mkulima wa kisasa
Member
- Dec 27, 2011
- 11
- 1
Sasa kujifanya ana mipango kabambe kumbe naye ni timu moja na masaburi na iddi simba kwenye sakata la UDA?
ama kweli JF mnajua kuibua ishu
ama kweli JF mnajua kuibua ishu
mkuu utaambiwa una wivu......Ukitaka kujua kama huyu Jerry hafai nenda Kariakoo utazamae drainage, foleni na jinsi maduka yalivyokuwa hayana mpangilio
acha kutufanya sote wajinga humuWanaJF,
Wakati mwingine tuwe na kiasi katika kumlaumu ama kumpongwza mtu, naomba niwakumbushe kwamba system ya nchi hii ni ngumu sana na zaidi ni nyimi sana. Kuna wakati chadema walitamka kutokutambua matokeo yaliyompa urais JK na kwa maana ingine kutomtambua kabisa rais. Lakini mwisho wake ni JK yuleyule ndio mwenye final say hata kwenye kuweka mapesa kwenye mifuko ya maendeleo ya majimbo chini ya wabunge wote.
Silaa sikutegemea atafanya lolote la kushangaza ikiwa huko nyuma hakuna chochote kilichofanyika cha maana sana. Anashindwa kufanya mambo mengi kwa sababu nguvu yake haishindi system ma mkae mkijua ccm iko makini kuwakwamisha chadema katika kila jambo. Aibu tuliyovuna ya chadema kwenda ikulu kumshauri mtu wasiyemtambua inatosha kuonyesha kwamba Silaa hana cha kufanya hata awe anashinda vijiweni kwa sie akina choka mbaya.
Ndio nasema ni afadhali katiba yetu mpya, kama ni kweli itaandikwa, ipunguze madaraka ya rais ili pawepo na universal balance. Kama tutapoteza muda kutaka kujua Silaa kafanya nini kwa mwaka mmoja tu ihali hata serikali haiwezi kulipa mishahara kwa watumishi wake tutakuwa tutakuwa ni wavivu wa kufanya tafiti na kutoa mijadala.
Siku zote, hatutaweza kumpima mtu utendaji wake kwa kumvizia ama kumlinganisha na mwenzake, tunampima mtu kulingana na mipango mkakati yake na hali halisi. Hapa JF nishaona sana watu wanaanza kupoteza sifa ya u great thinkera na badala yake gossips zimekuwa ni sehemu ya mijadala yetu, tuwe wakweli, kama Silaa anauza sura basi ni sawa mwacheni auze sura kwani nyie mlikuwa wapi kumhoji wakati mnamchagua? Ama niulize hili, mlikuwa wapi kumdodosa kabla ya kukmasim madaraka hayo makubwa.
Mwisho napenda kuwashukuru wote mliochangia thread hii, na ni wakati huu sasa ambapo naitisha wote msitishe kuchangia kwa kuwa hakuna hoja nziti za kumlaumu mtu ndani ya mwaka mmoja. Kama mtu ataendelea kuchangia hoja hii ni sawa kwa kuwa katiba inaruhusu mawazo binafsi yasiyovunja sheria.
Nawatakia mwaka mpya wenye baraka na mafanikio, na kwa Silaa, nakuomba punguza kwenda kwenye kumbi za starehe na gari la umma wakati usio wa kazi, gari hilo ni nyenzo kwako katikz kufanyz kazi zako rasmi za umeya na sio mara Double Tree, mara mlimani city, mara rose garden, babu unajishushia.
Ni mimi,
Pangu Pakavu,
Nawasalimia.
Gotta love JF!Hii thread ya Hossam aka pangu pakavu ameandika Jerry William Silaa mwenyewe.
Jerry mimi ni rafiki yako wa siku nyingi sana, wakati tunaogelea wote mto msimbazi na tunasoma wote Ukonga Primary School, kwa mwalimu Nyandindi, Ntilu, Buyobe, Best etc.
Jerry my friend you need to do more than what you are doing now, maisha ya ukonga hata kwenu Pugu yamekua magumu sana, just badilika na uwe makini kwenye mambo yako... Achana na mambo ya ujana, kama kipindi kile ulivyokua... Pls elewa now unatumikia umma!
Mfumo mbovu wa serikali inayoongozwa na chama chako ndio imefikisha watu wengi katika daraja la kushindwa maisha.Halmashauri ni taasisi inayofanya marketing and PR na katika hilo meya huwezi kumwacha kila aliyetumia neno "kuuza sura" ameonyesha uwezo wake finyu wa kufahamu mambo, kama wanavyosema wanazuoni "intellectuals discuss issues not personality" najua ni ngumu mtu akijiangalia umri wake na achievement alizorecord kukubali failure, ila it doesnt make u a better person kwa kushambulia wengine.
mfumo mbovu wa serikali inayoongozwa na chama chako ndio imefikisha watu wengi katika daraja la kushindwa maisha. ni janga kubwa kuliko unavyodhani na kukejeli jamii inayokata tamaa
Anajiandaa kugombea jimbo gani? Wacha na miye nizichange nikagombee, maana bongo siasa ndiko kwenye ulaji!mawaidha mazuri sana haya kwa jerry, kama hawezi kukuelewa na kuendeleza nyodo na dharau, atashughulikiwa muda muafaka ukifika.
Tunafahamu anajiandaa kuwania ubunge 2015 tunakusanya kuni za kumkaanga kuanzia JF hadi mitaani!