Jeshi la Polisi laonyesha utii kwa Dr.Slaa na kumdharau JK (AMIRI JESHI MKUU)

Mchekechoni

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
279
19
Kufuatia hotuba ya Amiri Jeshi Mkuu, JK, ya 28/02/2011, kuhusiana na maandamano ya cdm kanda ya ziwa chini ya viongozi wake wakuu, ni dhahiri kuwa polisi wamefyata mkia na kuacha maandamano hayo yasonge mbele bila kubugudhiwa. Hii inaashiria kuchepuka kwa jeshi hilo kutoka utii wake kwa mkuu wa nchi na kuachana na matakwa ya ccm kudhibiti cdm. Kesho waziri mkuu, Pinda anaenda bukoba kujaribu kufukia mashimo ya Dr.Slaa na Mbowe (bila shaka baada ya kupokea simu kali toka kwa JK akiwa safarini ulaya). Je atafanikiwa kuzima moto uliowashwa na cdm?
 
Kama ziara hiyo ni ya dharula bac cdm ni tishio kwa sisiem

PM, Pinda kapata trip ya (ghafla?) kuzunguka wilaya zote za mkoa wa kagera, ratiba inaanza rasmi kesho na wanaccm wote mtoe sapoti ili kukinusuru chama na (sumu?) ya cdm!
 
PM, Pinda kapata trip ya (ghafla?) kuzunguka wilaya zote za mkoa wa kagera, ratiba inaanza rasmi kesho na wanaccm wote mtoe sapoti ili kukinusuru chama na (sumu?) ya cdm!

Hivi mkisha andika huu uzushi huwa mnapitia bahasha kinondoni? wenzenu siku hizi wana ruzuku nimemuona Mshumbuzi na gari mpya,
 
Ni siku nyingi sana watanzania tulikuwa tunasubiri hali ya siasa ya sasa hivi TZ. Kulikuwa na utitiri wa vyama vya upinzani TZ na wengine kwenye foleni ya Tendwa kusajiliwa.
Kwa nchi tunazoita zimeendendelea vyama vikubwa vya siasa ni viwili tu.
Na TZ tumeshafika hapo. Tuna CDM na CCM. Kwa kiasi fulani democrasia inakua. Tendwa anaanza kupungukiwa na kazi.
 
Kwani mhishomiwa ktk hotuba yake aliamuru polisi wazuie maandamano au aliwaomba wananchi wasiitikie, kitu ambacho wananchi wanaonekana hawakuafiki kabisa. Polisi, wanatimiza wajibu wao wa kulinda raia na mali zao na siyo kuzuia maandamano.
 
Hivi mkisha andika huu uzushi huwa mnapitia bahasha kinondoni? wenzenu siku hizi wana ruzuku nimemuona Mshumbuzi na gari mpya,

cjakuelewa mjepu, uzushi ni upi, kwamba pinda anaenda bk au kuwa safari yake ni ya ghafla?
 
Kuanzia hapa hadi kuhusisha na ziara za matembezi za CDM

Yeah, nimekusoma tano kwa tano! Pitia threads za mh.Regia tangu kuanza kwa maandamano ya cdm kanda ya ziwa (pamoja na picha!) na hitimisho la maandamano hayo kwa kanda hiyo leo kwa mikutano ya hadhara katika wilaya za mkoa wa kagera, hapo utagundua kuwa counter-attack toka ccm ni muhimu ili ku-neutralize nguvu ya cdm!
 
Anakwenda kupoteza heshima yake ni bora angeenda jimboni kwake akanywe chai au aendelee kukaa magogoni anywe madhiwa
 
Huyu mzee nyota yake inafifia siku hadi siku,mwisho wa siku atabakia majivu. Mwanaume bila makali ni bora uvae skirt tu...anaenda enda tu,inaweza ikawa sio wish yake, ila ndo ivo
 
Strategy kama hii ya kufukia fukia mashimo ilishatumika na ccm dhidi ya cdm kwa mafanikio kidogo wakati wa kampeni za urais 2010, ila kwa sasa mmmh, no comment!
 
Kwa kweli Pinda anasikitisha sana haswa anapopigwa picha kama ile ya kumpokea Mkuu pale uwanja wa ndege. Lol, Mzee mzima angechagua heshima yake ingekuwa bora kuliko hicho cheo.
 
Kwani mhishomiwa ktk hotuba yake aliamuru polisi wazuie maandamano au aliwaomba wananchi wasiitikie, kitu ambacho wananchi wanaonekana hawakuafiki kabisa. Polisi, wanatimiza wajibu wao wa kulinda raia na mali zao na siyo kuzuia maandamano.

Kwenye hotuba yake fisadi Kikwete alisema maandamano ya CHADEMA hayakubaliki hata kidogo kwasababu yanahatarisha amani na utulivu. Hiyo tu ni amri kwa jeshi la polisi, sema walishindwa wangeyazuia vipi kwasababu walionyesha kuandamana kwa amani tangu mwanzo. Walijaribu kumkamata Dr Slaa na wabunge wawili bila kuwa na sababu maalum wakawaachia! Hata hao polisi (walio wengi) wana maisha magumu, wanaishi kwenye nyumba za mabati kwasababu ya CCM nao wanapenda mabadiliko ila maadili ya kazi yao yanawazuia lakini nadhani nguvu ya umma ikipamba moto nao watajiunga tu!
 
Kama ziara hiyo ni ya dharula bac cdm ni tishio kwa sisiem

sasa we mbona unafurahisha hapa ndo umechangia nini sasa?moja kwa moja we ni cdm.sasa inamaana ulikua bado hujakiamini chama chako ama?
Angalizo mimi sio cdm.
 
ndiyo nani tena huyu?

hapo mjepu anamchokonoa Jenifa Mshumbusi, mchumba wa Dr.Slaa(bado hawajafunga ndoa), I hope ana evidence juu ya umiliki wa hiyo gari. Anyway, turudi kwenye mada yetu katika hii thread, kile nilichoandika jana juu ya PM, Pinda kwenda bk kujaribu kufuta nyayo za cdm na kurudisha heshima ya chama tawala na mjepu akashabikia eti ni uzushi tu, tayari kimethibitika kuwa ni kweli kwa ushahidi wa gazeti la leo la mwananchi na vyombo karibu vyote vya habari. Haya ccm kazi kwenu, tuone kama mtaweza kujibu mapigo ya mbowe, dr.slaa na timu nzima ya cdm iliyokuwa kanda ya ziwa!
 
Back
Top Bottom