Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,577
Coach Parcells, kwa kifupi,May someone please explain what this is all about?
1. Baada ya ICC kuitioza Tanesco walipe zile US$65m plus interest ambazo zinaitwa tozo za Dowans.
2. Tozo hiyo inapaswa isajiliwe na Mahakama Kuu hapa nchini ili iweze kuwa enforceble by lacal laws, yaani Tanesco wawajibike/kulazimishwa kulipa.
3. Kabla mahakama kuu haijatoa uamuzi wa kuisajili tozo hiyo, tayari kuna kesi nyingine 4 zimefunguliwa mahakama kuu kupinga kulipwa kwa tozo hiyo.
4. Hivyo uamuzi wa mahakama kuu kuisajili tozo hiyo unaweza kuchelewa mpaka Desemba 2011 au zaidi ili kuzosikiliza pingamizi hizo.
5. Ili mshitaki Dowans asizidi kupoteza haki zake, ameipandisha Tanesco kwenye mahakama ya Uingereza, akiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kukazia hukumu ya ICC, kwa kuiomba itoe kibali cha kuzishika mali za Tanesco zilizoko Uingereza au Jumuiya ya Ulaya ili mali hizo zitumike kama dhamana/security ya kuishinikiza Tanesco kulipo tozo husika.
6. Hiyo mahakama hiyo ya Uingereza imeitaka Tanesco kulipa Dola Milioni 5 zitumike kama security kusubiri uamuzi wa Mahakama kuu ya Tanzania kuisajili tozo ya Dowans.
7. Mahakama hiyo imeridia msimao wa mkataba ule ambao kwa ridhaa yao wenyewe waliamua uamuzi wa ICC ndio wa mwisho na haukutakiwa kupingwa wala kucheleweshwa.
My Take.
Wana bodi wenzangu, hii ni issue ya kisheria na sio kisiasa, nawashauri tupunguze kidogo politics kwenye masuala ya kisheria. Niliwahi kusisitiza, ule mkataba ni mkataba bomu, Tanesco walijifunga na hawana pa kutokea dawa ni kulipa tuu!.
Ila pia naungana na hoja za Tanesco kuwa wao hawalipi kwa vile aliyewaingiza kwenye mtego huo ni serikali, hivyo ni jukumu la serikali kulipa na sio Tanesco.
Nyerere angekuwa ni rais wa nchi hii, tungevunja uhusiano na ICC, tusingelipa chochote!, mitambo tungetaifisha!, hao wawekezaji wa ulaya wangefungasha virago vyao na kwenda makwao wakatengeneze dhahabu na gesi zao huko viwandani kwao. Wachina wangetuletea teknolojia ya kuichimba dhahabu yetu, gesi yetu na mafuta yetu huku faida asilimia 100%, ikibaki ni mali yetu, kuliko sasa wanavyochimba hawa maharamia kwa jina la waweklezaji, wakikomba asilimia 98% huku wakituachia asilimia 2% eti ndio royality!.
Lakini kwa vile siye yeye, waliopo wanaheshimu utawala wa sheria, wawekezaji ndio tunawanyenyekea na kuwalamba miguu, amini nawaambieni, Tozo tutalipa, tena sio Tanesco, bali serikali kwa kodi zetu!.