JF Exclusive: UVCCM Yajibu vikali Magazeti ya Raia Mwema na Mwanahalisi - Yasema Yamezua habari!

Je si ingekuwa vema wakajibu hata malalamiko ya Mwakyembe alitoa kuh kutishiwa usalama wake???
 
Raia Mwema - Muungwana ni Vitendo

Vijana wawalipua Lowassa, Rostam

?

Machi 23, 2011

?

Mwandishi Wetu

??Wamo pia Sitta, Makamba na Dk. Magufuli

??Wadaiwa wanaipunguzia umaarufu CCM

??DC aambiwa asifikiri kwa tumbo, atumie bongo

BAADHI ya wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wanawaona Edward Lowassa na Rostam Aziz kuwa sababu ya kuporomoka kwa umaarufu wa chama chao.

Maoni hayo yalijitokeza katika mkutano wa baraza hilo uliomalizika Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.

Wote, Lowassa na Rostam wanahusishwa na kampuni ya kufua umeme ya Richmond ambayo ndiyo chanzo cha Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu Februari 2008 na Rostam, Mbunge wa Igunga na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM anahusishwa na kampuni mrithi wa Richmond, Dowans iliyompa nguvu za kisheria* ya kuendesha shughuli zake.

Aliyeamua* “kujilipua”* na kujitwisha mzigo wa kueleza maoni hayo ni Mrisho Gambo, ambaye ni Mjumbe wa Baraza Kuu wa Mkoa wa Arusha* na wakati akitoa dukuduku lake*hilo alishangiliwa sana na wajumbe**wenzake ambao awali walibaki kimya wakisikiliza kwa shauku.

Vyanzo kadhaa vya habari vimeiambia Raia Mwema ya kuwa Gambo*alieleza bayana kuwa vigogo hao ndio waliokipunguzia mvuto CCM hasa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Lakini habari hizo zinasema pia kwamba* maoni hayo ya Gambo yalipingwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo ambao ulidhihirisha wazi kuwapo mgawanyiko miongoni mwa wajumbe.

Gambo alipingwa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isaac, akisaidiwa na Hussein Bashe, ambaye katika mkutano huo alitangaza kuwa ana maslahi na Rostam kwa kuwa ni mwajiri wake. Isaac ni mjumbe wa Baraza hilo kutoka kundi maalumu la Wazazi.

Lowassa, Rostam tatizo

Kwa mujibu wa habari hizo, Gambo alisimama kuzungumza wakati wa mjadala wa changamoto zinazoikabili UVCCM na kueleza kuwa wazungumzaji wengi katika mkutano huo walikuwa wakizungumza kwa kuzunguka hoja za msingi.

Katika maelezo yake, mtoa habari wetu anamnukuu* Gambo akisema* kuwa tatizo la kupoteza mvuto kwa CCM ni Richmond na Dowans, kauli ambayo ndiyo iliyomuinua kitini Isaac akihoji Gambo alikuwa na maana gani.

Lakini Gambo akiendelea kujieleza aliuliza:* “Nani humu ndani asiyeijua Richmond na Dowans? Nani asiyejua kuwa Edward Lowasa alijiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond? Nani asiyejua kuwa Rostam Aziz ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na wakati huo huo ana mamlaka ya kisheria ya umiliki wa Dowans?

“Nani hafahamu ukweli kuwa Lowassa na Rostam ndio wanaokipotezea mvuto CCM? Wananchi watakuwa na makosa gani wakihusha Dowans na CCM wakati viongozi wake wakubwa ndani ya chama wanahusika na chama hakijawafanya chochote?

“Watanzania wanakerwa sana na Richmond na Dowans na lazima CCM iwashughulikie wahusika wote ili kujenga taswira mpya kwa chama chetu.”

Mjumbe huyo kutoka Arusha akionekana kujiamini alisema viongozi hao wamekuwa na mkono katika kashfa ya Richmond ambayo ndiyo msingi wa CCM kupoteza mvuto kwa kasi.

Aliongeza* Gambo: “Tanzania inatakiwa kulipa zaidi ya Sh. bilioni 94 kwa ajili ya kashfa ya Dowans ambayo ni muendelezo wa Richmond. Kama ikiamuliwa kulipa, fedha hizi zitalipwa na wakulima na wafanyakazi* wa Taifa hili kupitia kodi zao. Lazima tuwafikirie Watanzania hawa.”

Lakini katika maoni yake, Isaac alimtetea Lowassa akisema ya kuwa mwanasiasa huyo hakuhusika na Richmond bali alitolewa kafara na viongozi wenzake wa Serikali na CCM, jambo ambalo baadhi ya wajumbe walitafsiri kuwa alimlenga Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete.

“Nani asiyejua kwamba Lowassa alitoswa? Nani asiyejua kwamba alitolewa kafara?”, alisema Isaac kabla ya Gambo kuruhusiwa kuendelea na kutoa kauli ambayo ilionekana dhahiri kumkera DC huyo, ambaye aliwahi kuwa ndani ya UVCCM kabla ya kuteuliwa kuwa DC.

Baada ya maelezo hayo ya Isaac, Gambo aliruhusiwa kuendelea na akasema: “Isaac tuanze sasa kufikiri kwa kutumia kichwa na si kufikiri kwa kutumia tumbo. Mtu ukiwa mnafiki ukiwa kijana, ukizeeka lazima utakuwa mchawi.”

Tafsiri ya maneno hayo kutoka kwa vijana waliozungumza na Raia Mwema, mjini Dodoma, imeelezwa kwamba ni kuwaonya vijana wasikubali kutoa maoni yao kwa kuangalia watu wanaowalipa fedha na kwamba Gambo alikuwa anazungumza kwa maslahi ya chama chake, Serikali na Watanzania kwa ujumla akihoji ni kwa vipi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM - Rostam Aziz ashiriki kudai Watanzania bilioni 94 kwa niaba ya kampuni ya nje?

Kwa mujibu wa Gambo, kauli ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete ya chama hicho kujivua gamba ni lazima itekelezwe kwa vitendo katika mazingira ya ukweli.

Hata hivyo, akizungumza katika mjadala huo kujibu hoja dhidi ya Lowassa na Rostam, Mjumbe mwingine Hussein Bashe alikiri kuwa na maslahi binafsi na Rostam ambaye ni mwajiri wake katika moja ya kampuni zake. Bashe ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari inayomilikiwa na Rostam.

Bashe alikiambia kikao hicho kwamba mjumbe mtoa hoja hana ushahidi wa kutosha, na kwamba wenye matatizo CCM ni John Magufuli (Waziri wa Ujenzi) na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, na kwamba Rostam na Lowassa hawana matatizo.

Inadaiwa kuwa Bashe alimtaja Magufuli kama mtu anayeichonganisha CCM na wananchi katika bomoa bomoa ya majengo aliyoianzisha na baadaye kuzimwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Alimtaja Sitta kuwa ndiye aliyechochea suala la Richmond kwa kuliweka wazi kupitia Bunge.

Makamba abanwa mbavu

Katika mkutano huo, Katibu Mkuu, Yusuf Makamba naye hakusalimika. Alibanwa na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho ambacho yeye ni mjumbe akielezwa kuwa yeye ni chanzo cha CCM kufanya vibaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Lakini akijetetea aliegemea mgongo wa Mwenyekiti wake Kikwete huku akiwaangushia lawama na kejeli wasaidizi wake waliokwenda kugombea ubunge.

Akitumia baadhi ya maneno makali, Makamba aliwatupia lawama Naibu Katibu Mkuu,* George Mkuchika, Katibu wa Uenezi, John Chiligati, Mweka Hazina, Amos Makala na aliyekuwa msaidizi wake, Saidi Mtanda. Wote walishinda ubunge katika majimbo yao.

Alifanya hivyo baada ya kuelekezewa mashambulizi ya moja kwa moja kuwa amevuruga au kupunguza ushindi wa CCM katika uchaguzi huo.

Aliwataja viongozi hao kama sababu za yeye kushindwa kumudu vyema harakati za kampeni za Uchaguzi Mkuu, akibainisha kuwa hali hiyo ilimlazimu Mwenyekiti Kikwete kuunda kamati za ziada kwa ajili ya kampeni.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya gazeti hili ndani ya mkutano huo, kati ya wajumbe waliomshambulia moja kwa moja Makamba ni aliyekuwa anawania kuteuliwa na CCM kuwania ubunge Kinondoni, Shy-Rose Bhanji, akirejea uzoefu aliopata wakati wa mchakato huo.

Shy-Rose Bhanji ni mjumbe wa Baraza hilo kutokana na nafasi maalumu kutoka Jumuiya ya Wanawake (UWT).

Shy-Rose anadaiwa kumweleza moja kwa moja Makamba kuwa ndiye tatizo la CCM kupoteza mvuto na hasa wakati wa kampeni kwa kuvuruga uchaguzi.

Katika mashambulizi yake, Shy-Rose anadaiwa kumweleza Makamba kuwa hafai (kiuongozi) na kumshauri kuachia ngazi. Msingi wa hoja zake unadaiwa kujikita katika kile kinachoelezwa kuwa mara kwa mara Makamba alitoa kauli zisizo na hekima wala busara za kutosha.

Hata hivyo, Makamba anadaiwa kujibu sehemu ya mapigo dhidi yake hasa katika maeneo mahsusi ya kutoa kauli zisizo na busara ya kutosha kwa kumshambulia binafsi Shy-Rose, kabla ya mjumbe mmoja kumtaka Mzee huyo kutumia kauli za busara na yeye kujibu, “na mimi ni binadamu”.

Kama vile mtu aliyekuwa amejiandaa na akijua aina ya mashambulizi dhidi yake, Makamba anadaiwa kupewa nafasi katika mtindo wa “taarifa” (point of information) na kuanza kuwasilisha utetezi wake baada ya baadhi ya wajumbe wengine kumwona kama Katibu Mkuu wa chama, aliyeshindwa kutimiza wajibu wake kikamilifu.

Makamba apata watetezi

Inadaiwa kuwa ndani ya kikao hicho, Makamba anadaiwa kupata watetezi, akiwamo Bashe, ambaye alipata kuwania kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo la Nzega kwa tiketi ya CCM.

Bashe alishinda kura za maoni lakini alikatwa na Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM-Taifa kwa madai kuwa uraia wake ulikuwa na utata.

Utata huo baadaye ulifutwa.

Katika utetezi wake kwa Makamba, Bashe anadaiwa kuwaeleza washiriki wa mkutano huo kuwa kama ni chama kukosa ushindi uliotarajiwa si makosa ya Makamba pekee na kwamba kama Makamba hafai, basi, mwenye tatizo ni Mwenyekiti wa chama aliyemteua.

Inaelezwa kuwa Bashe alisema na kuhoji kuwa kwa nini alaumiwe Makamba kwani hata wao wenyewe (vijana-CCM) wajiulize wamefanya nini kusaidia
chama hicho.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa bado maelezo hayo hayakupoza au kufuta hisia za wajumbe wengi wa mkutano huo wakiamini kuwa uongozi wa Makamba bado ni tatizo kwa mafanikio ya juu ya CCM wakati wa uchaguzi, baada ya uchaguzi na hata wakati ujao.

Wengi wameendelea kuwa na maoni kuwa anahitaji kupumzishwa ili kukinusuru chama hicho, wakirejea mifano ya kauli zake ambazo baadhi ya wana-UVCCM kwenye ‘korido’ wanaziita za “kuropoka”.

Utetezi binafsi wa Makamba

Baada ya wajumbe kuonyesha mawazo tofauti kuhusu udhaifu wa Makamba, naye alipata nafasi ya kuzungumza na kujitetea akitumia rungu la uzee.

Anadaiwa kueleza kuwa yeye ni mzee wa miaka 72 na kama binadamu anaweza kuwa na kasoro za kiutendaji.

Katika hatua nyingine alirejea mifano kadhaa ya matukio aliyopata kuyatolea kauli, na kusisitiza kuwa kama kufanya hivyo ni makosa (kuropoka) atajiuzulu.

Vyanzo vya habari vinamnukuu Makamba akisema kuwa kwanza viongozi wenzake wa sekretariati karibu wote hawakuwapo ofisini, wakiwa wamekwenda kugombea ubunge.

Kutokana na hali hiyo* ndiyo maana Kikwete aliunda kamati nne zenye majukumu tofauti zilizoongozwa na Kanali (mstaafu) Abdulraham Kinana, Zakia Meghji, Kingunge Ngombale Mwiru na Luavi (Msaidizi wa Rais-siasa kutoka Ikulu).

Kwa mujibu wa utetezi wake, yeye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati hizo na kwa kazi ilivyofanyika inabidi apongezwe.

Makamba na kuropoka

Katika utetezi wake pia Makamba anadaiwa kusisitiza kuwa hakuna sababu yenye mantiki kwa yeye kujiuzulu kwa kuwa yote aliyofanya yalikuwa kwa
nia njema, kumsaidia Mwenyekiti wa CCM, akitumia mifano.

Alitoa mfano wa kauli yake kumtetea Mwenyekiti wake alipokemea viongozi wastaafu na wanaharakati waliowahi kukutana ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam
wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kushinikiza Serikali ichukue hatua kali dhidi ya vigogo wasio na maadili.

Katika kongamano hilo, baadhi ya wazungumzaji walipendekeza kuwa kama Serikali itashindwa kuwachukulia hatua basi itoswe.

Kutokana na hali hiyo Makamba aliibuka na kudai kuwa wanaodai Rais Jakaya Kikwete atoswe ni wendawazimu na alirejea kauli hiyo ndani ya Halmashauri Kuu ya CCM alipoulizwa.

Kauli hiyo ya Makamba kwa wakati ule ilitafsiriwa kuwalenga mawaziri wakuu wa zamani ambao ni Dk. Salim Ahmed Salim, Joseph Warioba na Frederick Sumaye, walioshiriki kongamano hilo pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku.

“Kama kumtetea Rais (kuwaita washiriki wa kongamano wehu) ni kosa basi nipo tayari kujiuzulu,” anadaiwa kusema Makamba akithibitisha kuwa si mropokaji.

Makamba, Lowassa, Shamsi Vuai

Tukio jingine alilotumia linatajwa kuwa ni kauli ya Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa wakati wa mgogoro wa kiti cha umeya, Arusha.

Katika mgogoro ule, Lowassa aliibuka na kushauri vyama vya CCM na CHADEMA wakutane kuzungumza ili kumaliza mgogoro huo.

Akitoa maelezo yake ya utetezi Makamba anadaiwa kueleza kuwa Lowassa ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM hivyo angepaswa kuwasilisha mawazo
yake huko na si kupingana na wana-CCM wenzake hadharani ambao kwa mujibu wa taratibu na sheria walishinda kiti cha umeya wa Arusha.

