Elections 2010 Jeshi la polisi latoa onyo kupitia Clouds FM

Kwani TBC haipo ? au ndo kujipendekeza,kura zihesabiwe upyaaaaaa basi tupate ukweli nani kashinda kihalali
 
watu wanapewa pesa ili waandamane??
Waandamane kwa sababu zipi?
Polisi ingesolve kwanza chanzo cha hayo maandamano.
 
I was in zanzibar in 2001, residing at mlandege street, one of the elders aproached me one evining as I was from mtendeni, along mchangani busy road, and offered me 10usd, on consideration that I should appear the next morning for demonstration. hii ni techinik ya kutumia vijana wasio na kazi maalumu ili kufanikisha hila zao, chunguzeni sana mbona wenyewe hawajitokezi, unataka kumuweka mtu ikulu unkesha barabarani halafu yeye yupo kwake anakunwa kitambi na mkewe, huku mtaani kwetu kila jioni kuntuvikao tusito na maana na kuna strange faces zinchea vikao hivyo ktk baa bubu, jamaa wankuja na magari ya ukweli yakiwa tinted, nimeshuhudia kama mara mbili hivi nitajipenyeza one day then nikifanikiwa nitawapa nyuz wanajf

Wambaje?

Wewe ni mzanzibar muunguja au mpemba? acha zuga hakuna kizanzibari kinachoongewa hivyo mie nimekaa na kutembea zanzibar karibia yote sijasikia hayo maneno yenye rangi nyekundu.
 
Kwani TBC haipo ? au ndo kujipendekeza,kura zihesabiwe upyaaaaaa basi tupate ukweli nani kashinda kihalali

Mimi nimemsikia Kova asubuhi mida ya saa mbili kasoro akielezea hiyo issue TBC1 na akasisitiza mikusanyiko isiyokuwa na kibali cha polisi ni kinyume cha sheria na hawajui inalengo gani. Akaongezea kwa kusema kama hao watu wana nia njema nasi wangetoa taarifa ili wapate ulinzi na wajue kuwa Jeshi lipo imara kukabiliana na uvunjivu wowote wa amini. Amesema kuna watu wengine waliokamatwa mapema kwenye matukio ya kule tandika wengine mpaka watoto wadogo wa miaka kumi walipo ulizwa walikuwa hawajui hata nini walikuwa wanashangilia na wapi wanaenda.

Kamanda Kova amesema watakaoshinkwa hata kama hawatakuwa na uelewa wa jambo hilo watachukuliwa hatua shtahili. Ameomba watu wenye nia njema watoe taarifa mapema watakapo ona hali kama hiyo inatokea ( polisi shirikishi ) na kuonya wanaumia ni pamoja na wapita njia wengine na watoto wadogo wa shule.

My take:

Kama watu wanaamua kufanya maandamano basi watumie njia stahili ikiwa pamoja na kutoa taarifa polisi na sio kutumiana messages kinyemela hatuwezi kujua kama hizo message zina baraka kwa viongozi waandamizi wa chama chochote cha upinzani au laa.

TBC1 ilikuwa ya kwanza kutangaza na Kova alikuwa live.
 
hehe.. sio kwamba jeshi limepeleka tangazo clouds...!! clouds ndio wamewatafuta ili kujuwa msimamo wa jeshi kutokana na kauli ya kichochezi ya mzee slaa
 
Sina imani na Polisi kwani walianza kutisha toka zamani kwa nia ya kulinda wizi wa kura unaofanywa na CCM.
 
acheni woga jamain huwezi kudai haki ukiwa ofisini. bahati nzuri hawa askari tunakaa nao mtaani, tutaanzia huko huko.
 
Hakuna haja ya Kova kubwabwaja -- yeye atume vikosi vyake akawakamate wale waandaaji wa fujo hizo anazosema. Hawa polisi hovyo kweli kweli, wanapenda tu kutoa vitisho kwa amri ya akina Makamba na Rostam, basi.
 
Pumbavu kabisa hao polisi wenyewe wamepigika kinoma na life, wao ni kuburuzwa. kwanza kwanini wapeleke tangazo couds??? jinga kabisa!!!!!
 
jeshi la police limetoa onyo kwa vikundi ambavyo vinapanga kufanya fujo na maandamano kwani imesemekana kuna watu wanatoa fedha kuwapa watu ili wakusanyike kufanya vikao visivo rasmi na maandamano ya kuchochea vurugu, pia jeshi la police linaendelea kufanya upelelezi kumsaka mtu anayefanya kazi ya kulipa na kuandaa mikusanyiko hii. JESHI IMEPELEKA TANGAZO HILI CLOUDS FM NA LIMETANGAZWA KTK KIPINDI CHA LEO TENA NA DINA MARIOS. mh hofu sasa imetanda sijui itakuaje

Wanafikiri wanavyofanya wao ndio na wengine. Vurugu hizi ni uchungu wa kura ya mtu kuchezewa. Ni njia ya kutaka kuwakamata viongozi wa Chadema. Hivi CUF hawana maumivu haya?
 
Hakuna uhakika wowote kuwa anayeandaa ama kuhamasisha maandamano kama ni Dr.SLAA/Viongozi wa CHADEMA.
Hizi zaweza kuwa ni hujuma... Angalieni msije muitikia msie mjua.
Kama ingekuwa ni Uongozi wa CHADEMA wasingekuwa na sababu yeyote yakufanya mambo kinyemela/kimya kimya..
Wangetoa sababu za MSINGI za kuandamana na kutumia vyombo vya habari vilivyo huru ingawa viko adimu sana.
Jamani muwe na composure...mambo mazuri hayataki haraka.Msifanye mambo kwa msisimko.
Subirini tangazo na msimamo wa viongozi wenu.
Jiepusheni na roho mbaya ya uasi....
Mungu Ibariki Tanzania.
 
yaah waambie tutaanza kwa kuchoma CLOUDS FM na TBC, wakaanze kulinda hapo, kina kinjekitile walituokoaje??
waende huko na mishahara yao ya kima cha chini.....................
OCD- 756,000 - Basic Salary hao FFU 156,000 na wengine wanalazwa kwa nyumba za mabati zinachoma kama nini ............. bado wanakumbatia ujingaa..............

hawa polisi sijui wanatumia utashi gani!!!
Hawaoni njaa na shida wanazopata kwa ajili ya hawa mafisadi waliopo madarakani?
 
rube mtahaba anataka kugombea ubunge kwao ndo mana si unajua ccm kwa kulipa fadhila za mafisadi
 
Hakuna uhakika wowote kuwa anayeandaa ama kuhamasisha maandamano kama ni Dr.SLAA/Viongozi wa CHADEMA.
Hizi zaweza kuwa ni hujuma... Angalieni msije muitikia msie mjua.
Kama ingekuwa ni Uongozi wa CHADEMA wasingekuwa na sababu yeyote yakufanya mambo kinyemela/kimya kimya..
Wangetoa sababu za MSINGI za kuandamana na kutumia vyombo vya habari vilivyo huru ingawa viko adimu sana.
Jamani muwe na composure...mambo mazuri hayataki haraka.Msifanye mambo kwa msisimko.
Subirini tangazo na msimamo wa viongozi wenu.

hata jina lako linaonekana wewe ni ccm kaa utulie na uccm njaa wako. wenzako wanachakachua mikataba ya mabilion we unaishia kupewa kofia na flana
ambayo ukifua tu haikutoshi acha njaa dogo. alafu kuna umri wa kupenda ccm sio wewe vijana we need changes na sio ujima

Jiepusheni na roho mbaya ya uasi....
Mungu Ibariki Tanzania.
acha njaa dogo we huoni haya ccm ni wazee na vijana wachache wasiosoma alama za nyakati
 
jeshi la police limetoa onyo kwa vikundi ambavyo vinapanga kufanya fujo na maandamano kwani imesemekana kuna watu wanatoa fedha kuwapa watu ili wakusanyike kufanya vikao visivo rasmi na maandamano ya kuchochea vurugu, pia jeshi la police linaendelea kufanya upelelezi kumsaka mtu anayefanya kazi ya kulipa na kuandaa mikusanyiko hii. JESHI IMEPELEKA TANGAZO HILI CLOUDS FM NA LIMETANGAZWA KTK KIPINDI CHA LEO TENA NA DINA MARIOS. mh hofu sasa imetanda sijui itakuaje

Huu uongo tu, gud tym
 
ina maana jeshi limeona the right place ya tangazo lao ni clouds..ok hiyo sio issue, kipindi cha dina marios..Mungu wangu jeshi letu..wasitishe watu, kama watu wanadai haki zao fujo itatokea wapi?? wamezoea kuita mikusanyiko fujo hata kama watu wamekusanyika na kukaa kimya..hiyo ni mbinu ya kutisha watu tuu..wangekuwa iraq au afganstan wangejua nn maana ya fujo..hapa bongo watu wanaandamana tu na hakuna fujo..
 
Clouds fm? Wanaumwa! Katiba ya jamhuri inaniruhusu ku assemble,ku express idea na freedom of movement wapo hapo? Ijue katiba,watawala acha kuropoka,tena kwenye redio za mafisadi!
 
hehehehe hehehehe hehehehe
NGUVU ya UMMA haizuiwi kwa risas.
wajenge jela mpya za kuweka watu maana zilizopo hazitztosha
Jela watakwenda wao akina Kova. Athubutu kuua hata mmoja atakuwa kawasha moto.
 
Back
Top Bottom