JF Exclusive: Dr. Ulimboka kwa maneno yake mwenyewe * Dakika chache baada ya mateso *

Waungwana tunapofanya maamuzi lazima tujue hasara na faida. Kweli Dr Ulimboka kapigwa, lakini mwenendo wake huu wa kuhamasisha migomo umeua watanzania wangapi?.

Kwa wenzetu wale Wanaharakati, mbona Uamsho wamepigwa sana huko Zanzibar na hatujawasikia mkitetea? Waislamu waliuliwa Mwembechai hatukusikia Vijana wa Kasikazini mkija juu kuonesha Uchungu. Tutumie akili tusisukumwe na MIHEMUKO.

What do you mean?
 
Mazungumzo ya Mwanakijiji na Dkt. Ulimboka muda mfupi baada ya kupatikana
Posted: 27 Jun 2012 12:04 PM PD

Audio kwa Hisani ya Wavuti blog Tafadhali Bofya Mazungumzo ya mwanakijiji.

Kwanza nimtakie Nafuu ya haraka Dr Ulimboka na pole kwa Familia yake.

Huu ni wakati mgumu na kila mtu atakuwa na maoni yake baada ya kusikiliza mahojiano hayo maoni yangu ni kuwa Mwankijiji amelichukuwa hili swala kishabiki kwa kuelemea upande Fulani

Pamoja na kulaani tukio lililomkuta Dr Ulimboka jambo ambalo wengi wetu tumelifanya. Mwanakijiji anatanguliza Madai/Tuhuma kuwa Kuna kila Dali kuwa Watu wa Usalama au Vyombo vya Usalama Vimehusika.

Na baada ya tuhuma ndio anajaribu, tena kwa mtu wa pili kujaribu kutafuta ukweli kama Dr Ulimboka anajuwa waliomteka ni Polisi au nani?
Yepi Maoni yako baada ya kusikia mahojiani hayo?
 

Yaani mimi nimekosa raha kabisa, hili linaweza kumtokea yeyote yule kisa kudai haki ambayo anaona anastahili au kukosoa utendaji wa hii Serikali ya wauaji.. Wanataka kuua mtu kwa kudai haki za madaktari tu!!! Hii Serikali haistahili kuendelea kuwepo madarakani.

Waungwana huyu mwenzetu na familia yake wanahitaji msaada wa kuweza kumuuguza. Naomba kutoa wazo ili uanzishwe mchango wa kumsaidia Dr Ulimboka.

Pamoja na kuwa kipigo alichopata Ulimboka hakikubaliki, reaction inayotoka kwa watu is so biased kiasi cha kufuta huruma ambayo tunaweza kumpatia huyo Ulimboka. Inasikitisha kuwa hata madaktari wamekumbwa na hiyo bias kiasi cha kusaliti ethics zao. Kwanza hatujapata ushahidi wa kuunganisha kilichompata Ulimboka na mgomo wa madaktari.
Ikiwa tutaunganisha mgomo wa madaktari na kilichompata Ulimboka then tutoe pia fare sympathy kwa walioteseka na waliopoteza maisha yao kutokana na mgomo wa madaktari.
Credibility ya madaktari, ambayo nasikitika kuwa imepotea kutokana na nia yao ya kuruhusu kupotea kwa maisha ambayo wameapa kuyalinda. Itakuwa vigumu sana kurejesha credibility

Inawezekana wengi wa wanaoshabikia mgomo sio madaktari kwa hiyo doctors be very careful. Msikubali kutumiwa, kwani baada ya hapo it will be you alone to pick the lost credibility in your consultion rooms
 
Hapana shida, nawe ndipo ukomo wa ufikiri wako ulipoishia. Mbuzi ni mbuzi hawezi kuwa simba na wala hatumlaumu!

Kavunjwa taya, anaweza kusema? kavunjwa mbavu anaweza kusema? kavunjwa makalio anaweza kusema? sasa avunjwe nini ndio anyamaze? kwi kwi kwi teh teh teh!

Huyo alichapwa makofi tu, hajahukumiwa kifo, ni chambo tu, tunawatafuta wavuvi.
 
