Jerry Muro awaanika askari kwa rushwa, nini kitatokea?

Kama video ingeweza kwenda mbali zaidi! Kuna maamuzi mengine wanayofanya viongozi wetu unaona kabisa wanasukumwa kama toroli, no logic inside.

Leka
 
jamani wale wanatumwa mfano mzuri kuna boss mmoja wa trafic kibaha amehama kituo kikuu akahamia kiofisi kidogo pale barabani, na hili linasababishwa na hali halisi ya nchi wakubwa najilipa mishara mikubwa hawa wadogo hawana kitu
 
Hiv hiki si kile cha ITV alirusha huko nyuma alipokuwa mwajiriwa wa ITV au ni kipya karekodi tena?? Na ninakumbuka IGP Said Mwema aliwafukuza kazi wale askari waliohisika kipindi kile.
Aliwafukuza kazi wapi wewe....uliza uambiwe
 
Kipindi kinaendelea TBC1, amewaonyesha 'live' askari wa Makambako - Iringa wanavyochukua rushwa na akasema hiyo ni awamu ya kwanza na watanzania wasubiri awamu ya pili, akiendelea kuwaanika wanaofanya hivi, je watamwacha aendelee kuwaumbua?

Safi sana Jerry!

Dr Pimbi,
Kazi kama hii ndio tunayoitaka Watanzania. Ni kweli kuna 'risk' lakini tukiogopa ku-take risk, ndiyo hayo tunayoyaona mtu kaiba watu wananywea kwamba ni kigosile ukimgusa uhai hauna. Zaidi tumtie moyo Jerry Murro
 
Hii nchi inaendeshwa kama genge. Majibu ya Mkuu wa PCCB Iringa na mwenyekiti wa usalama barabarani mkoani humo kwamba wanapambana na rushwa ya barabarani yanatia kinyaa. Hata Msiika hakuwa na jibu zaidi ya kujikanyaga. Hao askari 11 inasemekana wamesimamishwa kazi na kutakiwa kuandika maelezo ya kina. Sikuelewa hayo maelezo ya kina ni yanini wakati kuna ushahidi wa video ambao wahusika hawawezi kuukana. Polisi wanazuga tu. Baada ya muda mambo yatakuwa yale yale. Ila hao wananchi waliolalamika kuwa huwa wanatoa kati ya shs 30,000 na 100,000 wajiandae kutoa mara 10.
 
Hiyo kali; huyo alikuwa na njaa. Ungemwambia aombe hela ya chai kuliko kutumia visingizio vya kipuuzi hivyo. Kama aliingia ndani ya gari ungewasha gari na kuondoka nae ukiwa ume-lock gari kabisa

Mwanamke (Sugar wa Ukweli) afanye hivyo wakati yuko na mtu aliyehitimu mafunzo ya ukora CCP MOSHI?

nGUMU HIYO MKUU!
 
Acha wale moto,walikuwa wamefikia pabaya walikuwa wanataka rushwa kwa nguvu,mie kuna siku alinichomolea ufunguo kwenye gari kisa handbreak za gari niliyokuwa nayo hazifanyi kazi vizuri!!!

mwenzio mie walinisimamisha wawili na vitambi vyao wakaanza kucheki gari kila kona mala gari mpya ilitafutiwa kosa weee halionekani mwishowe nikaulizwa una Try Angle nikawaambia nadhani kucheki kwenye boneti no hiyo kitu ..wakanitoa mshiko wa lala salama au nigeuze gari kituo cha police :mad:
 
kijana atatafutwa huyo kama ana gari ndo itakuwa kasheshe...kioo kikiwa na ufa kidogo ..faini ...Side mirror zimewekwa upande faini ..
kazi buti Jerry

Kijana kajiandaa siyo bure aende na arusha ajionee na kurekodi yaani gari la police limefura mahela elfu moja moja , mbilimbil , tano tano kwenye dash body hawana hata aibu kuna staili utakuta wapo juu kidogo ya eneo linaitwa kikatiti, au pale kibaoni na pale mto nduruma wanapokea rushwa waziwazi wapo na wale wa bomang'ombe wanakuwa pale njiapanda ya kwenda KIA na baada ya hapo utawakuta pale kwa wasomali wanakung'ang'aniza uwape hela kuna mmoja nilikuwa natoka arusha kwenda dar kwa hiyo nikawa nimechukua pesa ya tahadhari njiani basi nikafika kwa wasomali hhheee jamaa nikamwambia mie sina hela basi akaanza kunipapasa mfukoni maana ulikuwa umetuna na kusema hela si hizi apa yaani nilitamani nimnyuke risasi
 
hahahah kaaaaaaaazi kweli kweli haa wanaomba kwa lazima ..Ndo maana wagosi waliimba Traffic huyooo
 
sinkala-albums-sinkala-picture861-trafic.jpg
 
Iko hivi mkuu Mzawa Halisi:

Hizi issue za rushwa zinajulikana mpaka zinafanyikaje. PCCB ukiwauliza wanaweza kukwambia kesi kama hizo wanafahamu na wamefanyia utafiti siku nyingi na walishawasilisha mbele ili zifanyiwe kazi.

Si za polisi tu, hata scandal kubwa tu.

Kwanini iwe maamuzi ya zimamoto?

It went public!

Ikishaenda public na wananchi wakaona na wakaona serikali haichukui maamuzi basi maanake serikali hiyo ni "MFU" na ukizingatia huu ni mwaka 'muhimu' kwao basi wanaweza kuharibu kila sehemu.

