Nani mmiliki wa jengo la TANESCO Ubungo?

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Aug 8, 2009
2,907
3,260
Wandugu salama,
Kuna ukweli wowote kwenye hili, hapa nilipo kuna malumbano yanaendelea juu ya nani mmiliki wa lile jengo la makao makuu ya TANESCO pale ubungo, pia inasemekana kutokuwa mali ya serikali ndio sababu iliyomfanya Magufuli kutaka kulibomoa ili kumkomoa mmiliki.

Je, wadau kuna ukweli wowote kwenye hili?

Tan Ubungo.jpg
 
Duh? Hata kama sio la serikali ndo ubomoe rasilimali ya pesa mingi ivo? Si bora kulitaifisha sasa kama wanataka kukomoana. Kuchukua maamuzi ya "tukose wote" ni utoto!

Magufuli Mvinyo anafuata Sheria liwe jengo la papa wa vatcan au papa kwa ufisadi
lipo kwenye road reserve cha kufanya ni sheria ifuate mkondo wake we unasema jengo la
fedha nyingi lisivinje utasema hata mtu mwenye fedha nyingi asifungwe !
 
Kiwanja ni cha Tanesco hivyo Jengo ni la Tanesco ila the developer sio Tanesco.

Jengo hili lilijengwa kwa mujibu wa sheria ya zamani. Kwa majibu wa Sheria zamani ya mwaka 1936, kweli jengo liko kwenye road reserve. Sheria mpya ya Ardhi 1999, ilifuta sheria ya 1936 na kupunguza road reserve, na ile ya 1936 ikaja kuchomekewa tena mwaka 2007 hivyo sehemu ya jengo hilo kuingizwa kwenye road reserve!.

Sababu ya kuvunjwa kwa jengo hilo ni kitoa fursa kujengwa kwa flyover pale Ubungo na sio kumkomoa yoyote!.

Majengo yote yaliyojengwa kwenye road reserve kabla ya 2007 yanapaswa kufidiwa, hivyo hakuna ukomoaji wowote!.
Update
Kama Hii Ndio Situation ya Bomoa Bomoa ya Ubungo na Kimara Bila Fidia, Then Faraja Pekee ni Kuwa, Watafidiwa Tuu!.

Paskali
 
Back
Top Bottom