JF FC-The Dream Team

timu imeshavunjwa baada ya kuona hawa waliochaguliwa wanacheza kama mwaikimba. maximo(balantanda) bado hajaita kikosi kipya. je wapenda nani atoke nani aingie?. Mia
 
Baada ya Stars kutolewa nimeona ni bora tuanzishe Stars yetu mbadala ndani ya JF ambayo nina uhakika hata ikienda Bondeni mwakani lazima kombe la Dunia lije Bongo......Timu hiyo ni kama ifuatavyo: 1.Share…..(Huyu bwana nimeangalia kwenye ile thread ya CHAN Live alikuwa upande wa Dihile sana,hope atatusaidia sana golini,atakuwa kama Juma Pondamali vile).
2.Shadow(Huyu yeye namfananisha na David Mwakalebela yaani).

3.Mwazange(Huyu atatupa vitu vya mzee mzima Alphonce Modest).

4.Bubu Ataka Kusema( mkoba wenyewe huu kama Salum Kabunda ‘Ninja’).

5.Belo( Hiki ni kisiki kama George Magere Masatu).

6.Invisible(Huyu ni Kiungo mkabaji mithili ya Hayati Method Mogella ‘Fundi,yeye ndiye Nahodha wa JF FC).

7.Masanilo( Winga tereza wa upande wa kulia,yeye anacheza kama Abubakar Salum ‘Sure Boy’).

8.Mfumwa(Huyu ni kiungo mshambuliaji yeye atacheza mithili ya Hussein Aman Marsha).

9.YoYo(Huyu ni mshambuliaji wa kati mwenye uchu wa magoli mithili ya Zamoyon Mogella,tutegemee magoli mengi jamani).

10.Hofstede(Atamsaidia YoYo pale mbele kumalizia mipira ya vichwa itakayotoka winga za pembeni,pia atamalizia krosi,atacheza kama Abeid Mziba ama Innocent Haule).

11.Icadon(Winga ya kushoto huyu,yeye atacheza kama Edy Lunyamila).


Reserves: Mkama P(GK),Mzalendo Halisi,Amwanga,Kana Ka Nsungu,KGM,Invincible,Alpha na Pasco…


Manager wa timu atakuwa Nziku akisaidiwa na mzee mzima Ben na YourNameIsMine(kocha wa makipa).


Kamati ya Ufundi itaongozwa na Mzee Mwanakijiji akisaidiwa na Mzee wa Gambosh Nyani Ngabu,wajumbe wengine wa kamati watakuwa ni: Rev.Kishoka,Mkandara,FMES,Kuhani,Mkandara na Mpaka Kieleweke.


Kamati ya saidia JF FC ishinde itaongozwa na Mama akisaidiwa na First lady,pia watakuwepo Belinda Jacob.Kelly01,Neemah,Philemon Michael,GT,Balantanda mwenyewe,Susuviri ,Son of Alaska,Mtanzania,Nyambala,Mwikimbi,Mbu na Maxence Mello…


YALE YALE MAMBO SIMBA NA YANGA.......SIE PRISONS,MTIBWA TUNAITAJI KAZI


ahaaa JF DREAM TEAM.....
 
Back
Top Bottom