JF Exclusive: Hotuba ya Nyerere 1995

Asante sana mkjj kwa hotuba hii. Wengine wakati inatoka tulikuwa bado hatupati taarifa kama hizi kutokana na mawasiliano.
 
Kwa kweli anatakiwa kuenziwa kipekee kwa mengi aliyotufanyia. cha ajabu tunaishia kuweka hotuba zake wiki ya kuadhimisha siku yake, vipi kuhusu yale aliyoyasema?

Pia naona uongozi wa sasa unataka kumfuta kabisa katika uso wa kumbukumbu........
alifanya mema mengi....sijui kama huko mashuleni bado wanamsoma mwalimu Nyerere ,hotuba zake zinaelekea kupotea ...nadhani in 10 years to come nadhani hatutasikia habari za hayati Mwalimu Nyerere
 
Pia naona uongozi wa sasa unataka kumfuta kabisa katika uso wa kumbukumbu........

FL1.. unachosema kina ukweli mkubwa kuliko unavyodhania! siyo uongozi tu hata watu fulani katika academia wangeweza wangefuta kabisa historia yake ndio maana wanaogopa sana watu kujua Nyerere hasa alisema nini!
 
Anayeota kufuta hotuba za Mwalimu anajaribu kufuta historia ya NCHI hii. Hawezi. Watawala wetu wanaweza wakaendelea kujifanya kusahau aliyoyasema katika mambo mbalimbali ikwemo Muungano wetu, siasa yetu ya Ujamaa na Azimio la Arusha, Elimu, afya, ulinzi na usalama wa Nchi yetu, lakini hadi leo hawana majibu mbadala ya yale aliyoyasema na kuyasimamia Mwalimu.
 
Hotuba imechanwachanwa vipande na kuwekewa misisitizo na chumvi za Mwanakijiji, kama kawaida yake akikusaidia nyaraka. Inakosa mtiririko, hujui mwenyewe Nyerere alisema nini baada ya nini. Mwanakijiji anadhani anatusaidia kuelewa, maana sisi wazito sana.

Msanii wa Kimarekani, Chriss Rock, anapenda kusema kwamba mtu anaekupa kitu kwa vimasharti ni kama mjomba aliyekusomesha shule, lakini akakunajisi. Ndio Mwanakijiji na michango ya nyaraka "zake."
 
Hata kabla ya kifo chake aliona na kushuhudia jinsi watu wake walivyomuasi, alitumia pesa nyigi kuwasomesha elimu bora nje ya nchi akitarajia wataweza kuikomboa Tanzania kutoka kwenye umasikini, ila wao ndiyo wakalifutilia mbali azimio la arusha na kuleta ubepari ambao hata hawaujui miiko yake. Wakawasikiliza kina Reagan na Thatcher ambao yeye siku zote alipingana nao kiitikadi, na matokeo yake wakauruhusu ubepari, Tanzania ikazidi kudidimia. Nchi za Asia, kama China zilikataa haya masharti na sasa zinapaa wakati marekani na mabepari wengine wanadidimia. Kiongozi yeyote aliyekuwepo katika awamu ya pili na ya tatu ameshiriki kuizamisha Tanzania, hatakiwi kuwepo hata mmoja madarakani.Vijana wenye itikadi mpya za kimaendeleo na kizalendo jitokezeni kuiokomboa Tanzania kwa kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao, hii ndiyo njia pekee yakuikomboa nchi yetu.
 
Hotuba imechanwachanwa vipande na kuwekewa misisitizo na chumvi za Mwanakijiji, kama kawaida yake akikusaidia nyaraka. Inakosa mtiririko, hujui mwenyewe Nyerere alisema nini baada ya nini. Mwanakijiji anadhani anatusaidia kuelewa, maana sisi wazito sana.

Msanii wa Kimarekani, Chriss Rock, anapenda kusema kwamba mtu anaekupa kitu kwa vimasharti ni kama mjomba aliyekusomesha shule, lakini akakunajisi. Ndio Mwanakijiji na michango ya nyaraka "zake."

Mwanakijiji yasikukatishe tamaa haya..natamani sana kupata hotuba zaidi za Mwalimu...najua nyingi zinawakera wana CCM wa sasa zinawakosoa na kuwaumbua mno. Mwalimu Tutakukumbuka Daima.
 
Tindikali, mwache Nyerere aitwe Nyerere na apambwe maua na wale wanaotaka kumpamba yeye na maneno yake! Mzigo uki kichwani kwa Mwanakijiji wewe jasho lakutokeani buddy!
 
ni kweli......ila je niwangapi wanaaccess hapa???na ukishawakumbusha then???its high time kuweka mikutano jangwani....kuwagusa wengi,its high time tuache kusurpport mawazo kwa kutingisha vichwa na kiutikia 'yes....the guy was genius' tuanze kupambana na kujiunga kuelekea ulimwengu wa kiukweli na vitendo.

Ni muhimu wapenzi wa Nyerere wakachanga na kuanzisha kituo chao cha Televisheni na radio ili kuweza kuonyesha 'maajabu' ya hotuba za Nyerere ambazo hadi leo zina utamu na vionjo vinavyokubaliana na hali halisi ya wakati huu ingawa zingine zilitolewa miaka 40 na ushei iliyopita. Lakini tahadhari: huenda televisheni na radio hizo zikapigwa vita kama ambavyo chochote kinachotaja ama kujihusisha na jina la Nyerere kinavyoandamwa!
 
Hotuba imechanwachanwa vipande na kuwekewa misisitizo na chumvi za Mwanakijiji, kama kawaida yake akikusaidia nyaraka. Inakosa mtiririko, hujui mwenyewe Nyerere alisema nini baada ya nini. Mwanakijiji anadhani anatusaidia kuelewa, maana sisi wazito sana.

Msanii wa Kimarekani, Chriss Rock, anapenda kusema kwamba mtu anaekupa kitu kwa vimasharti ni kama mjomba aliyekusomesha shule, lakini akakunajisi. Ndio Mwanakijiji na michango ya nyaraka "zake."

Nimeweka hotuba yenyewe hapo mwisho na unaweza kuisoma na kuona kuwa yote ni fikra za Nyerere.
 
Mwanakijiji yasikukatishe tamaa haya..natamani sana kupata hotuba zaidi za Mwalimu...najua nyingi zinawakera wana CCM wa sasa zinawakosoa na kuwaumbua mno. Mwalimu Tutakukumbuka Daima.

hahahaha wala usiwe na shaka, ningekuwa mtu wa kukata tamaa kirahisi ningekata tamaa zamani. Yote ni sehemu ya mapambano ya kifikra.
 
Wakuu zangu,
Haya Haya nimesharudi nipo mjini T dot...Nina mengi sana ya kujadiliana haswa kuhusiana na mustakabali wa nchi yetu. Na niliahidi kuandika mengi sana, hivyo tuweni pamoja kufahamishana...Moja kubwa ambalo naweza jivuniani ni kwamba nimepata darasa kubwa la fikra za Wadanganyika,hivyo kufahamu vizuri WATU wana upeo gani na wanaipeleka wapi nchi yetu...
Ukistaajabu ya Mussa ya Firauni yatakushinda!
 
Tindikali, mwache Nyerere aitwe Nyerere na apambwe maua...

Na hicho ndio ninachokisema, nakubali kabisa kabisa. Tumwache Nyerere awe Nyerere, na tuache wanaompamba maua wampambe. Kabisa.

Lakini tusiyachanganye hayo mawili!

Weka ya Nyerere kama yalivyotoka mdomoni mwake au kwenye kalamu yake. Ukishamaliza hilo ndio sasa umuimbie mapambio kwa uchambuzi wako wewe kama wewe Boramaisha au Mwanakijiji. Na mimi nitajiunga huko kwenye uchambuzi huko, mbali na kuparaganyisha historia ya Nyerere.

Mwanakijiji anasema anataka kuwapa kizazi cha sasa kumbukumbu kuhusu Nyerere, siasa za wakati ule, maandishi yake, maneno na mengine ya historia yetu kwa ujumla. Lakini utawapaje kizazi kipya historia ya Nyerere na hotuba na vitabu vyake kwa kuchomeka ya kwako wewe katikati ya sentensi za Nyerere?

Aliyoyasema Nyerere yabaki bila mawaa, hata kama unaona alikosea Kiswahili, hakupanga aya zake vizuri, usidanganye kizazi kipya kwa kuhariri ya Nyerere.

Aliyoyasema Nyerere yabaki bila mawaa, hata kama unaona alikosea Kiswahili, hakupanga aya zake vizuri, usidanganye kizazi kipya kwa kuhariri ya Nyerere.

na kwanini hilo lisifanyike? kwa sababu hiyo hotuba ya Mei Mosi haikuwa imeandikwa hivyo, ilitolewa bila kuonesha transition ya kutoka mada moja kwenda nyingine au kurudia rudia maneno.. itakuwa ni ujinga kuweka hotuba hiyo "kama ilivyo" kwa ajlii ya watu kusoma, kwa sababu itakuwa ni ngumu kusomeka! Hili linafanywa sehemu zote duniani inapokuja kwenye kuandika hotuba zilizotolewa off the cuff.. Ukijua hili unaweza kuelewa kwanini hotuba hiyo iko hivyo.
 
Wakuu zangu,
Haya Haya nimesharudi nipo mjini T dot...Nina mengi sana ya kujadiliana haswa kuhusiana na mustakabali wa nchi yetu. Na niliahidi kuandika mengi sana, hivyo tuweni pamoja kufahamishana...Moja kubwa ambalo naweza jivuniani ni kwamba nimepata darasa kubwa la fikra za Wadanganyika,hivyo kufahamu vizuri WATU wana upeo gani na wanaipeleka wapi nchi yetu...
Ukistaajabu ya Mussa ya Firauni yatakushinda!

Bob tupe yaliyojiri huko ulikokuwa
 
tumuache Nyerere apumzike kwa amani.......
tukitaka kumuenzi kweli ni kufanya vitendo vya kweli vya kizalendo......
enough about Nyerere...................
 
n

...Hili linafanywa sehemu zote duniani inapokuja kwenye kuandika hotuba zilizotolewa off the cuff..

"Off the cuff" umejuaje? Umejuaje kwamba hotuba ya Nyerere aliitoa "off the cuff"? Ndo maana nakwambia unajivisha mamlaka ya usemaji wa ofisi ya Marehemu Mwalimu Nyerere. Umejuaje Nyerere alibwabwaja tu "off the cuff"?

Aidha, wanaotoa hati ya hotuba rasmi sio walioisikia uwanjani au kwenye radio kama wewe na mimi. Bali ofisi ya mtoa hotuba, tena mara nyingi kabla ya tukio. Wewe unajivika kilemba ukoka kama mamlaka ya nyaraka za rais mstaafu.

Kizazi kipya unachosema unakiandikia historia watakaposoma hayo yako na wakute rekodi za wengine zikionyesha kuwa Mwanakijiji hakuwa mamlaka ya alichoandika na kukisema Julius Nyerere kwa sababu anaongeza chumvi zake.

congratulations kwa kututushushia hii hotuba, lakini ingekuwa vizuri ikiwa kwenye audio
 
Back
Top Bottom