Jeshi la wananchi (kambi ya gongo la mboto) limeasi?

Hii habari binafsi nimesimuliwa na mkazi wa g.mboto kwa njia ya simu "Ebwana kuna mwanajeshi kavamiwa na wananchi kapigwa kweli kisa eti wanasema wanajeshi walifanya makusudi kulipua mabomu" kiukweli nlifadhaishwa sana,gafla akapga simu tena "jamaa wamerudi wanagawa kpgo hapa nipo njian nakimbia" jamaa unapoleta hoja kama hiyo nivema utoe sababu zilizosababisha kuliko kuleta hoja ambazo zitatuwekea uadui na walinzi wa taifa letu! Kiukweli jamaa wanafany kazi ngumu mno,binafsi nimetokea mipakan 'hawalali kutulinda sisi' inaleta hasira unamlinda mtu tena kwa kujitolea then mnampga mmojawao What are we expecting?

kazi kubwa mno????? walipwa kod zetu... ata kama wananchi ndo wameanza kwani wao wapo juu ya sheria??? why wachukue sheria mkonono????
polis /jeshi usalama wa raia?????:A S 13::nono::shetani::shetani:

POLIS JESHI...UHASAMA NA RAIA WEMA WAZALENDO WANAOWALIPA KWA KODI ZAO.....

Kama wananguvu sana hawa wanajeshi wangekaziwa mashamba makubwa wasaidie kulima na kuzalisha chakula nchi ....
 
Wanajeshi waliomuua Fundikira wafikishwa Mahakamani! Wednesday, January 27, 2010

Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira, marehemu, Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi wakiwa katika chumba cha Mahakama leo

Washtakiwa wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Geni Vitus Dudu na mashtaka yameendeshwa na wakili wa serikali Monica Mbogo aliyekuwa akisaidiwa na Beatrice Mpangala
 
Askari wa barabarani apigwa na wanajeshi wa JWTZ
Wednesday, May 20, 2009 11:49 AM
ASKARI wa usalama barabarani Sajenti Thomas Mayapila amepata kipigo kutoka kwa wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania [JWTZ] kwa madai kuwa walicheleweshwa kupita katika taa za makutano ili kuendelea na safari zao. Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 1:30 asubuhi katika makutano ya barabara ya Morogoro na Sum Nujoma eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kwa kawaida eneo hilo la Ubungo maarufu kama ‘Ubungo Mataa' linakuwa na usumbufu wa aina yake kwa kuwa kunakuwa na misururu ya magari katika pande zote nne kutaka kupita katika mataa hayo na kupelekea hadi askari wanaoongoza magari hayo kuchanganyikiwa.
 
Hii habari binafsi nimesimuliwa na mkazi wa g.mboto kwa njia ya simu "Ebwana kuna mwanajeshi kavamiwa na wananchi kapigwa kweli kisa eti wanasema wanajeshi walifanya makusudi kulipua mabomu" kiukweli nlifadhaishwa sana,gafla akapga simu tena "jamaa wamerudi wanagawa kpgo hapa nipo njian nakimbia" jamaa unapoleta hoja kama hiyo nivema utoe sababu zilizosababisha kuliko kuleta hoja ambazo zitatuwekea uadui na walinzi wa taifa letu! Kiukweli jamaa wanafany kazi ngumu mno,binafsi nimetokea mipakan 'hawalali kutulinda sisi' inaleta hasira unamlinda mtu tena kwa kujitolea then mnampga mmojawao What are we expecting?
Aidha wewe ulizaliwa 'enzi za mawe' ukagandishwa kwenye chemba za gas kama Austin Powers na leo hii ndio 'umerudishwa duniani' hivyo bado una mawazo ya enzi za mawe AU wewe kazi yako ni mwanajeshi na kabila lako ni mkurya na umeishia darasa la saba!!!
 
Hii habari binafsi nimesimuliwa na mkazi wa g.mboto kwa njia ya simu "Ebwana kuna mwanajeshi kavamiwa na wananchi kapigwa kweli kisa eti wanasema wanajeshi walifanya makusudi kulipua mabomu" kiukweli nlifadhaishwa sana,gafla akapga simu tena "jamaa wamerudi wanagawa kpgo hapa nipo njian nakimbia" jamaa unapoleta hoja kama hiyo nivema utoe sababu zilizosababisha kuliko kuleta hoja ambazo zitatuwekea uadui na walinzi wa taifa letu! Kiukweli jamaa wanafany kazi ngumu mno,binafsi nimetokea mipakan 'hawalali kutulinda sisi' inaleta hasira unamlinda mtu tena kwa kujitolea then mnampga mmojawao What are we expecting?
Ndugu yangu Napo, hii taarifa ya kwamba kuna mwanajeshi alipigwa ndo naisikia toka kwako. Mimi jana wakati napokea kipigo sikuambiwa kosa langu ni nini? Na kama hiyo ndiyo sababu, huoni kama tuna jeshi la vichaa? Hivi huyo mwanajeshi alipigwa na kila mwananchi wa gongo la mboto? walikuwa wananchi wangapi waliompiga huyo mwanajeshi? Iwaje sasa wanajeshi watuibukie wote bila kujali kwamba wengine tuna majukumu yetu na heshima zetu, wanatushushia kipigo njiani tena tukiwa na watu tunaowaheshimu?

Kama hii ilikuwa ni revenge ya wanajeshi hawa dhidi ya wananchi wachache waliompiga huyo mwanajeshi (bila shaka walipigana kwenye ulevi), basi nashawishika kuamini kwamba jeshini kuna watu wasio na akili timamu. Lakini pia inashangaza sana kusikia eti wanajeshi wanalinda nchi kwa kujitolea. Kauli kama hii ni ya watu wasiokuwa na uwezo mzuri wa kufikiria na kuchambua mambo. Kama wanajeshi wanajitolea kuwalinda wananchi, walimu wanaliokuwezesha wewe kujua hata kuandika haya unayoyaandika wasemaje, na madaktari wanaookoa uhai wa watanzania kila kuchapo wasemaje? Mahakimu je, wanaofanya kazi ya kutetea haki zinazodhulumiwa wasemaje? Uanajeshi ni ajira kama zilivyo ajira nyingine zozote. Wanalipwa mshahara na malupulupu kibao. Kama wanaona kazi wanayoifanya ni ngumu sana kwa ajili ya taifa hili, kwanini wasiache na kuingia katika kazi nyingine ambazo siyo ngumu.

Ninafikiri kuna haja ya kulitafutia kazi hili jeshi letu, maana tangu lipigane na Iddi Amini halijapata kazi nyingine ya kufanya, ndiyo maana linafanya mazoezi ya kuwalipulia mabomu wananchi wake na mazoezi ya kutudunda sisi baadala ya kudunda maadui wa nchi hii. Kila siku wahamiaji haramu wanaingia nchini na wakenya kibao wanakuja kutuulia tembo wetu na faru wetu kule Serengeti na hakuna chochote kinachofanyika. Hilo jeshi linalinda mipaka ya wapi, na hawa maharamia wanaowinda ndovu wetu wanaingilia wapi? Jeshi la Tanzania naweza kusema ni jeshi ambalo ni corrupt, halina tena sifa za kulinda usalama wa nchi.
 
Katika namna ambayo inatia mashaka, kambi ya jeshi ya gongo la mboto imeendeleza mfululizo wa mauaji, ukatili, unyama na ubabe kwa wananchi wasio na hatia. Wakati wananchi wakiendelea kuugulia maumivu ya mabomu yanayoaminika kulipuliwa kwa makusudi na wanajeshi hao wa gongo la mboto, jana wanajeshi hao walitinga mitaani na kuanza kutembeza kichapo kwa raia wasio na hatia. Kwangu mimi, hii ni ishara kwamba wanajeshi hawa wa kambi ya jeshi ya gongo la mboto hawapo kwa ajili ya ulinzi wa wananchi bali wapo kwa ajili ya kuangamiza na kuteketeza wananchi wa maeneo ya jirani. Hii inanipa shaka pia kwamba wanajeshi hawa wanye hasira na wananchi, wanaweza kuyalipua tena mabomu yaliyobakia pale ghalani ili kuwamaliza kabisa wananchi walio karibu na kambi hii au wa Dar es salaam nzima kwa kuwa tumeambiwa yaliyobakia ni makubwa zaidi ya yaliyolipuka.

Kuna ushahidi mwingi wa kimazingira unaoonyesha kwamba mabomu ya gongo la mboto yalilipuliwa kwa makusudi ili kuwaua na kuwaangamiza watanzania wasio na hatia. Ushahidi mmojawapo ni kitendo cha wanajeshi hao kuhamisha familia zao mapema asubuhi kabla ya milipuko na kutokuwepo kwa wanajeshi wengine hapo kambini isipokuwa walinzi. Kama wanajeshi hawa walijua kungekuwa na milipuko hiyo, kwanini hawakuwatangazia wananchi ili wakae mbali na maeneo ya jeshi? Huu ni ushahidi tosha kwamba pana uasi hapa! Kwa mazingira ya ulipukaji wa mabomu, na kwa yale yaliyofanyika jana, ya wanajeshi kuwavamia raia wasio na hatia na kuwachapa, najiridhisha kwamba wanajeshi wa kambi hii wameshaasi, na hivyo siku si nyingi wanaweza kushika bunduki na kuingia mitaani kutuua kwa risasi baada ya jaribio la kutuua kwa mabomu kutokuzaa matunda yaliyotarajiwa.

Mwisho natoa wito kwa wakaazi wa gongo la mboto na maeneo ya jirani kuandaa maandamano ya kulipinga jeshi hili lililoasi na pia kumpinga Kikwete kwa kuwa ameshindwa kusoma alama za nyakati na kuchukua hatua.

