Jenista Joakim Mhagama

Mnataka Da Jenny alione bunge lijalo katika tiviii siyo?

Vyovyote vile, kwani hata wananchi siku hizi nao wameamka, usipotimiza wajibu wako utaliona kwenye TV tu? Mi namfagilia haswaaa! Kwani katimiza wajibu wake.

Na hii ni changamoto kwa wabunge wengine wote, msisahau kwamba tulio wapa tiketi ya kwenda kwenye jumba hilo ni sisi wananchi, badala yake mna fika huko mnakuwa wanafiki, eti mnamalizana pembeni! what is that?

Kama kuna kumalizana pembeni basi haina haja ya kuwa na kipindi cha bunge.. waende wamalizane huko huko pembeni!
 
Rwagubiri,
Naona wajibu wenyewe wanatekeleza kwa kusoma alama za nyakati, kwani wanajua kuwa 2010 ileeeeee pale.
 
baada ya kikao kuahirishwa siku ile nilicheka sana ...kuna picha ilitoka ..mbunge suleiman kumchaya[ambaye amepata kuwa msaidizi wa mkapa siasa]..na moja wa wabunge wa lindi anakotoka ghasia...akiwa amemkumshika mkono anamkokota ..mama ghasia ...huku mama wa watu wazi akionekana na majozi ya kulia...na hasira ...kutokana na mabomu aliyorushiwa na jenista...inaonekana bifu lao litakuwa kali sana hawa!!..

kuna aliyeuliza marriage status ya maama ghasia ...ameolewa na mtaalamu abdulrahman ghasia ambaye ni mwenyekiti wa TFF wilaya huko lindi...[sidhani kama ameshastaafu TFF]

Sio kweli mumewe anaitwa Yahya Mhata na ni afisa wetu wa ubalozi India. TFF alikuwa zamani

BUNGE LA TANZANIA

MAJADILIANO YA BUNGE

MKUTANO WA KUMI NA MBILI

Kikao cha Kumi na Tano Tarehe 1 Julai, 2008

………Mheshimiwa Spika, mwisho lakini sio kwa umuhimu, napenda kuwashukuru wazazi wangu, baba yangu, Mzee Abdulrahman Mohammed Ghasia na Mama yangu – Kashi Balozi kwa malezi yao na pia napenda kumshukuru mume wangu Mr Yahya Mhata na wanangu kwa kunitia moyo na pia kwa kunivumilia pale ninapotea muda wao katika kutimiza majukumu yangu ( Makofi )

Last edited:
Naunga mkono njia aliyotumia Mhagama, sababu kuu ni kwamba njia 3 zimetumika kuomba majibu au utendeaji wa kazi tatizo lenyewe. 1: Yeye mwenyewe kumuona waziri husika, 2: Kuomba msaada wa ofisi ya waziri mkuu na, 3: kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa. Sasa kama wewe njia zote zimeshindikana unafanya nini? Hivyo alichofanya ni binafsi naona ni sahihi kabisa.
 
Rwabugiri,
Maneni mazito sana Mkuu.

Mie sijali kama huyu Mhagama ana sifa gani na kafanya nini huko nyuma. Hawa viongozi wetu wamejiachia sana. Wakiwa wanatunguliwa namna hii walau wataanza kuwa makini. Si mnaona hata Masha sasa hatumsikii? Nafikiri kashashika adabu yake. Sidhani kama bado anakunywa ovyo Rose garden na kuropoka (iliandikwa humu JF). Viongozi wetu walijiachia/wamejiachia sana sana utafikiri akina dada wakishaolewa, kutunza miili yao inakuwa historia. Siku anaolewa mwembamba, hapo ongeza sasa azae, atajaa utafikiri anaenda kucheza Sumo (akina dada don't take it personal na hii si akina dada wote na nafahamu wengine huwa ni matatizo ya hormons).

Mama Mhagama, shambulia hawa wote. Na maadamu imeandikwa "achezae na upanga basi hufa na upanga", wapinzani wa Mhagama wameshapewa mfano wa jinsi ya kumkoma nyani. Kwani alikuwa wapi miaka yote nyuma? Na yeye atakomwa (na naombea akomwe) wakati wa uchaguzi. Hili joto likiwa kali, litatusaidia kujenga miiko ya viongozi kwani mtu ukimess up, wanakuondoa kwani utawapakazia wote.
Hongera CHADEMA na hasa Dr. Slaa na Zitto kwa kuleta huu mchezo wa Mabomu ingawa muasisi wa mabomu ndugu Mzindakaya ALIRUBUNIWA ki-siasa na Mkapa na akapata kitu kidogo na sasa mabomu yake kayafiata kabisaaa. Shame on you Mzindakaya na Mafisadi wote waliokuingiza kwenye Mduara wao.

Edited. Imekaa Sawa sasa.
 
Last edited:
Edit hapo na kuandika ALIRUBUNIWA. Original imeshabadilishwa.

Thanks. Turudi kwenye mada sasa. Kwa kupima inaonyesha kuna tofauti kubwa kati ya issues za wabunge wa upinzani na baadhi ya issues za wabunge wa CCM.

Hile ni National Assembly, na matatizo yake ni lazima yakae kitaifa-taifa. Mama Mhagama inaonyesha ana upungufu fulani. Na huu upungufu unawakabili wabunge wengi na ndio maana bunge letu ni muhuri wa serikali.

Wabunge wengi hawaelewi ni sehemu gani za kupeleka matatizo. Pamoja na kuwa Mama Mhagama alitaka kulipua mabomu lakini sio waziri anayeshugulia waalimu hasa wa shule za msingi.

Inanipa wasiwasi kuona hata baadhi ya wanaJF mnafikiri alichofanya Mhagama ni sawa.

Matatizo yanayowapata waalimu kati majimbo ya Zitto, Slaa, Mhagama ni sawa. Lakini Zitto na Slaa hawajandika listi ya matatizo ya waalimu na kumpelekea waziri Ghasia.
 
Mnataka Da Jenny alione bunge lijalo katika tiviii siyo?

Hapan shaka Jenny atingia bungeni 2010 kwa mbwembwe.
Chenga alo zianza Bungeni ni za Maradona!
Wabunge vyenga mwawala mawaziri mulikuwa wapi siku zote?
 
Huyu dada Jina la awali ni Jenista Ngonyani,Mama yake alikuwa ni mwenyekiti wa UWT mkoa wa Ruvuma miaka kadhaa ya nyuma. Alisoma Diploma ya ualimu katika chuo cha ualimu Korogwe na baadae akawa mwalimu katika shule ya wasichana ya Songea. Aliolewa na Bwana Mhagama mwaka 1992 kwa sherehe ya kufana sana. Mhagama alikuwa ni mhasibu katika idara moja ya serikali. Alituhumiwa kufanya ubadhirifu wa fedha za umma na baadae akabigwa chini.

Kwa sasa huyu dada haishi na mumewe, amenunua nyumba hapo Dom, akitunzwa na wazee. Dada ni mwana mtandao ambaye jina lake kama mambo yangekwenda vizuri lilikuwa linakuwa siku hadi siku. Haya mageuzi ya wapiganaji wachache wa ufisadi yanazidi kumuweka katika hali ambayo siyo nzuri sana, na ni kama ile ndoto ya kwenda juu inaanza kufifia.

Huyu ndiye Jenista Ngonyani.
 
Sioni tatizo lolote katika suala hili. Jenista Mhagama, kama mbunge yeyote mwingine, ana haki ya kukokosoa na kutoa maoni yake mengine yoyote kwa uhuru. Sioni umuhimu wa hoja hii hapa JF zaidi ya majungu tu!
 
Thanks. Turudi kwenye mada sasa. Kwa kupima inaonyesha kuna tofauti kubwa kati ya issues za wabunge wa upinzani na baadhi ya issues za wabunge wa CCM.

Hile ni National Assembly, na matatizo yake ni lazima yakae kitaifa-taifa. Mama Mhagama inaonyesha ana upungufu fulani. Na huu upungufu unawakabili wabunge wengi na ndio maana bunge letu ni muhuri wa serikali.

Wabunge wengi hawaelewi ni sehemu gani za kupeleka matatizo. Pamoja na kuwa Mama Mhagama alitaka kulipua mabomu lakini sio waziri anayeshugulia waalimu hasa wa shule za msingi.

Inanipa wasiwasi kuona hata baadhi ya wanaJF mnafikiri alichofanya Mhagama ni sawa.

Matatizo yanayowapata waalimu kati majimbo ya Zitto, Slaa, Mhagama ni sawa. Lakini Zitto na Slaa hawajandika listi ya matatizo ya waalimu na kumpelekea waziri Ghasia.

Mkuu angalia hizo fact zako mkuu, Kama Hawa Ghasia yeye ndo waziri anaye husika na utumishi, sasa ulitaka apeleke wapi? ili hali ni madai ya watu kuajiliwa/kuwa watumishi?

Si hilo pia mkuu, ok, tuseme alikosea akapeleka kusiko, kwanini asijibiwe kwamba apeleke sehemu fulani ndiko kunako husika? Kumbuka haya madai ni ya myaka mitatu mkuu!

Yaani kama ni Kumkoma nyani, Mhagama did it!, Dada Hawa anachopaswa fanya ni kukubali yaishe ashughulikie hayo matatizo na liwe ni fundisho kwake.

Hizi bla bla za kutafuta eti tumchafue Mhagama kwa vile kasema kweli zilaaniwe kwa nguvu zote, Tunahitaji watu kama Mhagama wanao timiza wajibu wao wa kuiwajibisha serikali.
 
Binafsi ninamheshimu sana huyu mama, ni mchapa kazi, anamawazo ya kujenga na yenye manufaa kwa watu wake (hasa jimboni kwake). Hali hiyo imewafanya wapiga kura wake kumpenda sana. Anapendwa sana jimboni kwake, nadhani ni Mbunge pekee anayependwa na wananchi kati ya wabunge wote wa Mkoa wa Ruvuama.

Mhe. Jenister ni mwanamama shupavu maybe kuliko wamama wengine waliopo bungeni. Nimekutana naye ktk vikao kadhaa, nimemkubali, anastahili kupewa support.
 
Mkuu angalia hizo fact zako mkuu, Kama Hawa Ghasia yeye ndo waziri anaye husika na utumishi, sasa ulitaka apeleke wapi? ili hali ni madai ya watu kuajiliwa/kuwa watumishi?

Si hilo pia mkuu, ok, tuseme alikosea akapeleka kusiko, kwanini asijibiwe kwamba apeleke sehemu fulani ndiko kunako husika? Kumbuka haya madai ni ya myaka mitatu mkuu!

Yaani kama ni Kumkoma nyani, Mhagama did it!, Dada Hawa anachopaswa fanya ni kukubali yaishe ashughulikie hayo matatizo na liwe ni fundisho kwake.

Hizi bla bla za kutafuta eti tumchafue Mhagama kwa vile kasema kweli zilaaniwe kwa nguvu zote, Tunahitaji watu kama Mhagama wanao timiza wajibu wao wa kuiwajibisha serikali.

Alikosea niambie hao waalimu wanafundisha shule gani? Sekondari au za msingi?

Je hao walimu walikuwa na mikataba gani ya kazi na katika mikataba hiyo ya kazi ni nani mwajiri wao? Unataka kusema ni wizara ya utumishi?

Sipo hapa kutetea serikali. Lakini masuala ya kuuliza ukosefu wa chumvi bungeni sio kumkoma nyani.
 
Ameolewa na ana wajukuu....amesota sana Songea huko amejizeekea..usione viji lotion tu vile ila hakuna kitu pale...ni fitina tu nae anataka akumbukwe hata unaibu waziri....msimu ujao
 
Naungana na machungu ya Jeanista kubeba kilio cha watumishi wake, lakini nasimama na Hawa Ghasia kwa mujibu wa rekodi za utumishi, waliajiriwa wakiwa darasa la saba, wakajiendeleza wengine mpaka form four, wengine form six, rekodi zao hazikupelekwa utumishi, hivyo mpaka leo ni darasa la saba.
Kwa mijibu wa Programu ya Kuboresha Utumishi wa Umma, PSRP, serikali, haitoi tena ajira kwa darasa la saba. Na wa kidato cha nne, lazima wawe wamehijimu kijikozi chochote kingine.
Wale form four karibu wote wasio na kijikozi chochote, wamesukumwa kusoma vijikozi hata mshenzi ili kulinda ajira zao. Walioshindwa, wamepunguzwa kazi.
Ili kuwalinda wale darasa la saba waliopo serikali, serikali imeanzisha programu ya PPP inayohushisha makampuni binafsi kuwachukua ma std7 wote na kuwaajiri, halafu wanaendelea kutoa huduma serikalini kupitia hizo kampuni ajira.
Utakuta kazi za umesenja, ulinzi, mapokezi, zote zimehamia sekta binafsi. Secretarial ndio zinafuatia.
 
Alikosea niambie hao waalimu wanafundisha shule gani? Sekondari au za msingi?

Je hao walimu walikuwa na mikataba gani ya kazi na katika mikataba hiyo ya kazi ni nani mwajiri wao? Unataka kusema ni wizara ya utumishi?

Sipo hapa kutetea serikali. Lakini masuala ya kuuliza ukosefu wa chumvi bungeni sio kumkoma nyani.

Mkuu kama shida ya wananchi ni chumvi, na anaye paswa kuwapa chumvi kajibweteka hatimizi wajibu wake, ukimkumbusha alete hiyo chumvi si ndo wajibu wako? si ndo umemkoma kwani hujataka enda mmalizane pembeni?

Sasa yeye kama alijua hilo swala lina husu wizara nyingine kwanini asingetoa majibu elekezi kwamba hilo swala lipelekwe sehemu fulani?

Mkuu katika yote, ni kwamba Hawa hakutimiza sehemu yake, ama la kutatua tatizo, ama kutoa majibu elekezi.

Hata hivo hii kwamba si wizara ya Hawa inayo husika unaiibua wewe hapa, mbona Hakujibu hivo bungeni akaishia kutoa majibu rahisi kwamba ni darasa la saba hawastahili kuajiriwa?

Bado nasimama upande wa Mhagama na nampongeza sana kwa kutimiza wajibu wake!
 
Nimekuuliza swali moja je hao ni waalimu wa msingi au sekondari? Umeshindwa kujibu?

Kwa kuwa elimu yao ni darasa la saba basi ni waalimu wa shule za msingi. Na kama ni waalimu wa shule za msingi basi masuala yao ya ajira yanamalizwa na halmashauri za wilaya.

Na kama sheria inasema kuwa darasa la saba hana ajira, kwanini uyaite majibu ya waziri ni rahisi? Watu hawana sifa za kupewa ajira? Na kama wanasifa wapeleke nondo zao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom