Jerry Silaa kashindwa kazi?

Nguruvi3,

Ahsante sana mdau kwa maelezo yako na hoja zilizojitosheleza.

Kama ni msikivu, Jerry na akusikie kwa hoja na ushauri ulioutoa. Hapa tunatafuta uwajibikaji wa viongozi ili kuchochea upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi pamoja na maendeleo yao.

Kama atatimiza wajibu wake kikamilifu na maendeleo yakashuhudiwa na wananchi, watampongeza. Lakini akijisahau sisi tutamkumbusha kupitia JF ama forum nyengine kadri inavyowekana.
 
Last edited by a moderator:
...............Tumenunua malori 9 ya taka kuongeza nguvu. Tunanunua greda 2 na moja tulilonalo yutakuwa 1st council sio tu kumiliki greda zaidi ya moja bali matatu kwa ajili ya kuchonga njia za mitaani ambazo ni unpaved...................

Nimekusoma na nimeona kuna shida zifuatazo.....just kwa kuanzia

Sustainability ya hizo liability
Creativity katika kutekeleza majukumu ya Ilala kiufanisi zaidi.........(inaelekea kama ni business as usual)

Mkumbuke mnazungumza na mtu wa Gongolamboto, mtume na Yesu tu ndio walitolewa nyongo.
Kwa wasionifahamu mimi sirembi maneno na kuwaambia watu wajibu wao.
Ndio maana nasema na narudia kusema Kuendesha council sio rahisi kama mnavyodhani, naamini natekeleza wajibu wangu 300% na wakati wote nakumbusha kila mtu atimize wajibu wake kwa mujibu wa katiba na sheria.

....and this one proves my point....."business as usual"........Mh Jaji Mstaafu Lubuva naye alikuja na sentiment similar to hizo hapo juu........meaning business as usual...........

Well, I'm giving you benefit of doubt kwa kuwa bado ni mgeni na ni kijana na ninaamini uko open kupokea mawazo mbadala na utakuwa ready kuleta/kushinikiza mabadiliko..........
 
JERRY SLAA NA MIKAKATI YAKE YA KUTAFUTA UBUNGE JIMBO LA UKONGA 2015:
Siku zote kiongozi bora wa uma ni yule anayekubali kukosolewa na kujisahisha pale inapobidi ili kuboresha ufanisi wa kazi yake. Jerry utake usitake kwenye hili lazima tukukosoe kwa facts, wewe umekuwa diwani katika kata ya ukonga kwa muda mrefu na hiki ni kipindi chako cha pili ambapo awamu ya kwanza ulikuwa naibu meya na sasa ni meya kamili lakini hakuna chochote kile cha maana ulichokifanya pamoja na mbunge wako wa awali Makongoro Mahanga na sasa Mama Eugene Mwaiposa ambaye amekuwa kama mbunge wa viti maalum na si wa jimbo. Sihitaji kuzungumzia takwimu ulizozitoa humu ndani because I know they have nothing to do na wananchi wa kawaida zaidi ya kuwafaidisheni wewe na maswaiba zako, ambao ni mafisadi wakubwa. Hatuyafanyi haya kwa kukukomoa bali tunakukumbusha wajibu wako. Naomba niweke record sawa humu JF ili watanzania waelewe haya tunayoyazungumza wananchi wenzako wa Ukonga:

Suala la huduma za serikali za mitaa Ukonga:
Hii ni changamoto kubwa ya kwanza ambayo inakela sana wananchi wa Ukonga na maeneo mengine ya Manispaa ya Ilala. Katika maeneo yote Wenyeviti wa serikali za mitaa ya Ukonga ambao wote ni maswaiba wako wazuri unaowatumia kukupigia kampeni za kuusaka ubunge 2015, wamejifanya miungu watu na wanataka waabudiwe na wamekuwa wafujaji wazuri wa fedha za uma. Mathalani rafiki yako mkubwa ndugu Alfred Kipondya, mwenyekiti wa mtaa wa Madafu ambaye ni kinara wa kuwachangisha wanachi michango isiyokuwa na kichwa wala miguu. Mmekuwa mkishirikiana nae kula pesa za miradi mbalimbali ya uma kama huu wa maji Mzambarauni kama ambavyo nimeelekeza hapo chini. Hali kadhalika unatueleza mmeongeza magari ya kuzoa taka ya municipal council ilihali wewe na Kipondya mnaendelea kuwachangisha wananchi kila kaya 3,000Tshs fedha ambazo zinaingia katika kampuni yenu binafsi, na hili ninakuombeni acheni mara moja mkija kwetu na wafungulia mbwa. Mbaya zaidi umekuwa ukiwashinikiza wenyeviti pamoja na watendaji wa serikaliza mitaa wakusanye 2,00Tshs kwa kila mtu anayekwenda kwa ajili ya kusainiwa document yoyote ile, ili muulize vizuri swaiba wako Kipondya hatokaa anisahau pale aliponiomba hela kwa ajili ya kunisainia document hukuakitaka kunipa risiti ya cash book yenye muhuli wa serikali ya mitaa. Wananchi huwa tunajiuliza Ilala Municipal Council kwenye hayo makusanyo mnayokusanya si kuna fedha mnazorudisha zitumike katika ofisi zetu za kata pamoja na serikali za mitaa, zinafanya kazi gani?? Jamani mbona hamtuonei huruma? Gharama za maisha zimepanda acheni kutunyonya sana.

Suala la Mgogoro wa Ardhi Kinyerezi:
Halmashauri ya Ilala imepitisha mpango wa upimaji wa viwanja kwenye maeneo ambayo watu wanaishi kule kinyerezi, ambapo mmewaambia wananchi wachangie gharama za upimaji ambapo katika kila square metre moja wanatakiwa kuchangia shilingi 1500. Ukishindwa kulipia gharama kwa ajili ya upimaji unanyang’anywa eneo na unalipwa fidia. Na unajua fika kesi iko mahakamani ambapo wananchi wanapinga gharama ya uchangiaji na hali kadhalika mnajua fika kabisa hata kama mtu akishindwa kulipa gharama za upimaji, gharama za ufidiaji haziendani kabisa na gharama ahalisi za ardhi. Mwanasheria wako wa manispaa ya Ilala aliieleza mahakama kuu mbele ya Judge Shangwa kwamba fedha hizo mnazotaka kuwalipa wananchi mmezikopa bank. So mnataka hizo interest ndio wananchi wawasaidie kulipa?? Huu ni mradi ambao una harufu ya ufisadi na wewe unahusika moja kwa moja kwenye hili pamoja na maswaiba zako.

Mradi wa maji Ukonga Mzambarauni:
Mh mstaiki meya Jerry Slaa hili linaniuma sana kwani lina nigusa sana na watu wa Ukonga hawatokaa walisahau milele katika kipindi chao chote cha maisha yao hapa Duniani. Wananchi wote walichangishwa shilingi 5,000 Tshs kwa kila kaya kwa ajili ya mradi huu tena uchangiaji huo ulikuwa ni wa lazima kwa ajili ya kuondoa shida ya maji, na mkawaambia wananchi mtawasambazia mabomba kuanzia pale mzambarauini kwenda sehemu zingine mbalimbali kama Madafu,Mombasa, Gongo la Mboto, Mwisho wa Lami, mpaka Mazizini. Hivi huwa ukipita pale Mzambarauni roho huwa haikuumi kuona mmekula pesa za wananchi na huduma hakunailiyopatikana?? Muogopeni mwenyezi mungu tendeni haki panapostahili.