Naamini unaweza kuuliza mbona maamuzi kama haya yasichukuliwe kwenye kesi kubwa, videos za scandals kubwa hizi zipo, wakizihitaji wanapewa; zikipelekwa kwenye vituo vya Televisheni vyetu hakuna hata kimoja kitakubali kuonyesha! Kila mmoja anaangalia 'maslahi yake ya biashara' na wengine 'maslahi ya wakubwa'. Basi inakuwa ngumu sana. Tunabaki kukabana na vijidagaa hivi (traffic) na polisi wanaokula rushwa za elfu 10 mpaka laki 1 etc wakati mijamaa inayokula rushwa inayoweza kujenga Hospitali ya kuhudumia taifa zima inatesa mtaani na ndugu zetu wanaangamia tukiwaangalia.

Ngumu kueleza...

Mkuu usiendelee zaidi manake mtu unashindwa kuelewa kama kuna watu wanaweza kufikiri na kujua jambo kubwa na dogo ni lipi. Sie tunaita materiality of an issue!

Aliwafukuza kazi wapi wewe....uliza uambiwe

Mkuu si utuambie nini kilitokea kama unajua ili nasi tujue kama tulizugwa au laaa?

mwenzio mie walinisimamisha wawili na vitambi vyao wakaanza kucheki gari kila kona mala gari mpya ilitafutiwa kosa weee halionekani mwishowe nikaulizwa una Try Angle nikawaambia nadhani kucheki kwenye boneti no hiyo kitu ..wakanitoa mshiko wa lala salama au nigeuze gari kituo cha police :mad:

FL, Unajua hivi vitu vya kwenye gani ni simple sana na ukiondoa vile very basic ambavyo labda ni ghali kama motorvehicle lisence, vingine can be manageable, ni kwamba tu some people hatujataka kucomply.

Mfano mimi kwenye gari nina kila stika, on top nimenunua fire extinguisher ambayo inaweza hata zima nyumba inayoungua, nina triangle mbili za uhakika, kila kitu nimejaribu kiko sawa and zaidi nimeprinti ile "road traffic act" ya 1973 kama sikosei with all amendments, pia kuna tangazo liko kwenye web ya polis nimeprint with all relevant documents nikaweka kwa folda moja. Kwa sababu huwa nazunguka zunguka tz mikoani, huwa nikisimamishwa tu naanza kumpa hiyo folder apekue anachotaka na siongei chochote. Huwa wanachoka manake nilisha pelekana na mmoja mpaka kwa mkuu wa kituo. Kati ya sehemu nilizo pita pita sijaona usumbufu wa kijinga kama niliokuta mbeya ndo ikanipelekea kuja na mpango huo. Ndio inaweza kuwa gharama lakini unafanya once and for all. Hivi sasa mpaka wengine wamesha ni crame hawahangaiki na mimi manake mimi SITOI RUSHWA kama kweli ikibainika ni kosa then nalipa fine ya 20K, na kitu cha msingi ukishalipa usiishie hapo hakikisha unapata excheque gvt receipt otherwise unaweza kuwa umetoa hongo tena kubwa ya 20k bila kujua kwa maana haitakuwa submitted to the accounts kama hujapewa hiyo risiti halali.

Otherwise big up Jerry for the work
 
Kwani wale wa Kibaha mpaka Chalinze Jeshi la Polisi liliwafanya nini na lilichukua hatua gani?
Ndipo tuje tujue hatma ya hawa wala rushwa wa Iringa nao watafanywa nini au porojo tu? Tunaomba Muro wamulike sasa na mafisadi.
 
Hapa pia katika hili hakuna jipya.Watanzania watendaji kama akina Muro wapo tatizo mfumo mzima umeoza. Hakuna asiyejua kwamba traffic Police wanachukua rushwa na pia hakuna asiyejua mishahara ya askari haitoshi ingawa hii si kwa askari peke yao.

Wanachofanya askari hapa ni kutumia nafasi zao kujinufanisha bila kuwaangalia wengine, binafsi sioni tofauti kati ya alichofanya Ndullu (Govennor) na wanachofanya police hawa maskini tofauti ya msingi ni dau na mazingira. Mazingira ya Ndullu yametulia wakati ya askari ni ya kujidhalilisha!! Njaa haina jasiri ndio maana watoto wa mjini wanasema "adui yako muombee njaa"

Kinachotakiwa kifanyike kama nilivyo msikiliza Msika (msemaji wa police) kwamba kuna mipango ya kuboresha maisha ya askari kama kuwaandalia mifumo ya vyama vya kuweka na kukopa ndani ya jeshi ili wasijidhalilishe mbele ya jamii. Hili ndilo linalotakiwa kufanyika. Vinginevyo kuwafukuza kazi na kutowafukuza vyote vinafanana.

Niliwahi kuwa na rafiki yangu ambaye alikuwa traffic baada ya kubadilishwa kurudi usalama wa raia alikuwa tayari kuacha kazi kwa kuwa anakwambia bila kuchangisha maisha hayawezekani na hakusita kuniambia ndio maana askari wengine wanaingia front (kufanya shughuli za kihalifu usiku) na kuwabambikia watu kesi ili ikiwezekana waweze kupata chochote. Jamani hali ni mbaya, jipu halitibiwi linakamuliwa.
 
Kweli kabisa mkuu. Jerry anafanya kazi nzuri sana. Lakini matokeo ya kazi hii sasa amejitafutia title mpya, "ENEMY OF THE PEOPLE". Nchi hii bila kupata madikteta ambao hawajali kuitwa enemies of the people hatutafika popote.
 
kama sio juhudi zako jerry murro x3
matrafiki wangeumbuka liniiiiiii
kama sio juhudu zako jerry murro x3

hope hii ni njia sahihi ya kuwaenzi waanga wetu
 
haswaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,ooooooh kama siooooooooooooooooo
 
traffic corruption is a soft touch!tunataka prosecution kwa EPA,meremeta,twin tower,etc
 
Back
Top Bottom