Jeshi la wanamaji Iran lainusuru meli na kuwatia nguvuni maharmaia 12

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
100
Jeshi la wanamaji Iran lainusuru meli na kuwatia nguvuni maharmaia 12
iran%20navy%20mapambano.jpg


Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeinusuru meli ya mizigo katika Bahari ya Hindi na kuwatia mbaroni maharamia 12 kufuatia mapigano ya masaa 48.
Akizungumza mjini Tehran, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran Admeli Habibollah Sayyari amesema meli hiyo ya mizigo iliyokuwa ikielekea Iran ilishambuliwa Machi 26 na Maharamia ambao walichukua udhibiti wake. Jeshi la Wanamaji la Iran lilipokea habari kuhusu tukio hilo, lililojiri kilomita 3000 kutoka maji ya Iran, na kufika hapo mara moja. Makomando wa Jeshi la Wanamaji la Iran walipambana ana kwa ana na maharamia hao ndani ya meli hiyo kwa masaa 48 na hatimaye waliwatia mbaroni maharmia 12 na kuinusuru meli hiyo na wahudumu wake. Imearifiwa kuwa watu wawili wasiokuwa Wairani waliuawa katika tukio hilo. Admeli Sayyari amesema maharamia hao watakabidhiwa vyombo vya Mahakama Iran. Manoari za kivita za Iran zinalinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi kwa lengo la kukabiliana na maharamia. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO limepongeza mafanikio ya Jeshi la Wanamaji la Iran katika kukabiliana na maharamia. :scared::fencing:
 
Kwa hii ishu USA na Israel roho zao mbaya zitakuwa zinawauma sana...
 
Back
Top Bottom