Imekuwaje hawa wanajeshi waanze tu kuasi? Hivi wanapokwenda kwenye kazi za kijeshi, ndani na nje ya nchi wanalipwa malipo yao jinsi inavyostahili? Hivi hali za wanajeshi wetu zikoje? Hawana jambo lolote linalowasumbua sumbua kuona kama hawathaminiwi?
Je nidhamu ndani ya jeshi nayo ikoje na hii inaanzia juu kabisa mpaka kwa wanajeshi wa vyeo vya chini! If we want to be fair with the guys, we have to know the root cause of the problem. Vinginevyo tutegemee kuona mambo mengi yasiyoridhisha kama tatizo lolote lile lipo na halitafutiwi utatuzi
 
Ndugu yangu Napo, hii taarifa ya kwamba kuna mwanajeshi alipigwa ndo naisikia toka kwako. Mimi jana wakati napokea kipigo sikuambiwa kosa langu ni nini? Na kama hiyo ndiyo sababu, huoni kama tuna jeshi la vichaa? Hivi huyo mwanajeshi alipigwa na kila mwananchi wa gongo la mboto? walikuwa wananchi wangapi waliompiga huyo mwanajeshi? Iwaje sasa wanajeshi watuibukie wote bila kujali kwamba wengine tuna majukumu yetu na heshima zetu, wanatushushia kipigo njiani tena tukiwa na watu tunaowaheshimu?

Kama hii ilikuwa ni revenge ya wanajeshi hawa dhidi ya wananchi wachache waliompiga huyo mwanajeshi (bila shaka walipigana kwenye ulevi), basi nashawishika kuamini kwamba jeshini kuna watu wasio na akili timamu. Lakini pia inashangaza sana kusikia eti wanajeshi wanalinda nchi kwa kujitolea. Kauli kama hii ni ya watu wasiokuwa na uwezo mzuri wa kufikiria na kuchambua mambo. Kama wanajeshi wanajitolea kuwalinda wananchi, walimu wanaliokuwezesha wewe kujua hata kuandika haya unayoyaandika wasemaje, na madaktari wanaookoa uhai wa watanzania kila kuchapo wasemaje? Mahakimu je, wanaofanya kazi ya kutetea haki zinazodhulumiwa wasemaje? Uanajeshi ni ajira kama zilivyo ajira nyingine zozote. Wanalipwa mshahara na malupulupu kibao. Kama wanaona kazi wanayoifanya ni ngumu sana kwa ajili ya taifa hili, kwanini wasiache na kuingia katika kazi nyingine ambazo siyo ngumu.

Ninafikiri kuna haja ya kulitafutia kazi hili jeshi letu, maana tangu lipigane na Iddi Amini halijapata kazi nyingine ya kufanya, ndiyo maana linafanya mazoezi ya kuwalipulia mabomu wananchi wake na mazoezi ya kutudunda sisi baadala ya kudunda maadui wa nchi hii. Kila siku wahamiaji haramu wanaingia nchini na wakenya kibao wanakuja kutuulia tembo wetu na faru wetu kule Serengeti na hakuna chochote kinachofanyika. Hilo jeshi linalinda mipaka ya wapi, na hawa maharamia wanaowinda ndovu wetu wanaingilia wapi? Jeshi la Tanzania naweza kusema ni jeshi ambalo ni corrupt, halina tena sifa za kulinda usalama wa nchi.

Napo na lukolo,nimesoma kwa makini msg zenu,hili nitatizo kubwa sana binafsi naona suala hili lifuatiliwe kw umakini ijulikane ipi sababu,raia kumpga mwanajeshi na vilevile mwanajeshi kupga raia! Wote kwa pamoja wanatakiwa waungane ili tukomboe nchi yetu kwani ipo vbaya(ufisadi umezagaa) na hakuna 2naloambiwa zaidi yakuchekewa tu! Wananchi pia 2we na subira kwan inawezekana pia hawa jamaa 2nawaonea hawajahucka nalolote na nyiny wajeshi 2we na subira kuliko kuzama ktaa nakupga raia wema tena wenye uchungu na ndugu zao waliopotea pamoja na mali zao kbao! JESHI la WANANCHI wa Tz,inasound umoja (jeshi na wananchi)! Shida nini Jameni??? Tulindi taifa,2ondoe ufisadi na maadui wa nchi yetu!
 
kujitolea???kwani kazi ya ujeshi ni wito??vp hawalipwi hawa??

Hata na mimi nilikuwa najiuliza hivyo kwani wanafanya kazi hiyo bure?

Halafu unawapiga wananchi wanaokamuliwa kodi ili wewe upewe mshahara mkubwa na uwalinde vizuri? Mbona kwengine hatusikii wanajeshi wakiingia mtaani na kupiga watu wasio na hatia? Kumbukeni walivyokuwa wakifanya Kunduchi katika miaka ya karibuni.
 
Back
Top Bottom