Jeshi la Polisi haliweki usalama zanzibar bali linalipiza kisasi...

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
[h=1]Polisi wadaiwa kufanya unyama[/h] Posted on October 31, 2012
Salum Bakari Muya anayedaiwa kuteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kisha kunyonyolewa nywele na baadhi ya vikosi vya ulinzi na usalama nchini ambapo alisema vikosi hao wakiwemo polisi ambao pia walikuwa na silaha.

MTU moja mkazi wa Mkele jana alinusurika kuuawa katika msako wa kuwakamata watu wanaotuhumiwa kusababisha vurugu zilizotokea wiki moja iliyopita mjini Zanzibar.
Vurugu hizo ziliibuka Oktoba 17 mwaka huu baada ya kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMUIKI) Sheikh Farid Ahmed Hadi kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Oktoba 16, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa bahari mjini hapa jana, kijana aliyenusurika kuuawa, Salum Bakari Muya alidai aliteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kasha kunyonyolewa nywele polisi ambao pia walikuwa na silaha.

Sehemu ya ngozi aliyokatwa kijana huyo na jeshi la polisi

Alisema kabla ya kukutwa na tukio hilo alikuwa amekaa na wenzake wakiwa wanasubiri tenda ya mizigo ya kusafirisha kwa kutumia magari ya punda.
“Nilikuwa nabangaya – yaani kubangaiza –wakatokea polisi sita, walipofika nilipokaa wakanifunua kofia na kunikata kipande cha ngozi na nywele kichwani kwa kisu,” alisema Salum.
Alidai polisi waliomfanyia ukatili huo ni wa kikosi cha FFU na kwamba baada ya kitendo hicho waliamua kumpeleka kituo cha afya cha JKU kilichopoa Saateni kwa matibabu ya awali.
Salum alidai kuwa baada ya kupata matibabu katika kituo hicho cha JKU iliamriwa kwamba apelekwe Hospitali Kuu ya Mnazimoja kwa vile alikuwa anavuja damu nyingi.
Hata hivyo alisema alishangaa kabla ya kufika Mnazimoja polisi hao waliamua kumtekeleza katika eneo la kwa Abbas Hussein, kilometa chache kutoka walipomtoa hospitali ya JKU.
“Hawakunifikisha Manazimoja, wakaniacha na kuondoka huku wakisema ubaya ubaya mtakoma waambie na wenzio,” alisimulia Salum akiwa na bandeji aliyofungwa wakati anapata huduma ya kwanza.
Alisema baada ya kutelekezwa na polisi aliamua kwenda Welesi huko Kikwajini kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa uliompata.
Baada ya kusimulia mkasa huo, Salum ambaye alifuatana na kaka zake walioomba wasiandikwe majina baadae alipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.
Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamishana wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema bado hajapopewa taarifa na kwamba iwapo mwathirika atalalamika kituoni polisi watachukua hatua ya kucunguza.
“Tumezoea kulalamikiwa, kama mtu amefanyiwa ukatili kwanini asiripoti kituo cha polisi, hapo ujue kuna jambo anaficha,” alisema Kamishna Mussa.
Lakini baada ya kuelezwa na mwamdishi wa habari hizi kwamba kijana huyo amepelekwa hospitali na kaka zake, Mussa alisema aliahidi kufuatilia tukio hilo.
Kitendo cha Salum kufanyiwa ukatili na watu wanaodaiwa kuwa polisi kimetanguliwa na matukio ya vijana wenguine wawili kuuawa wakati wa utekelezaji wa zoezi la msako huo mjini Zanzibar mwezi Oktoba mwaka huu.
Imedaiwa kuwa Hamad Ali Kaimu aliuawa Ijumaa iliyopitama wakati akiwa mikononi kuwa polisi katika eneo la Magomeni na Salum Hassan Mahanju alikufa baada ya kupigwa risasi katika maeneo ya Amani Fresh na watu waliotajwa kuwa maofisa ulinzi na usalama.
Mbali na vijana hao, askari mmoja Koplo Said Abdulrahman aliuawa na watu wasiojulikana huko Bububu baada ya tukio la kutoweka Sheikh Farid.
Tokea kuanza kwa vurugu hapa Zanzibar jumla ya watu watatu wamefariki ikiwa mmoja ameuwa na watu wenye hasira huku jeshi la polisi likidaiwa kuwauwa vijana wawili hali sio shuwari kufuatia unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na jeshi la polisi kwa kisingizio cha kuwatafuta wahahalifu.Wakati jeshi la Polisi visiwani Zanzibar likiendelea kuwasaka wahalifu, baadhi ya wananchi wamejitokeza kulalamikia juu ya operesheni hiyo ikiwemo ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na jeshi hilo uliosababisha kifo cha kijana mmoja akiwa mikononi mwa polisi. Bonyeza hapa kupata taarifa hiyo.
Kufuatia kadhia hiyo DW ilimtafuta Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa na alikuwa na haya ya kusema Bonyeza hapa Tafadhali.
Lakini Pia alitafutwa Kamishna wa Haki za Binaadamu Zanzibar, Bw. Zahor Juma Khamis ambaye naye alikuwa na haya ya kuiambia DW. Bofya hapa tafadhali.

[url]http://zanzibariyetu.wordpress.com/2012/10/31/polisi-wadaiwa-kufanya-unyama/#comments

[/URL]
 
Bahati mbaya tu kinyozi alikuwa kalewa, hizo zinaitwa WAR CASUALTIES.

Si mlitaka ukombozi, huo hapo. Uzuri huko hamna mkristo wa kumsingizia
 
Hiyo kali.
Polisi wakikuona tu wanakuvua kofia na kukata ngozi.

Pelekeni upuuzi huu pembeni. Mnaficha kitu.
 
Salum alidai kuwa baada ya kupata matibabu katika kituo hicho cha JKU iliamriwa kwamba apelekwe Hospitali Kuu ya Mnazimoja kwa vile alikuwa anavuja damu nyingi.
Hata hivyo alisema alishangaa kabla ya kufika Mnazimoja polisi hao waliamua kumtekeleza katika eneo la kwa Abbas Hussein, kilometa chache kutoka walipomtoa hospitali ya JKU.
"Hawakunifikisha Manazimoja, wakaniacha na kuondoka huku wakisema ubaya ubaya mtakoma waambie na wenzio," alisimulia Salum akiwa na bandeji aliyofungwa wakati anapata huduma ya kwanza.
Alisema baada ya kutelekezwa na polisi aliamua kwenda Welesi huko Kikwajini kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa uliompata.

Hivi mtu unavuja damu nyingi kweli uache kwenda hospitali badala yake uende kwa waandishi wa habari?!!!

Hawakukumenya vizuri wewe
 
Baadhi ya watu humu ndani mnaandika habari za uchochezi, kinachofanywa na POLISI zanzibar ni uvunjifu wa haki za binadamu wa hali ya juu, CUF lazima waamke vinginevyo ndio CCM inaenda kuwapiga kanzu hivo wananchi hawatawaamini tena.
 
Bahati mbaya tu kinyozi alikuwa kalewa, hizo zinaitwa WAR CASUALTIES.

Si mlitaka ukombozi, huo hapo. Uzuri huko hamna mkristo wa kumsingizia

Hawa jamaa wajinga sana, Uamsho wako wapi na hela zao kutoka Uarabuni?
Walikuwa wanaua askari polisi wakifikiri lelemama!
Waandamane sasa na wanyolewe kwa chupa.
 
Baadhi ya watu humu ndani mnaandika habari za uchochezi, kinachofanywa na POLISI zanzibar ni uvunjifu wa haki za binadamu wa hali ya juu, CUF lazima waamke vinginevyo ndio CCM inaenda kuwapiga kanzu hivo wananchi hawatawaamini tena.

Huu samahani sana, ni unafiki wa hali ya juu.
Sijaona posti yako ya rambirambi alipouwawa yule sajenti wa polisi
 
Huu samahani sana, ni unafiki wa hali ya juu.
Sijaona posti yako ya rambirambi alipouwawa yule sajenti wa polisi

wewe ni mkaguzi wa post humu JF? au ni kule kuwashwa washwa alikosema mabumba mwenyekiti wa Bunge
 
Baadhi ya watu humu ndani mnaandika habari za uchochezi, kinachofanywa na POLISI zanzibar ni uvunjifu wa haki za binadamu wa hali ya juu, CUF lazima waamke vinginevyo ndio CCM inaenda kuwapiga kanzu hivo wananchi hawatawaamini tena.

Napata mashaka sana mtoto wa kike anaposema kunyoa ni uvunjifu wa haki ya binadamu, ina maana dada kwapa lako liko kama kichwa cha singasinga?

Kwani CCM ndio wenye hiyo saluni?
 
Baadhi ya watu humu ndani mnaandika habari za uchochezi, kinachofanywa na POLISI zanzibar ni uvunjifu wa haki za binadamu wa hali ya juu, CUF lazima waamke vinginevyo ndio CCM inaenda kuwapiga kanzu hivo wananchi hawatawaamini tena.
Kile kilichofanywa na wana uamsho si uvunjifu wa haki za binadamu? Kuharibu mali za watu na kuua polisi ni nini? Kutishia kuchinja maaskofu/wachungaji endapo Farid asipoachiwa ni nini? Kwanini mnakuwa wagumu kuanza kukemea madhambi mliyoanza kuyafanya wenyewe lakini mnakemea matokeo yake tu sasa?

Kumbe wazanzibari mnapenda haki na kuthamini maisha ya watu kiasi hiki? Mlikuwa wapi zamani wakati mnahubiri chuki na kutishia kuchinja watu?
 
Baadhi ya watu humu ndani mnaandika habari za uchochezi, kinachofanywa na POLISI zanzibar ni uvunjifu wa haki za binadamu wa hali ya juu, CUF lazima waamke vinginevyo ndio CCM inaenda kuwapiga kanzu hivo wananchi hawatawaamini tena.
Acha unafiki wewe mbona wananchi walivoua polisi hamkutokea kupinga kila kukicha mnawaabudu uamsho waje basi wawasaidie...Uislamu ni Janga la dunia achanane ni wendawazimu uamsho maana kabla mlikua mnaishi vizuri tu leo mnapigwa kama majambazi kwa sababu ya uamsho!!Anyway dini yenu yenyewe hairuhusu mwanadamu kuwa na amani so hata mkifa zenji nzima haina tabu kwetu,,,...potezea washari nyie
 
tabia hii ya kutukana dini za wengine imeshamiri sana hapa JF, cha kushangaza mod hawapigi ban watu hawa na badala yake wanaopigwa ban ni watu wengine kabisa na wasi wasi na integrity ya baadhi ya mods inapokuja dhana ya kudharau dini za watu
 
Acha unafiki wewe mbona wananchi walivoua polisi hamkutokea kupinga kila kukicha mnawaabudu uamsho waje basi wawasaidie...Uislamu ni Janga la dunia achanane ni wendawazimu uamsho maana kabla mlikua mnaishi vizuri tu leo mnapigwa kama majambazi kwa sababu ya uamsho!!Anyway dini yenu yenyewe hairuhusu mwanadamu kuwa na amani so hata mkifa zenji nzima haina tabu kwetu,,,...potezea washari nyie
Kasameheni bure hako kamdudu kako kwenye kipindi cha moon.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom