Jerry Muro, wapi alipo?

Angalau ciku hizi walikuwa wamepoa. Nakumbuka enzi ya Ruksa, mida ya saa mbili uciku ulikuwa unakutana na kundi la vijana kama 20 wamefunganishwa mashati eti walikuwa wazururaji! anayeleta ubishi wanamsingizia kuwa alikuwa na bangi. Hapo wadau wapo kazini ndo serikali yenu hiyo!
 
Mbona unatuchanganyia habari. Maskini kwa lipi? Ni mmoja kati ya watuhumiwa aliyedai kwamba alikuwa coerced kusema kwamba walitenda kosa ili aachiwe waendelee na mlengwa wao Jerry. Kwani hilo ni jipya kwa polisi wa Bongo?

MJM = Maskini Jerry Muro. Teh teh teh teh. Aah nimefurahi tu.
 
Mwenye update na hii kesi tafadhani atupe update naona sasa imekuwa kimya sana wameamua kumpotezea katika sura ya dunia?
Mdau mkereketwa
 
Choonde choonde jamani tunaomba kesi ya Cuf kuingiza silaha nchini, Jerry Muro, na Ishu ya Uraia wa Bashe, tuziache kama zilivyo zinaweza kuleta hali ya kutoelewana katika hiki kipindi cha uchaguzi, Tushirikiane kudumisha amani na mshikamano tuliorithishwa na mababu zetu na kuuzoea. Kidumu chama cha Mapinduzi
 
jina na sura ya Jerry Murro si ngeni machoni na masikioni mwa watanzania
tulio wengi,hasa kwa watu wanaopenda kufatilia nchi yao kupitia vyombo vya
habari. Na kama ulikuwa mfatiliaji basi jina Jerry Murro si ngeni kwako. kwanza
alianzia ITV na baadae alihamia TBC1 ambako alikutana na maruheruhe kwenye
kazi zake mpaka kufikia kupelekwa mahakamani. Swali langu ni mbona simuoni tena
kwenye kioo cha TBC1? au ukiwa na kesi uhurusiwi kujishughulisha na mambo ya
habari tena? au ameacha kazi TBC1?. Na ile kesi yake PASUA KICHWA bado anayo
au ilishakwisha? tunamisi manews ya Jerry wa kufichua uvundo wa chini ya kapeti.
 
Kama nitakuwa sahihi alishafukuzwa kazi,kwani kinachotakiwa ni kumuondoa kabisa kwenye mawazo ya watu,kumbuka kuwa tbc1 inatawaliwa na mafisadi.
 
jina na sura ya Jerry Murro si ngeni machoni na masikioni mwa watanzania
tulio wengi,hasa kwa watu wanaopenda kufatilia nchi yao kupitia vyombo vya
habari. Na kama ulikuwa mfatiliaji basi jina Jerry Murro si ngeni kwako. kwanza
alianzia ITV na baadae alihamia TBC1 ambako alikutana na maruheruhe kwenye
kazi zake mpaka kufikia kupelekwa mahakamani. Swali langu ni mbona simuoni tena
kwenye kioo cha TBC1? au ukiwa na kesi uhurusiwi kujishughulisha na mambo ya
habari tena? au ameacha kazi TBC1?. Na ile kesi yake PASUA KICHWA bado anayo
au ilishakwisha? tunamisi manews ya Jerry wa kufichua uvundo wa chini ya kapeti.
Aliwafuata mafisadi akifikiri kapata kumbe kapatikana. Sasa kwishney. Hivyo ndivyo ccm huwafanya wote wanaokuwa na kiherehere cha kupinga ulaji wao. Uwakenulia meno kumbe huwa ni chambo tu. Mwisho yanawakuta yaliyomkuta. aliyataka mwenyewe na kuyafuata mwenyewe huko TBC
 
Wimbo:
Chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi X 4
Nyerere... aahaaaa, vingozi wa chama wajenga nchi!!!
 
g waungwana nadhani kulikua na maswali mawili ya msingi. Kaisha fukuzwa kazi? Pia kesi iliishaje? Pliiz kama kuna mtu ana dits aziweke hapa, hata mi ningependa kujua whats goin on bout his case. Gracias
 
Kesi ya jerry Mulo bado inaendelea. Kesi yake nionavyo mimi imekaa kisiasa na kisanii zaidi.Kazi tbc nadhani imeota mbawa kwani chombo hicho ni chakifisadi na kiccm na mulo aligusa maslahi yao.kinamramba na chenge wanakesi za kuhujumu uchumi ila wanaendelea na kazi,lakini jerry naye kahisiwa tu kazi stop hapa panauma hii si nchi ila pagale la wanyang'anyi MUNGU tuokoe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom