Jeshi la Afrika Kusini laimwagia sifa Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,297
33,082
15th July 2009








Police1.jpg

Bendera ya jeshi la Polisi nchini Tanzania.



Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini (SANDF), Jenerali Godfrey Ngwenya, ameishukuru Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa Bara la Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jenerali Ngwenya alitoa shukurani hizo kwa Tanzania jana wakati yeye na ujumbe wake ulipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete Ikulu, Dar es Salaam.
“Tanzania ilitoa mchango mkubwa siyo tu katika ukombozi wa Afrika Kusini, bali katika kulikomboa Bara la Afrika,” Jenerali Ngwenya alimwambia Rais Jakaya Kikwete.
Jenerali Ngwenya alimwambia Rais Kikwete jinsi Afrika Kusini inavyothamini mchango wa Tanzania katika ukombozi wa Afrika Kusini na nchi nyingine hasa zile za Kusini mwa Afrika.
“Tunapokuja Tanzania, kwa kweli tunarudi nyumbani. Tumeishi hapa, mlituhifadhi sote hapa iwe ni ANC, PAC, Frelimo, ZAPU, ZANU…kila mtu alikuwa hapa,” alisema Jenerali Ngwenya na kuongeza:
Naye Rais Kikwete alimweleza Jenerali Ngwenya kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhifadhi historia ya ukombozi na vyama vya ukombozi kama ilivyotokea katika Tanzania.
“Shughuli zote za vyama vya ukombozi Kusini mwa Afrika zilianzia pale Kongwa, kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi yetu… Hii ni historia ya heshima sana katika nchi na bara letu, hivyo tutahakikisha kuwa tunaihifadhi historia hiyo,” alisema Rais Kikwete.


:: IPPMEDIA
 
"Tanzania ilitoa mchango mkubwa siyo tu katika ukombozi wa Afrika Kusini, bali katika kulikomboa Bara la Afrika,"

I think its about time you start thinking about Somalia, its a threat to East African nations, and you have a commendable military unit which can sufficiently deal with the militants in Mogadishu.
 
Back
Top Bottom