Jeshi la Iran: Tutapiga kituo cha nyuklia cha Dimona iwapo Israel itaishambulia nchi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,270
Naibu kamanda wa jeshi la Iran Jenerali Mas'ud Jazairi amesema kuwa Iran itajibu mashambulizi yoyote ya Israel dhidi ya vituo vya kuzalisha nishati ya nyuklia hapa nchini kwa kulenga kituo cha silaha za nyuklia cha Israel huko Dimona.

Jenerali Jazairi amesema kituo cha silaha za nyuklia cha Dimona ni shabaha rahisi kwa jeshi la Iran na kwamba iwapo utawala huo ghasibu utathubutu kushambulia Iran basi Tehran haitanyamaza kimya. Ameashiria pia vitisho na mipango ya Marekani ya kutekeleza mauaji ya kigaidi dhidi ya viongozi wa ngazi za juu wa jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na kusisitiza kuwa majibu ya Iran yataitia majuto Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Siku chache zilizopita utawala ghasibu wa Israel ulisema kuwa unafikiria kushambulia vituo vya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran.
 
Yetu macho baada ya Ghadaffi sasa Irani wanamalizia sasa.....
 
?Naibu kamanda wa jeshi la Iran Jenerali Mas'ud Jazairi amesema kuwa Iran itajibu mashambulizi yoyote ya Israel dhidi ya vituo vya kuzalisha nishati ya nyuklia hapa nchini kwa kulenga kituo cha silaha za nyuklia cha Israel huko Dimona.
Jenerali Jazairi amesema kituo cha silaha za nyuklia cha Dimona ni shabaha rahisi kwa jeshi la Iran na kwamba iwapo utawala huo ghasibu utathubutu kushambulia Iran basi Tehran haitanyamaza kimya. Ameashiria pia vitisho na mipango ya Marekani ya kutekeleza mauaji ya kigaidi dhidi ya viongozi wa ngazi za juu wa jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na kusisitiza kuwa majibu ya Iran yataitia majuto Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Siku chache zilizopita utawala ghasibu wa Israel ulisema kuwa unafikiria kushambulia vituo vya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran.

*
Sawa mkuu kwa taarifa ila mimi nina mashaka na uwezo wa Irani kama kweli Israel wataamua ku attack Nuc sites za Irani. Maana nadhani bado wanazo patriotic missiles za wakati ule wa Gulf war modified versions. Ila ni hatari kubwa kwa dunia yote!!!!!!!
 
Wiki iliyopita Prohet TB Joshua wa naija ametoa utabiri wake kwamba dunia umuombe mungu asaidie maelfu ya watu huko Iran kwani Israel inatazamia kutimiza lengo lake a kuipiga Iran. Hii ikiwa na kutaka kusukuma na kudondosha uchumi wa waarabu. Nafikiri vita kwenda Iran tena itasababisha dunia ya waarabu kuja kuleta tabu zaidi duniani kwa mabo ya Islamic fundamentalism and terrorism.
 
Sasa hii Dunia haina haki, Us akijisikia tu kwamba nchi yeyote inampinga anaipiga na kuharibu kama walivyofanya Libya sasa wanahamia Iran nadhani kuna umuhimu wa hizi nchi zingne kuungana pamoja ili tuwe na block 2 hapo heshima itakuepo..
 
Kwanza mtoa mada hajatuletea source ya habari yake tusije jadili pumba.
Pili suala la kushambuliwa Israel aliyelianzisha ni Iran alipotangaza kuwa atalifuta Taifa hilo kwenye Ramani ya Dunia lakini dunia yote ilikuwa kimya na sasa Israel imesema itaishambulia Iran tayari watu wameanza kutafuta mchawi mara US mara ......... suala la usalama wa Israel liko mikononi mwa Israel yenyewe msitafute mchawi.
 
Wiki iliyopita Prohet TB Joshua wa naija ametoa utabiri wake kwamba dunia umuombe mungu asaidie maelfu ya watu huko Iran kwani Israel inatazamia kutimiza lengo lake a kuipiga Iran. Hii ikiwa na kutaka kusukuma na kudondosha uchumi wa waarabu. Nafikiri vita kwenda Iran tena itasababisha dunia ya waarabu kuja kuleta tabu zaidi duniani kwa mabo ya Islamic fundamentalism and terrorism.

utabiri wa uwongo
 
Mungu tuepushe na vita hivyo.vita ni mateso kwa raia.hasa wazee wanawake na watoto.
 
Itakuwa safari ya mwisho Kikwete kwenda kutoa salamu za pole nchini Iran.
 
Back
Top Bottom