Jeshi la polisi kumkamata Dr. Slaa

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Ni kwa kutoa kauli za uchochezi katika mikutano ya hadhara Mwanza na geita. Polisi wanasema alitoa vitisho kwa serikali kwa kuipa serikali siku 3 iwatibu wabunge wa chadema walioshambuliwa na kulipa jeshi la polisi siku 7 likamilishe uchunguzi kwa sakata hili. Kauli hiyo inasemwa ni kinyume na sheria.

source: Star tv news
 
wanasema alitoa vitisho kwa serikali kwa kuipa serikali siku 3 iwatibu wabunge walioshambuliwa na kulipa jeshi la polisi siku 7 likamilishe uchunguzi kwa sakata hili. Kauli hiyo inasemwa ni kinyume na sheria.
 
Jeshi la polisi kumkamata Dr. Slaa kwa uchochezi?

Source Star Tv
 
wanasema alitoa vitisho kwa serikali kwa kuipa serikali siku 3 iwatibu wabunge walioshambuliwa na kulipa jeshi la polisi siku 7 likamilishe uchunguzi kwa sakata hili. Kauli hiyo inasemwa ni kinyume na sheria.

Kauli ya Slaa ni sawa na kama jeshi la polisi au serikali linatishwa kwa kuambiwa ukweli basi wawe kunguru tu mambingwa wa kuogopa duniani

SIAMINI JESHI LINASHINDWA KUKAMATA MAJAMBAZI NA MAFISADI LAKINI LINAMKAMATA ALIYEWAKUMBUSHA MAJUKUMU YAO
 
wanasema alitoa vitisho kwa serikali kwa kuipa serikali siku 3 iwatibu wabunge walioshambuliwa na kulipa jeshi la polisi siku 7 likamilishe uchunguzi kwa sakata hili. Kauli hiyo inasemwa ni kinyume na sheria.
Badala ya kuwatia mbaroni wakata mapanga wao wanataka wamtie mbaroni anayetaka watu watibiwe, am missing something here.
 
Wanadai alitoa matamshi kuwa polisi watoe tamko ndani ya siku tatu kuhusu kukatwa mapanga wabunge wa CHADEMA wao wametafsiri kama uchochezi na wanasema Dr. Slaa katoweka Mwanza kinyemela.
 
Jeshi la polisi mkoani mwz linamtafuta Dr Slaa kwa uchochezi wa kuwashawishi wananchi kuvamia vituo vya polisi na kuipa serikali siku 3 kuhakikisha wabunge wa cdm waliopigwa wanapona.
Source: star tv
 
Badala ya kukamata wahalifu waliowakata mapanga wabunge wao wanashughulika na Dr Slaa. Nchi hii kichwa cha mwendawazimu kweli

Jeshi la polisi nani analisukuma nyuma yake kufuata sheria kwa upinzani tu?,mbona wote waliohusishwa na ufisadi wasishugulikiwe?wao wameshika mpini sisi tumeshika makali ipo siku huo mpini utawaponyoka.
 
Naona sasa CCM wanataka kuvuruga mchakato wa katiba baada ya kuona mambo hayawaendei vyema. Hii ni njia moja ya kuleta vurugu zisizo na maana nchini ambayo hakuna atakaye kuwa salama. Ngoja tusubiri kama kweli polisi wetu ni professional au ni kichwa cha wanasiasa wendawazimu wanaofikiria ku-retain power badala ya ku-sustain country's development.
 
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza ametoa amri kwa dr.slaa kujisalimisha mwenyewe kituo cha polisi ili kutoa maelezo kwa kile kilichodaiwa kuwa ni uchochezi kwani alitoa siku saba kwa jeshi la polisi kuwatia hatiani wale wote waliohusika kuwacharanga mapanga wabunge wa CHADEMA.Anasema wameshindwa kumtia Dr.Slaa nguvuni kwani aliondoka Mwanza kinyemela hapo juzi kuelekea Dar.source star tv.
 
Polisi wetu wanashangaza, rahisi ni kuanzisha kesi dhidi ya Dr Slaa au kuwakamata wahalifu waliovunja amani na kujeruhiwa raia?? Basi tukubaliane jeshi la polisi ni la kuliinda majambazi na si raia!
 
Kwani kutoa siku 3 kunachochea vipi vurugu?. Wakimkamata tunajua ni kwa sababu anazoa zoa wanachama wa CCM na hiyo itaipaisha CHADEMA kwa mbali.
 
Wanasubir nini? Kwnini wacmkamate kwanza ndo watangazie umma? Wanaomba public sympathy or what? They are like a donkey lived for 30 years whch hopes to be a horse one day!
 
kamanda wa mkoa wa mwanza akiongea na vyombo vya habari leo amemtaka katibu mkuu wa chadema kujisalimisha, baada ya kutoa maneno ya uchochezi katika mikutano yake ya mwanza na Geita akiwataka wanainchi kuvishambulia vituo vya police endapo jeshi hilo halitawakamata wale wote waliohusika na kuwajeruhi wabunge wa chama hicho highness kiwia na mbunge mwenzake na amewapa siku saba jeshi la police kuhakikisha mbunge kiwia anapona haraka. Taarifa ya Habari star tv, saa 2 usiku.
 
Back
Top Bottom