefika. Suali lako hili limekua likirudi mara kwa mara, nadhani litachaguliwa katika masuali kumi ya kumuuliza mkuu Maxence. Asante sana Molemo
 
Good idea
first sijaona Kinga'sti akirespond na hii thread
why? tusije fika siku hiyo halafu hayupo?

Pili swali langu kwa uongozi wa JF....ni kuhusu member wa zamani William le Mutuz...

What really happened between JF na William?

je walimfukuza?alijitoa?why?
 
Pongezi wameshatoa wengi, swali langu ni kuwa how is JF funded? If its through conteibutions or otherwise, would you be kind to indicate all of its funding sources and or provide audited financial reports at least annually?

Note: I am askingnthis because JF has been associated with several prominent political figures and or parties particularly, when a several topics are deleted or edited without consent of the primary author or a member with ' mlengwa wa kushoto' ideas is banned!

Mkuu, suali lako limefika. I really hope to see it in the list of the top ten questions.
 
Ahsate sana Roulette kwa thread hii muhimu sana,

Kwanza kabisa, nakupongeza wewe na wakuu wote katika timu ya uendeshaji wa JF (chini ya kamanda Max) kwa kazi ngumu ila muhimu sana mnayofanya ya kuiendesha, tena kwa mafanikio makubwa. Huwa mara nyingi nasema kwamba, hata kama mambo mengi yanatushinda na tunaonekana vilaza/viazi (wajinga wa kutupa), JF imeonesha pasipo shaka kwamba Watanzania tunaweza kubuni na kutekeleza mambo yetu kwa kiwango cha juu kabisa cha mafanikio!!

Pili, naomba nikiri kuwa mimi binafsi nimekuwa nikiguswa sana na JF kama network na manufaa ambayo sisi members na wadau wengine wanayapata. Hata hivyo, ningependa kujua mpango mkakati wa kibiashara wa JF (JF business strategic plan) kwa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu (short term, medium and long term business strategies) ambazo zitaonesha jinsi management ilivyojipanga kuhakikisha hili jukwaa halifi kama policies zetu including ujamaa zilivyokufa kifo cha ajabu ajabu.

Pia, naomba Max atueleze ni kwa jinsi gani management ya JF imejipanga kuwashirikisha members katika kuipa uhai JF (financing and running) ili kuwapunguzia mzigo wadau wachache ambao wamekuwa wanatumia muda wao na resource zao nyingi kuhakikisha JF inaendelea kuwepo hewani!

Naomba niishie hapa ili wadau wengine waongezee!
Asante sana Babu kwa pongezi lako, na suali lako linaingika katika list ya masuali. Mwisho masuali mengine, kama hili na la mkuu MLOsi K. Mlutumbi zinaweza kuunganishwa ili kupunguza idadi ya masuali. Asante sana mkuu
 
Last edited by a moderator:
Roulette,
Kwanza nawapa pongezi za dhati Maxence Melo, Mike McKee, Invisible, na Mods wote wa JF pamoja na members wote wa JF kwa kuifikisha hapa JF na inaendelea kukuwa kasi.

Roulette, kuna umuhimu sasa kuwaalika wanasiasa ambao ni members humu JF (Verified User) kutoka vyama vyetu vya siasa kufanya Interview humu JF kwa mpangilio wa masuali kutoka kwa members wa JF.

JF Daima

Naunga mkono hoja! Nakumbuka mwaka jana alialikwa Dr. P. W. Slaa na ilikuwa nzuri sana licha ya mapungufu yaliyojitokeza. Mwenzetu Faiza Fox alipigwa ban kwa kuporomosha matusi ya nguoni kwa mgeni wetu baada ya kushindwa kuhimili hisia zake. Namshukuru mgeni kwa kuelewa na kumpuuza ingawa haikumsaidia FF kuepuka ban. Nawaomba tu tuzihimili hisia zetu hasa tunapokuwa na mgeni wa itikadi tofauti na zetu. Otherwise ni utaratibu mzuri na utafaida sana kwetu!
 
Last edited by a moderator:
nawaombea msamaha malaria sugu na faiza foxy(Jf contrevesial iconic figures).Je max yupo tayari kuwafungulia?
Swali la mwisho;Jf iko kwa maslahi ya nani?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Thats a very good thing to do. Congratulations Max and the whole team. Ni kitu cha kufurahisha sana kuona hii social network tuliyoanza nao kitambo imeweza ku stand the test of time and still be THIS STRONG and continue to be stronger.
Nakumbuka palikua na Darhotwire, Young African zote zikiwa zimeanzishwa kabla ya JF lakini ziko wapi!!!??

May I please make the following remark:-

The success of any social network relies on the members, I dare say more than the owner and moderators as significant as there work might be. There are certain key members that, in their unity (an unconsciously formed union it might be) have managed to pull many others and made this the most interesting and exciting forum in EAST AFRICA. I believe the secret to JF success lies in the characters and contributions of many of it's members though I am not trying to demean the extraordinary work done by the moderators in any way.

Having said this, I also believe that the death of JF will also be as a result of it's members as well. This demise will be brought by the following ways:-

1. Having an over crowding of I.D.I.O.T.S. Since it is very unfortunate that we can not filter who is able to join and comment in the forum, we have ended up being bombarded by nincompoops with ignoramus comments. This has discouraged the rate of "intelligent" people joining the forum as compared to THE OTHERS.
Indeed if it wasn't for the likes of ..........(there are many and mentioning a few might discourage the rest :) ) with there intelligent and thought provoking topics, posts,arguments and debates JF would have been HISTORY.

In addition these imbecilic comments and topics have the potential of making the forum appear LESS SERIOUS in the future.
I am sure we have seen people say things like "Imekua kama FB sasa" au "embu mwone huyu anafikiri hapa FB", hii yote inaonyesha ni upande gani JF inataka kuangukia.
Max, I wasn't there with you when you decided to start this network, neither can I claim an ounce of credit or direct contribution to this great achievement of yours, but what I can dare say is that I have an inclination of what I believe you had in mind when starting this, (How presumptious eh!!!) or at least what I would like to see in JF.

Now, if you, like me, believe that we have the above narrated threat be kind enough to consider my proposal. Can we give more key members in particular forums the ability to VOTE for or against the posting of a particular topic or post. i.e. instead of this matter being left solely to the moderators, certain members can be given VOTING POWER and a members credit or discredit for that matter can be achieved by the number of meaningful comments and topics he/she has contributed in certain forums.
This involvement of members will sure revitalize and positively contribute to the growth and credibility of our forum!

There are more details to this idea of mine and I am sure people will have many questions, however if you agree on the principle of the matter, halla, and we can continue the exchange.

Oh I was supposed to ask a question. Ok. So Max what do you think of the principle of the idea, we at JF are champions of Democracy shouldn't we be practicing it here, Power through the ballot box???

All in all GOOD WORK GUYS, HASTA LA VICTORIA SIEMPRE, JF 4 LIFE!!!! WHERE WE DARE TALK OPENLY!!
 
Naunga mkono hoja! Nakumbuka mwaka jana alialikwa Dr. P. W. Slaa na ilikuwa nzuri sana licha ya mapungufu yaliyojitokeza. Mwenzetu Faiza Fox alipigwa ban kwa kuporomosha matusi ya nguoni kwa mgeni wetu baada ya kushindwa kuhimili hisia zake. Namshukuru mgeni kwa kuelewa na kumpuuza ingawa haikumsaidia FF kuepuka ban. Nawaomba tu tuzihimili hisia zetu hasa tunapokuwa na mgeni wa itikadi tofauti na zetu. Otherwise ni utaratibu mzuri na utafaida sana kwetu!

Asante sana mkuu. wakati wa tathmini ya utawala wa Rais Kikwete tulifanya utaratibu wa thread mbili, moja ya members wote na nyingine ya wahusika tu (yani debaters na moderator wao wa siku hiyo). Na members wote walitoa ushirikiano mkubwa katika zoezi hilo. Tunaendelea kuboresha taratibu za interview, na inshallah tunaweza tukawaita verified members wengi zaidi kujadili masuala nyeti ya siasa ya nchi.
 
Good idea
first sijaona Kinga'sti akirespond na hii thread
why? tusije fika siku hiyo halafu hayupo?

Pili swali langu kwa uongozi wa JF....ni kuhusu member wa zamani William le Mutuz...

What really happened between JF na William?

je walimfukuza?alijitoa?why?

Suali lako limefika mkuu. Kuhusu King'asti, Jina lake lilitolewa in advance tukiamini kuwa ataweza ingawa possibility ya kutowezekana sababu ya technical problems she has been experiencing lately pia ipo. Ikitokea anaweza tutashukuru sana ila ikitokea kuwa hataweza kutakuwa hakuna jinsi na atawakilisha mwana jf mwengine. So far kuna mtu kapewa hio responsibility ya kuwasiliana nae akileta feedback tutawasilisha.
 
Last edited by a moderator:
Niwashukuru timu nzima ya Jf,pamoja na Maxence mello mwenyewe,Tokea nimejiunga na Jf nimebadilika sana kimawazo kimtazamo na nimekuwa mfatiliaji mzuri wa mijadala..Jamiiforums ni mwisho, Pia napenda ujamaa uliopo humu,watu tunafahamiana hata bila kujuana sura hili ni jambo la heri sana.

swali langu ni
1. kwanini Wana jf wengi hupenda kuficha uhalisia pindi wanapoanza kujisajiri?
2. Ni kweli Utakapo tumia jina lako la ukweli unaweza pata matatizo kutokana mada nzito na mwiba kwa serikali zinazojadiliwa humu.
Maoni.
Ni wakati muafaka wa kuanzisha jamiiforums Tv.Hii itasaidia kuwa alika member na kufanya live mjadara ndani Jf Tv.
 
Back
Top Bottom