Jerry Muro apokewa kwa shangwe na BAVICHA

Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa zamani wa TBC, Jerry Muro ( kushoto) akito salamu zake kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji cha Bavicha Taifa iliyoketi Mjini Morogoro kuanzia Septemba 14 hadi 18, mwaka huu.

Kiongozi wa vijana nchini kupitia chama kikuu cha upinzani -CHADEMA John Heche , Septemba 17, 2012 alifungua Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichohudhuriwa na wajumbe kadhaa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kikao hicho kilipanga kujadili ajenda mbalimbali za Vijana na baadaye kufikia kutoa tamko la pampoja kuhusiana na masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Hata hivyo katika Kikao hicho , Bavicha kupitia Mwenyekiti wake wa Taifa , walimkaribisha Mwandishi wa Habari na Mtangazani wa zamani wa TBC, Jerry Muro ili aweze kuwasalimia wa wajumbe wa Baraza hilo walioanza kukutana tangu Septamba 14 hadi 18, mwaka huu.

Katika salaamu zake , Muro alisema, yenye ni mwanaharakati na mtu anayependa kusema ukweli, hivyo kwake mtu kama huyo ni lazima amuunge mkono kama ilivyo kwa vijana wa Bavicha wanavyosimamia kusema ukweli na kuamua kuwaunga mkono.

Jerry Muro muda wote alikuwa akizungumza kwa hisia kali huku akishangiliwa kwa shangwe kuu na vijana hao wa BAVICHA

Taarifa yako haijitoshelezi..kuitwa topic hapa JF!
Kwenye red hujaeleweka ulitaka kumaanisha nini..
 
Haaa, welcome home bro!, ukimsikiliza muro utajuwa tu huyu ni wa kufiti CDM, ujasiri, kweli, mtetesi, asiye na tamaa, CDM ndo nyumbani kwake kwani wa CCM AWEZI KUWANAVYO: Tafuta jimbo kamanda!!!!!!!!!!!!!
 
usilolijua hakika ni usiku wa giza. nakukumbusha jambo dogo tu, Kingunge Ngombale Mwilu alikuwa anahudhuria vikao vya UCCM hadi miaka michache iliyopita, kama nani? FYI, kuna aina tatu za wanachama wa BAVICHA-mojawapo ni wanachama wa heshima ambao umri wao umepita miaka 35. Hawa hawawezi kugombea nafasi yoyote ndani ya Baraza ila ni washauri nk.
 
Mwandishi wa Habari na Mtangazaji wa zamani wa TBC, Jerry Muro ( kushoto) akito salamu zake kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji cha Bavicha Taifa iliyoketi Mjini Morogoro kuanzia Septemba 14 hadi 18, mwaka huu.

Kiongozi wa vijana nchini kupitia chama kikuu cha upinzani -CHADEMA John Heche , Septemba 17, 2012 alifungua Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichohudhuriwa na wajumbe kadhaa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kikao hicho kilipanga kujadili ajenda mbalimbali za Vijana na baadaye kufikia kutoa tamko la pampoja kuhusiana na masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Hata hivyo katika Kikao hicho , Bavicha kupitia Mwenyekiti wake wa Taifa , walimkaribisha Mwandishi wa Habari na Mtangazani wa zamani wa TBC, Jerry Muro ili aweze kuwasalimia wa wajumbe wa Baraza hilo walioanza kukutana tangu Septamba 14 hadi 18, mwaka huu.

Katika salaamu zake , Muro alisema, yenye ni mwanaharakati na mtu anayependa kusema ukweli, hivyo kwake mtu kama huyo ni lazima amuunge mkono kama ilivyo kwa vijana wa Bavicha wanavyosimamia kusema ukweli na kuamua kuwaunga mkono.

Jerry Muro muda wote alikuwa akizungumza kwa hisia kali huku akishangiliwa kwa shangwe kuu na vijana hao wa BAVICHA
hamna cha ajabu hapo. ni mchaga mwenzao.
 
yaani nimecheka kweli kweli. vijana wenyewe ndo hawa? hamna hata aibu. mizee kabisa hii. du!
 
hii ndio point yako?
mkuu sijaona hata mantiki ya hii post. we need to discuss ideas or in very low to discuss event. but with this thread we are discussing people. why wasting time with nonsense. utasema kwa nini ulifungua, fine ningejuaje kuwa hizi ni pumba.
 
mbali na uchaga kazi anachapa kijana.walimfanyia umafya tu baada ya kumuona anasonga mbele kwa kasi. mh! nchi hii bwana, ukujituma kazi tabu, wazembe na mafisadi tu ndo wanakubalika.
 
Huyu jamaa si ni fisadi?

wasiomjua Jerry wanamuona ni mtu wa maana saaana, kwa sisi tuliokuwa naye UDSM kabla hajapigwa disco na akaenda kuanza upya chuo Tumaini tunajua jinsi jamaa alivyo kilaza upstairs na anavyopenda pesa chafu za chapchap.
 
[h=2]Jerry Muro aibukia Bavicha[/h]Mtangazaji aliyejizolea umaarufu katika vipindi mbalimbali vya Televisheni ikiwemo kituo cha ITV, Jerry Muro, ameibukia katika mkutano wa kamati tendaji ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) na kuwataka vijana kufichua mafisadi wanaotumia vyeo vyao na fedha ili kuwanyonya wananchi.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa kamati hiyo tendaji, Muro ambaye kwa sasa ni mwanaharakati wa vijana, alisema vijana wanapaswa kupiga vita viongozi wanaotumia fedha na madaraka yao kufanya ufisadi na kusababisha wananchi kuishi katika hali ya umasikini.

Alisema hivi sasa nchi inakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendo vya ufisadi hivyo vijana kote bila kujali itikadi ya vyama wanapaswa kuhakikisha wanapigania maslahi ya nchi badala ya kunufaisha watu wachache wenye tamaa.

"Ni lazima mkumbuke kuwa asilimia 18 ya vijana wa hapa nchini ni vijana wasomi huku wakikosa ajira hivyo ni vyema wakachukua nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo kupigania harakati ili kuliletea taifa maendeleo,'' alisema Muro.

Aliongeza kuwa "nawahimiza vijana muwe mstari wa mbele katika kuitetea nchi na kuhakikisha inapata maendeleo sambamba na kuwafichua mafisadi ambao wamekuwa wakitumia vyeo vyao na fedha katika kuwanyonya wananchi."

Kadhalika, aliwataka Bavicha kuwa mstari wa mbele kuonyesha nidhamu ili kuwa mfano wa kuigwa na vyama vingine vya kisiasa nchini.

Kwa upande wake akifungua kikao hicho cha kamati tendaji kinachoshirikisha wenyeviti na makatibu kutoka mikoa yote, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche, alisema nchi imekuwa ikikumbwa na changamoto mbalimbali hususani za kisiasa, kiuchumi na hata kijamii hivyo inahitajika njia mbadala wa kuzitatua changamoto hizo hasa kupitia vijana.
 
Back
Top Bottom