Sehemu yake ya pili siwezi kuweka kwa sasa ili kuwaacha polisi wafanye kazi yao na tusije kuinfluence maelezo ya serikali.... Samahani kwa usumbufu wa nakala ya kwanzo ambayo ilikuwa haijahusisha sauti ya Ulimboka...

SIKILIA UPYA:
[video=youtube_share;jsfdj4SV1cg]http://youtu.be/jsfdj4SV1cg [/video]

Pole sana! Naona wame'mlimboka' tatizo langu mimi Watanzania wanapata ajali, wengine wanafumaniwa na kuchukuwa kipigo, wengine wanagongwa na magari, wengine magari yanagongana na wanapoteza viungo, wengine wanapigwa na wanaume zao, sasa hawa wote wakienda hospitali katika hali kama iliyomkuta Dr. Ulimboka wanakumbana na mgomo wa Madaktari, je mtu si anaweza kulemaa au kupoteza maisha?

Katika migomo iliyopita kuna watu walikuwa katika hali kama ya Dr. Ulimboka na hawakupata huduma ya kitabibu na wengine walikufa hawa wote ni watanzania wenzetu wao hakuna aliyewalimboka ni maradhi tu na kama yangepata matibabu maisha yao yangeweza okolewa, ndiyo maana bado nasema kuwa kugoma au kuasi kwa madaktari ni sawa na kuasi kwa jeshi ambao ni Uhaini, mwisho wake watanzania wanapoteza maisha.

Dkt. Ulimboka Bwana akusaidia upone haraka! Adha wanayopata watanzania wanapokosa tiba inakuwa sawa na hali kama yako ukikosa matibabu, Mwenyezi Mungu atuongoze kwa hekima na tuwaachie siasa wanasiasa!
 
Sina la kuzongumza ila nilijua haya yatafuatia na ndio maana mgomo wa kwanza nilisema wazi kuwa Ulimboka atawekwa mfukoni na ikishindikana atatafutiwa dawa yake - Kolimbiwa!. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba amekuwa bangusilo la mgomo ambao ungeweza kabisa kumalizika siku zile za mwanzo wakati madaktari walipogoma na kutaka waziri wajiuzuru kwanza ili mazungumzo yaendelee. hawa wasingebaidlisha mfumo maana tatizo ni la kimfumo.

Watanzania tumepumbazwa sana na sidhani hizo elimu zenu mnazochukua vyuoni mnazichukulia kama maandilizi ya msingi mzuri wa maisha bali ticket ya maisha bora. Binafsi yangu, nijaribu sana kufikiria nje ya box hasa napotambua kwamba ka ujumla wetu Healthcare imekuwa ikitumia zaidi ya asilimia 80 ktk matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) na yale ya Maendeleo kwa asilimia 19 kama tumeongeza sana labda imefika leo asilimia 30 nayo sina hakika, maana kwa mwendo huu sii ajabu tunaliwa zote hakuna fungu la maendeleo.

Sasa tunapokuja ktk swala la malipo mahala ambapo watu tunaitaka serikali ipunguze matumizi yake na kuweka nguvu zaidi ktk Maendeleo nashindwa kupata jibu rahisi haswa ktk mgogoro huu ambao unataka fedha zaidi ziende ktk recurrent. Na kulipwa kwa Wabunge na viongozi wetu wote ni mabillioni ya fedha kama mishahara, magari, nyumba na posho ati ugumu wa maisha kwao, haiwezi kupoteza ukweli kwamba wananchi tunaibiwa macho macho na hatuwezi pata maendeleo hata kidogo. Na sintokubaliana na yeyote anayetumia kigezo hiki hata kidogo kwa sababu tunahitaji zaidi ujenzi wa vyanzo (miundombinu) na sio malipo ya viongozi na wataalam kuwa kipimo cha maendeleo yetu. Nitaendelea kuamini maneno ya mwalimu ya kwamba fedha sio msingi wa Maendeleo na kama kweli tunapiga vita matumizi mabaya ya kodi za wananchi basi tuendelee kupiga vita malipo yasiyokuwa na tija kwetu, tutangulize Uzalendo.

Juzi tu wabunge wamejiongezea mishahara baada ya kuona posho hazikubaliki wananchi tumekaa kimyaa tunataka madaktari na walimu nao walipwe zaidi, fedha hizo zitatoka wapi?. Jamani jamani, sasa kama leo tunatumia asilimia 80 kwa matumizi ya kawaida tukiongeza mishahara ya watu na posho zao ina maana tutapunguza zaidi fungu la maendeleo maana huwezi toa sehemu nyigine yoyote. Haya ukitazama tena nimesikia donors wanatoa nusu ya budget nzima ya AFYA, hizi fedha zinatumiwa sii ktk maendeleo bali kujilipa wao na AFYA ndio ngome kubwa wanayoitumia serikali kuombea misaada maana tumeonyesha unyonge zaidi, sasa wakija tokea kina Ulimboka ambao lengo lao ni kukatisha hii misaada (bila kujua) mnafikiri kweli watawaacha?..
Tusichoke kumuombea Dr.Ulimboka lakini pia tukumbuke tupo vitani na adui yetu sii mwingine isipokuwa matumizi mabaya ya fedha za serikali.
 
Pamoja na lawama kutoka pande tofauti za jamii, hasa wanaosupport kupigwa kwa Dr. Ulimboka, bado nasisitiza huko tunakoipeleka Tanzania siko hata kidogo.
 
Dah natamani wakufanye wewe?
nyoka haezi kula mkia wake mwenyewe..
Halafu nashukuru umenijulisha kumbe ni serikali iliyofanya unyama huo
nimekujulisha au mi-emotion yako imekupelekea kwene conclusion uliyoikusudia?
Lakini si mbaya watatanguliza wengine,wao wataishi milele?
utakuta hilo limtu lililotoa oda ya kuuwa linakaribia miaka sabini au zaidi yaani maisha yanakaria usiku kwake linataka laana tu na sbbu ya kumwona lucifer.Ila amini usiamin yupo Mungu anayehukumu kwa haki.
haya mabreka..
 
Pamoja na kuwa kipigo alichopata Ulimboka hakikubaliki, reaction inayotoka kwa watu is so biased kiasi cha kufuta huruma ambayo tunaweza kumpatia huyo Ulimboka. Inasikitisha kuwa hata madaktari wamekumbwa na hiyo bias kiasi cha kusaliti ethics zao. Kwanza hatujapata ushahidi wa kuunganisha kilichompata Ulimboka na mgomo wa madaktari.
Ikiwa tutaunganisha mgomo wa madaktari na kilichompata Ulimboka then tutoe pia fare sympathy kwa walioteseka na waliopoteza maisha yao kutokana na mgomo wa madaktari.
Credibility ya madaktari, ambayo nasikitika kuwa imepotea kutokana na nia yao ya kuruhusu kupotea kwa maisha ambayo wameapa kuyalinda. Itakuwa vigumu sana kurejesha credibility

Inawezekana wengi wa wanaoshabikia mgomo sio madaktari kwa hiyo doctors be very careful. Msikubali kutumiwa, kwani baada ya hapo it will be you alone to pick the lost credibility in your consultion rooms
Uchafu mtupu. Napata kinyaa kabisa. Pptuuuuu!!!
 
Ktk larger picture everything could be justified. Jamii ni muhimu kuliko individual.

Do you think the strike has got anything to do with this individual? Mbona Papaa Msofe anafanya anayofanya na kila siku anapeta? Au kwasababu dogo ameonekana ni kiongozi sehemu ambapo wengine wangeamua kuwa vibaraka? Hivi kweli Dr. Ulimboka ni threat kiasi kwamba anastahili kufanyiwa aliyofanyiwa? And then waliofanya wamepata nini? Ubabe huzaa matatizo mengi kuliko hekima na usikivu. kama nia ya kumaliza matatizo yaliyopo sector ya afya ipo, hakutakuja kuwa na mgomo.Watu watakubaliana kukaa meza moja na kuweka vipaumbele vya nini kianze na kipi kifuatie baadae. Tanzania bwana viongozi wetu wana ego sana...sehemu yenye tatizo dogo badala ya kutumia hekima wanalikuza mpaka linakuwa kero kwa kila mtu.
Mkuu siamini madaktari ni watu waovu...ila njia zetu za kutatua mambo zimejaa fikra finyu. Badala ya kutatua tatizo sasa wameliongeza. Inamsaidia nani sasa?
 