Inadaiwa kuwa Makamba alisema kama kazi anayofanya kulinda nidhamu ya chama miongoni mwa wanachama na hasa viongozi wakuu ni kosa, atajiuzulu.

Makamba alirejea pia kauli ya Lowassa kuhusu tatizo la ajira kwa vijana ambaye alidai kuwa ni bomu linalosubiri kulipuka.

Katika hilo, Makamba ananukuliwa akisema; “CCM kilikaa kikapitisha Ilani ya Uchaguzi na Lowassa alikuwamo kama mjumbe wa NEC. Ilani hii ndiyo inayotekelezwa na Serikali. Kama anaona anayo mawazo mengine kwa nini asirudi NEC kuyaeleza? Ni kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Sasa kama kukemea suala hilo nikiwa kama Katibu Mkuu* ni kosa basi niko tayari kujiuzulu.”

Hakusita pia kurejea kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nadhoda, kuhusu tukio hilo la Arusha. Shamsi anadaiwa naye kutoa kauli ya kutaka CCM na CHADEMA kukutanishwa.

Anadaiwa kueleza kuwa kama kufanya utetezi huo dhidi ya Mwenyekiti wa CCM, nidhamu ya chama hicho na serikali ya CCM kwa ujumla, basi yuko tayari kujiuzulu.

Makamba na utani mkutanoni

Makamba anadaiwa kufanya utani ambao hata hivyo umegusa baadhi ya vijana hasa waliokuwa wakidai kuwa ametumia nafasi yake ya Katibu Mkuu kumsaidia mwanawe, Januari Makamba, kushinda uteuzi wa kuwania ubunge ndani ya CCM, Jimbo la Bumbuli.

Katika utetezi wake alikiri kumsaidia mwanawe lakini alifanya hivyo kama mzazi na si kama Katibu Mkuu wa CCM. Anadaiwa kutumia kauli za; “Nilikuwa shabiki wake kama mzazi na si shabiki wake kama Katibu Mkuu.”

Hata hivyo, katika kile kinachotajwa kuwa ni utani Makamba alisema yeye ni mzee wa miaka 72 na lazima amsaidia mwanawe, akihoji asipofanya hivyo posho zitatoka wapi?

Imeelezwa kwamba Makamba alitumia mgongo wa Kikwete kujitetea kuhusu uamuzi wake wa kuamua katika dakika za mwisho za kura za maoni za CCM wanachama wasio na vitambulisho vya kupigia kura kushiriki kura hizo, jambo ambalo limeelezwa kuwaathiri vijana wengi.

Akijibu hoja ni kwanini alifanya uamuzi kinyume na uamuzi wa NEC, Makamba alijitetea kutumia mgongo wa Kikwete kwa kusema, “Baada ya kupokea malalamiko mengi nilimpigia simu Mwenyekiti (Rais Kikwete) ambaye aliniambia kama ninaona sawa, basi, nifanye.”

Imeelezwa kwamba, pamoja na matatizo ya kiafya na umri, Mzee Makamba alilazimika kukaa katika kikao hicho cha UVCCM tokea mwanzo hadi mwisho, tofauti na vikao vingine vya siku zilizopita.

Maazimio ya mkutano Hatimaye mkutano huo ulifikia maazimio yaliyowasilishwa kwa waandishi wa habari. Kati ya maazimio hayo ni kuwashughulikia viongozi wakuu watakaokuwa wakitoa matamko hadharani licha ya kuwa na fursa ya kufanya hivyo katika vikao.

Imeelezwa azimio hilo lilisisitizwa na Makamba alipokua akizungumzia kauli za Lowassa na Vuai kuhusu mgogoro wa umeya Arusha ambapo alisema viongozi kama hao vijana wawashughulikie kwa kuwa wanakidhoofisha chama na kutaka jambo hilo liingizwe kwenye maazimio.

Kwa mujibu wa azimio hilo, kati ya adhabu atakazokabiliwa nazo muhusika ni kupigiwa kampeni ya kupingwa na UVCCM pindi atakapotaka kuwania nafasi ya uongozi ndani ya chama hicho, mara baada ya kujaza fomu husika kutimiza nia yake hiyo.

Kikao hicho pia kiliunda kamati ya watu wanane ikiongozwa na Bashe kwa ajili ya kukusanya maoni kuhusu kuikarabati UVCCM. Wajumbe wengine wengine ni Anthony Mavunde Dodoma, Rogers Shemwelekwa (Tanga), Fadhili Ngajilo (Iringa), Riziki (Pemba), Daudi Ismail (Zanzibar), Ashura Seng’ondo na Zuberi Bundara wa Tanzania bara.

Kamati hiyo ambayo imepewa hadi Juni mwaka huu kukamilisha kazi yake, imeelezwa kumpa nafasi mpya Bashe kuweza kurudi rasmi katika ulingo wa siasa baada ya kupata maumivu wakati wa kura za maoni aliponyang’anywa ushindi kwa madai ya kuwa si raia, madai ambayo yalishikiwa bango na Makamba, kabla ya kubainika kuwa hayana ukweli.
 
