JF Exclusive: OC CID Kawe... (inahusiana na Dr. Ulimboka)

inabidi Kova aingie tena studio kurekodi single nyingine
muvi ndio kwanza linaanza
 
Ahsante ndugu kwa taarifa, ila kwa yeyote anayekoncludi kuwa inahusika na kipigo cha ulimboka aacheni kukonkludi wasomi wa tz ajali ni kokote kila mtu anaweza kuipata leo yeye kesho inaweza kuwa kwako wewe unayeshabikia ata ukaangukiwa na mti je na wewe tukuingize kwenye list
 
HUYU OCD AMESAHAU KUWA KAMANDA KOVA ALISEMA KESI IKO MAHAKAMANI, HAIRUHUSIWI KUTAJA JINA LA ULIMBOKA! Ama kweli magamba yanaanza kudondoka yenyewe kabla hayajaondolewa. Sinema ya kamanda Kova inaelekea kuna scene hakuziandaa vizuri, kama hii sijui kama amejipanga vizuri
 
Chochote kibaya kikimtokea MOI, lazima watawasema madaktari
Bora nusu shari kuliko shari kamili, apelekwe India au SA kutibiwa
Ila ajali yake, na yale alio sema yafanyiwe uchunguzi wa kina...
Jamaa hakuwa kazini, Apelekwe India/SA Kwa pesa ya nani?.
 
Huyo afande akumbuke maneno ya pinda ''Liwalo na Liwe'' nitawadharau sana hoa madaktari wa MOI kama watamuacha huyo jasusi hivi hivi. Lazima wahakikishe wanapata taarifa muhimu, pili lazima aonje machungu ya Dr. Ulimboka, hamna kumpa dawa za maumivu! ''Liwalo na Liwe''
 
Hii vita ningumu wajameni...fikiria Waganga...vs Maasikari!!Mimi katambuga...hata naishia mwananyamara...polisi naishia...mtogole polisi post!!Sinema hili linaweza kuwa na epsode..usipo...
 
Get well soon OC CID msimuhukumu kamanda.

Mateso ya kuugua kwake ni makubwa sana kwani anaumia mwili lakini akili inaumia mara mbili, anatamani kurudisha muda nyuma asiwe ameshiriki mateso ya dr. Ulimboka, si hivyo tu, anaonjeshwa ladha ya kebehi zao kwamba kwani madokta ndio muhimu zaodi kuliko watumishi wengine wa serikali, manake mimi naliwaonya nikawaambia "si kwa busara muulizapo hivyo" mwenzenu anakinywea kikombe cha pakanga.
 
images


kwa maneno mengine aombe mungu maana hataweza kutembea tena maishani
 
Wale wote waliokuwa wanatukana madaktari wako wapi?na msiugue,hata upelekwe aga khan,regency wakishindwa utapelekwa muhi2 tu,mtapuputika mmoja mmoja,hivi vita vinaitwa'' NEVER END'' kuna baadhi ya wabunge wanasubiriwa kwa hamu sana pale.
 
Pole OC CID...kumbe na nyinyi huwa magari yanakosea njia na kuwagonga? Kama hukukosea kwa Dr. Uli haina sababu ya kuweweseka. Ila kama ulihusika, pole sana. We all face the same danger...monster anayetumaliza ni yule yule.
 
''mm sijahusika kabisa na kutekwa kwa Ulimboka. Jamani msinidhuru. Tena cku hyo mm ckuwepo'.. David Mapunda

OC CID Kawe (Mkuu wa Upelelezi) David Mapunda amepata ajali ya gari akiwa amesimama nje ya gari lake (gari lilitokea na kumgonga). Amevunjika pelvis na licha ya jitihada za kukwepa kupelekwa Muhimbili alijikuta anaishia mikononi mwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI). Vyanzo vya ndani vya Intelligensia iliyokuhubu vinadokeza kuwa Afande huyo wa polisi amejikuta aki"sema" mengi kuhusiana na "kutokuhusika kwake" na tukio la utekaji nyara, kuteswa na jaribio la mauaji ya Dk Ulimboka.

Kwa mujibu wa "Nzi" ambaye amekuwa akiendesha uchunguzi "mbadala" wa kukusanya intelligensia ya suala hili:

Kumekuwa na doria za kila mara ndani na sehemu mbali mbali za wodi za MOI mpaka staff wamefikia kulalamika juu ya hilo japo maaskari hao wamekuwa wakijibu kwa jeuri kwamba wapo kazini.
Ndugu na jamaa wa afande huyo wamekuwa hawana amani kwa hofu kwamba ma-dr wanaweza kulipiza kile alichofanyiwa mwenzao Dr. Ulimboka. Kumekuwa na maoni mchanganyiko kutokana na kuweweseka kwa afande huyo na kuropoka ovyo. Wapo wanaodai kwamba ''amri ya Ulimboka kukaa zaidi ya masaa matatu katika kituo cha polisi Bunju ni kutokana na order alizotoa afande huyo kwamba akae na asipatiwe matibabu ya haraka''.

Haijulikani kama ajali yake ni tukio lililokusudiwa kumnyamazisha daima au ni ajali ya kawaida.

Ni matumaini yangu madaktari watamtendea kwa kadiri ya uwezo wao wote kuokoa maisha yake.

Kati ya vituo vilivyooza nchini Tanzania ni cha KAWE. Na huyo afande ni mwiba kwa kuchukua rushwa. Anachukua rushwa wazi wazi na hafai kuitwa askari. Kituo cha polisi kawe kimulikwe manake kimezidi rushwa sana.
 
Hii ni habari inayovuta hisia kwa kila namna...

Kama ningekuwa MOI na niko zamu kumtibu afande Mapunda, ningejaribu kucheza mecho wa paka aliyeshiba ila kakutana na panya na kuamua kumkamata....Ambao wamewahi kuona huo mchezo, wataelewa ni kwa jinsi gani panya anapata nafasi ku-repent!!
 
Wale wote waliokuwa wanatukana madaktari wako wapi?na msiugue,hata upelekwe aga khan,regency wakishindwa utapelekwa muhi2 tu,mtapuputika mmoja mmoja,hivi vita vinaitwa'' NEVER END'' kuna baadhi ya wabunge wanasubiriwa kwa hamu sana pale.


Nadhani Stella Manyanya pressure itakuwa inapanda na kushuka!!
 
Huo utakuwa ni MZIMU wa Kamanda Dr Ulimboka unamtafuna huyo afande, Kila kitu kina faa kuwa Fundisho kwa watu waungwana, Hivi polisi anapomfanyia ukatili Dr amefikiria, Hivi Mwanasiasa anapomtukana Dr amefikiria, Hivi Polisi anapo mpiga virungu Mwanafunzi wa Chuo amefikiria? Hivi polisi napomzushia na kupakazia kesi za uongo Rais mtarajiwa amefikiria? Hivi Polisi anapotumwa kumwadhibu ama kupiga mabomu mtu anae mpigania haki zake amefikiria? sasa huyo afande hakufikiria kwamba kuna siku atamhitaji Dr Ulimboka? sasa subiri Dr ulimboka aje amkute hapo MOI. Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
ivi,kwa mfano hii ikawa KWELI KUWA NI kesi ya kufanya elimination kwa kukosa target ya mwanzo(dr ulimboka),itakuwa kali kweli,maana kama watu wametumwa kum-eliminate uyu OC CID nao wamekosea target,si itakuwa hatari sasa,maana nao itabidi itumwe timu ya kuwaeliminate waloshindwa kwenye hi ajali pia.list goes on
 
The above named patient was apparently well(falsely well), several sec, minutes, hours, days ago. When sustained an accident.. hayo ndio maneno ya madakitari wakiwa ward rounds, na kama ana pelvic fructure.. dah i feel sorry for him maana ni vyema ku r/o spinal injury by testing bulbocarvenosus reflex. Hapa ndipo patamu...
 
ye haendi india???

Hii ndio inaonyesha hao ma OCD na mazagazaga mengine wanatumika tu. Wenye "haki" ya kwenda India ndio watoa order- watekelezaji hawana lao. Kama alitumika kwenye mpango wa Ulimboka ni wakati sasa wakumrudia Mungu wake. Hichi kilichotokea ni signal tu (kwamba anakokwenda siko). Siamini kabisa kwenye coincidence. Kila kitu kinatokea kwa makusudi maalumu, sema tu wanadamu mara nyingi tunakosa utambuzi.. Nami nawaomba madaktari watende wema kwa kumtibu kama wagonjwa wengine. At the same time; it does not hurt wakirekodi vile anavyoropoka. Mara nyingi watu huwa wanasema kweli at their weakest point.

 
Back
Top Bottom