Ni Mattumaini yangu kuwa kwa nguvu za Mwenyezi Mungu Dkt Ulimbaka atapona na ataweza kutoa Maelezo ya Kisa na Tukio lililomkuta kwa Ufasaha zaidi. Kuna maswali mengi yanayohitaji Majibu na baadhi ya hayo ni Muhusika tu ndio anaweza kuyajibu, Na baadhi nyingine Itaweza kujibiwa na Wahalifu wa tukio hili watakapopatikana.
Kinchoshangaza na kusikitisha ni sisi hapa Jf wengi wetu kufikia uamuzi kuwa Serekali au Vyombo vyake Vimehusika. Nimejaribu kusoma makala kadhaa hapa ( people are just jumping to conclusion that the Government is Responsible to the act of harming Dr Ulimboka) Hata wale waandishi mahiri niliodhani wangeweza kuweka uwiano/balance ya kuonyesha kuwa Every one is innocent until proven Guilty! Wametekwa na wimbi la Huzuni na upendeleo.Nilitarajia kuona mjadala wa Upeo, lakini upeo wa wengi unaishia pale waliposimama, chini ya miguu yao.
 
Jujuman,
Mkuu wangu mbona mnatetea vitu ambavyo viko wazi kabisa?.. wameondoka wangapi ktk hali za utatanishi wakati inajulikana kabisa kwamba Wamekolimbiwa? Hivi ktk fikra zenu mnafikiri kitendo kama hiki serikali watakifanya wazi na kuacha ushahidi unaoonyesha wazi kwamba wanahusika? I mean how stupid can be! waridhishe watu wote kwamba serikali yetu inahusika.

Swala la mgomo wa madaktari ni hatari sana ktk utawala wa CCM na JK na usitegemee kabisa kwamba wangelifumbia macho. Tuombe Mungu Ulimboka atoke sala but still I doubt tutakuwa naye, maana mtu kufuatwa leaders club halafu akapotea sii swala la ujambazi wa kawaida ama kudaiana. Tumefika njia panda na yawezekana kabisa vifo vingine vikafuata. Na kwa pande zote mbili, hiii sio ktk kutafuta suluhu bali kukomeshana.
 
Asante mkijiji inatia uchungu sana. Hivi nyie mnaosema hakuna kitu sikiliza toka mwanzo hadi mwisho sio mnasikiliza mwanzoni halafu mnaanza kulaumu. Dr Ulimboka sauti yake inasikika anasema alivyopigwa nakupelekwa kwenye nyumba nzuri ila haitambui ni sehemu gani kwa vile alifungwa kitambaa cheusi usoni. Jamani tumshukuru mkjj kwa video yake hii.

Ila serikali imechoka na leo wametoa tamko Bungeni kuwa kesho litakalokuwa na liwe. Hili neno lina maana nyingi na wanaposema hivyo ujue kwamba 2015 kuachia ngazi kwa ccmafisi itakuwa ngoma yaani tutmwaga damu kama yaliyotokea kenya. Kama mgomo tu wa Madakatari ndio hivi. Itkuwaje kwa chama cha ccmafisi kuondolewa madarakani.

Hivyo Watanganyika wote tujiandae kwa kuwaondoa kwa kura na wakikataa kwa njia ya kura basi tutamwaga damu. Ila hatutakubali tena kutawaliwa na ccmafisi. Akina sijui nchemba wanasema wao na wanauchumi makini wa BOT ilikuwaje pesa zikaibiwa BOT.

Hivi hizi pesa za EPA, MEREMETA,TANGOLD, RADA, Ritchmond zingedhibitiwa na kulipwa madaktari, walimu hivi leo hii madakatari wangegoma. Matokeo yake wezi walimbiwa rudisheni. Akina Mramba, Yona, Mngoja, Chenge, Rostam, Lowassa wanadunda mitaani na tunawaabudu halafu useme kuwa serikali ya ccmafisi ni wasikivu. Yana mwisho na mwisho wao 2015.
Sasa hivi ni 2018. Hakuna lililofanyika. Hakuna cha damu kumwagika hakuna cha nini.
 
Back
Top Bottom