Jengo la washirika lumumba kulikoni?

KASRI

Member
May 2, 2009
93
22
Nilipigiwa simu na rafiki yangu aliyekuwa na biashara zake katika jengo hilo nadhani ni March 2008 kuwa jengo limeungua. Nilidhani ni sehemu ndogo tu lakini nimefika TZ home na kulikuta jengo kama gofu na ni zaidi ya mwaka sasa. Maswali yangu:
1. Kwa nini halijakarabatiwa hadi leo zaidi ya mwaka?
2. Washirika waliovuma miaka hiyo sasa wakowapi?
3. Uwekezaji katika majengo TZ nafahamu uko juu hadi huku US wanaulizia kuja huku TZ, vipi wamekosekana wakuwekeza?
4. Au siasa inatawala?
5.................. nina maswali mengi maana inashangaza gofu kuwa City Centre.

JF nijuzeni nisichofahamu.
 
Nilipata kuambiwa na jamaa last year kwamba owner wana mgogoro na insurance, sina uhakika kwa sasa nini kinaendelea
 
naaam likishaporomoka ndipo watachukua tahadhari.
wizi mtupu
 
owners ni Ushirika ambayo ilikuwa ni jumuiya ya chama nadhani.Sasa with that background tu unaweza kukisia tatizo liko wapi.
 
Jamani; fedha ndo mgogoro-wanahangaika ku-tafuta fedha kwa ajili ya ukarabati na general facelifting! kama kuna wawekezaji waoneni nadhani mtasaidia. Nimeshaona sehemu mbalimbali bakuli lao la kuomba hilo
 
Jamani; fedha ndo mgogoro-wanahangaika ku-tafuta fedha kwa ajili ya ukarabati na general facelifting! kama kuna wawekezaji waoneni nadhani mtasaidia. Nimeshaona sehemu mbalimbali bakuli lao la kuomba hilo

Jamani kweli fedha ndo tatizo au wakubwa wanatafuta sehemu watakayoweza kupata 10% ya uhakika?
Nafahamu TZ wapo watu wenye hela safi nyingi sana za kujenga, nje huko ndo wanagombania kuwekeza TZ nk.
  • Viongozi wa huo Ushirika ni watu wanaoona mbali kweli?
  • Au ni watu waliowekwa kwa kujuana ilimradi kulinda maslahi ya wengine?
  • Je USHIRIKA upo kibiashara kweli na wanakubali kukaa na gofu zaidi ya mwaka?
Wenye taarifa zaidi tujuzeni maana kama wangetangaza kutafuta wawekezaji sidhani kama lingekuwa GOFU hadi leo.
 
Na ukiendeleea kustaajabu ya Musa... Jengo hilo pia ni Makao makuu ya Kikosi cha maafa Tanzania ikiwemo Moto...
 
Na ukiendeleea kustaajabu ya Musa... Jengo hilo pia ni Makao makuu ya Kikosi cha maafa Tanzania ikiwemo Moto...
Duh!!! Ebwanaeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.....DUNG..DUNG...
Bado wapo hapo????????
Nakumbuka WIZARA YA VIWANDA, MSAJILI WA MAKAMPUNI (BRELA), FIRE HQ, BAHATI NASIBU YA TAIFA, GAZETI LA SANI NA AMBHA, CRDB BANK PLC, ETC walikuwa hapo. BADO WAPO???????????????????
KAma wapo basi NCHI inatisha kivileee.

Kwa jinsi jengo linavyoonekana huwezi kudhani kama serikali ina ofisi zake hapo.
Nakumbuka niliwahiu kukwama kwenye lifti mwaka 2002, vipi zipo mpya au wanatumia ngazi????
 
jamani ehh ile Tume ya uchunguzi bado inafanya kazi yake haijamaliza kazi ikimaliza kazi tu mtaona watendaji wakiwajibika.
 
Walishatangaza zabuni na kupata Mbia wa kushirikiana naye kulijenga. Awali walipanga kulikarabati, lakini baada ya kumpata Mbia walikubaliana kunyanyua kikwangua anga kingine ili kuwe na mapacha. tayari michoro ya jengo ilishaandaliwa na kukubaliwa na wanaushirika; hii ilikuwa mwishoni mwa mwaka jana. kwa sasa yawezekana kuna mambo wanayaweka vizuri kabla kazi haijaanza. Kimsingi ramani yao ni nzuri kwa madhari ya eneo lile na Jiji la Dar pia
 
nilipigiwa simu na rafiki yangu aliyekuwa na biashara zake katika jengo hilo nadhani ni march 2008 kuwa jengo limeungua. Nilidhani ni sehemu ndogo tu lakini nimefika tz home na kulikuta jengo kama gofu na ni zaidi ya mwaka sasa. Maswali yangu:
1. Kwa nini halijakarabatiwa hadi leo zaidi ya mwaka?
2. Washirika waliovuma miaka hiyo sasa wakowapi?
3. Uwekezaji katika majengo tz nafahamu uko juu hadi huku us wanaulizia kuja huku tz, vipi wamekosekana wakuwekeza?
4. Au siasa inatawala?
5.................. Nina maswali mengi maana inashangaza gofu kuwa city centre.

Jf nijuzeni nisichofahamu.

mkuu unashangaa nini hii ndio nchi ya mafisadi , akina ra wameona hakuna dili hapo.jengo la walala hoi , wao wanaingia ubia kama jengo la vijana ambako wanaona ulaji wa nje nje.

Pia nenda mikoani majengo choka mbaya , we bora ujirudie huku huku majuu tu usije ukashagaa mwisho ukawa kichaa.

Usilinganishe na huko kwenu ni kwenu tu
 
Back
Top Bottom