JF EXCLUSIVE: Sababu ya Kuachishwa kazi Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO

Huyu katibu wa wizara na bodi ya shirika la TANESCO kunatatizo.
1.Nani asioyejua kuwa serikali imekuwa ikiishinikiza tanesco kuingia mikataba mibovu inayoligalimu shirika na kushindwa kujiendesha?

2.Je!kama serikali imeshindwa kudhamini mkopo tangu mwaka jana na kushindwa kutoa rudhuku kwa shirika katibu mkuu alitaka Mhando atoe wapi fedha wakati yeye amegonga mwamba hazina?

3.Kimsingi bodi ya Tanesco pamoja na wizara ya nishati na madini wamechemka.

4.Technical issue hazina muda kwa mantiki hiyo huwezi kumwajibisha mtu kwa ule mgao wakati umeshindwa kutimiza mahitaji yake.
Nitashangaa nikisikia WABUNGE wanaipongeza bodi kwa kumsimamisha Mhanda
 
Kama Mkurugenzi na Katibu Mkuu wanashindwa hata kupigiana simu wakajulishana juu ya mgao wa umeme basi uhusiano kat ya Wizara na Tanesco una matatizo makubwa kuliko inavyoonekana. Yaani Katibu Mkuu naye anausikia mgao kwenye vyombo vya habari!!!!

Hv wewe Boya ZeMarcopolo umesoma barua ya Mhando kwa Katibu Mkuu kweli au ndo umekurupuka kuan
dika huu uharo, Mhando kasema kabisa alimpigia simu katibu Mkuu na baadae akaitwa akaitwa ofisin.
Da, Yule jamaa aliye post issue yako ya "Dr Chinja chinja Lugalo" hakukosea kabisa
 
Last edited by a moderator:
Hii kitu nimeipenda,angalau serikali imeamka usingizini.kama idara zote zingekuwa hivi wala tusingemwambia mfalme wetu ooops sorrry rais wetu dhaifu.ppooooooooooooos aluta continue!!!!!!!!
 
Wote waovu. Mhando alitakiwa kuwa na mipango ya dharura ya baadaye (future) na angejipa muda ili ikishindikana amwage unga. Kwa sababu maelezo yake yote anaonekana kama analalamika tu, sijaona sehemu aliyosema kulikuwa na future plan au ana future plan ya kuzuia tatizo. Kama CEO na mimi kama mtalaamu hajanishawishi. Let him go. Serikali najua imechapika,
 
1.Inaonekana kabla ya tarehe 15 May 2012, maamuzi ya kuanza mgao wa umeme yalikuwa chini ya mamlaka mengine ( labda Tanesco), kuna sababu gani ilipelekea serikali kupoka hayo mamlaka?

2. Na kama kwenye barua ya 15 May, ilikuwa inaipa mamlaka serikali ya kupewa taarifa za siku za siku za mabwawa? Serikalini kulikuwa na timu ya wataalamu kwa kushauri mamlaka husika kuhusu ulazima wa kuanza mgao, au bado ushauri ulibaki Tanesco na maamuzi serikalini?

3. Barua ya KM inasema Mhando achukue tahadhari zote kuhakikisha mgao hautokei, serikali imefanya nini kutimiza wajibu wake ?
 
Tanesco inatakiwa ivunjwe sehemu 3;

1. uzalishaji
2. usambazaji
3. uuzaji

Uzalishaji utakuwa huru. Mtu yeyote anaweza kuanzisha kiwanda halimradi ameongea na kampuni la usambazaji juu ya kununua na maswala ya capacity charges. Makampuni ya uzalishaji yanaweza kuwa sekta binafsi na mashirika ya umma

Msambazaji anatakiwa awe mmoja tu Tanzania. Huyu ndiyo atayekua muuzaji wa jumla wa umeme. Hili kampuni linapaswa kuwa sekta binafsi.

Wauzaji wanatakiwa wawe wa kikanda zaidi. Kila kanda iwe na muuzaji mmoja. Huyu muuzaji ndiya ataanzia kwenye transformer mpaka kuingiza nyumbani kwa mlaji. Leseni za uuzaji zitauzwa na EWURA kwa mnada, na inabidi ziwe aghali sana kuhakikisha kuwa wanunuzi ni watu serious.

Kwa hali ilivyo, ambapo Tanesco imetamalaki kila secta ya umeme, nchi haitakaa ipate umeme wa kutosha
 
Mo-Town na wengine, naingia miusa ya saa 3:30 nikitoka saa 5:00 nitawajibu kwa ufasaha ila Mhado hiyo ni stahiki yake!.

