Jeshi la Zanzibar

golwebo_mkuu

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
2,271
688
Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenzake akiwa Tanganyika. Sifa moja ya nchi kamili ni kuwa na jeshi la ulinzi la kulinda mipaka na watu wake. Lakini naomba niulize swala moja tu....
Hivi wandugu, Zanzibar kuna jeshi kamili? kwa nini mara kadhaa wanajeshi wanapelekwa zanzibar kutuliza hata fujo za wahuni tu? au JMT inahesabu zanzibar kama mkoa?
Mwenye ufahamu kuhusu muundo wa jeshi Zanzibar anifahamishe tafadhali!
 
Fuatilia hotuba ya Tundu Lissu Bungeni kipindi cha bajeti. Alieleza vizuri sana kuhusu hili. In short, Zanzibar ina Jeshi.
 
Zanzibar sio nchi, ilikuwa kabla haijajiunga na nchi nyingine Tanganyika. ina mgambo kama wale wa vijijini Mwanza.
 
Ina Mgambo wanaitwa KMKM..nchi hii kuna jeshi moja tu la ulinzi-JWTZ(Jeshi la Wananchi la Tanganyika)..na amri jeshi ni Rais wa Tanganyika..uyo rais wa mtaa wa Znz ni picha tu.
 
Ina Mgambo wanaitwa KMKM..nchi hii kuna jeshi moja tu la ulinzi-JWTZ(Jeshi la Wananchi la Tanganyika)..na amri jeshi ni Rais wa Tanganyika..uyo rais wa mtaa wa Znz ni picha tu.
Kazi kwelikweli. Uamsho wataamka sasa hivi.
 
Kuna nchi hazina jeshi na ziko salama bila ya matatizo yoyote, sio lazima nchi iwe na jeshi, mfano Andorra , San Marino , Lichtenstein na Monaco.Zanzibar wana jeshi la baharini KMKM ambao hulinda bahari ya Zanzibar. Kama Zanzibar ni nchi au si nchi huu ni mjadala mwengine
 
Ina Mgambo wanaitwa KMKM..nchi hii kuna jeshi moja tu la ulinzi-JWTZ(Jeshi la Wananchi la Tanganyika)..na amri jeshi ni Rais wa Tanganyika..uyo rais wa mtaa wa Znz ni picha tu.
Lakini huyu wa Tz kule hasemi kitu, hawezi kumfuta kazi hata mkuu wa wilaya...hii imekaaje ? Hawezi kugawa mkoa wala wilaya...lakini hiyo Picha inafanya hayo.
Mawazo yangu tu mkuu
 
Lakini huyu wa Tz kule hasemi kitu, hawezi kumfuta kazi hata mkuu wa wilaya...hii imekaaje ? Hawezi kugawa mkoa wala wilaya...lakini hiyo Picha inafanya hayo.
Mawazo yangu tu mkuu

Rais wa JMT ana madaraka makubwa sana hata visiwani, tatizo ni kuwa hawa viongozi wetu ni waoga na dhaifu kusimamia katiba au wanaivunja makusudi. Kamuulize Rais mstaafu Jumbe kama hakufutwa kazi na Mwalimu au muulize Seif Sharif
 
Lakini huyu wa Tz kule hasemi kitu, hawezi kumfuta kazi hata mkuu wa wilaya...hii imekaaje ? Hawezi kugawa mkoa wala wilaya...lakini hiyo Picha inafanya hayo.
Mawazo yangu tu mkuu

Jumbe alifukuzwa kazi na Nyerere. Kila jambo la Znz linaamriwa Dodoma. Znz ni mkoa yu kama Mwanza ama Iringa. Kikwete anao uwezo wa kupanga wakuu wa wilaya huko znz na bila shaka anafanya hivyo. Huyo anayeitwa Raidi wa znz ni geresha toto na kuwafunga domo wazanzibar.
 
Kazi kwelikweli. Uamsho wataamka sasa hivi.
amsho1.JPG

litaongozwa na huyu kamanda wao hatari
 
Seif na Jumbe wamefukuzwa kutoka kwenye CCM ( CCM ndo kilikuwa chama pekee , kwa hiyo hawakuweza kukaa madarakani bila ya tiketi cha chama ) , na kipindi kile hakuna wwa kumjibu Mwalimu , kibao kiligeuka alipokaa Salmin
 
Kumbe tunazungumzia ushabiki !!! sijasikia raisi yoyote wa TZ kutangaza/ kufukuza kazi wakuu wa wilaya au mikoa kule ZNZ , ukianzia kwa Mwalimu hata mpaka huyu .
 
Zanzibar sio nchi, ilikuwa kabla haijajiunga na nchi nyingine Tanganyika. ina mgambo kama wale wa vijijini Mwanza.
Mtoto wa mkulima mbona alishafunga mjadala? SIYO NCHI ni wilaya katika mkoa wa Dar au unataka tumwite aje alie hapa jf
 
Back
Top Bottom