Mkakati wako wa kuusaka Ubunge Jimbo La Ukonga-2015:
Hongera sana kwa kushiriki kikamilifu kupigania kupatikana kwa jimbo la Ukonga ambalo linaongozwa na very weak candidate Mh Eugene Mwaiposa,ambaye anafahamu kuwa hiki ndiyo kipindi chake cha mwisho na hatorudi tena kwenye nafasi hiyo. Kwa hili naomba nikupongeze kwa kuona umuhimu wa kuwa na jimbo letu la Ukonga, dhana ambayo tuliamini itasaidia kutuletea maendeleo eneo letu la Ukonga, lakini hali imekuwa tofauti kabisa zaidi ya kuwa chaka la watu kuvuna pesa. Nashukuru umekili kuwa kama kugombea ungegombea 2010 kwani ulikuwa moja ya waasisi wa kupatikana kwa jimbo. Lakini ukweli wenyewe wa hili uko moyoni mwako, na ninajua dhamira yako inakusuta kwenye hili. Chanzo cha wewe kutogombea ubunge 2015 kinafahamika wazi kwa wale tunaofutailia. Mshauri wako mkubwa siku zote amekuwa ni mzee wetu mpendwa Balozi Patrick Tsere (Kipenzi cha vijana) ambaye ulifanya nae kazi akiwa kama DC wa Ilala na wewe ukiwa kama naibu Mstaiki meya. Unafahamu vizuri jinsi ambavyo walikuwa hawaelewani na mstaiki meya wa wakati huo na sababu kubwa ilikuwa ni uelewa pamoja na elimu ndogo aliyonayo mheshimiwa huyo kwa hiyo walikuwa wakipishana mzee Tsere muda wote. Hali iliyopelekea Mzee Tsere kukutumia wewe zaidi kwenye masuala mengi, hili unaweza ukabisha ila likowazi ulisafiri sana kwenda ziara za nje kwa sababu hiyo tu. Ili fika mahali mambo yakawa hayaendi kwa ajili ya mgogoro huo,ndipo Mh Rasi alipoona amsimamishe kazi Tsere na baadaye kumpangia nafasi ya ubalozi Malawi (rejea maneno ya Mh Raisi siku anamwapisha Tsere Ikulu). Na ni mzee Tsere aliyekushauri usubiri kwanza usiingie kwenye ubunge uongoze Ilala Municipal Council. Sasa mikakati yako ya kuusaka ubunge wa jimbo la Ukonga umeizindua katika ma Bar mbalimbali na kijiwe chako kikubwa cha kukusanya taarifa ni Mangi Bar (Tokyo) ,chini ya swaiba wako mkubwa na tapeli namba moja Saidi Dezo. Hutopata kula za Ukonga kwa kuwanywesha watu bia ndugu yetu, chapa kazi tukuvalue kwa uadilifu na uwajibikaji wako. Majuzi ulikuwa Kampala International University-KIU,kwa ajili ya mkakati huoo na umemwaga hela ukiamini vijana wanakupenda la hasha yawezekana hizo ni ndoto za buriani. Umri wako ulionao bado ni mdogo, weweni kijana mwenzetu cha kushangaza umekuwa na lugha za kejeli hali kadhalika dharau kubwa watu, hasa vijana unatuona tuko kijiweni. La hasha yawezekana sasa tukawa hatuna cha kukusaidia ila japo salamu tutakuona kiongozi wetu unatujali. Umediriki kuanza kuchangisha fedha kwenye mitandao na sehemu mbalimbali (ushaidi tunao) kwa ajili ya mambo mbalimbali ya Jimbo la Ukonga lakini badala ya kutimiza lengo la uchangishaji huo badala yake umekuwa ukiyafanya hayo mambo kisiasa. Haya yote yana mwisho wake ndugu yetu tunakuomba utimize wajibu wako kama ambavyo tulikupa ridhaa ya kutuwakilisha.

Asante
Brigedia
 
JERRY SLAA NA MIKAKATI YAKE YA KUTAFUTA UBUNGE JIMBO LA UKONGA 2015:
Siku zote kiongozi bora wa uma ni yule anayekubali kukosolewa na kujisahisha pale inapobidi ili kuboresha ufanisi wa kazi yake. Jerry utake usitake kwenye hili lazima tukukosoe kwa facts, wewe umekuwa diwani katika kata ya ukonga kwa muda mrefu na hiki ni kipindi chako cha pili ambapo awamu ya kwanza ulikuwa naibu meya na sasa ni meya kamili lakini hakuna chochote kile cha maana ulichokifanya pamoja na mbunge wako wa awali Makongoro Mahanga na sasa Mama Eugene Mwaiposa ambaye amekuwa kama mbunge wa viti maalum na si wa jimbo. Sihitaji kuzungumzia takwimu ulizozitoa humu ndani because I know they have nothing to do na wananchi wa kawaida zaidi ya kuwafaidisheni wewe na maswaiba zako, ambao ni mafisadi wakubwa. Hatuyafanyi haya kwa kukukomoa bali tunakukumbusha wajibu wako. Naomba niweke record sawa humu JF ili watanzania waelewe haya tunayoyazungumza wananchi wenzako wa Ukonga:

Suala la huduma za serikali za mitaa Ukonga:
Hii ni changamoto kubwa ya kwanza ambayo inakela sana wananchi wa Ukonga na maeneo mengine ya Manispaa ya Ilala. Katika maeneo yote Wenyeviti wa serikali za mitaa ya Ukonga ambao wote ni maswaiba wako wazuri unaowatumia kukupigia kampeni za kuusaka ubunge 2015, wamejifanya miungu watu na wanataka waabudiwe na wamekuwa wafujaji wazuri wa fedha za uma. Mathalani rafiki yako mkubwa ndugu Alfred Kipondya, mwenyekiti wa mtaa wa Madafu ambaye ni kinara wa kuwachangisha wanachi michango isiyokuwa na kichwa wala miguu. Mmekuwa mkishirikiana nae kula pesa za miradi mbalimbali ya uma kama huu wa maji Mzambarauni kama ambavyo nimeelekeza hapo chini. Hali kadhalika unatueleza mmeongeza magari ya kuzoa taka ya municipal council ilihali wewe na Kipondya mnaendelea kuwachangisha wananchi kila kaya 3,000Tshs fedha ambazo zinaingia katika kampuni yenu binafsi, na hili ninakuombeni acheni mara moja mkija kwetu na wafungulia mbwa. Mbaya zaidi umekuwa ukiwashinikiza wenyeviti pamoja na watendaji wa serikaliza mitaa wakusanye 2,00Tshs kwa kila mtu anayekwenda kwa ajili ya kusainiwa document yoyote ile, ili muulize vizuri swaiba wako Kipondya hatokaa anisahau pale aliponiomba hela kwa ajili ya kunisainia document hukuakitaka kunipa risiti ya cash book yenye muhuli wa serikali ya mitaa. Wananchi huwa tunajiuliza Ilala Municipal Council kwenye hayo makusanyo mnayokusanya si kuna fedha mnazorudisha zitumike katika ofisi zetu za kata pamoja na serikali za mitaa, zinafanya kazi gani?? Jamani mbona hamtuonei huruma? Gharama za maisha zimepanda acheni kutunyonya sana.

Suala la Mgogoro wa Ardhi Kinyerezi:
Halmashauri ya Ilala imepitisha mpango wa upimaji wa viwanja kwenye maeneo ambayo watu wanaishi kule kinyerezi, ambapo mmewaambia wananchi wachangie gharama za upimaji ambapo katika kila square metre moja wanatakiwa kuchangia shilingi 1500. Ukishindwa kulipia gharama kwa ajili ya upimaji unanyang'anywa eneo na unalipwa fidia. Na unajua fika kesi iko mahakamani ambapo wananchi wanapinga gharama ya uchangiaji na hali kadhalika mnajua fika kabisa hata kama mtu akishindwa kulipa gharama za upimaji, gharama za ufidiaji haziendani kabisa na gharama ahalisi za ardhi. Mwanasheria wako wa manispaa ya Ilala aliieleza mahakama kuu mbele ya Judge Shangwa kwamba fedha hizo mnazotaka kuwalipa wananchi mmezikopa bank. So mnataka hizo interest ndio wananchi wawasaidie kulipa?? Huu ni mradi ambao una harufu ya ufisadi na wewe unahusika moja kwa moja kwenye hili pamoja na maswaiba zako.

Mradi wa maji Ukonga Mzambarauni:
Mh mstaiki meya Jerry Slaa hili linaniuma sana kwani lina nigusa sana na watu wa Ukonga hawatokaa walisahau milele katika kipindi chao chote cha maisha yao hapa Duniani. Wananchi wote walichangishwa shilingi 5,000 Tshs kwa kila kaya kwa ajili ya mradi huu tena uchangiaji huo ulikuwa ni wa lazima kwa ajili ya kuondoa shida ya maji, na mkawaambia wananchi mtawasambazia mabomba kuanzia pale mzambarauini kwenda sehemu zingine mbalimbali kama Madafu,Mombasa, Gongo la Mboto, Mwisho wa Lami, mpaka Mazizini. Hivi huwa ukipita pale Mzambarauni roho huwa haikuumi kuona mmekula pesa za wananchi na huduma hakunailiyopatikana?? Muogopeni mwenyezi mungu tendeni haki panapostahili.

Mkakati wako wa kuusaka Ubunge Jimbo La Ukonga-2015:
Hongera sana kwa kushiriki kikamilifu kupigania kupatikana kwa jimbo la Ukonga ambalo linaongozwa na very weak candidate Mh Eugene Mwaiposa,ambaye anafahamu kuwa hiki ndiyo kipindi chake cha mwisho na hatorudi tena kwenye nafasi hiyo. Kwa hili naomba nikupongeze kwa kuona umuhimu wa kuwa na jimbo letu la Ukonga, dhana ambayo tuliamini itasaidia kutuletea maendeleo eneo letu la Ukonga, lakini hali imekuwa tofauti kabisa zaidi ya kuwa chaka la watu kuvuna pesa. Nashukuru umekili kuwa kama kugombea ungegombea 2010 kwani ulikuwa moja ya waasisi wa kupatikana kwa jimbo. Lakini ukweli wenyewe wa hili uko moyoni mwako, na ninajua dhamira yako inakusuta kwenye hili. Chanzo cha wewe kutogombea ubunge 2015 kinafahamika wazi kwa wale tunaofutailia. Mshauri wako mkubwa siku zote amekuwa ni mzee wetu mpendwa Balozi Patrick Tsere (Kipenzi cha vijana) ambaye ulifanya nae kazi akiwa kama DC wa Ilala na wewe ukiwa kama naibu Mstaiki meya. Unafahamu vizuri jinsi ambavyo walikuwa hawaelewani na mstaiki meya wa wakati huo na sababu kubwa ilikuwa ni uelewa pamoja na elimu ndogo aliyonayo mheshimiwa huyo kwa hiyo walikuwa wakipishana mzee Tsere muda wote. Hali iliyopelekea Mzee Tsere kukutumia wewe zaidi kwenye masuala mengi, hili unaweza ukabisha ila likowazi ulisafiri sana kwenda ziara za nje kwa sababu hiyo tu. Ili fika mahali mambo yakawa hayaendi kwa ajili ya mgogoro huo,ndipo Mh Rasi alipoona amsimamishe kazi Tsere na baadaye kumpangia nafasi ya ubalozi Malawi (rejea maneno ya Mh Raisi siku anamwapisha Tsere Ikulu). Na ni mzee Tsere aliyekushauri usubiri kwanza usiingie kwenye ubunge uongoze Ilala Municipal Council. Sasa mikakati yako ya kuusaka ubunge wa jimbo la Ukonga umeizindua katika ma Bar mbalimbali na kijiwe chako kikubwa cha kukusanya taarifa ni Mangi Bar (Tokyo) ,chini ya swaiba wako mkubwa na tapeli namba moja Saidi Dezo. Hutopata kula za Ukonga kwa kuwanywesha watu bia ndugu yetu, chapa kazi tukuvalue kwa uadilifu na uwajibikaji wako. Majuzi ulikuwa Kampala International University-KIU,kwa ajili ya mkakati huoo na umemwaga hela ukiamini vijana wanakupenda la hasha yawezekana hizo ni ndoto za buriani. Umri wako ulionao bado ni mdogo, weweni kijana mwenzetu cha kushangaza umekuwa na lugha za kejeli hali kadhalika dharau kubwa watu, hasa vijana unatuona tuko kijiweni. La hasha yawezekana sasa tukawa hatuna cha kukusaidia ila japo salamu tutakuona kiongozi wetu unatujali. Umediriki kuanza kuchangisha fedha kwenye mitandao na sehemu mbalimbali (ushaidi tunao) kwa ajili ya mambo mbalimbali ya Jimbo la Ukonga lakini badala ya kutimiza lengo la uchangishaji huo badala yake umekuwa ukiyafanya hayo mambo kisiasa. Haya yote yana mwisho wake ndugu yetu tunakuomba utimize wajibu wako kama ambavyo tulikupa ridhaa ya kutuwakilisha.

Asante
Brigedia

Brigedia,

Kweli wewe mwanajeshi wa ukweli, na huu ndio uzuri wa JF, mtu anapewa ukweli wake peupeeee.

Haya sasa Jerry akanushe tena na haya ama apige kimya ama aendelee na dharau na kiburi chake lakini akae akijua mipango yake yote tunayo.

Sasahivi tunachohitaji ni maendeleo, hatuhitaji bla bla. Na hili la kula fedha za mradi wa maji ni kitanzi kwa Jerry hata ukitumia fedha nyingi kiasi gani, bia zako tutakunywa lakini kura zetu wana ukonga hutopata. Lakini muda bado upo unaweza kujirekebisha.
 
Kabla ya kuziita hizi liability creativity ungeuliza mfumo qa sasa unagharimu kiasi gani na ungejua kwanini tumeamua hivi.

Nimekusoma na nimeona kuna shida zifuatazo.....just kwa kuanzia

Sustainability ya hizo liability
Creativity katika kutekeleza majukumu ya Ilala kiufanisi zaidi.........(inaelekea kama ni business as usual)

....and this one proves my point....."business as usual"........Mh Jaji Mstaafu Lubuva naye alikuja na sentiment similar to hizo hapo juu........meaning business as usual...........

Well, I'm giving you benefit of doubt kwa kuwa bado ni mgeni na ni kijana na ninaamini uko open kupokea mawazo mbadala na utakuwa ready kuleta/kushinikiza mabadiliko..........
 
Mkitafuta uwajibikaji wa viongozi bila uwajibikaji wa wananchi ni kazi bure!

@Nguruvu3,
Ahsante sana mdau kwa maelezo yako na hoja zilizojitosheleza.
Kama ni msikivu, Jerry na akusikie kwa hoja na ushauri ulioutoa. Hapa tunatafuta uwajibikaji wa viongozi ili kuchochea upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi pamoja na maendeleo yao.

Kama atatimiza wajibu wake kikamilifu na maendeleo yakashuhudiwa na wananchi, watampongeza. Lakini akijisahau sisi tutamkumbusha kupitia JF ama forum nyengine kadri inavyowekana.
 
Karibu Q n A

Mkuu kama kweli wewe ni Jerry Slaa siasa za nini? umeulizwa swali hujibu isipokuwa unakuja kujenga fikra za watu kwamba kuna uadui na siasa. Binafsi tumekutana ukiwa bado naibu Meya na sijui kama unanikumbuka lakini nakushangaa sana unapochukulia mjadala huu hapa ni ktk mbinu za kukupakaza wakati ndivyo wananchi wanavyokuona.. Kwa nini usichukue muda na kuwasikiliza wao maana wasemayo hayana uongo na wala huyapingi isipokuwa huna majibu ktk utendaji kazi..
 
Kaka, nashukuru mungu tumeelewana na angalau umesema yalofanyika kwa kirefu sana.

Humu ndani huyu Mwita Manyara sijui Manyanga anaboa sana, huyu ilibidi mie jana nipakaziane nae kavukavu japo hajui hata asemalo maskini, kaishia kuniponda eti hoja zangu ni za hovyo huku akisahau asili yake na tabia ya makabila kama yake, niwie radhi kuwaweka wote wa kabila lake humo, huyu ni mtu tu anayehitaji kumhurumia na nahisi anatumiwa bila kujijua ama kwa kujua.

Nilimwambia kama anataka aje ofisini kwako akuhoji moja baada ya jingine kuliko kujifanya ujuaji humu JF. Kimsingi ni aibu kwa Mwita kusimamia hoja mfu bila kufanya utafiti. Mimi mkuu sikujui ila nililazimika kumuelimisha huyu jamaa bila mafanikio, mwisho wake mke wangu akaniambia nitafakari jinsi watu wanavyoweza kuwa wanafikiri kwa mujibu wa Dr Masaburi.

Pangu Pakavu.

acha kujigonga gonga ..wewe huoni JIJI lilivyo chafu? au tukuwekee picha kabisa..yeye anashindwa nini kusafisha eneo lake?
 
JERRY SLAA NA MIKAKATI YAKE YA KUTAFUTA UBUNGE JIMBO LA UKONGA 2015:

Suala la huduma za serikali za mitaa Ukonga:

Mkakati wako wa kuusaka Ubunge Jimbo La Ukonga-2015:

Hapa ndipo ninapoipendea JF ..na nina uhakika huyu J Slaa mwenye jazba hawezi kuchomoa mshale hata mmoja kati ya hii aliyopewa hapa. Meya kama ulikuwa hujui sasa unatakiwa ujue kuwa JF sio Facebook ..kwamba ukiandika hata upuuzi kama huu " niko bara nakula mishakaki" watu watakupigia makofi na ku like status yako bila kuangalia ufanisi wako ..na ndio maana nimeona post zako za nyuma umesema kuwa tuhamishie hoja zetu kule facebook kwa sababu kule kuna account zetu haisi..hata hapa ni halisi kwa sababu mambo unayoambia hapa ni kweli na wala sio uongo.tafuta maana ya forums utajua ..na mnahimiza watu waje kule facebook ili mlipize visasi.kwani nani hatuwajui nyi kwa visasi? .jibu ndondo na fanya kazi tuliyokutuma .
 
Mkitafuta uwajibikaji wa viongozi bila uwajibikaji wa wananchi ni kazi bure!
You mean we wananchi have made terrible mistake as our responsibility to put your there? Soon utasema mbona viongozi waliopita hamkuwasema!! Jerry umekuwa mlevi wa madaraka kiasi hiki!!! Oh boy!!!
 
Ndugu yangu anayehoji kwa hoja nitamjibu kwa hoja, lugha itayotumika nayo ina majibu yake. Na wengine naawacha maana sielewi hata wanachozungumza. Kama mtu haoni impact ya 62.5% increment ya revenue toka 16 B mpaka 26B sasa huyu majibu ambayo ningempa Judge Kaganda angeniita kwenye baraza.

Jerry calm down kidogo, wengi wanachokisema hapa ni kuwa mimi kama mtanzania wa kawaida sihitaji sana kujua wewe umeongeza mapato kwa asilimia ngapi, hiyo ni mipango yako wewe ya kimikakati. Mimi nahitaji kuona barabara zina street lights, safi na hazina mashimo, vyakula haviuzwi barabarani, mji ni msafi na mitaro ya maji machafu haijafumuka mitaani.

Hizo figure unazotupa hapa hata mtu akikataa huwezi kubishana nae cos hana ushahidi wowote. Watu wanachokiona ni reflection ya utendaji wako.

Tafadhali usiwe mbishi watu watakuhukumu kwa ushahidi unaoonekana na sio namba unazozitaja humu JF. Don't say we didn't warn you!
 
Jerry nimeona umekuwa ukijibu hoja zilizo nyingi lakini mbona za Bregadia hujibu?.Au amekuchana live?
 
Mh Silaa Jerry

Nilikuandikia kama ifuatavyo
Nimekusoma na nimeona kuna shida zifuatazo.....just kwa kuanzia

1.Sustainability ya hizo liability (malori na Graders)
2. Creativity katika kutekeleza majukumu ya Ilala kiufanisi zaidi.........(inaelekea kama ni business as usual)

Well, I'm giving you benefit of doubt kwa kuwa bado ni mgeni na ni kijana na ninaamini uko open kupokea mawazo mbadala na utakuwa ready kuleta/kushinikiza mabadiliko..........

Ukaja kunijibu kama ifuatavyo............

Kabla ya kuziita hizi liability creativity ungeuliza mfumo qa sasa unagharimu kiasi gani na ungejua kwanini tumeamua hivi.

Inaelekea una tatizo la uzoefu......sitakulaumu...kwani wewe bado ni kijana mdogo inabidi ujifunze zaidi......nilitegemea "labda ungeuliza kwanini nimeziita hizo lori na Graders liabilities.....ili nikupe experience yangu ambayo ingekupa pengine mtizamo tofauti na jinsi ya kupambana na mfumo uliopo na unaoulaumu.........

On another note.........kuna mkuu Chesty hapa anaeleza yafutayo

Jerry calm down kidogo, wengi wanachokisema hapa ni kuwa mimi kama mtanzania wa kawaida sihitaji sana kujua wewe umeongeza mapato kwa asilimia ngapi, hiyo ni mipango yako wewe ya kimikakati. Mimi nahitaji kuona barabara zina street lights, safi na hazina mashimo, vyakula haviuzwi barabarani, mji ni msafi na mitaro ya maji machafu haijafumuka mitaani.

Hizo figure unazotupa hapa hata mtu akikataa huwezi kubishana nae cos hana ushahidi wowote. Watu wanachokiona ni reflection ya utendaji wako.

Tafadhali usiwe mbishi watu watakuhukumu kwa ushahidi unaoonekana na sio namba unazozitaja humu JF. Don't say we didn't warn you!

Tafakari kwa umakini maoni ya Mkuu Chesty...............

Mh Jerry Silaa.............usiwe taken away na mawazo ya business as usual............
 
Jerry Slaa,
Mkuu wangu jaribu sana kuwa na staha ondoa jazba na kama ulivyoshauriwa kuna hoja ambazo huna sababu ya kuzijibu maadam ziko nje ya swali isipokuwa ni kashfa binafsi (personal) hivyo kwa majibu yako kama haya inaonyesha wazi weweni kingozi wa aina gani na kwa nini kazi hiyo ILOPEWA imekuwa ngumu kwako.

Maswali yetu ni rahisi kabisa kwamba jiji la Dar linazidi kuwa chafu, kwa mfano mdogo tu umezungumzia makusanyo ya fedha soko la Ilala ambayo yameongezeka toka umeingia madarakani na pia kuwezesha mfuko kupanuka zaidi kuliko zamani lakini kama fedha hizo hazifanyi kazi kuboresha soko hilo hilo likaonekana zuri na tofauti hizi fedha zinachukuliwa kama biashara tu...

Huwezi kusanya mabillioni ya fedha toka sehemu muhimu kama soko la Ilala lakini soko lenyewe haliboreki yaani linazidi kuwa baya na chafu watu wanapanga mali zao hadi barabarani ili mradi mnajaza wateja kuongeza pato. Vivyo hivyo sehemu nyingi za mji wetu zinazidi kuharibika wakati hizo fedha mnazotenga kwa maendeleo haziifanyi kazi inayotakiwa..

Swali jingine ni kwamba ikiwa leo Kingunge anaweza kusanya fedha za parking na akawalipa asilimia yenu nani mwenye jukumu la kuboresha Parking hizo?.. Na inakuwaje mtu binafsi kama Kingunge anaweza kusanya fedha bila vifaa vyovyote vya parking akitumia nguvukazi ya watu lakini City inashindwa kukusanya yenyewe hadi mnakodisha watu binafsi ambao hawaboreshi wala kuongeza pato la ukusanyaji kodi hiyo ya parking..

Mengine yatafuata kuhusu mapipa ya Taka ambayo kijana mdogo rafiki yangu aliwekeza Dar na kuyasambaza wilaya ya Kinondoni lakini Ilala amekwamishwa kupewa zabuni hiyo na sababu nazijua!. Sasa mwananchi ambaye yuko tayari kusambaza mapipa ya taka kando ya barabara manispaa yako (uwajibikaji wa mwananchi) anapokwamishwa na uongozi wa City (uwajibikaji wa kingozi) utaweza vipi kuwalaumu wananchi ambao wako tayari ktk uwekezaji lakini hukwamisha na Urasimu wa Halmashauri yako?
 
Ndugu yangu anayehoji kwa hoja nitamjibu kwa hoja, lugha itayotumika nayo ina majibu yake. Na wengine naawacha maana sielewi hata wanachozungumza. Kama mtu haoni impact ya 62.5% increment ya revenue toka 16 B mpaka 26B sasa huyu majibu ambayo ningempa Judge Kaganda angeniita kwenye baraza.
Thanks

Unadhani wewe kama wewe umechangiaje? na vipi kuhusu exchange rates, changes za policies nyingine na business environment??
 
Jerry Slaa,
Mkuu wangu jaribu sana kuwa na staha ondoa jazba na kama ulivyoshauriwa kuna hoja ambazo huna sababu ya kuzijibu maadam ziko nje ya swali isipokuwa ni kashfa binafsi (personal) hivyo kwa majibu yako kama haya inaonyesha wazi weweni kingozi wa aina gani na kwa nini kazi hiyo ILOPEWA imekuwa ngumu kwako.

Maswali yetu ni rahisi kabisa kwamba jiji la Dar linazidi kuwa chafu, kwa mfano mdogo tu umezungumzia makusanyo ya fedha soko la Ilala ambayo yameongezeka toka umeingia madarakani na pia kuwezesha mfuko kupanuka zaidi kuliko zamani lakini kama fedha hizo hazifanyi kazi kuboresha soko hilo hilo likaonekana zuri na tofauti hizi fedha zinachukuliwa kama biashara tu...

Huwezi kusanya mabillioni ya fedha toka sehemu muhimu kama soko la Ilala lakini soko lenyewe haliboreki yaani linazidi kuwa baya na chafu watu wanapanga mali zao hadi barabarani ili mradi mnajaza wateja kuongeza pato. Vivyo hivyo sehemu nyingi za mji wetu zinazidi kuharibika wakati hizo fedha mnazotenga kwa maendeleo haziifanyi kazi inayotakiwa..

Swali jingine ni kwamba ikiwa leo Kingunge anaweza kusanya fedha za parking na akawalipa asilimia yenu nani mwenye jukumu la kuboresha Parking hizo?.. Na inakuwaje mtu binafsi kama Kingunge anaweza kusanya fedha bila vifaa vyovyote vya parking akitumia nguvukazi ya watu lakini City inashindwa kukusanya yenyewe hadi mnakodisha watu binafsi ambao hawaboreshi wala kuongeza pato la ukusanyaji kodi hiyo ya parking..

Mengine yatafuata kuhusu mapipa ya Taka ambayo kijana mdogo rafiki yangu aliwekeza Dar na kuyasambaza wilaya ya Kinondoni lakini Ilala amekwamishwa kupewa zabuni hiyo na sababu nazijua!. Sasa mwananchi ambaye yuko tayari kusambaza mapipa ya taka kando ya barabara manispaa yako (uwajibikaji wa mwananchi) anapokwamishwa na uongozi wa City (uwajibikaji wa kingozi) utaweza vipi kuwalaumu wananchi ambao wako tayari ktk uwekezaji lakini hukwamisha na Urasimu wa Halamashauri yako?

Good questions Bob

Kusema ukweli kabisa, hadi leo siioni wala siijui vision ya Meya Jerry.... at one time alidiriki kusema kwenye formal meetings kwamba yeye anaangalia income kwanza (zaidi ya kikao kimoja cha huduma za jamii)

nadhani after hiyo income sasa arudi kwenye mstari kwani lengo kuu ni lazima liwe wellbeing ya watu wake pamoja na social justice

sioni vision yake ningependa sana Jerry unisaidie vision tu
 
Back
Top Bottom