Jeshi sasa laanza biashara ya ulinzi

Halafu kuna mashirika ya nje toka South Afrika na Ulaya yanafanya kazi hizo hizo sijasikia Watu wakiyalaumu ama kuyawekea mashaka kama JKT wakati wanatumia watu wale wale..
Kwa nini nasi tusiwe na chombo chetu cha kujivunia ambacho kinaweza kufanya ulinzi kama chombo cha kitaifa ambacho kinaweza kabisa kulinda nchi yetu.
 
Mimi naona nchi kuwa na Jeshi halafu kutumia hao hao wanajeshi kulinda kiwanda cha mfanyabiasha ni matusi mazito sana kwa vijana wetu wanaojiunga na hilo jeshi. JKT...Jeshi la Kujenga Taifa..key word "JESHI".

Kama wanaona wanaweza kufanya biashara basi walivunje hilo JKT kisha waanzishe kitu kama Blackwater ili afanye kazi au biashara watakazo.
 
Bingo, kila kitu kiwe na mandate yake. Mandate ya JKT sio kufanya umachinga wa ulinzi. Acheni sekta binafsi zifanye hayo mambo.

Kila siku tunakoroga vitu vyote pamoja na unapofika wakati wa kutoa thathmini tunashindwa.
 
Yebo Yebo,
Mkuu neno jeshi lisikutishe ukafikiria tuuu vita..Jeshi inaweza kuwa la zima moto ama kikundi ambacho kiko well equiped kuzuia magendo na wasibebe silaha. hapa swala ni JKT kubeba silaha ndilo linatisha na kweli kulingana na watu na maziungira yetu kuwapa vijana silaha kulinda wakati wana njaa mengi yanaweza kutokea. Hata hivyo Utaratibu kama wa Polisi au JKT wenyewe kuwa kuna mmoja wao tu ambaye anaaminika ndiye hubeba risasi za moto wengine wana baruti tu...Ni muhimu kuunda muundo mpya wa jeshi la ulinzi kwa kutazama mashirika ya nje yanafanya nini kuzuia tamaa za askari wao ktk ulinzi na ni precautional principal zipi hutumika ktk kuunda vyombo hivi.

Kisha kuna mashirika ya nje yanatupiga bao leo hii tena yanachunga hadi fedha za benki zetu. wanaweza piga mission wakachukua mabillioni ya fedha wakaingia kizani kama walivyotupata Green bank..Ni bora kuwa na mtu wako ambaye hata akikimbia atakwenda wapi! uwezekano wa kumkamata na kumrudisha hata akiwa nchi za nje ni mkubwa kuliko hao wageni ambao tunawatetemekea na kuwapa ulinzi.
 
JESHI limedekezwa mno wakidhani kazi ni kupigana kwa bunduki tu. Tukubaliane wana jf KUWA jESHI LA 2009 LINAHITAJI KUPANGWA ILI SIO TU KUFANYA KAZI ZA ULINZI BALI PIA KUZALISHA MATREKTA, KOMPYUTA, SATELAITI, MAGARI, NDEGE, MALORI YA KIVITA, NA VIFAA MBALIMBALI VYA KIRAIA NA KIJESHI KWA MATUMIZI YA wATANZANIA NA MAUZO NCHI ZA NJE!
 
Usinikumbushe MEREMETA na utapeli wa kiwanda cha jeshi cha magari yanayoitwa NYUMBU pale Kibaha, badala ya kuendelea nasikia siku hizi wanafua vyuma chakavu na kutengeneza ringi za baiskeli sio gari tena.
 
Back
Top Bottom