JESHI la Polisi Barabarani!

Mjanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,238
324
hivi karibuni nimekuwa nikisafiri mara kwa mara toka DSM kuelekea nyanda za juu za kusini,
nimeona jitihada zinazofanywa na askari POLISI usalama wa BARABARANI (TRAFIC)
jinsi wanavyosisitiza abiria kujifunga mikanda kwenye mabasi!
cha kushangaza ni namna gani ABIRIA wasivyotaka/hawana utayari wa kufuata taratibu
za usalama barabarani pindi wanaposafiri!

Naamini kabisa hizi taratibu ni kwa ajili ya kulinda maisha ya kila mtanzania anayetumia
chombo cha moto, lakini imekuwa ni tofauti sana, pengine kwa kutokuelewa umuhimu a
wa hii mikanda!

Swali, je hakuna sheria inayowaruhusu Trafic kumpiga faini ABIRIA anaye kaidi matumizi ya MIKANDA?
kama ipo kwanini isitumike? na kama hiyo sheria haipo serikali inasubiria nini kuileta??

Je kuna umuhimu wa kuelimisha ABIRIA juu ya umuhimu wa kufunga mikanda pindi wanaposafiri na hilo ni
jukumu la nani (SERIKALI au MMILIKI)??

naomba niishie hapa kwa leo!!
 
mikanda yenyewe ni michafu na mibovu, ukivaa ni ushahidi tu haisaidii kitu. anza na sumatra, trafic then mimi.
 
nafikiri pia kuna haja ya kuelimisha wenye magari kuweka mikanda imara na salama kwa afya ya watumiaji!
ila inaonekana pia kuwa abiria ndiyo chanzo cha uharibifu!
mbona mabasi kama Dar Express, Sumry na mengine ambayo ni luxurious wanaweza?
ila niliwahi kuboard Presision Air; pia nilikutana na mkanda mbovu...pata picha!
 
Back
Top Bottom