Jeshi Letu La Polisi na Jerry Muro, Je Maadili na miiko ya kaziutendaji vilizingatiwa

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
247
Jerry Muro ameweza kuthibitisha kuwa bunduki na pingu alikuwa akizimiliki kihalali.
Kauli alizokuwa akizitoa Kova kwa vyombo vya habari zilikuwa ni za ukandamizaji na zilikuwa zinaonyesha bayana kuwa kuna visasi dhidi ya bwana Muro.
Je kwa namna hiyo ya utendaji, jeshi letu ni chombo salama cha ulinzi wa jamii?
Kama sio, kwanini lisivunjwe kwa kukiuka miiko na maadili ya UPOLISI?
 
Sasa hivi naona nibaki kuwa msomaji tu wa hili sakata maana kila iitwapo leo mambo yanaenda yakiongezeka.
 
Hili sakata bana lazima limtokee KOVA puani, walioko chini yake wamemdanganya. Hainiingii akilini eti CCTV kamera imewanasa Muro na wale matapeli wamekaa meza moja HOTELINI, hivi zile meza za hoteli zinazuia watu kukaa pamoja, so mimi nikienda kukaa pale na wale jamaa matapeli CCTV ikikamata basi na mie mwizi au napokea rushwa? tafadhali KOVA, hiyo CCTV ilinasa na mazungumzo? ni ushahidi gani unaoushabikia ambao hata mtoto wa darasa la pili hawezi kukubaliana na wewe?. Dhairi ilipangwa wale jamaa wamtafute Muro wakae naye kwenye hiyo hoteli CCTV ikamate ili waweze jenga tuhuma dhidi ya Muro. Polisi hatuna imani na nyie kabisaaaaaaaaaaaaa
 
Habari ndiyo hiyo. Nami naamini katika hili. Penye udhia penyeza rupia. Hizo CCTV zingekuwepo za kufuatilia mambo hayo kwa nini wasingeziweka barabarani kuonyesha makosa ya madereva badala ya polisi wala rushwa?
 
Kwa vile hili suala lipo mahakamani ngoja tusubiri ushahidi utakaoletwa na upande wa mashitaka. Ila nasikia huyo dogo naye yumo sana kwenye mambo ya mshiko!
 
Hili sakata bana lazima limtokee KOVA puani, walioko chini yake wamemdanganya. Hainiingii akilini eti CCTV kamera imewanasa Muro na wale matapeli wamekaa meza moja HOTELINI, hivi zile meza za hoteli zinazuia watu kukaa pamoja, so mimi nikienda kukaa pale na wale jamaa matapeli CCTV ikikamata basi na mie mwizi au napokea rushwa? tafadhali KOVA, hiyo CCTV ilinasa na mazungumzo? ni ushahidi gani unaoushabikia ambao hata mtoto wa darasa la pili hawezi kukubaliana na wewe?. Dhairi ilipangwa wale jamaa wamtafute Muro wakae naye kwenye hiyo hoteli CCTV ikamate ili waweze jenga tuhuma dhidi ya Muro. Polisi hatuna imani na nyie kabisaaaaaaaaaaaaa

Mbona katika matukio mengine sijawahi kusikia CCTV cameras zikifanya kazi au zimeanza kufanya kazi kwa Jerry Muro? Hata kama kuna ukweli kwamba Muro alidai hongo kuna mambo mengi yanayonekana kama yamepikwa!
 
Jerry Muro ameweza kuthibitisha kuwa bunduki na pingu alikuwa akizimiliki kihalali.
Kauli alizokuwa akizitoa Kova kwa vyombo vya habari zilikuwa ni za ukandamizaji na zilikuwa zinaonyesha bayana kuwa kuna visasi dhidi ya bwana Muro.
Je kwa namna hiyo ya utendaji, jeshi letu ni chombo salama cha ulinzi wa jamii?
Kama sio, kwanini lisivunjwe kwa kukiuka miiko na maadili ya UPOLISI?
Amethibitisha lini leo,Maana Kova alisema kuwa mtu yeyote hana mamlaka ya kumiliki pingu...
 
Ya Jerry Muro yamepita - Sasa tupo na sakata la kuchinja watu huko Musoma - TZ saafi sana: kwenye science ya uzazi mwenendo kama huu unaitwa premature ejaculation - tunamaliza mambo muhimu haraka na kusahau
 
Kwani kesi ya huyu bwana imeisha vipi? Na je anaendelea kuwajibika katika kazi yake luningani hebu tupashane jamani
 
Back
Top Bottom