Pasco, kua uyaone mwanangu. Natamani hata ungepewa uCEO wa TANESCO angalau kwa mwezi mmoja tu uone namna ilivyo vigumu ku-perform kwenye mashirka ambayo serikali ina mkono ndani yake. Kwa usalama wa maisha yake, bila shaka Bw. Mhando ame-reserve jitihada zake alizofanya kabla ya kuamua mgawo uanze. Kwa nchi zetu hizi za kiafrika, ni jambo la hatari sana tena sana kuweka hadharani udhaifu wa wenye mamlaka hata kama wamekuonea kwa kiwango gani. Naamini hicho ndicho alichofanya Bw. Mhando.

Wakati unajibu hoja za Mzee Mwanakijiji umeonyesha kuwa kama serikali imekuwa inalaumiwa kwamba ni dhaifu, basi sasa imeanza kuwa serious na kwa kudhihirisha hivyo, imemsimamisha Bw. Mhando. Hiyo ndiyo hoja yako japo nimeeleza kwa lugha rahisi kidogo. Kimsingi, nakubaliana na wewe lakini mambo haya yanahitaji busara kidogo na tutakuwa tunajidanganya sana kwa kudhani kuwa kufukuza watumishi kazi ndiyo suluhisho. Kwa mawazo yangu, nadhani Bw. Mhando alipaswa apewe ONYO na kukumbushwa umuhimu wa kuzingatia maelekezo ya mamlaka iliyo juu yake badala ya kumsimamisha.
 
Duh inavyoonekana wanataka kujifanya wamechukua hatua ili wapate cha kujieleza wakati wa budget yao ikifika. Naona kama mnamtoa kafara tu mhando
Huo ndo ukweli, huyu anatolewa kafara ili budget ipite kwa urahisi. Ukweli mwingine ni ule aliougusia MMM kuwa serikali imeshindwa kumlisha ngombe lakini inategemea kumkamua atoe maziwa. Mhando alipaswa kuwa ameng'amua udhaifu huo na kujiuzulu mapema badala ya kungojea atolewe kafara. Serikali DHAIFU ndo kiini cha matatizo yote likiwepo hili la umeme.
 
Baada ya kupitia madai ya Katibu na majibu ya Mhandisi Mhando nimegundua kuna mambo makuu mawili:

1.Siasa
2.Matumizi mabovu ya madaraka!


Hayo yote nimeyaona yakitawala mezani kwa Katibu mkuu, anajaribu kutumia mamlaka aliyonayo kutawala kisiasa mambo ya kitaalamu yasiyohitaji siasa!

Anajaribu kutokeza akiitaka shikamoo/kunyeyekewa kitwana kwa mambo aliyopewa taarifa ya zaidi ya mamra moja (simu, barua na mdomo)

Sijui hapa Katibu anasimamia kuwa kosa la Mhando ni kuwa alichukua hatua kabila ya kujibiwa kwa maandishi au nini?

Bajeti haikwepwi kwa staili hiyo, walifanikiwa kwa Jah Hero lakini kwa hapa wamechemka kabisa!
Mkuu ni kweli kabisa Katibu Mkuu alivyoandika hiyo barua ni kama anamwandikia mtu mdogo sana hata mwanae hawezi kumwandikia barua ya kidhalau namna hiyo.
Na Mhando amenisikitisha kwa kuandika barua kinyonge sana na heshima sana. Kama ndo siasa basi huu mchezo ni mbaya.
 
Tanesco inatakiwa ivunjwe sehemu 3;

1. uzalishaji
2. usambazaji
3. uuzaji

Uzalishaji utakuwa huru. Mtu yeyote anaweza kuanzisha kiwanda halimradi ameongea na kampuni la usambazaji juu ya kununua na maswala ya capacity charges. Makampuni ya uzalishaji yanaweza kuwa sekta binafsi na mashirika ya umma

Msambazaji anatakiwa awe mmoja tu Tanzania. Huyu ndiyo atayekua muuzaji wa jumla wa umeme. Hili kampuni linapaswa kuwa sekta binafsi.

Wauzaji wanatakiwa wawe wa kikanda zaidi. Kila kanda iwe na muuzaji mmoja. Huyu muuzaji ndiya ataanzia kwenye transformer mpaka kuingiza nyumbani kwa mlaji. Leseni za uuzaji zitauzwa na EWURA kwa mnada, na inabidi ziwe aghali sana kuhakikisha kuwa wanunuzi ni watu serious.

Kwa hali ilivyo, ambapo Tanesco imetamalaki kila secta ya umeme, nchi haitakaa ipate umeme wa kutosha
Kwa wenzetu ndo wanavyofanya hivi,vinagwa uuzaji si lazima huwe wa kikanda.
 
Tangazo linasema hawa jamaa wamesimamishwa kwa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka, pamoja na bifu liliokuwepo baina yake na Maswi, kama kweli walikuwa na madudu ya ufisadi humo ndani sioni sababu ya kumtetea huyu jamaa.
Tangia hapo kasimamishwa yeye na wahasibu wake ikimaanisha tatizo liliomkamata ni ufisadi. Ukiwa kwenye nyumba ya vioo, tahadhari sana na mchezo wa kurushiana mawe!
 
yesu wangu,kumbe watu wanahangaika na umeme kumbe ni jitu moja kwa sababu zake binafsi ndilo linalosababisha,...mnh,.....:wacko:

kwake si kuna jenereta linalotumia kodi zetu! Hivi ndivyo hata hospitali zetu zinavyofanywa. Kwa sababu wao wana uhakika wa kutibiwa nje, basi hawana haja ya kuziboresha.
 
mengine tuyaache pembeni, hili la katibu mkuu wa wizara kuchukua maamuzi ya haraka kutaka kujua sababu za kukatika kwa umeme nalo ni hatu nzuri sana..........

Lakini hapa wanazungumzia siku ambayo umeme ulikatika bungeni isije ikawa ndio sababu ya kufanya maamuzi ya haraka, fanyeni hivyo hata umeme ukikatika pale hosipital ya temeke, Ilala, tandahimba na kwingineko
 
Tulilishwa sumu na kina kubenea kuwa akiondoka Idrissa Rashid basi Tanesko imemaliza matatizo yake,Mzee Juma Kapuya naye aliwahi kutulisha Sumu uwa akiondolewa Ndolanga Kwenye FAT basi Tz itakuwa Brazil ya Afrika leo kawaulize kama utapata jibu,Tanesko ni shamba la kijiji cha mafisadi kila mwenye anavuna,Muulizeni Ngeleja Supplier wa mafuta ya kuendeshea magenerator ni nni? Amepewa mkataba wa miaka mingapi ku supply mafuta ya mgao wa umeme? Hicho ndio kimemuondoa Ngeleja,Idrissa Rashid,Jairo na Mhando. Yaliyo kwenye magazeti is just a cosmetic to legalize the Deal, ujinga wetu ndo siri ya wizi kuna wengine wanashangilia mipasho bungeni,wengine wanapewa headline kwa kufukuzwa bungeni,wengine maarufu kwa kuomba miongozo,wengine maarufu kwa kulala,wengine kwa kutukana,wabunge wengine wamegeuka ma advocate wa Serikal bungeni.hakuna mwenye kujua kwa nini yupo bungeni mwingine amekariri kukosoa mwingine kakariri kuunga mkono hoja halatu tunaota kukomesha wizi labda kukomesha Taarifa za wizi na ubadhirifu lakini sio wizi na ubadhirifu wenyewe!
 
Jamani tusisome yaliwekwa hapa tukafikiri ndio habari yenyewe, uje hata huo mchezo wa balua inawezekana ni sehemu ndogo tu ya picha yenyewe, subirini mtayasikia

Huyu katibu wa wizara na bodi ya shirika la TANESCO kunatatizo.
1.Nani asioyejua kuwa serikali imekuwa ikiishinikiza tanesco kuingia mikataba mibovu inayoligalimu shirika na kushindwa kujiendesha?

2.Je!kama serikali imeshindwa kudhamini mkopo tangu mwaka jana na kushindwa kutoa rudhuku kwa shirika katibu mkuu alitaka Mhando atoe wapi fedha wakati yeye amegonga mwamba hazina?

3.Kimsingi bodi ya Tanesco pamoja na wizara ya nishati na madini wamechemka.

4.Technical issue hazina muda kwa mantiki hiyo huwezi kumwajibisha mtu kwa ule mgao wakati umeshindwa kutimiza mahitaji yake.
Nitashangaa nikisikia WABUNGE wanaipongeza bodi kwa kumsimamisha Mhanda
 
Matumizi mabaya ya kibadaraka.....okay tutayasikia kama habari hizi zirtakuwa transparent....lakini najua kuna jambo.
 
Back
Top Bottom