Jengo la 'Mwalimu House' ni kwa manufaa ya nani?

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
203
Itakumbukwa kwamba walimu wamekuwa wakikatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao midogo kwa ajili ya ujenzi wa jengo ambalo lilikamilika mwaka juzi, na linajulikana kama Mwalimu House. Lipo pale Ilala Boma. Jengo hili limepangishwa lakini haijulikani fedha zitokanazo na pango zinaingia kwenye mfuko gani, na walimu waliolijenga watanufaika vipi. Kuna wasiwasi kwamba fedha hizo zinaingia mifukoni mwa wajanja wachache. Mbaya zaidi ni kwamba walimu bado wanaendelea kukatwa fedha kwa ajili ya ujenzi. Ni ujenzi upi tena? Haieleweki. Wakuu wenye kufahamu undani wa jambo hilii wamwage data humu.
 
mhh.kweli eh.Lakini kwani msimamizi mkuu wa jengo hilo ni nani hasa?.je ni chama cha waalimu kwa maana ya Viongozi wake au kuna mtu,au bodi maalumu ya kusimamia mapato ya jengo?.
 
Wenzetu waliopo kwenye vyombo vya habari watusaidie kuchunguza suala hili. Waliandika tu habari za uzinduzi wa jengo lakini hawajatuambia wenye jengo lao, kwa maana ya walimu, wananufaikaje. Kuna taarifa kwamba vibopa fulani wa chama cha walimu wamekuwa wakigawana mahela na hali zao sasa hivi zimebadilika sana; yaani wamenawili mno kuliko kawaida. Kulikoni 'Mwalimu House'?
 
Mwenye jengo lake yuko Dodoma analilia kuongezewa posho, ngoja akirudi atawajibu
 
mhh.kweli eh.Lakini kwani msimamizi mkuu wa jengo hilo ni nani hasa?.je ni chama cha waalimu kwa maana ya Viongozi wake au kuna mtu,au bodi maalumu ya kusimamia mapato ya jengo?.
Endeleeni kuchangia akirudi kutoka Dodoma tutamuuliza.
 
Back
Top Bottom