Elections 2010 Jeshi kutumika kulinda tenda ya power tiller au kulinda mipaka?

Mtaka Haki

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
492
149
BADO MAMBO YA KUSHANGAZA YANAENDELA KUTOKEA KATIKA NCHI YETU YA TANZANIA.
SLAA AMESEMA KUMBE MNADHIMU MKUU NDIYE ALIYEPEWA TENDA ZA KUAGIZA TREKTA ZA KILIMO KWANZA ZA POWER TILLER.
KAMA NI HIVYO SHIMBO ANAPASWA KUACHIA NGAZI KWANI ITAKUWA IKO WAZI KUWA SHIDA ANATAKA KULINDA TENDA HIYO NA SIYO SHIDA YA KULINDA AMANI.
HAPA NDIPO MAHALI AMBAPO MIGONGANO YA MASLAHI KWA VIONGOZI WENGI IKO WAZI SANA.
TRAFIKI WANAKUWA NA MABASI YA ABIRIA NI KAWAIDA NK.
MGONGANO WA MASLAHI NI MKUBWA NCHINI.



FUATILIA TAARIFA HII YA TANZANIA DAIMA

Dk. Slaa afichua siri ya Luteni Jenerali Shimbo

• ATOBOA ALIVYOPEWA ZABUNI YA KULETA 'POWER TILLERS'

na Christopher Nyenyembe, Tunduma




MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbroad Slaa ametoboa siri ya mahusiano ya karibu kati ya Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulhaman Shimbo, na mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.
Alisema uhusiano wao wa karibu, ulimfanya Luteni Jenerali Shimbo apate zabuni tata ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) na ndio sababu ya kiongozi huyo wa jeshi kutoa kauli ya kuwatisha wapiga kura ili kulinda maslahi yao.

Dk. Slaa, alifichua siri hiyo jana wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma, kwenye uwanja wa michezo katika mkutano huo mkubwa unaoelezewa kuwa umevunja rekodi ya mahudhurio tangu kuanza kwa kampeni za urais.

Dk. Slaa ambaye amekuwa akivuta hisia za wengi kwenye mikutano yake ya kampeni, alisema Shimbo yuko kwenye mtandao wa Rais Kikwete, aliojiunga nao mwaka 2005 na ndio sababu ya kuamua kutoa kauli ya vitishio ili kumlinda Kikwete ambaye ni mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), asing’oke madarakani.

Akifafanua madai dhidi ya Luteni Jenerali Shimbo, Dk. Slaa alisema aliingizwa kwenye mtandao wa Rais Kikwete mwaka 2005, hivyo alimtaka afafanue kwamba kauli aliyoitoa hivi karibuni kuhusu usalama wa nchi ni ya JWTZ au yake binafsi inayolenga kulinda mahusiano yake na Kikwete.

Alisisitiza kuwa anajua kwa undani mambo ya Luteni Jenerali Shimbo na uhusiano wake na mtandao wa Rais Kikwete kwamba alijiunga nao mwaka 2005, akiwa askari wa juu wa jeshi ambaye kwa mujibu wa sheria, haruhusiwi kuegemea upande wowote wa mgombea au chama.

“Haya mambo matatu ninayowaambia nimeyafanyia utafiti wa kutosha ndani ya muda wa siku nne tangu Shimbo alipotoa kauli ya kuwatisha wananchi kuwa kuna baadhi ya vyama vya siasa vimeahidi kumwaga damu, nimempa siku saba yeye na IGP kuhakikisha viongozi wa siasa waliotoa kauli hizo, wanatupwa gerezani mara moja,” alisema Dk. Slaa.

Alisema kitendo cha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi huyo kujiingiza kwenye mtandao wa Kikwete, kumeibua hofu kuwa endapo Rais Kikwete akiangushwa kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka huu, siri yao itafichuka, ikiwemo ile ya ufisadi wa sh bilioni 15, zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mgodi wa Buhemba kupitia kampuni ya Meremeta.

Huku akionyesha kujiamini na kushangiliwa na maelfu ya wananchi wa Tunduma, Dk. Slaa alisema kutokana na uswahiba wa Shimbo na Rais Kikwete, alifanikiwa kupewa zabuni ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) kwa ajili ya Kilimo Kwanza na kusisitiza kuwa utafiti alioufanya ni wa kweli kwani unamlenga Kikwete na Shimbo na kuwataka wakanushe hadharani madai hayo.

“Hali hiyo ndiyo inayompa ujasiri, Luteni Jenerali Shimbo wa kusimama na kutoa kauli nzito kwa wananchi kupitia vyombo vya habari kuwa kuna dalili za uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi mkuu. Kauli hiyo ni ya uchochezi na haiwezi kuachwa hivi hivi kwa kuwa wahusika walioitoa wapo.”

“Nataka kujua Shimbo ametoa kauli ya JWTZ kama Shimbo au hiyo ni kauli ya jeshi. JK na Shimbo mnatupeleka pabaya, ofisa wa jeshi anatoa tamko la kuwatisha wananchi, kumbe lengo lake ni kulinda maslahi yake binafsi, tuambiwe hiyo kauli ni ya Shimbo au jeshi,” alisisitiza Dk Slaa.

Alisema kauli ya kuvitaka vyama vya siasa vikubali matokeo, haiwezi kuachwa bila kujibiwa ili apatikane mtu aliyeitoa na achukuliwe hatua kwani CHADEMA kamwe haiko tayari kuona damu ikimwagika.

Dk. Slaa alisema anakusudia kulipua hujuma nyingine ya umiliki wa maduka ya JWTZ yaliyotakiwa kuuza bidhaa kwa bei ndogo kwa wanajeshi, lakini sasa yanamilikiwa na vigogo wa jeshi hilo.

Mbali ya kuelekeza mashambulizi kwa Mnadhimu Mkuu huyo wa JWTZ, Dk. Slaa alihamia upande wa pili kwa kuwatuhumu baadhi ya askari polisi wa mji mdogo wa Tunduma kuwa wamekuwa wakifanya kazi za kupiga kampeni kwenye makanisa kwa lengo la kuwashinikiza wananchi wakichague Chama cha Mapinduzi (CCM) na mgombea wake, Rais Kikwete.

“Ndugu zangu tumepata taarifa kuwa kuna askari polisi wanapita kwenye makanisa wakiipigia kampeni CCM, namtaka OCD amfukuze kazi mara moja, kama hawezi naye anapaswa kujiuzulu, siku Dk. Slaa akiingia Ikulu sijui askari huyo atakapopotelea; askari msifikiri Kikwete ana hati ya kumiliki nchi hii kwa sababu hamjui Oktoba 31 nani atakuwa bosi wenu,” alisema Dk. Slaa.

Akielezea ahadi mbalimbali zinazotolewa na CHADEMA, Dk. Slaa alisema haziwezi kulinganishwa na za Kikwete ambaye amekuwa akifanya kazi kama afisa mipango na miradi wa CCM na sio kama mgombea wa nafasi ya urais kwa kuwa ahadi nyingi anazozitoa tayari zilikwishapitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais yeyote akija, anapaswa kuzitekeleza.

Alisema CHADEMA imelenga kujikita zaidi kwenye mambo ya msingi ya kitaifa kuliko kuendelea kutoa ahadi za papo kwa papo zisizoleta suluhu ya matatizo kwa Watanzania maskini.

Katika mkutano huo, Dk. Slaa alimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Mbozi Magharibi, David Silinde, na mgombea udiwani wa kata ya Tunduma (CHADEMA), Frank Mwakajoka, ambao wanaungwa mkono na mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma waliofurika kwenye uwanja huo.

Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Silinde alipopewa nafasi ya kuwasalimia wakazi hao, aliuhakikishia umma huo kuwa CHADEMA imejipanga kuzoa viti vyote 14 vya udiwani katika jimbo hilo na ana uhakika wa kumshinda mgombea wa CCM, Dk. Luke Siyame.
 
Huu ushahidi ni mzito na JK lazima ajibu mapigo vinginevyo sisi tutachukulia huu ndio ukweli wake.

Alisema kitendo cha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi huyo kujiingiza kwenye mtandao wa Kikwete, kumeibua hofu kuwa endapo Rais Kikwete akiangushwa kwenye kinyang'anyiro cha urais mwaka huu, siri yao itafichuka, ikiwemo ile ya ufisadi wa sh bilioni 15, zilizotolewa na serikali kwa ajili ya mgodi wa Buhemba kupitia kampuni ya Meremeta
.


Dk. Slaa alisema anakusudia kulipua hujuma nyingine ya umiliki wa maduka ya JWTZ yaliyotakiwa kuuza bidhaa kwa bei ndogo kwa wanajeshi, lakini sasa yanamilikiwa na vigogo wa jeshi hilo.

Huku akionyesha kujiamini na kushangiliwa na maelfu ya wananchi wa Tunduma, Dk. Slaa alisema kutokana na uswahiba wa Shimbo na Rais Kikwete, alifanikiwa kupewa zabuni ya kuingiza matrekta madogo (Power Tillers) kwa ajili ya Kilimo Kwanza na kusisitiza kuwa utafiti alioufanya ni wa kweli kwani unamlenga Kikwete na Shimbo na kuwataka wakanushe hadharani madai hayo.
 
Back
Top Bottom