WABUNGE NA VYAMA VINAVYOTAMANI KUHESABIWA UMAKINI TANZANIA:
TAFUTENI HARAKA ELIMU SAHIHI JUU YA MAANA, CHANGAMOTO NA USHIRIKI WA MAFANIKIO NDANI YA MFUMO MPYA WA 'SIASA ZA USHINDANI' ILI MUENDELEE KUMUDU NA KUDUMU

Ingawaje tunapozungumzia vyama nchini na vituko vinavyoendelea kushudiwa mle, wengine wakitafsiri vibaya matumizi ya MBINU ZA KISASA ZA KUTUMIA VEMA 'SILAHA SALAMA' YA MAANDAMANO inayokubalika pia ndani ya Katiba za nchi mbalimbali duniani wengine huanza kumwaga chuki kashfa na wakati mwingine hata kusababishia watu kucheka mbavu kuuma lakini baada ya kicheko ni wazi kwamba kuna mambo mengi sana ambayo watu na vyama, kama washiriki, kwa bahati mbaya hawajagundua kwamba tayari yamebadilika kabisa na kamwe hayatokaa yarudi kuwa kama zamani kisiasa nchini.

Kweli ni masikitiko makubwa sana kwamba watu wengine hufikiria kwamba mtu unaweza tu ukaingia kwa jambo lililoitwa 'jipya' lakini bado ukatumia tu mbinu zile zile, lugha zile zile, na kashfa zile zile na bado ukaendelea tu kufanikiwa; laa hasa!! Pindi usikiapo kuna mabadiliko, kwa wale watu wadadisi wa mambo, ni sharti utafute kujua ya kwamba (1) ni kitu gani hasa kilichobadilika, (2) kivipi kimebadilika, (3) kwa sababu zipi, (4) na huko nyuma hali ilikuaje na sasa yakoje, (5) je mimi mwenyewe naendana na au siendani na mfumo huo mpya kwa kiasi gani hasa, (6) nifanye jitihada zipi (si kwenda Mlingotini) zinazokubalika ili niendane na mfumo mpya kwa namna ambavyo nitapata uhakika wa kung'ara KIUTENDAJI (si ki-ndumba) ndani na nje ya chama changu kusudi nisiwe mzigo wa chama na wapiga kura wala kulazimika kupanda BP kila wakati ...

... na maswali kama hayo yafanyiwekazi KIUHAKIKA NA UNYENYEKEVU zaidi wa kutafuta kule upya wa KUJIVUA GAMBA LA ZAMANI kwa wakati mwafaka na kujivisha GAMBA MPYA NA INAYOKUBALIANA NA MAZINGIRA YALIOPO na kwa mtindo utakaompendeza zaidi yule bosi na au mlaji wako wa mwisho ambaye ni MHESHIMIWA MPIGA KURA.

Bila kufanya hivo basi niwaambieni HABARI MBAYA SANA kwamba kwa kipindi cha miaka michache ijayo, kwa tafsiri yangu ya mambo kitaaluma, bunge letu huenda ikabahatika kupata ugeni mkubwa wa Wabunge Vijana zaidi, Wasomi zaidi, na hata wakawashangaza zaidi wazee kwa kushinda kwao Uchaguzi kiurahisi zaidi bila hata kuhitaji utajiri mkubwa wa kuhonga mtu alimradi mtu huyu aje asome ninayoyaandika humu, akayafanyia HOMEWORK ya kufa mtu ndani ya miaka miwili mitatu hivi na kisha anapojitokeza ulingoni atakuta anazungumza lugha inayooana zaidi na mazingira yaliopo, akawa anazungumza na baadaye kushughulikia zaidi matatizo hasa yanaokubaliana fika na matarajio ya mabosi wake; waheshimiwa wapiga kura.

Nirudie kwamba kwa sasa hivi ni rahisi mno kwa mtu anayejua dhana ya SIASA ZA USHINDANI unaotegemea nguvu za idadi na U-smart wa watu wanaojitokeza kugombea ukilinganisha na kuendana kwao na mahitaji halisi ya wakati uliopo wa mlaji wa mwisho wa HUDUMA ZA KIUONGOZI anazotarajia kutoa akishinda.

Ndio nasema kwamba wapo wanasiasa wengi ambao bado huendesha mambo yao kisiasa lakini kwa kutumia fikra na mbinu za zamani katika kipindi ambacho ni tofauti kabisa. Huko nyuma siasa za fitina, majungu, kuunda zengwe, kupiga domo na kumwaga hewa tupu, kununua vyeo na wapiga kura, mtoto kurithiswa chama cha siasa cha kufuata, kurithishana uongozi na mambo kama hayo yote yalihesabiwa kuwa ndio ujanja zaidi mtu kuitwa mwanasiasa mahiri. Hii hali inaelezea hasa kwa nini Tanzania tumejitawala wenyewe karibia miaka 50 na mambo bado ni ki-mishen tauni tu toka ngazi ya kata hadi ofisi inayostahili heshima ya hali ya juu inayoitwa ikulu nchini. Ajabu kote huko kumebakia woga tu na wala si heshma kwao.

Kwa wale ambao walau tumewahi japo hata kusikia kitu 'MFUMO WA SIASA ZA USHINDANI' napenda niseme kwamba hii ni sayari nyingine kabisa ambayo pale bungeni kwetu Dodoma, kama sikosei, zaidi ya ile dadi kubwa ya wabunge karibia 400 huenda chini ya asilimia 10% tu ndio wanaoifahamu kwamba ni kitu gani hasa hiki. Lakini kwa kuwa siku zote wanasiasa huhesabika kuwa ni watu mashuhuri kwa kujua kila kitu (MR / MS I-KNOW-ALLS) naona nafasi ni finyu sana kwa wale wengine zaidi ya 360 kuhiari walau kujishusha na kwenda kutafuta elimu juu ya hili ili uwepo wao bungeni uendelee kuwa na uhakika pamoja na tija kwa jamii kutokana na yeye mwenyewe na au chama chake kama kundi zima.

Guys, an imagination of a possible political landscape without CUF around just but most ungratifying to witness.

The case would never be the same as it would apply to TLPs, NCCR-Mageuzis and the UDPs of this World that has practically been consigned into political Limbo courtesy of the prominently trenched Self-Seeking behaviour, The Politics of Double-Tongue lashing and Own Course Self-Agrandisement by many in their ranks.

Niliposema kwamba Juliasi yule wa DARUSO enzi zile wala si huyu hapa na kwamba kwa bahati mbaya mno akina Maalim Seif wamemfichia mi-faili nyeti zenye kuonyesha (1) sura halisi ya CUF, (2) Malengo ndani ya sera yao mpya ya 'Kujiunga Muafaka na Nguruwe Kuchakaza shamba Mabua yote' na hatima yake.

Ndio, na wamemficha pia Juliasi faili iliobeba (3) tafsiri za wananchi Bara na Visiwani kama kweli walichokua wanakitafuta CUF ilikuani UTULIVU tu Zanzibar au AMANI KAMILI kwa kurejesha kwanza HAKI NA MASLAHI KWA UMMA wa nchi hii.

Si utani na mikutano ya wenzetu inapoondoka Kidongo Chekundu pale kweupe Mnazi Mmoja hadi kule mitaa ya Mwisho wa Lami Gongolamboto, Mtoni kwa Azizi Ali Mara Manzese Kwa Bibi Mfuga Nyau ... kweli hii ni a Big Change in the Wrong Direction; yes it is a most demoralising experience and transition that bothe CUF are currently walking dow the political memory valleys kwa kupingana tu na Maslahi ya Wapigakura nchini.

In fact, a more compelling question that analysts would soon surrender to evader no more is that 'of what use is an army commander if all foot soldiers are long-gone?' I just tend to hope that the NOW apparent CUF Career Presidential Candidates Hon Maalim Seif Sharrif Hamad (Visiwani) and Prof Ibrahim Haruna Lipumba will, at least, seek an escape to some remote hotels may be around Uluguru Mountains and conduct a most sincere Worst-Scenario Self-Evaluation.

Yes, they would certainly need to do that long before they could similarly seek an independent expert hand to equally do the same to the very CUF as a party and ultimately hand down the CUF Secret Files stored far away in Chake Chake - Pemba to Juliasi Mtatiro and other remnant youths to help chat out a possible next course of action - either to Revive or Survive their own way and a lot sooner the better!!

To this end, I just DON'T see myself leaving out CHADEMA for a more freequent (4-Month Periodical Independent & Credible) monitoring and evaluation about their yesterdays, todays and tomorrows. Waberoya, Mwanakijiji and myself can most competetly string them to this own-face behind the mirror scene for a more re-assuring future.

And this is where all political parties, just like any other business establishment known around, are bound to most willingly go or never!! The market-based COMPETITIVE POLITICS that we tirelessly seek to live to-date (Democratic Multipartism) is just but more dynamic, most enveloping and so demand both at group and personal levels such that a POLITICAL HERO / HEROES of yesterday is NEVER guaranteed tomorrow unless they 24 / 7 choose to obay Philip Kotler's dictates to keep their eyes to the ground to catch the most correct scale of the electorates' next-day heartbeats and seek to serve them in the best way possible on TIME and in a WAY that a competitor (another political Party or an opponent within your party or across) would never far easily pick a match.

In a nutshell, after luoghing of my friend Julious Mtatiro's most impending political misfortunes, like is lately the case with CCM, with his political party CUF that daily diminishing in value in the eyes of the HONOURABLE ELECTORATES, may I point here that the Political Landscape is fast-adjusting with youth on the steerwheels, things turning high-tech almost in a speed of a click of a computer mouse away such that the yerteryears inherently incompetence and majungu / fitina in political arena shall soon NEVER be tolerated BUT only practical positive results in public goods to the general public that shal be mattering and not even a mere name of a political party of the neighbours shall ever count.

Wazee, huku ndiko tunakokwenda; hakuna watu kulala tena bungeni na kujigeuza wataalam wa kuzungusha maneno badala ya matunda kuonekana. Huko katika ulimwengu ulioendelea utasikia pengine chama chake Obama kimeshinda kwa wingi leo na keshokutwa kwenye Mid-term elections ukasikia wamepigwa chini zaidi ya nusu na Waheshimiwa Wapiga kura kwa kutoridhisha kiutendaji.

Nasema na ieleweke kwamba ule utamaduni wa 'HIKI NI CHAMA CHANGU NA FAMILIA YETU NZIMA tangu enzi za babu hivyo sitoweza kukihama' itakuja kutoweka bila hata ya wengi wetu kujua. Hatutopigia kura tena (1) SURA za watu, (2) MAJINA YA VYAMA bali tu (3) kwa kiasi Gani Wametuletea sisi Wapiga Kura Matunda tuliokua tukiyatarajia.

Hizo ndizo misingi halisi za siasa za ushindani huko tunakoelekea ambapo VIJANA WENGI NA WASOMI nchini ndio idadi yao inaendelea kuwa kubwa nchini. Hivyo kitendo cha Chama kubahatika kupewa ka-nafasi ya kuongoza na kisitumie vizuri KUJING'ARISHA mbele ya macho ya wapiga kura; badala yake kikajiroga kwenye kujiingiza kwenye Vitendo vya Kifisadi, basi siku kikipoteza nafasi hiyo ujue fika chama hicho kitatiwa LOCK-UP na wapiga kura kwa muda usiojulikana sawa yake KANU wa Kenya ambacho hivi leo kisiasa wala hakizungumzwi hata kwenye nafasi ya nne ki-umaarufu.

Na atakayesoma maoni haya ampitishie na kiongozi wake wa chama chake, kata, wodi, jimbo na taifa ili tukija kuwatia LOCK-UP kwa uwezo wa kura zetu wasije wakasingizia hawakuelewa kama sheria za mchezo wa siasa za ushindani ni tofauti kiasi hicho.

Mwisho nimalizie kwa kusema kwamba enyi mlioko madarakani ambao bado ndio mnaoonekana wakubwa kwa sisi Wapiga kura, malizieni salama utamu huo kwa vile wengi wetu hawajaeleweshwa; tangu hapo 2015 na kuendelea MPIGA KURA NDIYE ATAKAYEGEUKA MFALME kwa kipindi chote na wala si kwa wakati wa wiki 2 au 3 za uchaguzi tu.

Chukua hatua ewe unayefikiria kuja kua kiongozi wa ngazi yoyote hapo baadaye kidogo ili usije ukafa bure na shinikizo la damu kwenye mfumo mpya wa siasa ndani ya mipaka yetu!!
 
Hapa nimeona kauli mbiu ya UVCCM ni "kujenga na kulinda Ujamaa" Duh hii kali
 
vyanzo vya ndani vinadokeza kuwa barua hii haikupata baraka kutoka uongozi wa UVCCM Taifa; Shigela alipigiwa simu na mkubwa mmoja na kutaidwa kujibu mara moja na kuna uwezekano barua ililetwa kwake (kama barua moja ya miaka mitano hivi iliyopita) ikiwa tayari imeshachapwa na yeye alitakiwa kuweka sahihi tu.
 
Sikutegemea kama UVCCM ungeweza kukanusha kwa staili hii, inabidi wajipange upya, na kuacha kubabaikia mafisadi, :smash::smash::ballchain:
 
Hizi episodes za CCM sasa zinaanza kufanana na za Jerry Springer!

ahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kwa Jerry Springer ma bwabwa wengi ,hoja za ajabu yaani viroja kwenda mbele vululuvululubana umewatusi sana mafisadi ahahaaaaaaa
 
Mkuu MMKJJ, Nakushuru kwa taarifa nzuri, pia nikupongeze ...

...

Hiyo UVCCM ni mali ya Kijana wa Kikwete ndio mwenyekiti na ndio Katibu, ila wanapoona sasa wanabaki kombo wanachanganyikiwa na kulalama kama chura. CCM kukosa vijana walionauwezo itawagharimu sana maana iwapo ikitokea kushindwa uchaguzi hawata weza kusimama tena Milele watajiunga na wenzao KANU ya Kenya.

MBONA UVCCM URAMBO NA MIKOA MINGINE HATUWASIKII AU WATANZANIA NDIO
TUELEWE TAYARI WOTE WAMESHANUNULIWA KASORO TU UVCCM KILIMANJARO
TU NDIO BADO KUMESALIA WAZALENDO WA KWELI???


Nimeipendasa hiyo aya ya mwisho; UVCCM, kama haya yote tunayoyasikia na kuyasoma hivi sasa ni ya kweli basi na tuyalinganishe nyinyi wenzetu kujidondoshea chupi chafu ya kila mmoja wenu na siri zenu zote za chumbani sasa nje mithili ya mtu mwendawazimu anapojifulia nguo zake zote za ndani peupe pale katika ya soko la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Eehhe, na kundi la pili UVCCM ije maana sasa hatuna hata uhakika nani kala rushwa kweli ya Rostam Aziz na Edward Lowasa tukianzia na zile elfu 50,000/- mlizogawiwa kwenye bahasha ya khaki kutoka Jijini Arusha kule kwa machalii.

Lakini mpaka hapa napata imani kubwa sana na maelezo ya yule kijana kiongozi wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro na wale wa Mara, sasa hawa wa mikoa mingine sijui ndio Wa-Tanzania tuwaeleje ukimya wao huu wote kwamba ndio wako na Benno Malisa au yule kiongozi wa UVCCM Kilimanjaro. Waangalie ukimya wote huenda wananchi tukawaingiza kwenye rekodi mbaya buuure shauri tu ya kutokujieleza kwa wakati mwafaka.

Enyi UVCCM Urambo ni kweli Mhe Sitta huko hawafai tena kweli???????????
 
Kila siku nawambia kwamba CCM siku zote wanaongea nchi mazoea pamoja na kaulimbiu za mwaka wa 47, sera nazo za huko huko ndio maana vijana siku zote hatuwaelewi hiki chama cha hawa manajas wa ufisadi huku wengine mkawa hamuelewi.

Hapa nimeona kauli mbiu ya UVCCM ni "kujenga na kulinda Ujamaa" Duh hii kali
 
hoja hujibiwa kwa hoja,kwa hiyo walitakiwa kujibu hoja moja baada ya nyingine na sio kujumlisha mahesabu ya hoja,watambue ccm ni mlezi kwao kwa hiyo wakitendee haki kama henyewe kinavyo watendea
 
I support UVCCM

I know you do!! But it is for your own benefit!!! This would have been making sense if you would come up with reply on each accusations published. A general denial like that is a self defence mechanism!!!

Good for you
 
Ni ajabu katibu mkuu huyu kukomea kuwaonya tu badala ya kuwaburuza mahakamani, kwa tafsiri yangu naamini kwa asilimia 100 kuwa yaliyoandikwa yote yalisemwa. Hata Rai nao wameandika mambo yanayofanana na hayo ingawaje yakiwa na mlengo wa kumjenga Rostam na Lowassa zaidi
 
JK atatoka muda sii mrefu atasema vijana wanataka kuchukua nchi.Ngojeni mtasikia tu
 
UVCCM hawawezi kuwa tofauti na baba/mama yao CCM. Naomba na UWT nao wabadili jina waitwe UWCCM
 
MBONA UVCCM URAMBO NA MIKOA MINGINE HATUWASIKII AU WATANZANIA NDIO
TUELEWE TAYARI WOTE WAMESHANUNULIWA KASORO TU UVCCM KILIMANJARO
TU NDIO BADO KUMESALIA WAZALENDO WA KWELI???

Nimeipendasa hiyo aya ya mwisho; UVCCM, kama haya yote tunayoyasikia na kuyasoma hivi sasa ni ya kweli basi na tuyalinganishe nyinyi wenzetu kujidondoshea chupi chafu ya kila mmoja wenu na siri zenu zote za chumbani sasa nje mithili ya mtu mwendawazimu anapojifulia nguo zake zote za ndani peupe pale katika ya soko la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.

Eehhe, na kundi la pili UVCCM ije maana sasa hatuna hata uhakika nani kala rushwa kweli ya Rostam Aziz na Edward Lowasa tukianzia na zile elfu 50,000/- mlizogawiwa kwenye bahasha ya khaki kutoka Jijini Arusha kule kwa machalii.

Lakini mpaka hapa napata imani kubwa sana na maelezo ya yule kijana kiongozi wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro na wale wa Mara, sasa hawa wa mikoa mingine sijui ndio Wa-Tanzania tuwaeleje ukimya wao huu wote kwamba ndio wako na Benno Malisa au yule kiongozi wa UVCCM Kilimanjaro. Waangalie ukimya wote huenda wananchi tukawaingiza kwenye rekodi mbaya buuure shauri tu ya kutokujieleza kwa wakati mwafaka.

Enyi UVCCM Urambo ni kweli Mhe Sitta huko hawafai tena kweli???????????


Huyo Mwenyekiti wa UVCCM Tabora ni limbukeni kama kawaida amekurupuka sasa wenzake wanamkana kwamba ni tamko lake binafsi...AIBU KUUUBWA. UVCCM URAMBO tunamkubali mzee 6 na ataendelea kuheshimika tu. Soma habari kwenye NIPASHE ya leo 25/3 ndio utajua kuwa Chama kimepoteza dira na nidhamu yaaani hawajui watatokaje kwa hiyo ni kuharibu kwenda mbele...............TIME WILL TELL:drum:
 
Back
Top Bottom