Jerry Muro: From ITV to TBC1

Jamani,

Jerry Muro ameajiriwa TBC. Alilazimika kuondoka IPP Media (ITV), baada ya jitihada za kumzuia kwenda Marekani kwa kozi fupi kushindikana. Wakubwa zake ITV walijaribu kumzuia, bila ya sababu za msingi na ni kinyume cha jittihada za kuwaendeleza vijana, lakini waliomdhamini, Wamarekani wa USAID, walimpeleka baada ya kuona sababu za kumzuia ni "roho mbaya". Vivyo hivyo kwa kijana mwingine wa ITV, Sudi Mnette, ambaye naye walitaka kumzuia asiende Deutsche Welle, Sauti ya Ujerumani kwa kozi ya miezi sita, lakini akalazimika kuachana na ITV, kwa sababu kama za Jerry Muro na akaenda, akamaliza kozi, sasa ameajiriwa pia na TBC! Hayo ndiyo ya IPP Media na maendeleo ya vijana!

Bwassa

Ni kweli kabisa Bwassa,
Sudi Mnete amerudi toka Deutsche Welle sasahivi yuko TBC, kwa mtu anayefuatilia matangazo ya TBC atakuwa amemsikia au kumuona.Jery Muro naye ameshapata ajira TBC muda si mrefu ataanza kuonekana kwenye runinga ya TBC1.

Lakini suala la watangazaji mahiri kuondoka ITV/IPP sio suala geni, ni watu wengi sana wamekimbia, nadhani kuna tatizo la msingi IPP ambalo linahitaji kupatiwa ufumbuzi. Sasahivi taarifa za habari za ITV imeshakuwa ni kazi ya watu wawili, Nitwa na Chiku Lweno, sasa kwa kampuni kama IPP inakuwa inajiaibisha kwa kutolinda watangazaji wake tena hata wale mahiri.
 
Hivi ni ofisi gani mwajiriwa waweza kujiondokea tu ukaongeze maarifa bila ya kupata ruhusa? mara nyingi Kozi zinazohusiana na proffession huwa zinaandaliwa na section ya HR inayoitwa T&D. Ukitaka kuondoka na mwajiri akaona si busara uondoke kwa kipindi hicho basi mfanyakazi unajiuzuru, unayeya, ukirudi unaomba tena ajira, kama nafasi bado itakuwa ipo. vinginevyo kibarua ndo hivo kinakuwa kimeota nyasi.

sasa kama ITV hakuna idara ya HR hilo nano ni tatizo tata!
 
What of Misanya Dismas Bingi. Namkumbika sana huyu jamaa na wimbo wake wa asubuhi wa yeke yeke ua yeke yeke
 
Jamani,

Jerry Muro ameajiriwa TBC. Alilazimika kuondoka IPP Media (ITV), baada ya jitihada za kumzuia kwenda Marekani kwa kozi fupi kushindikana. Wakubwa zake ITV walijaribu kumzuia, bila ya sababu za msingi na ni kinyume cha jittihada za kuwaendeleza vijana, lakini waliomdhamini, Wamarekani wa USAID, walimpeleka baada ya kuona sababu za kumzuia ni "roho mbaya". Vivyo hivyo kwa kijana mwingine wa ITV, Sudi Mnette, ambaye naye walitaka kumzuia asiende Deutsche Welle, Sauti ya Ujerumani kwa kozi ya miezi sita, lakini akalazimika kuachana na ITV, kwa sababu kama za Jerry Muro na akaenda, akamaliza kozi, sasa ameajiriwa pia na TBC! Hayo ndiyo ya IPP Media na maendeleo ya vijana!

Bwassa

tunashukuru sana kwa information ila mbona mpaka sasa hajaanza kuonekana kwenye Luninga
Na kutangaza habari za ufisadi imefika mwisho cause pale TBC access denied
 
tunashukuru sana kwa information ila mbona mpaka sasa hajaanza kuonekana kwenye Luninga
Na kutangaza habari za ufisadi imefika mwisho cause pale TBC access denied
Jana nimeona Promo yake kizungumza na Karume, Ikulu ZnZ, Jerry anakuja na kipindi bomba sana ali mradi isiwe nguvu ya soda.
Habari za ufisadi wa ukweli sasa hapa ndio nyumbani kwake, sio kule kweli walikuwa mstari wa mbele kutangaza ufisadi, ili pia waliegemea sana kwa washindani wao wa kibiashara, huku fisadi ni fisadi tuu bila egemeo, Tido aliyeanzia RTD akamachure Sauti ya Kenya na Kukomalia BBC, anakijua anachokifanya TBC subirini tuu matokeo.
By the way hata kabinti fulani ka ITV nimekaona TBC

tuwatakie kazi njema.
 
Huyu Mengi kila siku anajigamba anasaidia Watanzania kumbe anajivisha ngozi ya kondoo wakati yeye ni chui, au huyo mama Mhavile ana matatizo gani na vijana-----anataka waanze kula kwake. Hii ishu, kwani hao jamaa kama hawana HR section hata Training depart nayo hawana, kwani huyu mhavile ni MD, ache mambo yake bana, halafu nafikiri ana ascent ya kichagga, lakini nae Jerry si hivo hivo? Hii ishu sasa.

Rom
 
100%

nimewahi kufanya hapo upande wa ICT kwa mda ,
waulize tu hata malipo wanayopewa! ni shiiiiida!
Kaka nakuaminia na bado unahasira nao...nakumbuka kila ukikuta TV channel ni ITV lazima ubadilishe!!
 
Nadhai hizo zote ni Blaa Blaa. Cha muhimu ni kujua yuko wapi na anafanya nini kutokana na kutoonekana ITV kwa muda mrefu
...Ananikumbusha siku alipokuwa anaripoti kuhusu vurugu za mkutano wa walimu pale Diamond Jubilee jamaa kwenye runinga huku anakwepa mawe yaliyokuwa yanatumwa kwa mzee G.Mkoba!!!!
 
I commend the good job done by Tido!! TBC is shining tena by far kuzidi hata TV za binafsi!!

Congratulations Tido and the whole TBC team!!
 
Jerry Muro kwa sasa yupo katika mikono salama. IPP kuna matatizo hakuna mtangazaji mzuri ambaye atakaa huko kwa muda mrefu. ITV yenyewe imekuwa haina mvuto kwa kukosa creativity, soon watashindwa na hata Mlimani TV.
 
I commend the good job done by Tido!! TBC is shining tena by far kuzidi hata TV za binafsi!!

Congratulations Tido and the whole TBC team!!
Mzee usifanye mchezo na ruzuku!!! TV binafsi mpaka wategemee matangazo!! kwa hiyo unavyo compare hapo hauzitendi haki TV binafsi!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom