Jengo la TANESCO na flyovers, which one's more important?

Ubungoubungo

JF-Expert Member
Jul 28, 2008
2,502
739
WAJEMENI, hivi kuvunja lile jengo la Tanesco pale ubungo tukajenga flyovers ya uhakika itakayorahisisha barabara zote nne zinazokutana pale ubungo mataa, na kubaki na jengo lile bila flyovers na kukiwa na foleni ya ajabu vilevile, kipi chenye maana zaidi kwa nchi yetu? kipi kinaleta hasara zaidi kuliko kingine? je?, kubaki na lile jengo lakini watu wanachelewa maofisini kutoka mbezi,kimara etc na mabasi au magari yanayoelekea mkoani etc watu wanafika maofisini kwa kuchelewa hivyo wamepunguza mda wa kufanya kazi na kuendeleza nchi...kipi chenya faida kuliko kingine?...si nasikia magufuli alikataliwa hoja yake ya kubomoa lile jengo ili zijengwe flyover pale?..kwani lile jengo lina garama gani ambayo tunailinda ambayo hatutakuwa tumecompensate indirectly tukijenga flyover pale?
 
Fly over moja haiwezi kutatua tatizo la foleni. Unaweza kuvunja jengo hilo ukajenga fly over Ubungo na magari kuvuka hapo kwa kasi lakini magari hayo yote yatakutana Shekilango, Magomeni, Fire kwa barabara ya Morogoro. Pia yatakutana Buguruni, Tazara brbr ya Sam Nojoma n,k.

Suluhisho la msongamano katika jiji hili ni kujengwa kwa barabara za pembezoni kwa kiwango cha lami (Ring roads) ili isiwelazima kwa magari yote kukutana katika eneo la Ubungo na makutano mengi kama hayo.

Hivyo sio busara kuvunja jengo hilo hizo zilikuwa propaganda za Maguful;i tu kujiotafutia umaarufu tuu!
 
WAJEMENI, hivi kuvunja lile jengo la Tanesco pale ubungo tukajenga flyovers ya uhakika itakayorahisisha barabara zote nne zinazokutana pale ubungo mataa, na kubaki na jengo lile bila flyovers na kukiwa na foleni ya ajabu vilevile, kipi chenye maana zaidi kwa nchi yetu? kipi kinaleta hasara zaidi kuliko kingine? je?, kubaki na lile jengo lakini watu wanachelewa maofisini kutoka mbezi,kimara etc na mabasi au magari yanayoelekea mkoani etc watu wanafika maofisini kwa kuchelewa hivyo wamepunguza mda wa kufanya kazi na kuendeleza nchi...kipi chenya faida kuliko kingine?...si nasikia magufuli alikataliwa hoja yake ya kubomoa lile jengo ili zijengwe flyover pale?..kwani lile jengo lina garama gani ambayo tunailinda ambayo hatutakuwa tumecompensate indirectly tukijenga flyover pale?

kama wanahela za kujenga flyovers waanze na TAZARA hapo ndo tutajua wako serious. wasitake kupata umaarufu tu kwa kubomoa jengo ka TANESCO.
 
Magufuli anatafuta umaarufu wa kisiasa,akumbuke hizo ni kodi za walala hoi ambao wanashindwa hata kujenga kibanda cha kuishi,kwa ufahamu wangu flyover ni barabara za juu kuna unazima gani wa kuvunja nyumba za wananchi kwa sababu hy,mbona china barabara zinapita dishani kwa watu ebu akajifunze huko ni ujinga mtupu kuvunja majengo kwa ajili ya flyover
 
Tatizo watanzania wengi hawazijui flyovers ndo maana wanadanganywa kirahisi na kina magufuli, sasa jengo la tanesco linahusiana vipi zaidi ya umaarufu wa kisiasa,, jaman tutembee kwanza tuone walichofanya wenzetu ndo tupige kelele...

I was in hitech city hyderabad,, yaani IT village imejengwa downtown na flyovers zinapita pemben yake, yaan well designed,,, feeder roads zinaingia kwa utaratibu mzuri huku ghorofa za kutosha zipo pembeni...

Tusidanganyane bongo hatuna mfumo wa feeder roads mzuri sasa hizo flyovers zitajengwa vipi bila feeder roads...

Tanesco pale haina ishu yeyote ya kubomolewa zaidi ya umaarufu wa kisiasa... Watu wanatafuta sifa kwa kelele... Wakati jengo linajengwa wao walikuwa wapi?

Jamani tufike hata south africa tu muone flyovers zilivyo sio kupiga kelele tu hapa... Maana tukisema za america au ulaya zile ni levo ya juu sana... Tusogee za africa tu,,, tujue kwanza zilivyo ndo tulete ushabiki,,,
 
Kwani Flyovers haziwezi kujengwa na jengo likaendelea kuwepo??
 
Magufuli anatafuta umaarufu wa kisiasa,akumbuke hizo ni kodi za walala hoi ambao wanashindwa hata kujenga kibanda cha kuishi,kwa ufahamu wangu flyover ni barabara za juu kuna unazima gani wa kuvunja nyumba za wananchi kwa sababu hy,mbona china barabara zinapita dishani kwa watu ebu akajifunze huko ni ujinga mtupu kuvunja majengo kwa ajili ya flyover
una nyumba njiani? panuka kifikra
 
Tatizo ni kwamba huwa tunapenda kutatua tatizo kwa hasara kubwa iso na faida. Sikatai hilo jengo na hata na mengine yakibomolewa. ni sawa tu. Tatizo ni kuwa, hao mainjinia wetu wanataka tu kumpendeza mtu. Jiulize, hapo ndio mwisho wa safari za magari kutoka Kimara?? Au Mjini au Bandarini?? Jibu ni hapana. Ni sehemu iliyoleteleza taabu kuongoza hayo magari.
Kama kulibomoa hilo jengo la umma kutaleta zaidi ya kupendezesha macho, na libomolewe ili magari yapite hadi mwisho wa safari bila msongamano. Ila kama msongamano utahamia kwingine, na hii ni lazima kwani yale magari yaliyokuwa yanakwama hapa sasa yatawahi kule kwingine, Mainjinia wapewe tuzo kwa kuleta mbadala.
Ningetamani kama atakaye amuru libomolewe, naye awe tiyari kuwajibika iwapo huo msongamano utahamia sehemi nyingine kwa sababu ya magari kupita pale kwa haraka sasa.
 
Back
Top Bottom